Usafiri enzi zile Mwanza yetu

haloh nimekumbushwa mantaline kichwa cha bedford na pia nimekumbushwa gola alafu zikibaki dk15 mpira kuisha tunawahi fungulia wuhwuh fungulia dog ayo ni mambo ya mechi pale ccm kirumba vipi ndugu unaikumbuka NAGASAKI iliokua inawabeba pamba?
 
Ndugu mashine za kariakoo kubwa zilianza kama sikosei miaka ya tisini, hapa naongelea miaka ya 86, 85 kurudi nyuma

Hizo mashine za kirumba ni zipi? zile za barabara ya kwenda mwaloni au?
 
Reactions: ram
haloh nimekumbushwa mantaline kichwa cha bedford na pia nimekumbushwa gola alafu zikibaki dk15 mpira kuisha tunawahi fungulia wuhwuh fungulia dog ayo ni mambo ya mechi pale ccm kirumba vipi ndugu unaikumbuka NAGASAKI iliokua inawabeba pamba?

Nagasaki kwa sana tu, unamkumbuka Mang'ombena Baiskeli yake?
 

We inaonekana tumeishapiganishina mbwa na wewe, Chale sugu namkumbuka ila hiyo ya kutoa jina la kariakoo kubwa bado kidogo.

Mbwa Mbabe kuliko wote wakati huo alikuwa anaitwa POWER walikuwa wanatoka mtaa mmoja na Mbwa anaitwa KOBRA, unamkumbuka huyu Mbwa?
 
unakumbuka ile mechi kirumba 1993 timu ya taifa la tanganyika ikiitwa victoria ililala 1-0 kwa zanzibar mwameja alikua anampiga chenga azizi wa zanzibar bahati mbaya akaanguka azizi akafung tukatolewa fainal ikawa zambia/uganda akabeba challenge cup
 
unakumbuka ile mechi kirumba 1993 timu ya taifa la tanganyika ikiitwa victoria ililala 1-0 kwa zanzibar mwameja alikua anampiga chenga azizi wa zanzibar bahati mbaya akaanguka azizi akafung tukatolewa fainal ikawa zambia/uganda akabeba challenge cup
nakumbuka nvua ilikuwa imenyesha mwameja aliteleza.
 
mang'ombe kama kama hakua wa igoma basi kisesa shabiki wa kutupwa wa tp lindanda mimi pia na mtaa wangu wote tulikua pamba karibu mwanza yote

Mang'ombe alikuwa wa Igoma jirani na Shule ya Msingi Igoma, alikuwa mfanyakazi Wa Mwatex wakati ule ikiwa juu sana katika uzalishaji Wa nguo! Kwenda kijijini kwao alikuwa hapandi bus, alikuwa anapiga peddle tu umbali wa 120km!
 

We achatu. etileo kumawatu wanajifanya wanaijua Mwanza kuliko sisi. babayake Chale sugu ndiye mwanzilishi wa jina Kariakoo.kamautakumbuka ndie aliee anzisha genge hilo alikuwa anauza karanga kwenye kimeza watu wakawa wanamcheka mtumuzima unauza karanga? ile meza kwa mbele akaiandika Kariakoo kwa rangi ya bruu. na ndie mtu wa kwanza kujenga nyumba mlimani maeneo hayo. mwaka 87 aliuza nyumba yake shilingi Elfu 68,000/" akahamia Bhusagara (Busagara) alipo fikahuko akajiita Dume la Busagara kwakua alikuwa na fedha nyingi kuwashinda wenyeji.
 
watoto wa mwanza walikua watundu sana nakumbuka mwaka 90 walikuanatabia ya kuzania tren pale steshen alafu wanashukia pale mwanza south maana ilikua inasimama sasa siku 1 ikapitiliza hadi fera madogo walirudi kwa miguu umbali wa 30km from town

hahahahahaha aisee hiyo nimeikubali mkuu, hao watoto waliisoma namba.
 
nakumbuka nvua ilikuwa imenyesha mwameja aliteleza.

jaman mwanza ya kipindi kile wakazi tulikua wachache laki kwenye mpira tulijaza ccm kirumba mpaka kwenye rami lakini leo wakazi utitiri lakini hata mechi gan hatujai
 

Chale sugu kesasa yuko sengerema,ni mganga wa jadi.
 
Chale sugu kesasa yuko sengerema,ni mganga wa jadi.

josho la kuogeshea dog nyamagana na ilemela lilikua 1 tu pale lilipojenjwa jengo la nssf kuna jama alikua ana dog mkar sana lakin alikua anafyta mkia akionagari
 
Chizi Fureshi TK hawapo ila QSS wapo,japo walisha hama ile mitaa ya Mwanza Hotel...Mwanza Mwanza...Fid Q=CHADEMA
Mkuu QSS hawajawahi kuwa jirani na Mwanza Hotel. Labda kama unazungumzia Jyoti Art Studio ndiyo waliokuwa pale jirani na ofisi za RFA lakini siku hizi nao wamehamia karibu na lilipokuwa duka la FM studio (wauzaji maarufu wa audio cassettes miaka hiyo). QSS miaka mingi wako pale Nyerere road jirani na Furniture Centre.
 

Tiba, na mimi namkumbuka sana huyu mzee Kalori. Wakati ule stand ya daladala nyingi na mabasi ilikuwa pale Tanganyika bus. Kama ulipita Mwaseco ilikuwa kipindi kile cha Mwalimu Mkono na Mwombeki? Kwa sasa wote hawa ni marehemu. Unakumbuka yule mzee mlinzi aliyekuwa na wake wawili wote wakiwa na uchizi fulani? Dereva mzee Hamis aliyekuwa akiendesha lile bus la shule likiitwa fisi na wanafunzi, pia mkewe mzee Hamis akijulikana kwa jina la mama Hamisi akiuza mihogo ya kukaanga kwa wanafunzi mida ile ya chai ya saa nne.
 

Nakumbuka kila kitu ndugu yangu wakati huo Mkuu wa shule alikuwa ni muha fulani akiitwa Mwitila alikuwa anakuja shule akiendesha pikipiki. Mwalimu Mwombeki Mama wa kujisikia utafikiri dunia yote yeye ndiye alikuwa mwanamke peke yake bila kumsahau Mwl. Malaya aliyekuwa anafundisha muziki, Mkuburo akifundisha biology, Mdashas akifundisha Geography na wengineo. Usije kuta wewe tulikuwa darasa moja!!!!!!

Tiba
 

N:B Mzee Kalori kwa sasa ni marehemu alifariki na kuzikwa kijijini Ruhunga Bukoba vijijini alikokuwa amenunua shamba.

Tiba
 
Wito studio si ilikua miti mirefu nyumbani kwa kina shyrose banji

Studio iliyokuwa pale miti mirefu kwaona Shyrose Bhanji ilikuwa inaitwa Lucky Photo Studio. Pale kulikuwa na bro mmoja mweupe mchaga akichana nywele zake staili ya afro hivi. Wito Studio yenyewe ilikuwa maeneo ilipo stand ya daladala za kwenda Mwaloni. Ukishuka ngazi za kutokea kituo cha polisi pale Tanganyika bus na kulipokuwa na restaurant ya Mwadeco kisha ukatize barabara studio ilikuwa kushoto mwa hiyo stand ya Mwaloni.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…