Nimekusoma sana mkuu. Ninachoungana mkono na watu wengi humu ni kuwa mara nyingi Zitto anatoa kauli au misimamo kwenye mambo ambayo yanamfanya awe very vulnerable politically, na hapa namaanisha mengine ana-win, mengine ana-loose. Ninachopingana na watu wengi humu, ni kuwa Zitto anatoa kauli hizi 'kwa kutumiwa' au kwa nia yeyote mbaya. Udhaifu wa ZZK, kama wengine pia walivyo na ya kwao, ni kuwa anajiamini kupitiliza kuwa yeye ndiye best politician and leader alive in Tanzania. Naamini kuwa ZZK hana mshauri wa kisiasa, wala haamini ushauri anaopewa.
Mimi siamini kama udhaifu huu wa ZZK utaivuruga CDM, au utasimamisha progress ya CDM hata kwa sekunde moja. Na pia ZZK bado namuweka kwenye kundi la highly potential leaders wa chama sasa na baadae, pamoja na madhaifu yake hayo...
Kama kweli nia yetu ya dhati ni kumpata kiongozi mzuri ni lazima tuangalie ni yapi viongozi waliopita bila kujali vyama yaliwafanya washindwe na kuangamiza Taifa na yapi yaliwafanya waweze kuongoza na kuliendeleza taifa kama limeendelea.
Uzoefu unaonyesha tatizo kubwa la viongozi wetu wengi ni kukataa sio tu kufuata ushauri bali hata kusikiliza. Sasa kila mmoja ampe kijana mwenzetu ZZK anayetaka kwa udi na uvumba kwenda ikulu je ana fit wapi.
Anashaurika
anasikiliza ushauri wa kitaalamu
ana busara na hekima
anaweza kutumia elimu yake kutatua matatizo yetu au kujikweza na kudharau kila mmoja
anaweza kufanya kazi na wengine hata pale wanapotaofautiana kwa personal issues?
anaweza kuvumilia wenzake
anaweza kutoa maamuzi magumu
je ni kigeugeu kwa asilimia ngapi unaweza kuamini anachosema ndicho ? kumbuka amesha sema zaidi ya mara moja kuwa hata gombea ubunge nk
Je ni mwadilifu wa kweli au ngonjera tu
Je ni mfitini na mchonganishi
Je anaweza kweli kutoka rohoni kushinda vishawishi hasa vya rushwa nk nk
Hapa nakubaliana na wewe 100%, naamini kabisa ZZK hatumiwi na CCM isipokuwa ZZK kweli anautaka Urais yeye na anajiamini kupitiliza. navyomtazama ZZK najua fika tuna kiongozi mwenye uchungu na nchi yetu lakini kisiasa anashindwa kucheza karata hizi inavyotakiwa na CCM wanatumia makosa kama haya kuwavuruga zaidi Chadema. Sijui ninam- Overestimate ZZK maanake anakuwa kama sii wa mujini kushtukia vitu hivi kutumiwa kama chambo halafu anataka watu wamuelewe. Anajimaliza mwenyewe kupambana na wapiga kura badala ya kupambana na CCM kama anavyofanya Bungeni..
mkubwa Mkandara
Je ZZK ataingia ikulu akijua fika team ya kumwingiza ikulu anaichafua na kuitibua kila kukicha
Je wote tunaamini ushindi wa kisiasa ni team work ?
Je ZZK hata kama ni mzuri vipi ni kweli anaweza kushinda mwenyewe??
Je ni nani yuko tayari kufanya kazi na kiburi cha ZZK
Kutumiwa au kutotumiwa hilo analijua mwenyewe kwa nini ZZK hataki kwenda vijijini kujenga Chama ila anasubiria tu safari ya Ikulu
Kama ni swala la kutumikia chama anajifananisha na nani???
Je ZZK anaona kutoka moyoni nafasi ya mwanachama wa kawaida au anawaona kama vyombo tu vya kumpeleka ikulu
Kwa kauli zake mwenyewe anajenga chama au anakivuruga??
Kama ni elimu ni wangapi wamesoma ndani ya CDM?
Je ZZK anakumbuka kuwa amelelewa na kukuzwa kama wengine.
Tujijenge kama viongozi na kuomba hekima kama suleiman ya kuongoza watanzania.