Urais, Halima, Nassari na Kigoma

Urais, Halima, Nassari na Kigoma

Status
Not open for further replies.
ccm wanafanya kila jitihada kuibomoa cdm kupitia kwa zitto,.nawapongeza viongozi makini wa cdm kwa kuwapuuzia mamluki.
 
Labda ni wewe tu ambaye hujui kuwa dr. Slaa ndiye raisi mtarajiwa wa jmt, kutinga ikulu kupitia tiketi ya chadema, na wananchi hawababaishwi na propaganda, wamekubali kukitosa chama maarufu na kikongwe kuliko vyote nchini kwa ajili ya chadema tarajio kuu la wananchi ni amiri jeshi mkuu kuwa dr. Slaa, usitarajie kuna kapukumeni na ubinafsi binafsi wake (zito) atawakengeusha freedom fighters. Ya zito ni mashuzi, kavimbiwa migebuka yeye na kufulila wake wanaoota kuifanya migebuka kitoweo cha kitaifa kwa mujibu wa tamasha lao la kibaguzi (kigoma)

Kama nilivyopost kwenye post moja hapo juu kwamba mapovu haya siyo bure yanakuwa driven na mambo mengi ukanda kwa vile hatoki kanda yangu, ukabila kwa vile hatoki kabila yangu, udini siyo dini yangu, upambe na ukuwadi kwa vile hayuko kwenye group langu, chuki binafsi and the like. Hivi ni mara ngapi watu wanaitana watu kutoka mikoa yao na kuchangishana kwa nini hili la zito liwe nongwa na liitwe la kibaguzi? Jamani hakuna mwenye hati miliki ya urais Tz any one can be rais. Watu wengine mnaonekana wabaguzi hivi kafulila ameiingiaje hapo? Inamaana kwa akili yako Kigoma haiwezi kutoa rais? Fikilieni kabla hamjaandika unaweza kufikili unamsaidia mtu au chama chako kumbe ndo unakiharibi kabisa na kionekana ni chama special kwa watu toka ukanda upi.
 
Kazi kweli kweli,hivi mna maana gani mnaposema rais lazima atoke Kigoma halafu mudai huo si ubaguzi?Kauli hii ingetolewa na mtu wa Arusha,Kilimanjaro ama usukumani kungekalika humu?Nina mashaka sana uwezo wa wengi wetu wa kufikiri humu,especially siku za karibuni baada ya watanzania wengi kupata access ya mtandao.
 
Haya tumekusikia....Zitto ndiye alieleta thread hii so najua yuko online hapa....unaonaje ukamuomba uanze kuishinae home wakati ukisubilia hiyo 2015? Maana nyinyi ndiyo vizabinazabina wenyewe mnaosababisha huyu mh.aeleweke vibaya
kwa viongozi wake. shame on u


Mie nasema wenzetu mahodari mpaka hasira za Mungu mnazijua.........haya makubwa.
 
WanaJF ile video ya Zito kuhusu wabunge wanaompigia debe urais bado?
Nauliza sababu inawezekana imeshatolewa nami sikuiona. Kimsingi naisubiri kwa hamu ili itoe nyeusi na nyeupe ya suala husika... mwenye latest atusaidie...
 
Alisema ataipost kwenye blog yake. nakushauri tembelea blog yake huenda ukakutana nayo.
 
Kesi iko mahakama ya waziri wa kazi. Hivyo hairuhusiwi kujadiliwa
 
sidhani kama utawaumbua jamaa zake.!
Awaumbue mara ngapi? Mimi naona Filikunjobe, Nassari na Halima Mdee washapata somo kwamba Zitto ni manipulative.

Sina shaka kama walisema mbona kawachana live tayari!

Waliingizwa mkenge wakubali tu
 
Pia inaweza ikawa ni mbinu ya kuitambulisha blog, ili aweze pia kupata matangazo baada ya blog kuanza kufahamika na kutembelew na watu wengi kwa siku.

Maumivu ya kichwa huanza polepole.
 
Bado anashauriana na Bollywood, na Hollywood, kuhusu bei ya kuitengeneza hiyo clip, bado tunaisubiri.
 
Director THE GREATEST RAY anamalizia editing wakuu then Nyepesi ataishusha hapa hapa msihofu!
 
Nilikuwepo uwanjani pale lake Tanganyika Kigoma, kilichoandikwa ndicho nilichosikia pia. Videos zitawekwa hapa na zitathibitisha.

Siwezi kuwaandikia mwananchi kwani mimi silalamiki kuhusu habari hiyo. Wenye kuilalamikia habari wameandika.

Mimi ninaamini gazeti la Mwananchi ndio gazeti pekee huru la kiswahili hapa nchini. Ndio gazeti pekee ambalo umiliki wake hauna maslahi na waandishi na wahariri wake ni mahiri, hawana njaa na hawapindishwi. Ndio maana huandika ukweli muda wote na wanapokosea hawasiti kurekebisha. Ndio maana ni gazeti linasomwa kwa wingi kuliko magazeti yote nchini. Hakuna gazeti linalofikia hata nusu ya mwananchi kwa kusomwa. Hivyo Mwananchi linaaminika na umma.

Najua kuna watu wana chuki binafsi na mwananchi kama gazeti na wahariri wa mwananchi kama binaadamu. Hayo wayamalize wenyewe huko walikochukiana.

Subirini video ndio tutajua habari ile imepikwa au ni ya kweli. Kwa tuliokuwepo uwanjani tunajua nani alisema nini.

Zitto
Ina maana waandishi wa magazeti mengine wana njaa?
Ni juzi tu wamemwomba radhi Membe kwa kuandika habari ya uzushi. Mi naona kama unawasifu kwa sababu wameandika habari yenye jambo la kukufurahisha kwa maana ya kuibua mjadala huu unaofanya sasa tuzungumzie jambo hili kama ambavyo ulitaka.
Kila la kheri katika harakati zako za Urais, ila naona kama unawahi sana kaka!
 
Nimekuelewa mkuu,Shauri japo kwa kifupi wafanye nini,kwan muda uliobaki ni mchache na maeneo ya vijijini bado ha2oni nguvu ya CHADEMA na huku ndio mtaji mkubwa wa kura ulipo?
Tumeshauri muda mrefu sana kuhusu chama kuunda viongozi wapya ambao sii wabunge, sii viongozi wenye majukumu makubwa nje ya chama. Lakini nadhani makao makuu na viongozi wa chama wanaelewa zaidi kwa nini maoni au mapendekezo yetu hazikuchukuliwa.

Mimi sizijui sababu zaidi ya ku speculate, nachoweza kukisia tu kama dhana ni kwamba viongozi wa zamani au waloshika madaraka leo wanashindwa kuwaamini vijana wapya waliojiunga kama kweli wamejiunga kwa nia ya dhati na Uzalendo kwa chama au ni mamluki wanaokuja kukiangamiza chama.. Ikiwa wao wenyewe hawaaminiani itakuwaje rahisi kwa wanachama na vijana wapya walojiunga? Pengine pia ule mfumo wa Kimapinduzi, Kimageuzi na uana harakati ya kwamba kiongozi wa chama ndiye kioo cha harakati zenyewe na wafuasi wake (wanafunzi wake) ndio waandishi na wasambazaji wa itikadi ya chama. Sasa kwa hili hapa, sielewi nani mwenye vision, ni - Mtei, Mbowe au Dr. Slaa..

Hata hivyo, muda unayoyoma hausubiri chama wala watu. Na kibaya zaidi bado tumeweka matumaini kwa watu wale wale ambao pasipo nguvu zao chama kitayumba.. Na kuijenga imani hiyo ya bila hawa.. Ndio tutawajengea mahekalu ya ufalme na milki ya chama maana watasema bila sisi chama hiki kingekuwa hivi?..Wataudai ufalme hadi Ikulu kama tulivyowaona kina Takadir na kwa bahati mbaya sana ndiko tunakoelekea.. Nitasema tena CDM tuna one last chance 2015.. Tumebaki na risasi moja tu kama tutashindwa kuitimia vizuri 2015 basi ndio imetoka. Inauma sana lakini ndio ukweli wenyewe, La muhimu zaidi ni kujiuliza Tumejiandaaje?
 
Miezi ya nyuma nilileta hii mada hapa jukwaani lakini kwa bahati mbaya MODs waliinyofoa dakika 20 baada ya kuiweka. Sina budi kurudisha hii mada baada ya sakata la Zitto Kabwe, Nassari, Halima Mdee pamoja na gazeti la Mwananchi. Kwa muda wa miaka kadhaa sasa, nimekuwa katika tasnia ya habari na lazima nikiri kwamba mengine yanayofanyika katika hii tasnia ni ya kukatiza moyo hasa kazi za wanahabari zinapoingiliwa na wanasiasa. Kwetu sisi wanawake inakuwa ni vigumu sana kukataa kutii haya maagizo ambayo mengine unaona kabisa ni za vitisho

Zitto Kabwe, January Makamba, Bernard Membe na hata Ngeleja kwa siku za nyuma alishiriki sana katika kuingilia kazi za waandishi. Kinara wao akiwa Zitto January na Membe. Hawa viongozi hasa Zitto wamezoea sana kujiandikia makala na hata habari kisha kumlazimisha mwandishi kuzichapisha ukurasa wa mbele kwa gharama yoyote ile. Wanatoa hela nyingi sana kwa waandishi na wahariri. Mbaya zaidi ni kwamba hawa viongozi wanajitengenezea kashfa au kutoka ndani ya vyama vyao.

Matokeo yake kesho wanaitisha waandishi tena kukanusha (kashfa) zao za kujipikia wakati ni wao ndio chanzo cha hizo habari. Lengo lao kubwa ni kutafuta huruma kutoka kwa umma wa kitanzania kwa vitu ambavyo havipo.

Kinachonishangaza ni kwa nini mtu ajichafue kwa kujitengenezea kashfa maadui feki ndani ya chama chake heti ndio wanaomchafua kumbe ni yeye mwenyewe alafu kesho yake akane hizo taarifa? Nadhani tunaelekea kubaya hawa watu wakiendelea nah ii tabia. Moja ya habari hizi ni zile zinazomlaumu Mbowe kam mtazikumbuka..

nawakilisha

Nimekuwa nami nikiandika kama wewe, lakini vibaraka wao wanakuja mara moja na kunishambulia, lakini time will tell. Hawa watu wana lao jambo. Kwa mfano mchango wa ZITTO wakati akichangia hotuba ya bajeti ya SAYANSI & TECH ulikuwa wazi ni wa kumfagilia rafiki yake, JANUARI MAKAMBA, ambaye naye alikuja kumfagilia rafiki yake, ZITTO, kwani alitumia dk12 na sekunde 36 kati ya dak30 alizopewa na mwenyekiti akijibu hoja moja tu ya ZITTO kwa style ya kufagiliana (there is reciprocity in their clandestine political blahblah): WANATUCHEZEA AKILI HAWA...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom