Utaratibu wa kumhudumia mama baada ya kujifungua

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
2,002
5,534
mahandbaby.jpg

Kula na kunywa katika masaa machache za kwanza


Kina mama wengi huwa tayari kula mara baada ya kujifungua, na ni vizuri kwao kula aina yoyote ya lishe bora wanataka. Ikiwa mama ambaye anazaa mara ya kwanza hahisi njaa, angalau anapaswa kuwa na kitu cha kula. Maji ya matunda au chai atmit ni nzuri kwa sababu itawapa nguvu. Wanawake wengi hutaka kunywa kitu kilicho na joto, kama chai. Baadhi ya maji ya matunda, kama maji ya machungwa, pia huwa na vitamini C, ambayo inaweza kumsaidia kupata nafuu. (Lakini anapaswa kujiepusha na soda kama Coke, ambayo ina sukari nyingi na kemikali lakini haina lishe.)

Iwapo mama hawezi (au hataweza) kula au kunywa ndani ya saa tatu baada ya kuzaa:
  • Anaweza kuwa mgonjwa.
  • Anaweza kuwa na huzuni (anasikitika, hasira, au bila hisia zozote). Mshawishi aongee kuhusu hisia zake na mahitaji yake.
  • Anaweza kuamini kwamba baadhi ya vyakula ni vibaya kula baada ya kuzaa. Mweleze kwa upole kwamba lazima ale ili apate nafuu kutokana na kuzaa na kupata uwezo wa kumpa mtoto wake huduma bora.
Ushauri juu ya lishe baada ya kujifungua

Baada ya kujifungua, ulaji wa mara kwa mara inapaswa kuongezwa ili kurudisha nguvu ya kunyonyesha pamoja na nguvu na afya yake. Anapaswa kula takriban 10% zaidi kuliko kabla awe mjamzito ikiwa hana shughuli nyingi au anafanya kazi yake ya kawaida na takriban 20% zaidi kama yuko na uwezo. Katika hali halisi, anashauriwa kuchukua angalau mlo mmoja au miwili zaidi kila siku. Ushauri wa lishe bora ni pamoja na:

  • Kushauri mama kula baadhi ya vyakula vilivyo na protini, nishati ya juu (kama vile familia inaweza kumudu), kama vile nyama, maziwa, samaki, mafuta, karanga, mbegu, nafaka, maharagwe na jibini, ili awe na afya pamoja na nguvu.
  • Kuchunguza iwapo kuna miiko za kitamaduni ambazo ni muhimu kuhusu kula vyakula ambavyo ni lishe bora zaidi kiafya. Kwa mfano, katika baadhi ya tamaduni kula vyakula vilivyo na protini nyingi huchukuliwa vibaya, vyakula vilivyotiwa viungo, au vyakula baridi baada ya kuzaa. Mshauri kwa heshima dhidi ya miiko haya na hayapaswi kujizuia na chakula chochote chenye lishe bora.
  • Kuzungumza na wanafamilia, kuhakikisha kwamba mwanamke anakula vyakula vya aina mbalimbali vya kutosha na kujiepusha na kazi ngumu ya kimwili.

Kuzuia upungufu wa iodini
Kuongeza madini ya iodini kwa chumvi huitwa iodination na inapendekezwa utumie chumvi iliyo na iodini kwa upishi katika kipindi baada ya kuzaa, hasa katika maeneo ya nchi ambazo tezi ni ya kawaida kama matokeo ya madini ya iodini kidogo sana katika mlo. Uongezaji wa madini ya iodini kwa chumvi imeonekana kuwa njia yenye ufanisi mno ya kuzuia upungufu wa iodini. Kutumia mafuta yenye iodini kwa njia ya kunywa au kudungwa sindano inaweza kutumika kama hatua ya muda mfupi katika maeneo endemiki ambapo ni vigumu kupatikana kwa chumvi iliyo na iodini. Mshawishi mama atumie chumvi iliyo na iodini kila siku wakati wa kipindi baada ya kuzaa, kama inapatikana. Hata hivyo, kama tezi inapatikana hapo, mama anaweza kupewa dosi ya mafuta iliyo na iodini baada tu ya kuzaa.

Kuzuia upungufu wa vitamini A
Mshauri mama jinsi ya kuzuia upungufu wa vitamini A, ambayo si tishio tu kwa kuona kwake, lakini pia ni kisababishi kikubwa cha upofu utotoni mwa watoto walionyonyeswa na mama aliye na upungufu wa vitamini A. Vitamini A katika mlo huongezea kinga dhidi ya maambukizi na ni muhimu hasa kwa utengenezaji wa maziwa ya mama yaliyo na virutubishi.

Mboga zilizo na rangi ya manjano kama karoti, matunda ya njano kama maembe, na mboga yenye rangi ya kijani kibichi kama vile mchicha na kabichi huwa na vitamini A nyingi. Vile vile ini, mafuta ya samaki, maziwa, mayai, na siagi.


Kuzuia upungufu wa ioni na folate
Upungufu wa damu kutoka mwanzo inaweza kuchochewa na madhara ya kuvuja damu kwa mama na ni moja ya kisababishi kikubwa cha vifo vya wajawazito katika kipindi baada ya kuzaa. Shawishi kina mama kula vyakula vilivyo na madini ya ioni (kwa mfano, mboga zilizo na rangi ya kijani kibichi, maharagwe, mbaazi na dengu, kuku na nyama nyekundu, nyama ya ogani kama vile ini na figo, na bidhaa za nafaka nzima), na vyakula ambavyo huongeza ufyonzaji wa ioni (matunda na mboga zilizo na vitamini C).

Usaidizi wa kihisia kwa mama

Jambo la kwanza unahitaji kuhakikisha ni kwamba mama na mtoto hawajatengwa na wanafamilia wengine kwa sababu za kitamaduni. Inashauriwa mama kuwa kila siku awe karibu na mtu kwa masaa 24 ya kwanza. Pia inapaswa wanafamilia kuwasiliana mara kwa mara na mhudumu wa afya kila siku wakati wa wiki ya kwanza ili kuchukua hatua haraka iwapo ishara zozote hatari zitatokea katika hali yake.
family.jpg


Baba wa mtoto anapaswa kuwa karibu na mama angalau kwa wiki ya kwanza katika kipindi baada ya kujifungua ili ampatie usaidizi wa kihisia na kumtunza yeye na mtoto Katika mazingira ya Afrika, utunzaji wa mama kawaida ni wajibu wa nyanya na/au mama mkwe. Kwa vile tayari wamepitia haya, wako katika hali bora wa kumpatia usaidizi wa kimwili na kihisia kwa mama na mtoto wake. Wanaweza kumwondoa kutoka shughuli za nyumbani za kawaida, ambayo inahitaji kuhamashishwa.

Ikiwa mama hana haja na mtoto wake
Baadhi ya kina mama hawahisi vizuri kuhusu watoto wachanga. Kunaweza kuwa na sababu nyingi kwa hii. Mama anaweza kuwa amechoka sana, au ni mgonjwa au anatokwa na damu. Anaweza kuwa hakutaka mtoto, au kuwa na wasiwasi kwamba hawezi kumtunza ama anaweza kuwa anafadhaika sana. Ishara kama hizi ni kama mama anaonekana kuwa na huzuni, utulivu, na hana hamu ya kitu chochote. Pia chunguza ishara zingine za tabia isiyo kuwa ya kawaida ambayo ni tofauti na ile yake ya kawaida kwani inawezekana amepata kichaa baada ya kujifungua.
depression.jpg


Dalili za kichaa baada ya kujifungua

  • Kusikia sauti au mlio wakati hakuna mtu pale
  • Kuona mambo ambayo si ya kweli
  • Kuhisi kama mawazo yake si yake mwenyewe
  • Kuhisi uoga kuwa anaweza kujidhuru au mtoto wake
  • Kupoteza uzito kwa ghafula na kukataa kula
  • Kukosa usingizi kwa masaa 48 au zaidi
 
Back
Top Bottom