Chimunguru
JF-Expert Member
- May 3, 2009
- 10,679
- 4,381
Wanaume wenzangu ndoa miaka miwili mitatu ya mwanzo ni mtihani! Ht mie tulifarakana Sana aliniona mbaya nikamuona mbaya. Lkn nilichokigundua baada ya miaka 16 ya ndoa yangu Kuna vitu vitatu au vinne inabidi uviangalie au uvifanye.
Kwanza chuja yale mapokeo ya kiume kwamba mke anapaswa kukufanyia/ kukupa huduma zote. Kukufulia, kukupikia, kupiga pasi, usafi nk. Jiulize mkeo ni full time housewife au ni mfanyakazi km wewe! Anachokipendelea Sana ni kitu gani? Hapa Sasa jua udhaifu wake ni ninj ili wewe uzibe hilo pengo au utafute namna ya kufanya. Mfano mdogo Mimi ni mngoni kwetu ukioa, baada ya km siku mbili mashangazi huja kula chakula alichopika Bibi harusi wanaita mpikiso na chakula huwa ni Ugali. Sasa bahati nzuri alikuja baba yangu mdogo na Mama mdogo tu. Mtoto wa watu kwao wanakula ndizi ndio chakula Chao ingawa walikuwa wakilima mahindi Mama yao ndo alikuwa anajua kupika Ugali wengine ni mtori, kitawa nk hahaha. Ili kuficha udhaifu tukawapiga Kwanza na castle za baridi na kuku choma wakapata starter swaafi wakasahau mpikiso. Ilipofika mida ya kupika Ugali wakawa wanapiga story sebuleni sisi tukazama jikoni Mzee baba nikazungusha Ugali swafi Ukaenda mezani wakala wakamsifia Sana! Nikawa nimeondoa aibu hapo tukawa happy! Jitahidi uzibe udhaifu wa mwenzio hatakusahau! Within a year tukawa na first born wetu kazi zikawa nyingi, tupo gheto chumba moja, sebule choo na jiko dada wa kazi analala sebuleni, wakawa hawakai miezi 2 wanaondoka.hapo mambo yakaanza kwenda kombo yaani nitoke kazini nikusaidie aisee kwa mwanaume na Yale mapokeo yetu ikawa ngumu Sana. Kilichonisaidia ni background yangu nilishazifanya Sana hizo kazi. Nikapiga moyo konde nikaanza saidia mama, amani na furaha vikatawala. Tulipopata house kubwa tukaweka Dada wa kazi ingawa hawakukaa baadae tukapata houseboi alikaa 4yrs alikuwa super.
Cha pili jitahidi kuwa msaada zaidi kwa mwenzio kuliko kuwa mzigo kwake. Usirudi toka kazini ukakuta msosi bado ukaanza kukoroma, kuwa mpole uliza Kama Kuna kikwazo saidia kutatua. Mwanamke anahitaji Sana faraja kuliko kusemwasemwa, akipata faraja kwa mwingine utashangaa!
Cha tatu Kauli. Hapa ndipo ugomvi mkuubwa huanzia. Mkeo ni mwenzio mpe kauli nzuri nzuri tumia ushawishi na SI kulaani kila kosa na kujuta. Rekebisha mwenyewe halafu muelimishe, kesho hatarudia tena.
Nne mfanye mkeo ndo best friend, mpe Siri zako zote unazoona zitajenga ndoa yenu! Na yeye hatakuficha Jambo. Mtaweza kufanya Mambo mengi Sana bila jamii inayowazunguka kujua. Mfano unataka nunua kiwanja, nyumba, gari mshirikishe mkeo, atakuwa na msaada Sana kwako mbeleni kuliko mke anashtukia tu unamwambia twende site, au gari inaingia nyumbani ndo anajua mme wangu kanunua gari!
Yapo mengi ila kwa kuacha mke sababu ya kupika hovyo mh Kuna mengine nyuma ya pazia. Inaonekana hamna ukaribu kabisa yaani wewe ni wale wanaume wanaorudi nyumbani saa nne usiku ukishakula unapiga kabao kamoja ka kutimiza wajibu unakoroma weee mpaka asubuhi unawekewa maji unaoga, unaacha alfu 10 mezani ya msosi wa siku unaenda kazini kimyaaa hamna story ni ubaba tuu! Huku nyuma mkeo anapata tabu! Baba yangu alikuwa akikaa na Mama yaani full story baba anacheeeka mpaka tunaona mapengo yake yoote ambayo leo na mie nnayo hayo hayo dunia hiiii