Urais 2015: Mtei amshukia Zitto

Urais 2015: Mtei amshukia Zitto

Kama kweli nia yetu ya dhati ni kumpata kiongozi mzuri ni lazima tuangalie ni yapi viongozi waliopita bila kujali vyama yaliwafanya washindwe na kuangamiza Taifa na yapi yaliwafanya waweze kuongoza na kuliendeleza taifa kama limeendelea.

Uzoefu unaonyesha tatizo kubwa la viongozi wetu wengi ni kukataa sio tu kufuata ushauri bali hata kusikiliza. Sasa kila mmoja ampe kijana mwenzetu ZZK anayetaka kwa udi na uvumba kwenda ikulu je ana fit wapi.
Anashaurika
anasikiliza ushauri wa kitaalamu
ana busara na hekima
anaweza kutumia elimu yake kutatua matatizo yetu au kujikweza na kudharau kila mmoja
anaweza kufanya kazi na wengine hata pale wanapotaofautiana kwa personal issues?
anaweza kuvumilia wenzake
anaweza kutoa maamuzi magumu
je ni kigeugeu kwa asilimia ngapi unaweza kuamini anachosema ndicho ? kumbuka amesha sema zaidi ya mara moja kuwa hata gombea ubunge nk
Je ni mwadilifu wa kweli au ngonjera tu
Je ni mfitini na mchonganishi
Je anaweza kweli kutoka rohoni kushinda vishawishi hasa vya rushwa nk nk



mkubwa Mkandara
Je ZZK ataingia ikulu akijua fika team ya kumwingiza ikulu anaichafua na kuitibua kila kukicha
Je wote tunaamini ushindi wa kisiasa ni team work ?
Je ZZK hata kama ni mzuri vipi ni kweli anaweza kushinda mwenyewe??
Je ni nani yuko tayari kufanya kazi na kiburi cha ZZK
Kutumiwa au kutotumiwa hilo analijua mwenyewe kwa nini ZZK hataki kwenda vijijini kujenga Chama ila anasubiria tu safari ya Ikulu
Kama ni swala la kutumikia chama anajifananisha na nani???
Je ZZK anaona kutoka moyoni nafasi ya mwanachama wa kawaida au anawaona kama vyombo tu vya kumpeleka ikulu
Kwa kauli zake mwenyewe anajenga chama au anakivuruga??
Kama ni elimu ni wangapi wamesoma ndani ya CDM?
Je ZZK anakumbuka kuwa amelelewa na kukuzwa kama wengine.


Tujijenge kama viongozi na kuomba hekima kama suleiman ya kuongoza watanzania.

Jambo moja ambalo linanifanya nisihofie wala kuona kama kauli za kukurupuka za ZZK zina madhara yeyote ni kwa sababu nimezizoea. Siku zote amekuwa akiongea vitu vinavyosababisha utata, lakini CDM imekuwa na buffering capacity kubwa juu ya hayo. Kwa hiyo hata sasa simwoni wala sioni tishio lolote la kauli zake.
La pili ni kwamba, nina uhakika 100% kuwa ZZK hatakuwa raisi wa kwanza wa nchi kupitia CDM, iwe 2015 au zaidi ya hapo.
Pamoja na hayo yote, bado namuona ZZK kama mtendaji mahiri na kiongozi shupavu wa baadae wa chama au hata nchi. Siku CDM ikiingia ikulu, naamini ZZK atakuwa na nafasi ya kiutendaji na kimaamuzi, hapo ndipo atakapotuthibishia kuwa yeye ni mchapakazi, mbunifu na mwadilifu (kama nimuonavyo mimi)
 
kama zitto anataka urais nchi hii kwa sasa ina matatizo mengi ya kutatuliwa kuliko cheo cha urais mii nilidhani angeendelea kusisitiza katiba ipunguze kabisa madaraka ya nafasi hii ili watu wasiitumie kamanafasi ya kujitanua bali kwa ajili ya kusikiliza wenzao na kufanya kazi kwa pamoja huyu jamaa ni muislam mwenzangu ila wote yeye na kikwete wananikatisha tamaa
 
Mbona unamwonea huyu Mzee? Mzee Mtei amesema "HUENDA HATA MIMI NIKATAKA". Hajasema anatangaza nia.

Huenda hata wewe au mtu yeyote yule mwenye sifa akatangaza nia ya kugombea u-Rais.

mkuu sio kwamba namuonea hiyo nia keshatagaza .. Mzee Mtei anajifanya mjanja kumkandia zito huku yeye akitangaza nia hapo hapo

 
Wana JF,

Natambua kuwa Katiba yetu ya nchi hajasema lolote kuhusu kupokezana madaraka ya Rais kwa kuzingatia kipengele cha dini lakini kwa muda mrefu sasa suala hili limekuwa likiamuliwa kwa kutumia busara ya kawaida. Historia inaonesha kuwa Rais wa kwanza wa nchi hii, Mwalimu Julius K. Nyerere alikuwa Mkristo lakini wakati anatoka madarakani alihakikisha kuwa Rais atakayekuja baada yake anakuwa Muislamu, na ndivyo ilivyokuwa kwa Rais Ali Hassan Mwinyi. Baada ya Mwinyi alifuatia Rais William Benjamin Mkapa ambaye tunatambua kuwa alikuwa Mkristo, na baada yake ni Kikwete ambaye ni Muislamu. Kama nilivyosema awali, utaratibu huu haujaandikwa mahali popote ikiwa ni pamoja na kwenye Katiba yetu lakini limekuwa likifanywa zaidi kwa kutumia busara. Sasa inashangaza sana kuona mtu kama Zitto Zuberi Kabwe ambaye ni muislamu, akitangaza nia ya kugombea Urais mwaka 2015! Naomba Zitto asahau katika hili. Na pia naomba muislamu yoyote mwenye ndoto kama za Zitto asahau katika hili kwani kwa kutumia BUSARA ya kawaida Rais ajaye mwaka 2015 ni LAZIMA AWE MKRISTO, awe anatoka CHADEMA au CCM. Huo ndio ukweli, na tena kwa kutumia busara ya kawaida tu. Zitto nakushauri usubiri hadi mwaka 2025, kwani ni katika kipindi hicho tutahitaji Rais Muislamu katika nchi yetu.

Nawasilisha.
 
Hatumchagui mtu kuwa rais kwa sababu ya dini yake na hatumkatai mtu kuwa rais kwa sababu ya dini yake. aliwahi kusema jambo kama hili Mwalimu Nyerere ingawa sikumbuki vizuri alilisemea wapi.
 
2015 hatuchagui kiongozi wa dini ondoa thread yako wa kijinga.
 
MAWAZO YA KIDINI KAMA HAYA YATATUANGAMIZA.
TUKIAMUA HIVYO ITABIDI TUFANYE NA YAFUATAYO.

usiangalie uraisi pekee, angalia na idara nyingine.
Itabidi iingize kwenye katiba hata ujumbe wa nyumba kumi.
Kama tunafanya tufanye kweli na sio tutanie.

Nyerere alitawala miaka mingi, inabidi waislam waendekee kutawala mpaka miaka ifike sawa na wakristo.
Baada ya hapo ndio tuanze kupokezana, tena wagombea wawe wanapendekezwa na watu wa dini husika, kama ni zamu ya waislam wao ndio wapendekeze wagombea.

Tena iwe kwa vyama vyote, kama ni zamu ya wakristo basi vyama vyote visimamishe wagombea wakristo.

HAPO TUTAKUA TUMELIANGAMIZA TAIFA LETU.
KAMA KILA MTANZANIA ATATENDEWA SAWA BILA KUBAGUA DINI, KABILA AU RANGI YAKE HAKUTAKUWA NA TATIZO LA UDINI.

TUNACHOKISHUHUDIA LEO NI MATOKEO YA KUBAGULIWA NA KUKANDAMIZWA KWA JAMII FULANI KWA MUDA MREFU KUTOKANA NA DINI YAO.
HAYA NI MATOKEO YA MIKONO YETU WENYEWE.
 
Wana JF,

Natambua kuwa Katiba yetu ya nchi hajasema lolote kuhusu kupokezana madaraka ya Rais kwa kuzingatia kipengele cha dini lakini kwa muda mrefu sasa suala hili limekuwa likiamuliwa kwa kutumia busara ya kawaida. Historia inaonesha kuwa Rais wa kwanza wa nchi hii, Mwalimu Julius K. Nyerere alikuwa Mkristo lakini wakati anatoka madarakani alihakikisha kuwa Rais atakayekuja baada yake anakuwa Muislamu, na ndivyo ilivyokuwa kwa Rais Ali Hassan Mwinyi. Baada ya Mwinyi alifuatia Rais William Benjamin Mkapa ambaye tunatambua kuwa alikuwa Mkristo, na baada yake ni Kikwete ambaye ni Muislamu. Kama nilivyosema awali, utaratibu huu haujaandikwa mahali popote ikiwa ni pamoja na kwenye Katiba yetu lakini limekuwa likifanywa zaidi kwa kutumia busara. Sasa inashangaza sana kuona mtu kama Zitto Zuberi Kabwe ambaye ni muislamu, akitangaza nia ya kugombea Urais mwaka 2015! Naomba Zitto asahau katika hili. Na pia naomba muislamu yoyote mwenye ndoto kama za Zitto asahau katika hili kwani kwa kutumia BUSARA ya kawaida Rais ajaye mwaka 2015 ni LAZIMA AWE MKRISTO, awe anatoka CHADEMA au CCM. Huo ndio ukweli, na tena kwa kutumia busara ya kawaida tu. Zitto nakushauri usubiri hadi mwaka 2025, kwani ni katika kipindi hicho tutahitaji Rais Muislamu katika nchi yetu.

Nawasilisha.

Edward Lowassa Vs Wilbroa Slaa
 
Kutangaza nia mapema ya kugombea uraisi 2015 ni uroho wa madaraka au ndio demokrasia?
 
Swali hilo hapo juu najiuliza kwa kuwa:-
1. Muda wa kutangaza nia bado
2. Anatajwa kuungwa mkono na wana CCM (Januari Makamba, Kigwangala, JK-Mkwe n.k)
3. Hatumii utaratibu wa Chama wa Mchakato wa Mgombea Urais
4. Njia aliyotumia kuutaka Umwenyekiti ndio hiyohiyo anaitumia kwa kuutaka Urais
5. Zitto haonekani mara nyingi kwenye M4C ya Chama
6. Mpaka sasa hajaoa (atakuwa Rais mseja?)
7. Ana mahusiano zaidi kwa CCM kuliko CDM (Hakutoka nje wabunge wa CDM walipotoka kupinga matokea ya JK 2010)
8. Anasafiri na JK nje ya nchi au mwenyewe bila mawasiliano na Chama.
9. Ongezea ...............
Nikosolewe kama siko sahihi lakini binafsi harakati za Urais za Zitto ndani ya CDM naona kama kutumiwa zaidi kuivuruga Chama kuliko kuutaka Urais na kuwa na sifa za kuwa Rais.
 
Kwanza badilisha hiyo post yako sio anauta, ni anautaka uraisi......kama umeshinda kuandika kitu kidogo kama hicho je?utweza kujibu hoja nzito zilizo komaa za wa baba?
 
MWASISI wa CHADEMA,Edwin Mtei amemtaka Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe kumwachia Katibu Mkuu wake, Dk Willbrod Slaa fursa ya kuwania tena urais mwaka 2015 kwa madai kuwa ndiye chaguo la watu kwa sasa.

Kauli hiyo ya Mtei inakuja siku kadhaa baada ya kuunga mkono kauli ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kwamba Dk Slaa awanie tena urais katika uchaguzi ujao huku yeye akijiondoa katika orodha ya viongozi watakaowania nafasi hiyo kupitia CHADEMA.

Akihojiwa na gazeti hili, Mtei alisema Zitto anapaswa kumwachia Dk Slaa apeperushe bendera ya chama hicho katika uchaguzi ujao kwa kuwa ndiye chaguo la wengi.

"Zitto atagombea baada ya Dk Slaa na kwa sasa amwachie katibu mkuu atupeperushie bendera ya chama katika uchaguzi ujao kwani ndiye chaguo la wengi," alisema Mtei.

Mtei alisema yeye anasimamia msimamo wa Mbowe na kamati kuu ya chama hicho kuhusu kumpendekeza Dk Slaa kuwania nafasi hiyo.

Alisema kila mmoja ndani ya chama amekuwa na hisia na mawazo tofauti lakini msimamo wake kwa sasa ni kumtaka Dk Slaa awanie nafasi hiyo ya urais na si Zitto. "Kila mmoja na hisia na maoni yake, Dk Slaa ana yake, Freeman na yake hata mimi nina hisia zangu na Slaa ndiye pendekezo langu nataka atupeperushie bendera," alisema Mtei. ( MWANANCHI JAN 3,2013)
 
Haya ni maoni tu ya Mzee Mtei jamani.Hayana maana nyingine yoyote. Msije mkadhani ni mwendelezo wa kipigo cha MP7
 
"Kila mmoja na hisia na maoni yake, Dk Slaa ana yake, Freeman na yake hata mimi nina hisia zangu na Slaa ndiye pendekezo langu nataka atupeperushie bendera," alisema Mtei. ( MWANANCHI JAN 3,2013)

Very good indeed
 
Huwa mnamkutaga wapi huyo Mzee Mtei? Huwa anaongea na gazeti lenu pekee?
 
Back
Top Bottom