Wamunzengo
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 810
- 321
Ingawa Lema uliamua kuepuka kumtaja moja kwa moja uliyemlenga, lakini mazingira na kumu-attack ZZK kwenye suala la posho nikijumulisha na kumbukumbu ya hivi karibuni kuhusu migogoro ndani ya CDM, ni wazi ulimlenga bw ZZK. Ingawa kwako ZZK anaweza akaonekana "mwepesi", nadhani namna tuu mjadala unavyoenda hapa, ni wazi umegudua bw ZZK ni ngoma nzito kwako. Umemu-attack kwa kutumia ngao ya CDM, lakini siamini kwenye hili, mi naichukulia hii ni personal attack.
Nyie wote (Lema na ZZK) ninawakubali sana hasa kwa sababu mpo kambi ninayoiamini sana ya CDM, ila lazima niseme kabisa kuwa mnatofautiana sana kiupeo wa kuelewa na kushughulikia mambo. Upeo wako lema ni mdogo ukilinganisha na ZZK.
Nikirejea athari zenu kwenye siasa za Tanzania, inaonyesha ZZK, ana athari nyingi chanya na nzuri kwa mustakabali wa nchi hii, rejea hoja kama za BUZWAGI, KUMNG'OA WAZIRI MKUU, MABILIONI YA USWISI, KODI KWENYE MADINI na zingine chache ambazo sizikumbuki haraka, kwa hiyo ni wazi bw ZZK ana uzani wa kutosha kisiasa kuliko wewe na hoja zake nyingi huwa ni za kitaalamu na zenye uchambuzi zaidi ukilinganisha na zako zinazotumia maguvu zaidi.
Ama nikireje kwako Lema, athari zako ninazozikumbuka sanasana ni ile ya kumkomalia waziri mkuu kuwa kasema uongo bungeni, ama nyingine labda ni kauli zako zilizojaa ujasiri ambazo umekuwa ukizitoa hapa na pale.
Lakini nikiwaweka kwenye mzani, inaonekana ZZK ana uwezo mkubwa wa kuitumia akili yake katika kuyaendea mambo hali ya kuwa Lema unaonekana unatumia zaidi nguvu kuliko akili, na hii huwa sio nzuri hasa kwenye masuala ya kijamii.
Mfano mzuri ni hiki kioja ulichokuja nacho hapa, nachelea kuita utumbo kwa sababu kwenye uwanja wa watu wenye kuchambua mambo, watu tunapigwa na butwaa. Katika hali ya kawaida, hii ishu ni nyeti, kwa sababu inatishia maslahi ya tawi ulilolikalia ambalo ni CDM, ingawa ukikurupuka unaweza usione hivyo. Hili suala linaharibu taswira ya CDM kabisa kwa kuionyesha CDM haina adabu na nidhamu ya ndani. Kumbuka unayemtengenezea mazingira ya tuhuma ni kiongozi wa ngazi ya juu na ni bosi wako. Kwenye masuala ya kinidhamu unaonekana huna nidhamu, hili suala ulitakiwa uliwasilishe kwenye vikao vya chama vilitolee maamuzi, na ikitokea chama kikashindwa ni bora wewe ukakihama chama kwa sababu kitakuwa hakiendani na mtazamo wako na yale unayoyaamini katika maisha yako. Kumbuka huna ujasili wa kudai una uchungu na umetumia nguvu nyingi kuijenga CDM kumzidi bw ZZK. Mimi binafsi naamini kama ni uchungu wa CDM bw ZZK ana uchungu zaidi kuliko Lema kwa sababu bw ZZK yupo siku nyingi na anafahamika ni moja ya mihimili iliyokijenga chama Bungeni na nje ya bunge.
Bw Lema huna hadhi ya kumu-attack personally Bw ZZK kihunihuni kama ulivyofanya. Kimaslahi ya Taifa mchango wake mpaka sasa ni mkubwa kuliko wako, kimaslahi ya chama bado mchango wake ni mkubwa kuliko wako. Kwa kifupi Lema, bw ZZK sio saizi yako, umeparamia mwamba unaokuzidi uwezo. Tuhuma zako zenyewe zimejaa hisia tuu na hazina mashiko, nakushauri uwe unaihusisha zaidi akili kwenye mambo yako kuliko misuli/nguvu.