Kigarama
JF-Expert Member
- Apr 23, 2007
- 2,492
- 1,239
Nakushauri Tuko usiondoke kwani wengine tunajifunza mengi kwenye mjadala wenu wewe na Molemo. Lakini mpaka sasa sijaona kama mjadala wenu umejikita kwenye kueleza nini hasa. Najua mnabishania kama ni haki au si haki kwa Zitto kutangaza nia yake ya kugomebea Urais. lakini pia mnabishana kama tendo hilo la Zitto linahatarisha uhai wa chama au la.
Sisi wengine hili la Zitto kutangaza kuomba kugembea Urais kupitia CHADEMA ni jambo LISILOJADILIKA. Kwani tendo hilo ni la kidemokrasia. Ingekuwa taabu sana kama Zitto angesema "iwe isiwe mimi lazima niwe mgombea Urais kupitia CHADEMA mwaka 2015" hapo tungemjia juu kwa kumuuliza yeye ni nani kwamba ni lazima yeye tu awe mgombea Urais kupitia CHADEMA.
Hoja ya pili kwamba kama kauli ya Zitto inayumbisha chama au la ni ya kijinga sana. Hivi CHADEMA ni dhaifu kiasi kwamba mwanachama wake akisema "nitagombea Urais mwaka 2015" inavurugika"? Wale wanaosema kauli hii ya Zitto inavuruga chama watuambie basi inavurugaje chama!? Sipuuzii ushawishi wa Zitto ndani CHADEMA bali nichotaka kuelezwa ni kwa nini ushawishi huo uonekane kama vile ni silaha inayotumiwa na Zitto kusambaratisha chama!!?