US Election Coverage 2008

US Election Coverage 2008

I think we are missing a point here! unless useme kwamba 82% ya waliompigia kura JK ni wajinga wa kutupwa kulinganisha na raia wa USA (ambao ndo walimpigia kura huyo huyo Bush)...! I dont agree! Swala la kukubalika, ni kwamba JK kila mtu alimuamini na tuliona atakuja na change zaidi ya fisadi Mkapa! kumbe alikuwa ameficha makucha! Jamani kama siyo sisi kujishusha, kuna kiongozi kati ya HRC na BO alishakuwa na kapriensi kuliko JK? Foreign 10?, finance, Nishati nk? lets be real! tukubali kwamba jamaa alikubalika na CV alikuwa nayo..sema tuu he screwed up kwa ujinga wake. to me not BO not Hillary, alikuwa na POSITION ya kufanya maamuzi kama JK..(hata kama ni maamuzi ya nchi maskini kama yetu!)

Obama mwanzoni alionekana saint..haya ya Wright yametoka wapi? na I tell you mpaka Nov. Mengine yatafumuka tuu..thats the game of politics! Na ndo tatizo la kuset high bar..kama akina Spitzer...people expect too much from you.... Ingekuwa vipi kama Obama 2002 angekuwa kwenye senate? angevote AGAINST vita ya Iraq? au 80% ya wa-USA waliokuwa wanasupport hii vita kipindi kile ni wajinga...please lets be real....what makes Obama na Kikwete be different ni systems tuu..kama Obama angekuja kuwa raisi wa Bongo..unafikiri tungebadilika leo? au JK angekwenda kuwa raisi wa USA..angefanya madudu yake (Iam not comparing impossibles)..but ukweli ni kwamba JK had enuf kapriensi to be a leader..kwamba amescrew up..ni kitu kingine!

Harafu watu mnaposema kwamba Obama had a judgement..nashindwa kulielewa..siwaelewi..which judgement? wamarekani wameanza kuichukia hii vita ya Iraq....baada ya mission kwenda kombo! Period. Je wangeshinda..Obama angeeambiwa ana judgement?, si angekuwa condemned kwamba siyo mzalendo?

Wakuu tusijishushe saana hata kama hatujaendelea kama wa-USA bado na sisi ni rightful occupants wa hii dunia kama wao! Mi mpaka leo naamini kabisa, JK alikuwa ni kiongozi lakini kwa sababu yuko kwenye rotten systems na yeye amezungukwa na mafisadi na anakosa will ya kuwashughulikia..ndo maana tuko hapa tulipo na wala si swala la kapriensi....

What I believe BO akiingia madarakani.....interests za Dems domestically zitabadilika nk..lakini interests za Marekani abroad..awe ni Democrat au Republican..hizo hazibadiliki!

Lastly kwa experience..nadhani tunachanganya vitu viwili..kapriensi na exposure! Hillary ana exposure kubwa kuliko Obama lakini siyo experience..ipi hiyo? na tunarudi kule kule..bwana swala la kukubalika kwa kiongozi lina mantiki sana katika siasa! Bill Clinton kilichomsaidia mpaka leo partly ni charisma aliyonayo (na record yake ofcourse)..ni mengi na hili siyo kwa Tanzania tuu..tunaoingizwa mjini...hata huko US, Urusi nk..wapiga kura wanaingizwa mjini tuu..sema tofauti yao na sisi..wana namna ya kujinasua wakigundua..sisi wapi!
 
Masanja,
inapendeza kuona unasema ukweli kama ulivyo mara nyingi....lakini nitasema kitu kimoja(hakina ushahidi), kwamba nikiwa likizo ya kusubiri matokeo ya O'level na baadae nikiwa A'level mwaka 94/95 mie nilikuwa against JK....family yangu ilikuwa inashabikia yeye ktk mchakato wake na BWM, nikaonekana sina adabu kupingana na wakubwa!! kisa kikubwa juu ya upinzani wangu ni instincts zangu, kwamba jamaa ni mswahili mno and therefore alikuwa hafai wakati ule na hafai sasa!!

mambo ya Obama, HRC na kuwa compared na JK juu ya kaperience/xposure umejijubu mwenyewe tena vizuri sana....bottomline hapa ni mazingira na ni hayo hayo yanayo mfanya JK awe hafai (TZ, US au popote pale) na mie toka nikiwa bwa' mdogo sana nililiona hilo kuwa hafai........hata leo kinacho ua team HRC ni uswahili wa kimarekani, I hope umenipata!!

asante.
 
"Well, I am running to be president of all 50 states.”

I thought she was only running for president of the big states, the important states? Cuz if she's running for president of all 50, she needs to go back and look at how many states she's actually won…

Huyu mama mnamwelewa vizuri lakini ???????? Yaani siamini kama hizi flip flop zinatoka kwa mtu niliyekuwa namwamini kwamba ni one of the strongest politician duniani.
 
....mie na pozi swali hapa, je itakuwa jambo la busara kwa Obama kuweka HRC kwenye tiketi kama VP!!?? zingatia mgawantiko na animosity iliyopo ktk hizi primaries.....

binafsi, nasema yes and no....maelezo yatakuja baada ya kuona michango ya wengine.

asante and happy friday kwa wooooooote, kuanzia pwani ya bahari ya hindi mpaka kwa ile ya pacific...

That might be a very convinient marriage but it will produce the worst leadership the US has seen in the recent living history. Hii animosity imekuwa kubwa mno na haiwezi kutoweka over night. Obama atakapokosea kidogo tu kwenye urais wake wapenzi wake hawatasita kusema kafanyiziwa na Hillary. Isitoshe, makamu wako lazima muwe karibu sana sio kuanzia jana bali kuanzia juzi na lazima muaminiane kwelikweli. Mambo ya convinient marriage yanafaa kwenye matukio ya muda mfupi kukidhi haja ya muda mfupi sio kwenye mambo serious kama urais.

Mimi binafsi ningewashauri wanaoweza kumfikia Obama wamshauri afute kabisa wazo kama hili. Vilevile fighter wangu Hillary asije akakubali kitu kama hiki, tena ataonekana yeye anapenda madaraka tu. Amuache Obama afanye kazi kwa nafasi kama atashinda huo uchaguzi.
 
Kitila ,

Kweli ndugu yangu unataka kumfananisha Obama na Kikwete ? Watu wote wenye akili timamu walishajua wanapata nini toka kwa Kikwete NAWAKUMBUSHA UONGOZI WA KISIASA IS ALL ABOUT KUKUBALIKA

Hoja yangu hamkuielewa. TZPride yeye alisema (angalia maneno yake nimeyanukuu hapo juu) kuwa kinacho matter hapa ni kukubalika tu basi. Nami nikamjibu na ninarudia tena kukubalika sio lazima kwamba unafaa. Ndipo hapo nikatoa mfano kwamba sisi watanzania ni mashuhuda zaidi wa hili kuliko mtu mwingine na ninashangaa mtanzania kutoa statement kama hii.
Je, na nyie mnakubali kweli kwamba "uongozi wa siasa is all about kukubalika? Au hamuelewi maana ya "all about"?
 
Hoja yangu hamkuielewa. TZPride yeye alisema (angalia maneno yake nimeyanukuu hapo juu) kuwa kinacho matter hapa ni kukubalika tu basi. Nami nikamjibu na ninarudia tena kukubalika sio lazima kwamba unafaa. Ndipo hapo nikatoa mfano kwamba sisi watanzania ni mashuhuda zaidi wa hili kuliko mtu mwingine na ninashangaa mtanzania kutoa statement kama hii.
Je, na nyie mnakubali kweli kwamba "uongozi wa siasa is all about kukubalika? Au hamuelewi maana ya "all about"?

sawa bwa'kubwa.....watakuwa wamekuelewa vizuri sasa.
 
Masanja: nimekupata mkuu lakini naomba uelewe kwamba 82% ya watanzania waliompigia kura Kikwete walifanya hivyo with very limited information. Usitake tuingie kwenye masuala ya siasa ya Bongo maana hapa si mahali pake, lakini kama Kikwete angekuwa vetted like Obama na Hillary, angekuwa kama Richardson na Dodd! Experience nyingi lakini nothing more.... Bongo hakuna vetting hakuna media inayofuatilia issues. Hiyo ya kumpigia debe nakuhakikishia watu wengi na wasomi walijua huyu JK hana uwezo wa kuendesha nchi mwaka 2005! Lakini baada ya yeye kushinda na rushwa huko Dodoma, wananchi wengi walijiambia MAYBE atatufaa...
Nakwambia Hillary na Obama wote are thousands of leagues above JK, and even we Tanzanians deserve better. Kwanza nilisoma kwenye thread zingine, unafikiri ni akina Obama wangapi wako nje ambao ni half casti au watanzania waliolowea nje na wanashindwa kuchangia maendeleo ya Bongo kutokana na archaic laws zetu. Lakini cheki Marekani wako open, baba yake BO ni foreginer lakini anagombania urais
Tungekuwa open like this, mbona tungepata maendeleo?
 
Msheshimiwa Kitila naona umenikalia kooni! Hebu ni define huko "kukubalika" nimaanishavyo mimi.
Mtu anaonyesha interest ya kuwa kiongozi. Waongozwa wanajiuliza: Anaweza? Anaaminika?Mzalendo? kafanya nini kabla? etc. Waongozwa wanafikai hitimisho; anaweza, anaaminika, mzalendo, anarekodi nzuri ya ufanyaji kazi.....Huko ndio KUKUBALIKA mgombea.
Jamani hili la JK kila siku watu mnalalamika, noi kawaida katika maisha..hata safari ya nchi ya ahadi walimlalamikia Mussa ambaye alipewa uongozi na Mungu. Mambo ya ovyop unaona anafanya JK sasa, angekua Lipumba, Mbowe, Salim or mwingineyo , huwezi jua huenda yangekuwa mambo ovyo zaidi. Asilimia 82% ya watz kuonwa ni wajinga na the few ellites(like Kitilla) kwa kuwa walimpa kura JK..ni unfair.Usipokubalika katika jamii hata kama unauwezo wa kiasi gani....haitakubali iongozwe na wewe. Why? wengi wenye miuwezo huwa si wazalendo vya kutosha..mwisho utaishia kuisaliti nchi. Kama BWM, amabye alikuwa na miuwezo kibao, akapigiwa debe na JKN akaukwa urais na akauza nchi yote!..minig sector was sold by BWM..we will never get anything from there! Miuwezo mingi uzalendo robo. Jamii kama inakukubali basi jamii hiyo wewe ni mfano wao...acheni kuwona hao muishio kwao kama ndo binadamu tofauti..hiyo ni mentality ya kitumwa. Usipokubalika hupati uongozi.Period! Haijalishi unayo mauwezi interm of ma PhD.
 
Ningependa kuona watz wote wanajisikia vizuri kuwa watz kuliko kujutia kama wengi wanavyo onyesha hapa JF.
"just a wish"
 
Obama Takes Lead in Superdelegate Tally
Sen. Barack Obama moved into the lead today in the last category that Sen. Hillary Clinton had claimed to have an edge -- support among the Democratic Party's superdelegates.

Sen. Barack Obama, D-Ill., has taken the superdelegate lead over Sen. Hillary Clinton, D-N.Y., in their battle for the 2008 Democratic nomination.
(AP Photo)The Illinois Democrat grabbed the superdelegate lead thanks to a switch by New Jersey Rep. Donald Payne and an endorsement from previously uncommitted Rep. Peter DeFazio of Oregon.

Those two votes gave Obama a 267-266 lead over Clinton. That is a huge shift since the days when Clinton boasted about a 60-plus vote lead among the party's pros back on Super Tuesday.
 
Masanja: nimekupata mkuu lakini naomba uelewe kwamba 82% ya watanzania waliompigia kura Kikwete walifanya hivyo with very limited information. Usitake tuingie kwenye masuala ya siasa ya Bongo maana hapa si mahali pake, lakini kama Kikwete angekuwa vetted like Obama na Hillary, angekuwa kama Richardson na Dodd! Experience nyingi lakini nothing more.... Bongo hakuna vetting hakuna media inayofuatilia issues. Hiyo ya kumpigia debe nakuhakikishia watu wengi na wasomi walijua huyu JK hana uwezo wa kuendesha nchi mwaka 2005! Lakini baada ya yeye kushinda na rushwa huko Dodoma, wananchi wengi walijiambia MAYBE atatufaa...
Nakwambia Hillary na Obama wote are thousands of leagues above JK, and even we Tanzanians deserve better. Kwanza nilisoma kwenye thread zingine, unafikiri ni akina Obama wangapi wako nje ambao ni half casti au watanzania waliolowea nje na wanashindwa kuchangia maendeleo ya Bongo kutokana na archaic laws zetu. Lakini cheki Marekani wako open, baba yake BO ni foreginer lakini anagombania urais
Tungekuwa open like this, mbona tungepata maendeleo?

Susu mkuu wangu unachoongea hapa ni kweli tupu! BUT lets not walk faster than the music!

Kucompare USA na nchi kama yetu we are missing a point(or losing a bearing?). Iam not trying to bring excuse here..NO..lakini USA nayo ina mapungufu yake ambayo hata mtanzania na umaskini wake asingetamani kuyaexperience leo he (after all we have enough already)! Hivi nikuulize hiyo marekani unayoiona, mtu mweusi ameanza kuthaminiwa lini? watu weusi wameanza KUPIGA KURA lini? kifupi democratic participation ya weusi imeanza juzi! walikuwa consigned kwenye dustbin ya history as a lost course kama Jamaa yetu......Infact mpaka leo wengi wanaamini kwamba wazungu wengi kumpa kura OBAMA ni minimalist approach (though me I believe BO is simply a better politician than his contemporaries..) USA ilikuwa ni preserve ya weupe tuu! Usione akina Wright wanaongea kwa machungu ukawalaumu people have undergone terrible suffering. na exploitation ya miaka mia mbili haitamalizwa na mwesui kuwa WH for four to eight years! rather to change the racial and economic structures of the society

JK ni lost case I agree lakini kama wanavyosema wengine lazima vile vile tuangalie JK alikuwa nani katika mazingira yetu. JK amekuwa FOREIGN MINISTER WA SOVEREIGN STATE (hata kama ni maskini haijalishi) ametuwakilisha raia million 40 kwenye international standing nyingi sana..., sasa obama na hillary hiyo kapriensi waliitoa wapi?? Ni wapi Obama ameshawahi kuiwakilisha serikali katika mazungumzo yoyote? ni wapi Hillary ameshawahi kuiwakilisha serikali kwenye mazungumzo yoyote? (si semi kwamba kapriensi ni serikalini tuu)..lakini experience waliyonayo ni ipi???? sema wote wana EXPOSURE na wamezaliwa na kuishi kwenye mfumo ambao umekamilika tayari. Wewe Susuviri.... Iam sure umefight kwenda huko uliko ukubwani (kunradhi kama wewe umezaliwa huko au wazazi wako walikuwa wanaishi huko)..reflect back unakotoka mpaka ulipofika na sasa unavyoiona dunia..ni viunzi vingapi umeruka?

Kifupi JK ni lost case I fully agree with you.. na amebetray matumaini ya watanzania lakini ukweli ni kwamba hawezi singizia kwamba hana uzoefu neither can we undermine his experience.....he KNOWS what he is doing, protecting his cronies, na kushindwa kupambana na maadui wanaotusumbua kama umaskini.

Hiyo ya kuwa vetted nadhani tunakosea kidogo kaka..why? usiwe kama Mkapa kwamba SI unit ya mwanahabari bora ni RIZI KHAN wa CNN (by the way sijui yuko wapi siku hizi)..bongo hiyo media iko wapi? magazeti yetu mengi ni vijarida vya watu..waandishi wengi ni njaa tupu....hakuna objectivity as you see here at JF na vichwa vya habari vya magazeti.....OK, assume hata JK angekuwa vetted...ni wangapi wana access na hiyo media? personally babu yangu ambaye ndo mpiga kura mahiri tangu uhuru hana TV, redio yake ni mkulima na inashika Majira na KBC ya Kenya! sasa hiyo vetting itamuaffect vipi? na mind you ni wangapi wana redio wachilia mbali hiyo Luninga?

Susu you are one of the people I admire for their objectivity..but mkuu wangu..tunapodiscuss matatizo ya Africa..lazima tujivue miwani ya western world tuingie kwenye hali halisi ya bara letu! Kusema kwamba JK hakuwa vetted kama BO au HRC..tunajidhulumu wenyewe...who will vet who in bongo? mkuu akina Wolf Blitzer, Oberlman, Mathews..bongo hatuna, wanaojaribu ndo akina Ulimwengu hao..wananyang`anywa uraia..upo?

Tuendelee na issues, otherwise I enjoy our diverse perspectives of seeing things. I think its health!
 
Masanja kaka yangu I like your arguments! And they actually do shw the other side. Unajua ni rahisi kuwa carried away na kuwa ' elitist' at times. Najua Bongo challenges ni nyingi sana lakini inanisikitisha kuona kwamba we have so much opportunities lakini we squander it and we remain poor.
Kuhusu Marekani na weusi wake, I absolutely agree and I am aware of the historic injustice. Na ndo maana nilimtetea Reverend Wright na kusema mtu mweusi yoyote hawezi outright akashindwa kuona uchungu wa huyu mzee. I am also aware that things will not change overnight lakini Obama amelenga kufanya kitu muhimu sana, he wants to change the political system, cheki jinsi anavyobadili fundraising, how he sets different standards for campaigning and the politics of distractions. Mimi nadhani he has actually touched on the essence of the problem. Na alikiri kwamba hawezi peke yake kufanya mabadiliko and that it will not be easy. i think hata akikaa Wh for 8 years hataweza kukamilisha all the changes but he can lay the foundation just like FDR lay the foundation with the New Deal for Social Security na marupurupu. Na kumbuka not only Black Americans waliodhulumiwa, maana hao Native Indians ndo kabisa kwa sababu America nzima ilikuwa in their land! But I believe that Obama is going to be one of the few progressive presidents in the entire history of America.
Kuhusu huyu JK wetu, we are stuck with him, but we should learn our lesson from his rule and the way he has been elected. We also have to change the politics and the campaigning, without reforms tusitegemee kupata viongozi bora.
BWM na waandishi wa Bongo had a ' special ' relationship maana there was no love lost. But also he had some legitimate criticism toward waandishi, unfortunately kama rais badala ya kubaki kulalamika how unprofessional the media is, angetakiwa kama a journalist by profession awasaidie, but ndo akazidisha ubabe. Nonetheless naona wapo waandishi ambao wanajaribu kuleta stori za maana ingawa freedom of information act ndo inasuasua. Jenerali Ulimwengu ni mwandishi na mwanafalsafa ambaye nadhani anaweza kutoa mchango mkubwa lakini peke yake hawezi kama tungeweza kuwa na diverse voices in the media kama Kristol na Joe Alter na Fareed Zakaria basi tungefika mbali katika kuanalyze masuala mbalimbali.
I would also like to point out that American media is not perfect but I think despite its faults there' s to some extent accountability inayowafanya viongozi wa kule wawe makini.
Lastly Masanja, I admit that it is always great to be ' elitist' na kubadilishana mawazo!
 
Ningependa kuona watz wote wanajisikia vizuri kuwa watz kuliko kujutia kama wengi wanavyo onyesha hapa JF.
"just a wish"

TZ Pride, hakuna patriotism kubwa kama kujaribu kuendeleza nchi na kuwa tayari kusema ukweli kuhusu uongozi wetu including our President. Hii patriotism unayotaka ni ya kinafiki kama ya Neo-cons wa Marekani akina Bush na Cheney, watu kama Obama walipohoji uhalali na manufaa ya vita vya Irak wakaitwa traitors, kumbe walikuwa wanasema ukweli. Jk ni Bush wetu and until we are not ready to call a spade a spade , we will continue to sink. Angalia wamarekani walivyofumba macho na kumchagua Bush for second term, sasa economy yao ni rock bottom, Iraq is worse than ever! Je akina Hillary na Democrats and Republicans wangesimama na kuwa wakweli Bush angechaguliwa tena kweli? Not really. So for this reason I believe because I truly love my country that we have to be honest and vocal in order to ensure nchi yetu inabadili mwelekeo ili kuleta manedeleo ya kweli. And yes there's buyer's remorse among Tanzanians, this is not what they voted for! And they have every right to express their regret, this does not make them less patriotic only more so!
 
TZ Pride, hakuna patriotism kubwa kama kujaribu kuendeleza nchi na kuwa tayari kusema ukweli kuhusu uongozi wetu including our President. Hii patriotism unayotaka ni ya kinafiki kama ya Neo-cons wa Marekani akina Bush na Cheney, watu kama Obama walipohoji uhalali na manufaa ya vita vya Irak wakaitwa traitors, kumbe walikuwa wanasema ukweli. Jk ni Bush wetu and until we are not ready to call a spade a spade , we will continue to sink. Angalia wamarekani walivyofumba macho na kumchagua Bush for second term, sasa economy yao ni rock bottom, Iraq is worse than ever! Je akina Hillary na Democrats and Republicans wangesimama na kuwa wakweli Bush angechaguliwa tena kweli? Not really. So for this reason I believe because I truly love my country that we have to be honest and vocal in order to ensure nchi yetu inabadili mwelekeo ili kuleta manedeleo ya kweli. And yes there's buyer's remorse among Tanzanians, this is not what they voted for! And they have every right to express their regret, this does not make them less patriotic only more so!


You spot it!

Susu mi naamini wajibu wa kizazi chetu ni kujifunza haya mabadiliko ya dunia na tuyatumie katika kubadilisha fikra hata za watoto wetu. waamini kwamba inawezekana! na wao wana nafasi za kuyafanya bora zaidi, kuliko walivyoyakuta. Mfano,I believe that my child when I get one, he/she must be BETTER THAN ME! Kama leo tunaweza shuhudia historia ikibadilishwa USA (hata kama BO asingeshinda lakini to me, jamaa amepata mafanikio makubwa katika kureaafirm anachokiamini. wengi wetu especially waafrika tunachoka haraka na kukata tamaa haraka! tukishaambiwa haiwezekani we take NO for granted! Kwa huo mwendo we can go no where!

Well, as you say it..its great exchanging views lakini hali ya bara letu kweli inatisha..you wonder what is instore for us..muarobaini wa matatizo yetu ni nini? ni western democracy? ni rule of law? ni kufutiwa madeni yote? ni kipi kitatuinua? Ni kipi hatujawahi kujaribisha tukijaribishe sasa? ambao tungeona kama wangelead tukafuata.ndo hao..anyway, tuendelee..But to me Ia m really learming alot katika huu mjadala wa BO! I hope unanipata.

Niruhusu nikutakie weekend njema ndugu!
 
Bring it on...

Unajua nyani mimi nina majukumu ya kuwa convince wamarekani wenyewe wampigie kura Obama!
Na nimefanikiwa kwa hilo mara nyingi!
Sasa na kwenye jukwaa la kisiasa tuna majukumu ya nyumbani!
Hivyo basi nikaweka kwenye mizani na kujikuta nikikosa uhondo!

Hata hivyo uhondo ninao mimi kwasababu the guy is prevailing and we're proud of it!

Posting zote ambazo niliziposti before zimeprove kuwa kweli na sasa kurudia maneno over and over inachosha!


Unajua wengine tuna uwezo wa kutabiri matokeo ya kisiasa!
So basi..Kwasababu tuko kwenye vugu vugu la mgawanyiko wa rangi..Then tuna majukumu ya kujaribu kulifanyia hilo kazi ili kuweza kukileta Chama pamoja!


Nilikwambia toka mwanzo ndani ya moyo na kwenye damu ya Clintons ni ubaguzi ambao umeshindwa kujificha kutokana na kuwa issue ya uraisi ni nzito na madaraka ni matamu.


Kwa hiyo ina maana kwa watu kama hawa weusi kuwa kazi ya urais ina off limits pale inapokuja kwenye race!


Superdelegates wanaona hilo pia!

Wamegundua kuwa kama Clintons wasingetumia ubaguzi then Obama angekuwa keshatangazwa!

Hata takwimu za ushindi wa Clinton dhidi ya Obama zinaonyesha kuwa ushindi wake ni finyu as opposed to Obama ambaye mara zote yeye amekuwa akisweep!


Ushindi ambao Mama huwa anaupata ni baada ya kuingiza race na chuki kwenye dakika za mwisho mwisho ili kupelekea hisia za woga kwa wazungu wenye kuwatizama weusi kwa jicho la woga! Huku waki justify kwa kuwaita "White blue color workers!" Hawajawahi kuwa na credible win based solely on the issues! Hdi avizie kashfa za kibaguzi!
Kwa hilo amemsaidia Obama na kumjenga tayari kwa mpambano na Mc Cain!


Mama anaweza kuwa yuko right kwasababu asilimia kubwa ya wamarekani weupe ni mabaguzi!
Hivyo basi haamini kabisa kuwa Obama atashinda na hivyo kupelekea hofu ya kuipoteza white house kwa mara nyingine!


Hakuna mahesabu yoyote yenye kuweza kumsaidia mama kushinda nomination na kwa kadri migawanyiko inavyozidi kuendelea kwa muda mrefu kwenye kuelekea uchaguzi mkuu then muda wa ku heal unakuwa very thin!



Clintons simply hawaamini kuwa difeated na watu ambao wao wanafikiri kazi yao inatakiwa kukaa kimya tu ,kuomba na kusubir misaada!
Wanataka wam marginalize kama walivyofanya kwa kina Rev Jesse Jackson pamoja na Sharpton! Kwamba hawa ni mbwa wabwekaji tu na tutawapa mifupa very soon in order to shut up their holla!
Obama has proven to be a different case!

Wanaona kuwa si haki kijana mweusi wa juzi tu aje kuwapindua wao ambao wamewekeza kwa hali ya juu ndani ya chama! Lakini ndo demokrasia hiyo!

The likes of BET owner!

Kwanza hata BET sitizami tena na time sina!

Wish kubwa ya Mama ni yeye awe rais na Obama vice!
Na ndio maana Obama akamwambia how is it right and i am the one who's winning?
Mama yeye ana dai kuwa she ana coalition ya nguvu na kuwa wana nguvu ndani ya chama!
Superdelegates nao wanawaambia kuwa weusi wana make 50% ya wanachama na kuwafanyia viroja chama kitatetereka!
Pagumu sana hapa!
Ila muda si mrefu tutafanikiwa kumove forward na kumface Mc Cain!
 
Tatizo lenu nyinyi maniacs hamna hoja zaidi ya kulia ubaguzi. Mnaamini mkilia hivyo basi mtaachwa kwa sababu hakuna mtu anayependa kuonekana mbaguzi. Leteni hoja kabambe na si kulia lia ubaguzi.
 
Tatizo lenu nyinyi maniacs hamna hoja zaidi ya kulia ubaguzi. Mnaamini mkilia hivyo basi mtaachwa kwa sababu hakuna mtu anayependa kuonekana mbaguzi. Leteni hoja kabambe na si kulia lia ubaguzi.

Yani posting yangu ndiyo unaijibu na huu upuuzi mfupi hivi?
Kwanini usitoe maelezo?
Ama unapenda changamsha genge kama rafiki yangu Ali Paramba pale Majengo Moshi?
Weka hoja bana na si tukauli twa kipuuzi kama utu just for the sake of argument!
Otherwise inaniwia vigumu kupoteza muda kwenye mabishano hovyo!
 
Punguza kwanza hiyo mi font yako. Naona giza nikianza kusoma mabandiko yako...
 
Back
Top Bottom