Urais, Halima, Nassari na Kigoma

Urais, Halima, Nassari na Kigoma

Status
Not open for further replies.
Ama kweli Zitto ana damu ya kunguni maanake.. Dah..
Hapana Mkuu, sikubaliani na wewe...Zitto hana damu ya kunguni! Matatizo anayoyapata Zitto ni ya kujitakia, kuna wakati anashindwa kupima uzito wa kauli zake, kwa mfano;

KadaMpinzani said:
Juni 13, 2008 - Zitto, je una lolote la kusema kuhusiana na kauli yako uliposema kwamba 2010 hautogombea ubunge na utarudi shuleni ??
Nilisema sitagombea ubunge mwaka 2010. Bado ninasimamia maneno yangu mpaka sasa. Sijabadili msimamo huo. Nilisema pia katika mahojiano haya na mwandishi huyu;
http://allafrica.com/stories/200803311770.html
Katika mahojiano hayo alielezwa Zitto Kabwe kama The Country's One-Man Backbench! Unadhani Wabunge wenzake huko Upinzani walijisikiaje baada ya hilo tambo? Hilo tuliache ila mwaka 2010 aligombea baada ya habari kuzagaa kwamba aliombwa kufanya hivyo kutoka maeneo mbali mbali na tatizo lake kubwa lilikuwa ni kuchagua agombee kupitia jimbo gani...Dar, Geita, Kigoma na wapi sikumbuki! Huyo ndiye Zitto.

Likaja la vita ya Comoro, haya ndiyo maneno ya Zitto;
Tanzania funded the operation in Comoro. I can say it athoritatively. The Comoro Operation was 100% funded by Tanzania! France provided an exit for Col. Bacar! Comoro wasnt a proxy war....... take it or leave, thats the truth! The whole truth.....
Lakini baadaye yakazuka ya wakina Shimbo.
Likaja la utendaji wa Idris Rashid na Tanesco - one of the best CEOs,
Machi 2, 2009 - He, yamekuwa hayo tena......... Haya niliyasema toka Septemba 2006. Nikarudia mwaka 2007 na 2008. Huko nako nilihongwa na nani? Huo ndio msimamo wangu toka naingia bungeni kuwa nitasave term moja kisha niende kwenye kazi ninayoipenda ie kufundisha, utafiti na kuandika vitabu.
Likaja la utendaji wa Kikwete - one of the best Presidents,
Likaja yaliyomo kwenye Ripoti ya Bomani...
na mengine mengi...big up kwa JF na kumbukumbu zake!
Likaja la ununuzi wa miambo chakavu ya Dowans,
Niliwahi kumwonya Zitto hapo zamani;
Machi 2, 2009 - I am really sad I have missed this very very interesting debate. However I believe there's more to this than meets the eye. If I were Zitto, I would try as much as I can to stay out of this fray. From afar I see a tsunami building and a fall-out that is inevitable - young Zitto might soon not have a leg to stand on. The key players are pushing him on while they stay on safe ground and he, to their delight, is dancing to their tune. They have been in this game for well almost two decades and this new young man is an exhilarating find in their search for freshness.

Dowans, Dowans, Dowans...who the heck is Dowans - reminds me of the Anglo Leasing of Kenya. It has no face yet it exists and enters into business contracts with the government of the United Republic of Tanzania worth billions. It reminds me of Kagoda - no face but draws billions from the Central Bank. Would Zitto bless Kagoda if it came to our rescue and offered us a panacea out of our predicament ? For someone from our own elective legislative assembly, to come out and support this relationship that smells like rotten fish, is itself degrading enough.

We are going to see a lot of these underhand dealings as we move closer and closer to 2010 - history has a bad habit of repeating itself !! Poor Zitto !!
That was then, this is now...tunarudi kule kuleee!
 
Ukisoma ujumbe wa Zitto between the lines utapata message yote kuhusu mbio za urais 2015.

Kina Mdee walivyopinga inawezekana wanamaanisha kuwa they were under influence of alcohol or other substance so hawakujitambua.

Hata hivyo wanasiasa wa Bongo imefika wakati watambue kuwa technology itawaumbua, wamuulize Hillary Clinton na story yake ya sniper fire ya Serbia...
 
Suala la Urais lisitupotezee muda kwani kuna mambo mengi sana ya kujadili kuhusu nchi yetu.
Utasemaje "suala la urais lisitupotezee muda tujadili kuhusu nchi" wakati wewe mwenyewe ndio ulilianzisha ? Huoni kwamba kutangaza nia ya Urais mwanzoni kabisa mwa kipindi cha ubunge ni dharau kubwa kwa wapiga kura Kigoma Kaskazini?

Hotuba za Wabunge wote zilirekodiwa kwenye video neno kwa neno na video hizo zitawekwa wazi kwenye blogu yangu kama sehemu ya documentary ya tamasha lile la kihistoria.
Nilidhani umesema hukutaka tamasha litangazwe ile liwe "tukio la Kigoma" lakini unageuka unasema litatangazwa kwenye blogu yako, kwa hiyo ulitaka kuhodhi habari ili uje uzitangaze kwenye blog yako? Eti ulitaka liwe "tukio la Kigoma," kwa hiyo kitu kikiwa "cha Kigoma" basi hakitangazwi? Logic ya wapi hiyo? Unawafanya watu wa Kigoma ni kama "uncontacted tribes" wa misitu ya Amazon ambao wakionekana tu na waandishi basi hawana tena ile purity ya u bushmen!?

..maana katika ziara ile sikuita mwandishi hata mmoja maana nilitaka liwe tukio la Kigoma tu.
Umesema mhusika aliyekua anaalika wabunge ni Mwasiti Almasi, na unasema hukutaka kuita waandishi, kumbe waliokua na mamlaka ya kualika na kukataa kualika sio wewe peke yako, sasa mbona ulitaka kuhodhi mamlaka ya kualika na "kukataa" waandishi?

Chama changu bado hakijatangaza rasmi mchakato ... Mwanachama wa chama chetu atakaye kubalika na jamii na wajumbe wa mkutano wa uteuzi ndiye atakuwa mgombea wetu. Kwa sasa hayupo na hivyo tusipoteze muda kujadili jambo hili.
Kama unasema chama bado hakijatangaza mchakato wa mgombea Urais wewe mbona unaanza kutupa dondoo za jinsi mchakato utakavyokua, wewe ndio taasisi ya Mkutano Wa Uteuzi? Hahahaaha.... Zitto ndio una udhaifu wa kujieleza namna hii?
 
Utasemaje "suala la urais lisitupotezee muda tujadili kuhusu nchi" wakati wewe mwenyewe ndio ulilianzisha ? Huoni kwamba kutangaza nia ya Urais mwanzoni kabisa mwa kipindi cha ubunge ni dharau kubwa kwa wapiga kura Kigoma Kaskazini?

Nilidhani umesema hukutaka tamasha litangazwe ile liwe "tukio la Kigoma" lakini unageuka unasema litatangazwa kwenye blogu yako, kwa hiyo ulitaka kuhodhi habari ili uje uzitangaze kwenye blog yako? Eti ulitaka liwe "tukio la Kigoma," kwa hiyo kitu kikiwa "cha Kigoma" basi hakitangazwi? Logic ya wapi hiyo? Unawafanya watu wa Kigoma ni kama "uncontacted tribes" wa misitu ya Amazon ambao wakionekana tu na waandishi basi hawana tena ile purity ya u bushmen!?

Umesema mhusika aliyekua anaalika wabunge ni Mwasiti Almasi, na unasema hukutaka kuita waandishi, kumbe waliokua na mamlaka ya kualika na kukataa kualika sio wewe peke yako, sasa mbona ulitaka kuhodhi mamlaka ya kualika na "kukataa" waandishi?

Kama unasema chama bado hakijatangaza mchakato wa mgombea Urais wewe mbona unaanza kutupa dondoo za jinsi mchakato utakavyokua, wewe ndio taasisi ya Mkutano Wa Uteuzi? Hahahaaha.... Zitto ndio una udhaifu wa kujieleza namna hii?

Umechambua very objectively. Thank you.
Nadhani anachokifanya Zitto ni kuweka bayana kuwa CHADEMA haina de facto mgombea wa urais, kwa sababu momentum among most CDM supporters au fans to be precise ni kuwa mgombea wa 2010 ndio atakayegombea 2015. Sasa Zitto anawaandaa watu kisaikolojia na mchakato wa kutafuta mgombea.
 
Wewe zito ni mnafiki sana kijana Mzee wewe uliyezoea majungu huna lolote umeshafilisika kisiasa
 
Capture.PNG tuwe wavumilivu tuisubiri hiyo video
 
Zito alitaka kuhujumu Chama kwa kuweka zero kwenye bajeti huenda alilipwa hela ndefu sana na ccm
 
Umechambua very objectively. Thank you.
Nadhani anachokifanya Zitto ni kuweka bayana kuwa CHADEMA haina de facto mgombea wa urais, kwa sababu momentum among most CDM supporters au fans to be precise ni kuwa mgombea wa 2010 ndio atakayegombea 2015. Sasa Zitto anawaandaa watu kisaikolojia na mchakato wa kutafuta mgombea.
the only problem kuhusu wewe ni unafiki na tamaa ya kupata cheo kupitia ccm

nikikuona tu nasikia kichefuchefu
 
the only problem kuhusu wewe ni unafiki na tamaa ya kupata cheo kupitia ccm

nikikuona tu nasikia kichefuchefu

Mkuu, thread inahusu Zitto Kabwe na wabunge walioenda kushiriki tamasha Kigoma. Kama vipi, anzisha thread ya kuelezea kichefuchefu chako. Unachokifanya hapa ni kuwatia kichefuchefu watu wanaotaka to stick to the topic...
 
Unacheza na maneno wewe Zitto! lazima una hila nyuma yako! kumbuka wakati wa uchaguzi mdogo wa arumeru mashariki uliibuka na maneno yako haya tata kama mchawi!! kwamba unautaka urais!! yani watu tuko biz tunahangaika kuhakikisha Joshua anapita katika AM, wewe ukaibuka ki vile, tafsi ya wengi wetu ilikuwa wewe ni kuadi unatumika tu na wa upande wa pili! ili kutunyongesha kulichukua jimbo hilo au we unafikiri logic hasa ilikuwa nini katika uchaguzi ule we kuibuka na kaule kama ile?

Haya hata hayo ya upuuzi wk hayajakauka leo linazuka hili!
Zitto wewe ni mtata sana, tena mnafiki mkubwa!
Hila mbaya kama hizi za kuuendea uongozi mkuu wa nchi yetu leo zinamtokea JK puani! hata kama kajilimbikizia mali kiasi cha kutisha hana heshima tena! atabakia kuwa kiongozi wa ovyo aliyeshindwa kuliongoza taifa lake na watu wake!

Haya we endelea tu! lakini kumbuka siku zote mwisho wa ubaya ni aibu!
JK sasa anaaibika! Tafakari!
Huwa spendi kuchangia thread kama hizi lakini niulize hivi ni nani mwenye hati miliki ya kugombea urais Tanzania? Mbona watu mnatoka mapovu sana oh Zitto anataka urais ah nimekosea ulahisi. Unapoeleza kuwa mwenzako hafai kwa hili jiulize kwa nini hafai, je wewe unafaa? Kitu gani kinakufanya umpinge ni mapenzi yako kwa Tanzania au wewe mwenyewe unautaka, au ni kuwadi wa anayeutaka hivyo unamwona Zitto anawazidi kete? Ukisoma between lines baadhi ya post zina hidden aganda kama ukabila, ukanda, udini, uvyama, ukuwadi, na yanayoifanana na hayo. Mytake Kama mtanzania Zitto anayohaki kugombea kama hutaki kajinyonge
 
Zitto amekanusha habari zilizoandikwa na gazeti la Mananchi kwamba wabunge Halima Mdee, Deo Filikunjombe na David Kafulila kwenye tamasha la Muziki lililofanyika huko Kigoma walimsafishia njia ya Kugombea Urais uchaguzi Mkuu ujao. Zitto amekanusha habari hizo kwamba kitu kama hicho hakikuwepo na onyesho lilikuwa ni entertainment na wala halikwua la kisiasa. Halima Mgee pia amekanusha habari hiyo.

Kwa kanusho hilo la wazi na hadharani ambalo amelitoa nampongeza, kwani ni mbinu zinazofanywa na CCM kugombanisha wanachadema na kuwaparaganisha. Msimamo kama huo ndio tunaotaka na ndio unaosaidia kuziba nyufa na kuimarisha nyumba isiyumbe.

Mkuu Candid Scope nadhani hujamsoma vizuri zitto, ama la umemsoma lakini hukumuelewa. Jisomee tena haya maneno ya zitto hapo chini halafu utafakari upya mtazamo wako juu ya kauli ya zitto katika huu mkorogano.

Nilikuwepo uwanjani pale lake Tanganyika Kigoma, kilichoandikwa ndicho nilichosikia pia. Videos zitawekwa hapa na zitathibitisha.
 
Last edited by a moderator:
Zito alitaka kuhujumu Chama kwa kuweka zero kwenye bajeti huenda alilipwa hela ndefu sana na ccm

Nakubaliana na wewe kabisa hii kitu iliniuma sana in future CDM wateue kamati ya kutengeneza bajeti ni si mtu mmoja, serikalini bajeti hatengenzi waziri ni idara yenye wataalamu waliobobea katika accounts, finance and statistician.Hili litakuwa somo in future.Asante zitto kwa kukosea limekuwa somo
 
Katika gazeti la Mwananchi la tarehe 23 Julai 2012, kulikuwa na habari yenye kusomeka 'Wabunge wamsafishia Zitto njia ya Urais 2015'. Habari hii imeleta mjadala mara baada ya kutoka na kusomwa. Mjadala umekuzwa zaidi baada ya Wabunge ndugu Halima Mdee na ndugu Joshua Nassari kukanusha maneno waliyonukuliwa kusema. Napenda kusema masuala yafuatayo.

Moja, Waheshimiwa Wabunge Halima Mdee, Joshua Nassari, Kangi Lugola, Esther Bulaya, Deo Filikunjombe, Raya Ibrahim, Amina Mwidau na David Kafulila walihudhuria tamasha la vijana wa Kigoma All Stars kwa kualikwa na Mratibu wa kundi hilo Mwasiti Almasi.

Wabunge wengine walialikwa lakini hawakutokea wakiwemo Joseph Mbilinyi, David Silinde, Amos Makala, Vicky Kamata na Peter Serukamba. Wabunge hawa hawakualikwa na mimi na wala sikufanya mazungumzo nao yeyote ya awali au kuwaambia au kukubaliana nini cha kuzungumza au hapana. Tamasha lilikuwa la muziki na halikuhusika kabisa na siasa.

Waheshimiwa wote walipewa nafasi ya kusalimia na wote walizungumza. Wabunge waliozungumza kwa muda mrefu kidogo ni ndugu Halima Mdee, Joshua Nassari, Deo Filikunjombe na Kangi Lugola.

Hotuba za Wabunge wote zilirekodiwa kwenye video neno kwa neno na video hizo zitawekwa wazi kwenye blogu yangu kama sehemu ya documentary ya tamasha lile la kihistoria.

Pili, sikuhusika kwa namna yeyote ile na kuandikwa kwa habari hii iliyozusha mjadala. Wala sikujua kama habari hii ingeandikwa maana katika ziara ile sikuita mwandishi hata mmoja maana nilitaka liwe tukio la Kigoma tu.

Kama mwandishi kaandika ambayo wabunge hawa hawakuyasema basi itaonekana kwenye videos hizo. Wabunge wenyewe wanajua kwenye nafsi zao nini walisema Kigoma na kipi kiliwasukuma kusema walioyasema Kigoma. Nisingependa kuhusishwa kwa njia yeyote ile na matamshi yao, habari iliyowanukuu na hata makanusho yao. Maana mwisho wa siku ukweli ndio utasimama.

Suala la Urais lisitupotezee muda kwani kuna mambo mengi sana ya kujadili kuhusu nchi yetu. Taharuki ambazo watu wanazipata masuala ya urais yanapotajwa zinashangaza sana.

Chama changu bado hakijatangaza rasmi mchakato wa kupata mgombea Urais. Hivi sasa chama hakina mgombea Urais mpaka hapo mchakato utakapotangazwa ambapo wanachama wataruhusiwa kuomba kupeperusha bendera ya chama. Mwanachama wa chama chetu atakaye kubalika na jamii na wajumbe wa mkutano wa uteuzi ndiye atakuwa mgombea wetu. Kwa sasa hayupo na hivyo tusipoteze muda kujadili jambo hili.

Mzee Thabiti Kombo alituachia usia tunapokuwa tunazungumza. Alisema 'weka akiba' sio akiba ya fedha, bali ya akiba ya maneno. Tuweke akiba ya maneno. Tusimalize yote.

Zitto

In red - I can see something very interesting there.

In green - hapo ni kama unajaribu kutuambia kitu kwa sauti ya chini.

In blue - Umeona hapana...wamekukera sana kiasi cha kushindwa kuvumilia hivyo umeamua kwa tahadhari kudhihirisha yaliyoandikwa na gazeti tajwa, katika kauli hii ni kama umeamua kujibu mapigo yao.

In Yellow - Hapa naona umeamua kuweka kila kitu wazi japo bado kwa kauli ya tahadhari lakini inayotoa picha nzima ilivyo, kuonyesha kuwa hawana namna ya kuyakana matamko na kauli zao....... I see.
 
MWELEWENI ZITTO<

aliyetoa mwaliko ni Mwasiti wa Kigoma

Aliyeandaa tamasha ni Zitto kwa niaba ya Kigoma all stars.

Tamasha lilikuwa kwa ajili ya wanaKigoma

Tamasha lisilete utengano wa kiitikadi. Km kakako au dadako akiwa na itikadi tofauti na wewe huwezi kumtenga katika suala lolote la kijamii. Kuwaalika akina mdee,bulaya na wengine wote si tatizo bali ni kujumuika pamoja. Siasa ni hoja na si chuki.


Twende taratibu Zitto:

1. Je kuna uhusiano wowote wa Moja kwa moja kati ya Mwasiti Almasi na kamanda Halima Mdee, Joshua Nassari, na
hao waheshimiwa wa magambaEsther Bulaya, Deo Filikunjombe bila CONNECTION yako?
2. Je ni kwanini unadhan kamanda Mdee na Nassari wamekana kilichoandikwa na Mwananch?
3. je ni kwanini hiyo Story itoke kwenye gazeti la mwananchi pee yake na siyo mengine?

ni hayo kwanza ikija video nitaendelea isipokuwa imechakachuliwa
 
Kwa maelezo uliyotoa zitto ina onekana ana unga mkono yaliyo andikwa na gazeti la mwananchi.
 
MWELEWENI ZITTO<

aliyetoa mwaliko ni Mwasiti wa Kigoma

Aliyeandaa tamasha ni Zitto kwa niaba ya Kigoma all stars.

Tamasha lilikuwa kwa ajili ya wanaKigoma

Tamasha lisilete utengano wa kiitikadi. Km kakako au dadako akiwa na itikadi tofauti na wewe huwezi kumtenga katika suala lolote la kijamii. Kuwaalika akina mdee,bulaya na wengine wote si tatizo bali ni kujumuika pamoja. Siasa ni hoja na si chuki.
Mkuu, maswali nimemuuliza Zitto, vipi amekutuma umjibie? well, nijibu nifaham juu ya hayo maswali? Zitto ni mzushi na mchonganishi, please mwache ajibu nae nitaeleza ukweli ulivyo hapa hapo jamvin.
 
xaxa mkuu unaxema kuna mambo mengi ya kujadili kuhuxu nchi yetu, lakini tena unataka kutuwekea fideo ya neno kwa neno. ya nini xaxa? uoni kama ni kutaka kuendelea kujadili mambo yasiyo ya msingi kwa nchi yetu?

we xi uxeme tu kama hawakuxema au walixema?!
 
Zitto ndugu yangu wewe ni mnafiki. Hii tabia umekuwa ukiifanya kwa muda mrefu. Unaleta habari tatanishi tena muda mwingine unajijengea kashfa feki alafu kesho yake unarudi kuikana. Mwenendo wa leo ni hule hule. Nina uhakika 100% kwamba kuna mkono wako mwananchi. Na wewe pia hilo unalifahamu kaka yangu. hii tabia ni mbaya hachana nayo. madaraka tunapewa na wananchi usiyalazimishe. niliwahi kukuambia hii miaka miwili nyuma tulipoonea kule dodoma

Kama unajua maana ya mnafiki naona wewe umekaa kinafiki zaidi! Hiki ulichokiandika ni uthibitisho tosha!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Ukisoma ujumbe wa Zitto between the lines utapata message yote kuhusu mbio za urais 2015.

Kina Mdee walivyopinga inawezekana wanamaanisha kuwa they were under influence of alcohol or other substance so hawakujitambua.

Hata hivyo wanasiasa wa Bongo imefika wakati watambue kuwa technology itawaumbua, wamuulize Hillary Clinton na story yake ya sniper fire ya Serbia...

Mkuu hapa Zitto kaumbuka, unafiki wake umeonekana LIVE, vipande vya video ku-upload inachukua muda kani unless anataka kuchakachua. anataka kuingia ikulu kwa mgogo wa media, which is very bad.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom