Urais, Halima, Nassari na Kigoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Urais, Halima, Nassari na Kigoma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zitto, Jul 24, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #1
  Jul 24, 2012
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Katika gazeti la Mwananchi la tarehe 23 Julai 2012, kulikuwa na habari yenye kusomeka 'Wabunge wamsafishia Zitto njia ya Urais 2015'. Habari hii imeleta mjadala mara baada ya kutoka na kusomwa. Mjadala umekuzwa zaidi baada ya Wabunge ndugu Halima Mdee na ndugu Joshua Nassari kukanusha maneno waliyonukuliwa kusema. Napenda kusema masuala yafuatayo.

  Moja, Waheshimiwa Wabunge Halima Mdee, Joshua Nassari, Kangi Lugola, Esther Bulaya, Deo Filikunjombe, Raya Ibrahim, Amina Mwidau na David Kafulila walihudhuria tamasha la vijana wa Kigoma All Stars kwa kualikwa na Mratibu wa kundi hilo Mwasiti Almasi.

  Wabunge wengine walialikwa lakini hawakutokea wakiwemo Joseph Mbilinyi, David Silinde, Amos Makala, Vicky Kamata na Peter Serukamba. Wabunge hawa hawakualikwa na mimi na wala sikufanya mazungumzo nao yeyote ya awali au kuwaambia au kukubaliana nini cha kuzungumza au hapana. Tamasha lilikuwa la muziki na halikuhusika kabisa na siasa.

  Waheshimiwa wote walipewa nafasi ya kusalimia na wote walizungumza. Wabunge waliozungumza kwa muda mrefu kidogo ni ndugu Halima Mdee, Joshua Nassari, Deo Filikunjombe na Kangi Lugola.

  Hotuba za Wabunge wote zilirekodiwa kwenye video neno kwa neno na video hizo zitawekwa wazi kwenye blogu yangu kama sehemu ya documentary ya tamasha lile la kihistoria.

  Pili, sikuhusika kwa namna yeyote ile na kuandikwa kwa habari hii iliyozusha mjadala. Wala sikujua kama habari hii ingeandikwa maana katika ziara ile sikuita mwandishi hata mmoja maana nilitaka liwe tukio la Kigoma tu.

  Kama mwandishi kaandika ambayo wabunge hawa hawakuyasema basi itaonekana kwenye videos hizo. Wabunge wenyewe wanajua kwenye nafsi zao nini walisema Kigoma na kipi kiliwasukuma kusema walioyasema Kigoma. Nisingependa kuhusishwa kwa njia yeyote ile na matamshi yao, habari iliyowanukuu na hata makanusho yao. Maana mwisho wa siku ukweli ndio utasimama.

  Suala la Urais lisitupotezee muda kwani kuna mambo mengi sana ya kujadili kuhusu nchi yetu. Taharuki ambazo watu wanazipata masuala ya urais yanapotajwa zinashangaza sana.

  Chama changu bado hakijatangaza rasmi mchakato wa kupata mgombea Urais. Hivi sasa chama hakina mgombea Urais mpaka hapo mchakato utakapotangazwa ambapo wanachama wataruhusiwa kuomba kupeperusha bendera ya chama. Mwanachama wa chama chetu atakaye kubalika na jamii na wajumbe wa mkutano wa uteuzi ndiye atakuwa mgombea wetu. Kwa sasa hayupo na hivyo tusipoteze muda kujadili jambo hili.

  Mzee Thabiti Kombo alituachia usia tunapokuwa tunazungumza. Alisema 'weka akiba' sio akiba ya fedha, bali ya akiba ya maneno. Tuweke akiba ya maneno. Tusimalize yote.

  Zitto
   
 2. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #2
  Jul 24, 2012
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
 3. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #3
  Jul 24, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Bora umetokea mwenyewe hapa la sivyo habari imefanywa ya udaku kwenye gazeti la Mwananchi pamoja na vibaraka wa Magamba wamepata maneno ya kutokea
   
 4. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #4
  Jul 24, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  unajua mh. watu tumetrace nyuma huko yaani habari zako kwenye gazeti la mwananchi zinaandikwa na mwandishi mmoja (Ramadhani Semtawa)..na zote huwa zinazua mgogoro mkubwa sana kwenye jamii....leka tutigite imefanyika karibu siku 6 zimepita alikuwa wapi kuandika? na je ni kweli umemuweka mfukoni huyu mwandishi?...
   
 5. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #5
  Jul 24, 2012
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Zitto ndugu yangu wewe ni mnafiki. Hii tabia umekuwa ukiifanya kwa muda mrefu. Unaleta habari tatanishi tena muda mwingine unajijengea kashfa feki alafu kesho yake unarudi kuikana. Mwenendo wa leo ni hule hule. Nina uhakika 100% kwamba kuna mkono wako mwananchi. Na wewe pia hilo unalifahamu kaka yangu. hii tabia ni mbaya hachana nayo. madaraka tunapewa na wananchi usiyalazimishe. niliwahi kukuambia hii miaka miwili nyuma tulipoonea kule dodoma
   
 6. Avanti

  Avanti JF-Expert Member

  #6
  Jul 24, 2012
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 1,209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  The truth will unfold soon! Weka video kamanda!
   
 7. m

  mamajack JF-Expert Member

  #7
  Jul 24, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  hayo ndiyo maneno,halafu pia kuwa na nia ya kuwa rais,haina maana utakuwa rais.
  kweli kabisa tuweke akiba.
   
 8. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #8
  Jul 24, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Nitaipigia Kura Chadema iwapo itamsimamisha Dr Slaa sio Zitto wala mbowe
   
 9. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #9
  Jul 24, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,340
  Trophy Points: 280
  Mh Zitto,

  Hiki ndicho ulipaswa ufanye na umefanya, nakupongeza.
  Mkanda huo uwekwe hapa pia tafadhali.

  Kuhusu taharuki, elewa kuwa katika jamii kuna kukinzana kwa mawazo. Ningekushauri usiende huko ujikite katika sintofahamu iliyotokea.

  Kwa upande wangu taharuki si Urasi ni dalili ya tatizo kubwa. Hilo tuliache kwanza.
  Mwisho, nigekushauri pia uwaandikie Mwananchi kwasababu suala hili limeleta usumbufu sana.
   
 10. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #10
  Jul 24, 2012
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Miezi ya nyuma nilileta hii mada hapa jukwaani lakini kwa bahati mbaya MODs waliinyofoa dakika 20 baada ya kuiweka. Sina budi kurudisha hii mada baada ya sakata la Zitto Kabwe, Nassari, Halima Mdee pamoja na gazeti la Mwananchi. Kwa muda wa miaka kadhaa sasa, nimekuwa katika tasnia ya habari na lazima nikiri kwamba mengine yanayofanyika katika hii tasnia ni ya kukatiza moyo hasa kazi za wanahabari zinapoingiliwa na wanasiasa. Kwetu sisi wanawake inakuwa ni vigumu sana kukataa kutii haya maagizo ambayo mengine unaona kabisa ni za vitisho

  Zitto Kabwe, January Makamba, Bernard Membe na hata Ngeleja kwa siku za nyuma alishiriki sana katika kuingilia kazi za waandishi. Kinara wao akiwa Zitto January na Membe. Hawa viongozi hasa Zitto wamezoea sana kujiandikia makala na hata habari kisha kumlazimisha mwandishi kuzichapisha ukurasa wa mbele kwa gharama yoyote ile. Wanatoa hela nyingi sana kwa waandishi na wahariri. Mbaya zaidi ni kwamba hawa viongozi wanajitengenezea kashfa au kutoka ndani ya vyama vyao.

  Matokeo yake kesho wanaitisha waandishi tena kukanusha (kashfa) zao za kujipikia wakati ni wao ndio chanzo cha hizo habari. Lengo lao kubwa ni kutafuta huruma kutoka kwa umma wa kitanzania kwa vitu ambavyo havipo.

  Kinachonishangaza ni kwa nini mtu ajichafue kwa kujitengenezea kashfa maadui feki ndani ya chama chake heti ndio wanaomchafua kumbe ni yeye mwenyewe alafu kesho yake akane hizo taarifa? Nadhani tunaelekea kubaya hawa watu wakiendelea nah ii tabia. Moja ya habari hizi ni zile zinazomlaumu Mbowe kam mtazikumbuka..

  nawakilisha
   
 11. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #11
  Jul 24, 2012
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Siwezi kumjibia Semtawa na sijawahi maisha yangu kumtuma habari Semtawa au mwandishi yeyote yule. Mimi sio mhariri. Waliozoea kufanya hivi ili waandikwe wanadhani wote tunafanya hivyo hivyo.
   
 12. J

  Jimmy Naff New Member

  #12
  Jul 24, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mhhhhhhhh!!!!!namkubali sana mh.Zitto na ndie mgombea rais kijana mpya wa 2015,hata mkileta majunguhili taifa ni la vjana kwa ajili ya mustkabali wa taifa lao.
   
 13. n

  nsanu Member

  #13
  Jul 24, 2012
  Joined: Jun 26, 2012
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zitto iyo video weka hapa JF ili tufahamu ukweli
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #14
  Jul 24, 2012
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Nilikuwepo uwanjani pale lake Tanganyika Kigoma, kilichoandikwa ndicho nilichosikia pia. Videos zitawekwa hapa na zitathibitisha.

  Siwezi kuwaandikia mwananchi kwani mimi silalamiki kuhusu habari hiyo. Wenye kuilalamikia habari wameandika.

  Mimi ninaamini gazeti la Mwananchi ndio gazeti pekee huru la kiswahili hapa nchini. Ndio gazeti pekee ambalo umiliki wake hauna maslahi na waandishi na wahariri wake ni mahiri, hawana njaa na hawapindishwi. Ndio maana huandika ukweli muda wote na wanapokosea hawasiti kurekebisha. Ndio maana ni gazeti linasomwa kwa wingi kuliko magazeti yote nchini. Hakuna gazeti linalofikia hata nusu ya mwananchi kwa kusomwa. Hivyo Mwananchi linaaminika na umma.

  Najua kuna watu wana chuki binafsi na mwananchi kama gazeti na wahariri wa mwananchi kama binaadamu. Hayo wayamalize wenyewe huko walikochukiana.

  Subirini video ndio tutajua habari ile imepikwa au ni ya kweli. Kwa tuliokuwepo uwanjani tunajua nani alisema nini.
   
 15. KML

  KML JF-Expert Member

  #15
  Jul 24, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 863
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  mambo ya siasa hayo
  Siasa mchezo mchafu
   
 16. Bams

  Bams JF-Expert Member

  #16
  Jul 24, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 2,971
  Trophy Points: 280
  Kwa maelezo haya, hatuna sababu ya kuwa na mashaka tena. Zito kujiandikia habari, kisha kuwalazimisha wanahabari kuiweka habari yake ukurusa wa mbele kwa kuwalipa fedha nyingi waandishi wa magazeti, HIYO NI HONGO. KWA HIYO ZITTO NI MTOA RUSHWA KWA MASLAHI YA KISIASA. NA SIKU ZOTE MTOA RUSHWA AKIPATA NAFASI ANAKUWA MPOKEA RUSHWA. KWA UCHAFU HUU UNAOFANYWA NA ZITO, kama baada ya uchaguzi tutaendelea kumwona Zito kwenye nafasi za juu za uongozi wa CHADEMA, sitakuwa na imani na CHADEMA tena, aheri nijue tu kuwa hatuna wa kututoa mahali tulipo. Maana uchafu huo anaoufanya Zitto ni dhahiri CHADEMA watakuwa wanaujua, na je wamechukua hatua gani?
   
 17. Avanti

  Avanti JF-Expert Member

  #17
  Jul 24, 2012
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 1,209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kamanda andikia wino bana! Kwa nini kujitesa!
   
 18. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #18
  Jul 24, 2012
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Porojo
   
 19. M

  Mkojo Member

  #19
  Jul 24, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unacheza na maneno wewe Zitto! lazima una hila nyuma yako! kumbuka wakati wa uchaguzi mdogo wa arumeru mashariki uliibuka na maneno yako haya tata kama mchawi!! kwamba unautaka urais!! yani watu tuko biz tunahangaika kuhakikisha Joshua anapita katika AM, wewe ukaibuka ki vile, tafsi ya wengi wetu ilikuwa wewe ni kuadi unatumika tu na wa upande wa pili! ili kutunyongesha kulichukua jimbo hilo au we unafikiri logic hasa ilikuwa nini katika uchaguzi ule we kuibuka na kaule kama ile?

  Haya hata hayo ya upuuzi wk hayajakauka leo linazuka hili!
  Zitto wewe ni mtata sana, tena mnafiki mkubwa!
  Hila mbaya kama hizi za kuuendea uongozi mkuu wa nchi yetu leo zinamtokea JK puani! hata kama kajilimbikizia mali kiasi cha kutisha hana heshima tena! atabakia kuwa kiongozi wa ovyo aliyeshindwa kuliongoza taifa lake na watu wake!

  Haya we endelea tu! lakini kumbuka siku zote mwisho wa ubaya ni aibu!
  JK sasa anaaibika! Tafakari!
   
 20. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #20
  Jul 24, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280

  sawa ukipata mda pitia link http: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/132732-zitto-kabwe-stop-using-ramadhan-semtawa-kuivuruga-chadema.html ambayo tunapata wasi wasi kuwa unamtumia huyu bwana.hizi ni baadhi ya makala anazoandika huyu....hizo video umeshaweka kwenye blog yako? nakuomba na hapa uziweke..

  urafiki wako na davidi Msacky unatajwa kuw nae yuko nyuma ya project hii ya uchonganishi ndani ya chama (chadema)...unasemaje juu ya hili?

  ni kweli wewe unatumiwa na ccm kukivuruga chama?(chadema)
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...