Kwasasa tusimwite Zitto mnafiki,tuwe na subira tuone video tutajuwa nani mnafiki kwenye hili.Zitto huwa anasema yeye ni mtu wa principle,ngoja tuone kama ataweka video.
mkuu tatizo sijui wengi humu mmeanza kufatilia nyendo za zitto mwaka huu? Kumbuka zitto alivyochonga dili na waandishi wa habari eti wamemuwekea sumu na kalazwa hospitali!
Mkuu ukitaka kumjua vizuri zitto alivyo we just fatilia nyendo zake kuanzia 2009 hadi leo ndo utamwelewa vizuri.
Mkuu Mkandara,
Labda kama nitakuwa nimeyaelewa maelezo ya Zitto vibaya, nimesoma na hajakanusha lolote lile lililoandikwa na Mwananchi, zaidi amesema kilichoandikwa ndicho kilishosemwa.
Kwahiyo nadhani hali ni kama ilivyokuwa jana hadi hapo tutakapo pata mkanda.
Sina wasi wasi kuwa mkanda utachakachuliwa kwasababu walioongea wapo nao watathibitisha ukweli wa kauli zao kama kuna uwalakini. Hii itaondoa wingu nene na zito linalonyemelea sehemu muhimu sana ya siasa za nchi yetu.
Ni mapema sana kutoa hukumu hadi video iwekwe.
Ninarudia kusema hili tatizo ni kubwa sana kuliko mnalivyoliona.
Labda niwe muwazi kidogo, hizi ni dalili za mvutano ndani kwa ndani. Mvutano huo si wa kisiasa ni mvutano wa makundi ya kimasilahi. Mvutano huu ni kama ule Juliana (makamu mwenyekiti BAVICHA) aliouleta na kuzua tafrani ambao CDM wameufunika chini ya kapeti kwa staili ya CCM.
Niliwaonya CDM kuwa lazima chama kisimame kama taasisi inayoongozwa na sheria, kanuni na maadili. Hapa ndipo CDM ilipo leo!
Bila kutoka nje ya mada, Mheshimiwa Zitto weka video ili ukweli uonekane.
Tujue Mwananchi Ltd wamesema nini, Nassar na Halima wamesema nini na Zitto anasema nini.
Ni kwa njia hiyo tu hali na mtafaruku uliopo unaoweza kutumiwa vizuri sana na 'wapinzani' wa CDM kuizamisha utakuwa na ufumbuzi.
Baada ya hapo nasi tutaweka maoni yetu, maswali na majibu. Ukiliangalia hili suala kuanzia tamasha hadi mtafaruku unaofukuta kuna mengi ya kujadili. Kwanza tutoe natural justice ya kusikiliza kila mmoja. Tumemsikia Nassar, Halima, sasa Zitto ana video tumsikilize.
Lakini pia Mwananchi Ltd, nina uhakika wanasoma JF, suala hili ni muhimu sana mkalitolea maelezo. The credibility and integrity of your organization is on the line and seriously compromized. The damage is big, probably it will cost you down the road.
Zitto yupo CHADEMA kwa kazi maalum aliyotumwa na CCM.
Kuweni naye makini sana.
Kumbukeni : NCCR MAGEUZI~ Masumbuko Lamwai~ Johh John Guninita.
sasa : CHADEMA~ZITTO Z KABWE~ (Kuna watu walikuwa wajumbe waBaraza kuu la UVCCM
wapo sasa Chadema)
Zitto ni mratibu wao-
mkuu tatizo sijui wengi humu mmeanza kufatilia nyendo za zitto mwaka huu? Kumbuka zitto alivyochonga dili na waandishi wa habari eti wamemuwekea sumu na kalazwa hospitali!
Mkuu ukitaka kumjua vizuri zitto alivyo we just fatilia nyendo zake kuanzia 2009 hadi leo ndo utamwelewa vizuri.
Mkuu ni kwamba tu critics mmeongezeka.Back in a day hapa,aliingia kwenye ile kamati ya madini ya JK,na kuanzia pale binafsi I was doubtful about his many moves.Kulikuwa na mjadala mkali sana kwasababu JK alipewa pa kupumulia na Zitto since tuhuma zilkuwa kwamba pesa zile dnizo zilimwingiza JK madrakani, alichanganywa na baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi kwenye kamati,watuhumiwa ambao chama chake ndicho kilikuwa kikiwatuhumu kipindi kile,akaja kuonekana kusympathise na utawala na baadhi ya mahasimu wakuu wa chama chake, ndo baadaye yakaja mambo ya Dowans, akiwa bega kwa bega na kina RA nk.Kisingizio kikiwa kuwa uadui wa kisiasa siyo big deal,lakini akisahau ni issue nyeti kwa taifa.
So kiukweli,nilikuwa nikiizungumzia issue hii specifically kwasababu ameahidi hapa kuweka video.
wanajf siku hizi nimegundua kwamba sias imeingilia hata mawazo yenu bora kwa manufaa ya nchi hii na kwa heshima ya jukwaa hili.
Zitto kama mwananchi wa Tanzania huru si dhambi kama akisema anatamani kuwa rais kwani hata watoto husema wanatamani kuwa nani anapoulizwa hata wewe ukiulizwa watamani kuwa nani unaweza sema kile unacho tamani.
Sioni kama kuna tatizo kwenye hilo kwa kuwa Katiba inamruhusu kufanya hivyo na kama sifa zinazo takiwa zitakuwa zimetimia.
hivyo sipendi kuona wanajf kupoteza nguvu zenu kujadili mambo ambayo yatafanyika miaka mitatu ijayo, tusimezwe na magamba ndio wanagombea nani atakuwa mgombea wakati huu, sisi kazi yetu ni kukosoa na kujadili hoja zenye tija na manufaa kwa taifa.
Mheshimiwa Zitto katika hili unatupa utata! ukizingatia hoja zako za mwanzo na huu utetezi wako kwa Gazeti Mwananchi tunapata mashaka si haba kuwa kanushi yako haina rangi yako halisi!
Nilikuwepo uwanjani pale lake Tanganyika Kigoma, kilichoandikwa ndicho nilichosikia pia. Videos zitawekwa hapa na zitathibitisha.
Siwezi kuwaandikia mwananchi kwani mimi silalamiki kuhusu habari hiyo. Wenye kuilalamikia habari wameandika.
Mimi ninaamini gazeti la Mwananchi ndio gazeti pekee huru la kiswahili hapa nchini. Ndio gazeti pekee ambalo umiliki wake hauna maslahi na waandishi na wahariri wake ni mahiri, hawana njaa na hawapindishwi. Ndio maana huandika ukweli muda wote na wanapokosea hawasiti kurekebisha. Ndio maana ni gazeti linasomwa kwa wingi kuliko magazeti yote nchini. Hakuna gazeti linalofikia hata nusu ya mwananchi kwa kusomwa. Hivyo Mwananchi linaaminika na umma.
Najua kuna watu wana chuki binafsi na mwananchi kama gazeti na wahariri wa mwananchi kama binaadamu. Hayo wayamalize wenyewe huko walikochukiana.
Subirini video ndio tutajua habari ile imepikwa au ni ya kweli. Kwa tuliokuwepo uwanjani tunajua nani alisema nini.
This what I call great thinking! Hebu tu-assume kuwa kweli Mdee na Nassari walinukuliwa sahihi-ni vipi sasa baada ya kuona kuwa kauli zao maybe zilitokana na kuwa carried away na jinsi maandalizi na tamasha lenywe lilivyofana, na sasa wakagundua kuwa zimeleta mtafaruku ndani ya chama chao, then wakaamua kukanusha for the well being ya chama, iweje Zitto aamue kuwaumbua kwa kusisitiza kuwa walinukuliwa sahihi, bila kujali kuwa anakiweka chama (in this case na sisi wapenda mabadiliko) katika wakati mgumu? Haikotosha kumfanya aone kuwa wabunge wenzie waliropoka, na ni jukumu lake kuwasitiri for the betterment of their party and Tanzanians at large? Iko wapi busara ya kiuongozi sasa Zitto? Yani wapi kisemwe nini na kwa wakati gani? (Rejea kauli za Mukama kwenye msiba ya Bob Makani). Wewe unachotaka hapa ni kutuaminisha kuwa walisema hivyo na ndicho kilicho sahihi, na uko tayari kulisimamia hilo at the expense ya mtafaruku ndani ya chama! Sasa nani unategemea atachagua Rais mbinafsi hivyo? Tulikosea kwa JK, haturudii tena!
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe (pichani), ameibuka na kuzungumzia sakata la urais mwaka 2015 alilohusishwa nalo na wabunge wenzake mjini Kigoma na hatimaye wabunge hao kukanusha baada ya kuibuka kwa mjadala mkali dhidi ya kauli zao.
Zitto ambaye amekuwa akiandamwa mara kadhaa na wanasiasa ndani na nje ya chama chake, baadhi wakimtuhumu kuwa mamluki na wengine wakimuekezea kuwa ni mwanasiasa mwenye malengo makubwa hapo baadao, amesema:
"Katika gazeti la Mwananchi la tarehe 23 Julai 2012, kulikuwa na habari yenye kusomeka ‘Wabunge wamsafishia Zitto njia ya Urais 2015′. Habari hii imeleta mjadala mara baada ya kutoka na kusomwa. Mjadala umekuzwa zaidi baada ya Wabunge ndugu Halima Mdee na ndugu Joshua Nassari kukanusha maneno waliyonukuliwa kusema. Napenda kusema masuala yafuatayo.
"Moja, Waheshimiwa Wabunge Halima Mdee, Joshua Nassari, Kangi Lugola, Esther Bulaya, Deo Filikunjombe, Raya Ibrahim, Amina Mwidau na David Kafulila walihudhuria tamasha la vijana wa Kigoma All Stars kwa kualikwa na Mratibu wa kundi hilo Mwasiti Almasi. Wabunge wengine walialikwa lakini hawakutokea wakiwemo Joseph Mbilinyi, David Silinde, Amos Makala, Vicky Kamata na Peter Serukamba. Wabunge hawa hawakualikwa na mimi na wala sikufanya mazungumzo nao yeyote ya awali au kuwaambia au kukubaliana nini cha kuzungumza au hapana. Tamasha lilikuwa la muziki na halikuhusika kabisa na siasa.
"Waheshimiwa wote walipewa nafasi ya kusalimia na wote walizungumza. Wabunge waliozungumza kwa muda mrefu kidogo ni ndugu Halima Mdee, Joshua Nassari, Deo Filikunjombe na Kangi Lugola.
"Hotuba za Wabunge wote zilirekodiwa kwenye video neno kwa neno na video hizo zitawekwa wazi kwenye blogu yangu kama sehemu ya documentary ya tamasha lile la kihistoria.
"Pili, sikuhusika kwa namna yeyote ile na kuandikwa kwa habari hii iliyozusha mjadala. Wala sikujua kama habari hii ingeandikwa maana katika ziara ile sikuita mwandishi hata mmoja maana nilitaka liwe tukio la Kigoma tu.
"Kama mwandishi kaandika ambayo wabunge hawa hawakuyasema basi itaonekana kwenye videos hizo. Wabunge wenyewe wanajua kwenye nafsi zao nini walisema Kigoma na kipi kiliwasukuma kusema walioyasema Kigoma. Nisingependa kuhusishwa kwa njia yeyote ile na matamshi yao, habari iliyowanukuu na hata makanusho yao. Maana mwisho wa siku ukweli ndio utasimama.
"Suala la Urais lisitupotezee muda kwani kuna mambo mengi sana ya kujadili kuhusu nchi yetu. Taharuki ambazo watu wanazipata masuala ya urais yanapotajwa zinashangaza sana.
"Chama changu bado hakijatangaza rasmi mchakato wa kupata mgombea Urais. Hivi sasa chama hakina mgombea Urais mpaka hapo mchakato utakapotangazwa ambapo wanachama wataruhusiwa kuomba kupeperusha bendera ya chama. Mwanachama wa chama chetu atakaye kubalika na jamii na wajumbe wa mkutano wa uteuzi ndiye atakuwa mgombea wetu. Kwa sasa hayupo na hivyo tusipoteze muda kujadili jambo hili.
"Mzee Thabiti Kombo alituachia usia tunapokuwa tunazungumza. Alisema ‘weka akiba' sio akiba ya fedha, bali ya akiba ya maneno. Tuweke akiba ya maneno. Tusimalize yote."
-Imetokeaje kuwa yeye binafsi ana Video ya tukio hilo wakati anasema hakuwa mwenyeji wa tukio hilo? Hata kama mwandaaji mwingine asiye Zitto alichukua mkanda huo, sasa umefikaje mikononi mwa Zitto?
-Kwa nini imechukua muda mrefu gazeti hili kuandika habari hii (almost one week), tena kama lead story?
-Kwa nini Zitto anatetea objectivity ya gazeti hili wakati gazeti hili hili wiki hii limechapisha apology kwa Membe na balozi mbalimbali kwa kuwasingizia?
-Kwa nini Zitto anatetea gazeti kuliko kutetea makada wenzake katika suala linaloweza kuvuruga chama chake?
-Je kwa nini Zitto anaelekea kuthibitisha utabiri wa Steven Wassira kuwa Chadema itavurugika kabla ya mwisho wa mwaka?
-Pamoja na Zitto kuonekana kupuuza suala la urais katika ufafanuzi wake, kwa nini anaelekea kushabikia na kupenda ikubalike kuwa wabunge hao walisema kuwa yeye anafaa kuwa rais wa taifa letu?
Ama kweli Zitto ana damu ya kunguni maanake.. Dah.. sasa watu wa kujiuliza sana kuhusu kauli zao ni kina Halima Mdee, Joshua Nassari, Deo Filikunjombe hawa ndio waliokuwa ma MC wakitangaza jukwaani lakini lawanma analaumiwa Zitto ambaye hakusema kitu isipokuwa habari kuandikwa gazetini.
I mean jamani jamani hata kama tuna chuki kiasi gani kwa Zitto lakini haya maneno hakuyasema Zitto ila wameyasema hawa watu wengine walokanusha..Hivi kweli Zitto akiitoa hapa video na zikaonekana wamesema maneno hayo tunawachukia wao au bado atakuwa Zitto na gazeti la mwananchi?..bila shaka bado itakuwa Zitto no matter afenyeje maana kisha kuwa nuksi kwa baadhi yenu...
Hivi kuna ubaya gani haswa kumshabikia mtu?...Hivi kwlei mnatafuta ukweli au basi tu Zitto kawakalia vibaya sana, mbona mimi namshabikia Mwanri wa CCM all the way to be the best candidate for President..Ahahaha! kesho wekeni magazetini basi kwamba Mkandara amshabikia Mwanri!.. Khaaa tuuu!
Jamaa kaanza kujiona superstar sana baada ya kuona ana kubalika, anadhani yy ni zaidi ya chama, mzee wewe siyo zaidi ya chama, na labda unakubalika kwenu kigoma tu kwenye jimbo lako, kwanini kila mara chokochoko ndani ya chadema zinahusiana na jina lako? Bora upumzike siasa ufanye kazi za professional yak
o kama ulivyo kwisha wahi kusema
Zitto amekanusha habari zilizoandikwa na gazeti la Mananchi kwamba wabunge Halima Mdee, Deo Filikunjombe na David Kafulila kwenye tamasha la Muziki lililofanyika huko Kigoma walimsafishia njia ya Kugombea Urais uchaguzi Mkuu ujao. Zitto amekanusha habari hizo kwamba kitu kama hicho hakikuwepo na onyesho lilikuwa ni entertainment na wala halikwua la kisiasa. Halima Mgee pia amekanusha habari hiyo.
Kwa kanusho hilo la wazi na hadharani ambalo amelitoa nampongeza, kwani ni mbinu zinazofanywa na CCM kugombanisha wanachadema na kuwaparaganisha. Msimamo kama huo ndio tunaotaka na ndio unaosaidia kuziba nyufa na kuimarisha nyumba isiyumbe.
Zitto amekanusha habari zilizoandikwa na gazeti la Mananchi kwamba wabunge Halima Mdee, Deo Filikunjombe na David Kafulila kwenye tamasha la Muziki lililofanyika huko Kigoma walimsafishia njia ya Kugombea Urais uchaguzi Mkuu ujao. Zitto amekanusha habari hizo kwamba kitu kama hicho hakikuwepo na onyesho lilikuwa ni entertainment na wala halikwua la kisiasa. Halima Mgee pia amekanusha habari hiyo.
Kwa kanusho hilo la wazi na hadharani ambalo amelitoa nampongeza, kwani ni mbinu zinazofanywa na CCM kugombanisha wanachadema na kuwaparaganisha. Msimamo kama huo ndio tunaotaka na ndio unaosaidia kuziba nyufa na kuimarisha nyumba isiyumbe.
Mkuu umemwelewa Zitto kweli?Kwasababu nadhani Zitto anaungana na habari za gazeti la mwananchi,where as hao wengine wanapinga,so Zitto kasema ana video.Isitoshe ana imani kubwa na gazeti hilo.Kwenye bandiko lake,hajaonyesha kama ana shida yoyote na kilichoandikwa na gazeti.Sanasana wanaoipinga habari hiyo,amesema hajali sana kuhusu mazungumzo hayo kwasababu muda bado wa kugombea urais na pia anashangazwa na taharuki za watu pindi issue ya yeye na urais ikitajwa.
Mkuu umemwelewa Zitto kweli?Kwasababu nadhani Zitto anaungana na habari za gazeti la mwananchi,where as hao wengine wanapinga,so Zitto kasema ana video.Isitoshe ana imani kubwa na gazeti hilo.Kwenye bandiko lake,hajaonyesha kama ana shida yoyote na kilichoandikwa na gazeti.Sanasana wanaoipinga habari hiyo,amesema hajali sana kuhusu mazungumzo hayo kwasababu muda bado wa kugombea urais na pia anashangazwa na taharuki za watu pindi issue ya yeye na urais ikitajwa.
Nimekuelewa, ila kitu kimoja ni dhahiri gazeti limekuwa na mahali waliposimamia kuandika, sidhani kama gazeti wametunga habari hiyo. Kuna uwezekano mkubwa wabunge hawa walitamka hayo lakini sasa hivi wanakanusha walichokisema. Zitto amekuwa mwazi kwa kueleza kwamba ataweka ushahidi wa Video na hivyo kuonyesha ukweli ambao wabunge waliongea kuhusu yeye siku ya tukio kwa sababu wanazojua wao wenyewe.
Kukanusha kwamba jambo hilo halikuzungumzwa au lilizungumzwa ni ushahidi wa video clip ambazo Zitto ataziwakilisha, na papo Zitto kaeleza wazi suala la nani kuwa mgombea wa urais si mtu binafsi ila ni suala la wanachama na chama. Hii inaeleweka na nidhahiri. Alichokosea Zitto kukisema ni kipi?
Nimekuelewa, ila kitu kimoja ni dhahiri gazeti limekuwa na mahali waliposimamia kuandika, sidhani kama gazeti wametunga habari hiyo. Kuna uwezekano mkubwa wabunge hawa walitamka hayo lakini sasa hivi wanakanusha walichokisema. Zitto amekuwa mwazi kwa kueleza kwamba ataweka ushahidi wa Video na hivyo kuonyesha ukweli ambao wabunge waliongea kuhusu yeye siku ya tukio kwa sababu wanazojua wao wenyewe.
Kukanusha kwamba jambo hilo halikuzungumzwa au lilizungumzwa ni ushahidi wa video clip ambazo Zitto ataziwakilisha, na papo Zitto kaeleza wazi suala la nani kuwa mgombea wa urais si mtu binafsi ila ni suala la wanachama na chama. Hii inaeleweka na nidhahiri. Alichokosea Zitto kukisema ni kipi?
sijasema Zitto amekosea chochote,ila nilidhani hukumwelewa vyema,ila sasa inaonekana umefanya hivyo.Pia kama hujanielewa,mi nasubiri tu video,sina la ziada mkuu.
sijasema Zitto amekosea chochote,ila nilidhani hukumwelewa vyema,ila sasa inaonekana umefanya hivyo.Pia kama hujanielewa,mi nasubiri tu video,sina la ziada mkuu.
Huhitaji kuwa na phd kujua kuwa zito anajipigia kampeni, lakini ajue anajiharibia, slaa chunga maneno unayoongea ukiwa na zito kwa sababu yataweza kutumia agants you baadae
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.