Urais, Halima, Nassari na Kigoma

Urais, Halima, Nassari na Kigoma

Status
Not open for further replies.
Mkuu hapa Zitto kaumbuka, unafiki wake umeonekana LIVE, vipande vya video ku-upload inachukua muda kani unless anataka kuchakachua. anataka kuingia ikulu kwa mgogo wa media, which is very bad.

anatengenezewa fideo na januari magamba.
 
xaxa mkuu unaxema kuna mambo mengi ya kujadili kuhuxu nchi yetu, lakini tena unataka kutuwekea fideo ya neno kwa neno. ya nini xaxa? uoni kama ni kutaka kuendelea kujadili mambo yasiyo ya msingi kwa nchi yetu?

we xi uxeme tu kama hawakuxema au walixema?!


kuna binti mmoja wa udsm huwa anapenda sana kutumia hizo ''x''palipo na ''s''
 
kuna binti mmoja wa udsm huwa anapenda sana kutumia hizo ''x''palipo na ''s''

una maanisha mimi ni binti? dah!

umejiandikisha fitambulisho fya taifa lakini? leo nimeamka saa 9 usiku.
 
Nyie pigeni kelele lakini 2015 Rais ni Dr Slaa, kama hutaki tafuta kamba ukajinyonge

Dr Slaa akae pembeni bwanaa, amepigwa chini 2000 Watanzania wamesha mkataa ntuu huyo tunamtaka Zitto 2015, mkilazimisha dr Salaa tutapigia vyama vyengine.

Sent from my Z3 using Tapatalk 2
 
umejiandikisha fitambulisho fya taifa lakini? leo nimeamka saa 9 usiku.


hahaha!!

nilienda kujiandikisha nilipowapa kitambulisho cha kupigi kura ikaonekana mimi sio raia wa nchi...hahahha..leo sijaamka saa tisa...kwema lakini?...wewe umeshaiona fideo ya zitto?
 
Hivi hili tamasha lingefanyika KARATU, na wabunge hawa hawa wakasema SLAA ni jembe na anafaa kuwa rais 2015 na gazeti la mwananchi likaripoti kungekuwa na kelele zote hizi?
 
Nimekuelewa, ila kitu kimoja ni dhahiri gazeti limekuwa na mahali waliposimamia kuandika, sidhani kama gazeti wametunga habari hiyo. Kuna uwezekano mkubwa wabunge hawa walitamka hayo lakini sasa hivi wanakanusha walichokisema. Zitto amekuwa mwazi kwa kueleza kwamba ataweka ushahidi wa Video na hivyo kuonyesha ukweli ambao wabunge waliongea kuhusu yeye siku ya tukio kwa sababu wanazojua wao wenyewe.

Kukanusha kwamba jambo hilo halikuzungumzwa au lilizungumzwa ni ushahidi wa video clip ambazo Zitto ataziwakilisha, na papo Zitto kaeleza wazi suala la nani kuwa mgombea wa urais si mtu binafsi ila ni suala la wanachama na chama. Hii inaeleweka na nidhahiri. Alichokosea Zitto kukisema ni kipi?
Zitto anashambuliwa kwa tabia ya kujiandikia habari na kisha kuwapa waandishi wa habari waichapishe ukurasa wa mbele kwa malipo maalum kama yalivyo matangazo ya biashara.
 
... Sasa Zitto anawaandaa watu kisaikolojia na mchakato wa kutafuta mgombea.
Kama anatuandaa kwa mchakato mbona anasema kwamba tusifuatilie maswala ya Urais kwa sasa bali masuala ya nchi? Iweje tena yeye mwenyewe aanze kutuandaa mapema??

Amesema chama hakijatangaza mchakato halafu hapo hapo akatupa dondoo za mchakato!
 
Suala la Urais lisitupotezee muda kwani kuna mambo mengi sana ya kujadili kuhusu nchi yetu. Taharuki ambazo watu wanazipata masuala ya urais yanapotajwa zinashangaza sana.



Mzee Thabiti Kombo alituachia usia tunapokuwa tunazungumza. Alisema 'weka akiba' sio akiba ya fedha, bali ya akiba ya maneno. Tuweke akiba ya maneno. Tusimalize yote.

Zitto

Masikini Zitto.....mwili wako ni wa Yakobo ila Sauti ni ya Esau. Una umri wa ujana ila fikra na tamaa za kizee.....angalia hiyo statement yako ya kwanza, halafu ujiulize wewe binafsi ni mara ngapi umelianzisha suala la urais tena ukilihusisha moja kwa moja na wewe?

Statement ya pili uliyoinukuu toka kwa mzee Thabiti Kombo, inaonyesha umeipenda bila kuielewa, sababu naiona kuwa ni kauli ambayo umekuwa ukiiamini moyoni lakini unaipinga kabisa kichwani na katika matendo yako na unaifuata pale tu unapoiona kuwa unaweza kuitumia kama silaha kwa wengine.
Siasa na Urais, vitu hivyo kwako vimegeuka kuwa quicksand because when your on them you keep goin down and in no time no one will hear you callin, and hence you end up self destructing....thats it, you cab take it or drop it, but will always remain and last in life time.
 
  • MWANANCH WAMEANDIKA HIVI....
Anthony Kayanda, Kigoma na Fred Azzah Dar

IKIWA imebaki miaka mitatu kabla ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika nchini mwaka 2015, wabunge wawili vijana wamewataka wakazi wa Mkoa wa Kigoma kujiandaa kumpata kutoka eneo hilo.

Kauli za Wabunge hao zimekuja kipindi ambacho mchakato wa Katiba unaendelea huku kukiwa na uwezekano wa umri wakugombea urais kushuka hivyo kuwawezesha wanasiasa wengi vijana akiwamo Zitto, kugombea nafasi hiyo.

Wakizungumza katika tamasha kubwa lililokutanisha mamia ya wakazi wa Mkoa wa Kigoma, Deo Filikunjombe ambaye ni mbunge wa Ludewa (CCM), Joshua Nasari wa Arumeru Mashariki (Chadema) na Halima Mdee, Kawe (Chadema), walisema wanaamini Rais wa 2015 atakuwa Mbunge wa Kigoma kaskazini na ambaye ni mzaliwa wa mkoa huo.

Katika kauli yao hiyo, wabunge hao walisema Mbunge huyo ameonyesha umahiri mkubwa katika kusimamia mambo ya kitaifa bila upendeleo, jambo linalomfanya kujijengea umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi, hivyo kuonekana wazi kulibeba vema kundi la Vijana wa Taifa hili.

Akimzungumzia kuhusu rais ajaye kutoka Kigoma, Filikunjombe alisema kundi la vijana lazima liungane kuhakikisha kuwa linatoa viongozi watakaopigania maslahi yao na Taifa kwa jumla ili kuleta ukombozi wa kifikra na kimaendeleo kwa maslahi ya jamii.

"
Lazima mtambue kuwa, Tanzania ni nchi yetu sisi wote na lazima vijana wote bila kujali itikadi zetu za kisiasa tunatakiwa kujipa moyo kwamba tunaweza kufanya makubwa katika kuleta maendeleo ya jamii katika nchi yetu," alisema Filikunjombe na kuongeza:

"Vijana wa Kigoma mnabahati ya kuwa na Wabunge wazuri na ninaamini miaka michache ijayo lazima mkoa huu utoe Rais wa Tanzania."

Huku akishangiliwa na umati mkubwa wa watu waliokusanyika katika uwanja wa Lake Tanganyika mjini hapa kuhudhuria tamasha hilo lililopambwa na wasanii nyota wa kizazi kipya kutoka Mkoa wa Kigoma, Filikunjombe alisema; "Zitto anastahili kuwa rais".

Mbunge huyo wa CCM ambaye katika siku za karibuni ameonekana kuwa mshirika mkubwa wa kisiasa wa Zitto na Chadema, alisema Zitto anafaa kuwa Rais kwani amefanikiwa kuwaunganisha watu na kuleta umoja miongoni mwao, jambo ambalo linadumisha umoja wa kitaifa.

Kauli ya Nassari
Kwa upande wake Nasari, alisema Mkoa wa Kigoma umejitokeza wazi kuwa na wanasiasa mahiri na wenye vipaji vya hali ya juu katika kupigania maslahi ya wananchi pamoja na kupambana na ufisadi unaodidimiza uchumi wa taifa letu na kuwanufaisha wachache kwa kutumia nafasi zao.

"Leo, ni mara yangu ya kwanza kufika Kigoma, lakini kwa jinsi ninavyoona mpangilio mzuri wa shughuli hii, naamini kabisa kuwa, Zitto Kabwe aliyeandaa hafla hii na kuwakusanya wasanii wa Kigoma kuwa kitu kimoja anafaa kabisa kuwa rais ajaye wa Taifa letu. Na haya ninayasema kwa uhakika bila hata chembe ya mzaha," alisema Nassari.

Huku akishangiliwa na mamia hayo ya wakazi wa Kigoma, alifafanua kwamba wanasiasa vijana wamejipanga kuwatetea wananchi na hususani kundi la vijana katika kuondoa matatizo mbalimbali yanayowasibu katika maisha kwa kuwajengea mazingira mazuri ya kufanya kazi zao za uzalishaji mali.

Mdee amliza Zitto
Katika hatua nyingine, Mbunge wa Kawe Halima Mdee (Chadema) alimliza Zitto jukwaani baada ya kumuelezea kuwa ni ‘jembe’ katika mambo mbalimbali na mtu mwenye uchungu na maendeleo ya taifa.

Mdee aliyepewa nafasi ya kuwasalimia Wananchi alisema amekuwa na Zitto tangu Chuo kikuu cha Dar es Salaam na kwamba kutokana na ujasiri na umahiri wake katuika kutetea masilahi ya wanyonge na taifa, anafaa kuwa mmoja wa viongozi wa juu katika Taifa.

‘Ndugu zangu watu wa Kigoma, kwa kweli mna bahati sana, achilia mbali kuwa na vipaji katika sanaa ya muziki na michezo hasa mpira wa miguu, lakini mna wanasiasa wakali ambao ni tishio hapa nchini. Mimi namkubali sana Zitto Kabwe na ninaamini kuna siku atakuwa kiongozi wa juu katika nchi yetu," alisema Mdee.

Mdee alipongeza ushirikiano wa wananchi wa Kigoma na kusisitiza kuwa unatakiwa kuenziwa na kuigwa na mikoa mingine.

Zitto akiri kutoa machozi

Zitto alipoulizwa na gazeti hili alikiri kudondosha machozi jukwaani kutokana na Mdee kuzungumza kwa hisia kali na hivyo maneno yake kumchoma na kushindwa kujizuia jukwaani.

"Kwa kweli Halima Mdee alizumgumza maneno mazito sana na alinikumbusha mbali enzi za Chuo kikuu tukiwa kwenye harakati za kutetea maslahi ya wanachuo na pia nimekuwa naye kwenye harakati za kisiasa ndani ya Chadema, ndiyo maana nilishindwa kujizuia na kuanza kutoa machozi," alisema Zitto.

Alisema amefarijika kuwaona wabunge wenzake kutoka vyama vya CCM, NCCR Mageuzi, Chadema na CUF wamefika Kigoma kumuunga mkono katika uzinduzi wa wimbo wa 'Leka dutigite' ulioimbwa kwa pamoja na wasanii wa muziki wenye asili ya Kigoma.

Zitto alisema Mkoa wa Kigoma kwa muda mrefu umekuwa nyuma kimaendeleo hivyo, kuufanya kudharauliwa na watu wengi hata kama hawajui lolote juu ya eneo hilo.

‘Wapo watu wanaotubeza kwamba mkoa wetu ni masikini na haufai kuishi, na kasumba hii imejengeka hadi kwa baadhi ya watumishi wa Serikali. Ndiyo maana sishangai ninaposikia kwamba kuna watumishi wa Serikali wanakataa kuhamia Kigoma. Lakini hii dhana sasa itaisha," alifafanua Zitto.

Wabunge waliohudhuria

Wabunge waliofika Kigoma kwenye hafla hiyo ni Mdee, Amina Mwidau wa viti maalumu (CUF), Esta Bulaya ( Viti maalumu (CCM), Filikunjombe (CCM), Kangi Lugola wa Mwibara, David Kafulila (Kigoma Kusini, NCCR-Mageuzi), Nasari (Arumeru Mashariki Chadema) na Raya Ibrahim Khamis wa viti maalumu kutoka Pemba.

Kauli ya Nape
Alipoulizwa Katibu Mwenezi wa CCM Nape Nnauye kuhusu Filikunjombe kumtabiria Zitto kuwa Rais wakati anatoka upinzani, alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa hajasikia wala kulisoma popote.

“Nyie andikeni kwanza halafu ndiyo nitaweza kusema, kwa sasa siwezi kusema chochote kwasababu sijasikia kitu chochote ama kusoma popote pale jambo hilo,” alisema Nape

ZITTO KWA UUNGWANA UGEWAKANA MWANANCHI KULIKO KUWATETE, HAYO MANENO HAWAKUYASEMA... HIYO VIDEO YENYE HAYO MANENO IPO WAP? BORA UMEUMBUKA... TULISHAKUSHAURI UHUSIANO NA MEDIA. KWASABABU NAAMINI MEDIA ZINATAKIWA KUKUFUATA SIYO WEWE KUWATAFUTA...
 
Zitto Kabwe mwanzoni alipoingia kwenye SIASA alitimiza WAJIBU wake vizuri KITAIFA na KICHAMA. Zitto ni jasiri,mwelewa,msemaji mzuri ila Kadiri siku zinavyokwenda anazidi kujitoa ktk mtizamo wa kuwa MTETEZI wa MASLAHI ya chamana TAIFA na kujikita ktk MASUALA BINAFSI.Kwa sasa fuatilieni anachokifanya ZITTO BUNGENI hakina TIJA kwa CHAMA chake na hata mengine anayoyafanya bungeni unaweza ukafikiri yana tija kwa taifa lakini kiundani anajaribu kujijenga YEYE BINAFSI.

Kwa kuthibitisha angalia jinsi alivyochukua ile HOJA ya KUIWAJIBISHA SERIKALI mwezi wa nne iliyoibuliwa na TUNDU LISSU yeye akaifanya kama ni ya kwake.Wtz ni vizuri mumfatilie vizuri huyu mtu ANACHOSEMA na ANACHOTENDA siku zijazo tusipokuwa MAKINI anaweza akawa ni TATIZO ogopa mtu anayependa SIFA tena sifa hizo zimwendee YEYE kama YEYE na si CHAMA chake au TAIFA lake.

Ninahisi ZITTO bado anatumiwa na USALAMA wa TAIFA kuyumbisha UELEKEO wa UPINZANI na kama si hivyo basi namshauri ZITTO arudi kwenye mstari kama zamani ili UKOMBOZI wa TAIFA uendelee bila kukoma mimibinafsi nampenda sana ila staili yake anayokwenda nayo inantia mashaka.

Ninajua ZITTO anajiandaa kwa URAIS wasiwasi kama akikosa nafasi ya kugombea ndani ya CHADEMA itakuwaje? Bila shaka ataasi au atazidi kukihujumu CHADEMA kama alivyofanya uchaguzi uliopita akakisaidia NCCR kupata WABUNGE badala ya kusaidia WAGOMBEA wa CHADEMA.Mwisho CHADEMA fanyeni UCHAGUZI wa VIONGOZI wenu mapema na pili MGOMBEA URAIS achaguliwe mapema ili wale ambao ni watu wachokochoko wajulikane mapema na wabainishwe ili wakati wa uchaguzi twende sambamba bila WASALITI.Pia hilo litasaidia kuanza kumjenga sehemu mbalimbali za nchi.Mkichelewa ni kuwafanya watu wa mjini wamjue vijijini wanakosa fursa.THE EARLIER THE BETTER CDM amkeni.
 
Miezi ya nyuma nilileta hii mada hapa jukwaani lakini kwa bahati mbaya MODs waliinyofoa dakika 20 baada ya kuiweka. Sina budi kurudisha hii mada baada ya sakata la Zitto Kabwe, Nassari, Halima Mdee pamoja na gazeti la Mwananchi. Kwa muda wa miaka kadhaa sasa, nimekuwa katika tasnia ya habari na lazima nikiri kwamba mengine yanayofanyika katika hii tasnia ni ya kukatiza moyo hasa kazi za wanahabari zinapoingiliwa na wanasiasa. Kwetu sisi wanawake inakuwa ni vigumu sana kukataa kutii haya maagizo ambayo mengine unaona kabisa ni za vitisho

Zitto Kabwe, January Makamba, Bernard Membe na hata Ngeleja kwa siku za nyuma alishiriki sana katika kuingilia kazi za waandishi. Kinara wao akiwa Zitto January na Membe. Hawa viongozi hasa Zitto wamezoea sana kujiandikia makala na hata habari kisha kumlazimisha mwandishi kuzichapisha ukurasa wa mbele kwa gharama yoyote ile. Wanatoa hela nyingi sana kwa waandishi na wahariri. Mbaya zaidi ni kwamba hawa viongozi wanajitengenezea kashfa au kutoka ndani ya vyama vyao.

Matokeo yake kesho wanaitisha waandishi tena kukanusha (kashfa) zao za kujipikia wakati ni wao ndio chanzo cha hizo habari. Lengo lao kubwa ni kutafuta huruma kutoka kwa umma wa kitanzania kwa vitu ambavyo havipo.

Kinachonishangaza ni kwa nini mtu ajichafue kwa kujitengenezea kashfa maadui feki ndani ya chama chake heti ndio wanaomchafua kumbe ni yeye mwenyewe alafu kesho yake akane hizo taarifa? Nadhani tunaelekea kubaya hawa watu wakiendelea nah ii tabia. Moja ya habari hizi ni zile zinazomlaumu Mbowe kam mtazikumbuka..

nawakilisha


...Hapa Mkuu Umeua na Umemaliza Kila Kitu! Ndio maana tunashuhudia sasa Mwananchi Ikiomba msamaha kwa habari iliyoandika 'Kwa Bahati Mbaya' Miezi KUMI NA NANE iliyopita!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom