Ijue siri kuu ya mahusiano katika Ulimwengu wa Roho

Nyenyere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
14,243
10,090
Ndugu zangu, amni iwe nanyi,

Nimekuwa nikisema maandishi mbalimbali humu jamvini ambayo kwa baadhi yenu wamenichukulia kama adui wa wanawake na wengine kujifunza baadhi ya mambo ambayo yatakuwa msaada kwenye maisha yao.

Pia, katika mojawapo ya mada zangu niliwahi kusema kuwa nitaandika kwa habari ya agano la bikira na Agano la shahawa. Wengi waliomba niandike kwa habari hiyo, nami napenda kusema kuwa leo ndio siku iliyokubalika mbele za Mungu niseme kuhusu SIRI HII NZITO katika lugha nyepesi kueleweka na kila atakayesoma. Hivyo basi, tuwe tayari kujifunza MAMBO MAZITO ambayo huathiri maisha yetu ya kila siku.

Baada ya mada hii nitatafuta siku nami nitasema kwa habari ya KUPIGA PUNYETO kwenye ulimwengu wa roho na jinsi tendo hili linavyohusiana moja kwa moja na kukosa mafanikio ya kimwili na kiroho maishani. Naomba tualikane kwa wingi ili tujadili pasipo hasira tuweze kujinasua na kikosi ya kujitakia.

Amani iwe nanyi nyote
Amina.

***********************************
SEHEMU YA KWANZA
***********************************

Kwa vile wako waliojiandaa kupinga ninachoandika, basi na twende kwa ushahidi wa maandiko.

SEXUAL INTERCOURSE
Hili ni tendo la kubadilishana nguvu kati ya mwanamke na mwanamume. Kiasili mwanadamu kaumbwa akiwa na nguvu kuu mbili:

1. Emotional energy - nguvu za hisia
2. Reproductive energy - nguvu za uzazi

Emotional energy
Nguvu hizi hutoka kwa mwanamume na kumwingia mwanamke kuanzia wakati wa mahaba na hukamilika wakati wa kuingiliana. Mwanamume akimwingilia mwanamke huweka nguvu hizi ndani yake nazo hudumu humo. Mwanamke yeye hupokea na kuzihifadhi nguvu hizi na hivyo kuwa ndani yake kwenye nafsi. Hapo mwanamke na mwanamume huwa nafsi moja (wameunganisha nafsi zao kutengeneza nafsi moja).

Mwanzo 2
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
²³ Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.
²⁴ Kwa (sababu) hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja (watakuwa mtu mmoja).

** Adamu alianza kwa hisia dhidi ya Eva, akamwita mfupa katika mifupa yangu nk. Baada ya kutengeneza na kupeleka emotional energy ndipo tunaona sababu halisi ya ndoa:

Kuambatana na mke(to bond) sio kuhama kwenu, ni kuunganika kuwa kitu kimoja. Hili ni tendo la kiroho linalokamilishwa na kuingiliana kimwili. Hebu ona mfano huu:

Mwanzo 34

² Shekemu, mwana wa Hamori, Mhivi, mkuu wa nchi, akamwona (Dina) akamtwaa, akalala naye, akambikiri.

Huyu mwana mfalme alimwona binti wa Yakobo kwenye nchi yao, akamtamani, akaomba mchezo kisha akalala naye, akambikiri . Kilichotokea ni nini?

³ Moyo wake ukaambatana na Dina binti Yakobo, akampenda huyu msichana, akasema na huyu msichana kwa maneno mazuri.

** Aligundua kumbe binti ni bikira, ndipo moyo wake UKAAMBATANA naye (to bond) . Ndio maana Biblia inasema mwanamume atawaacha wazazi, yaani emotional energy zake atazigeuza na kuzielekeza kwa mkewe, sio kila mwanamke!! Hizo nguvu atazihifadhi ndani ya mwanamke kwa njia ya sex na kuleta muunganiko wa nafsi mbili kuwa kitu kimoja. Kumbe mwanamume wakati wa kujamiiana hutoa nafasi yake na kuiunganisha na nafsi ya mwanamke na kuihifadhi ndani ya mwanamke!!!

Tendo hili hufanywa katika ulimwengu wa roho, lakini katika mwili mwanamume humwaga shahawa na mwanamke hutoa damu ya bikrakama ushuhuda Kitendo cha kutoa bikra ni kuweka agano la ndoa katika ulimwengu wa roho huku MUNGU akiwa shahidi.

Kisha wakati wa tendo hili mwanamke hutoa majimaji yenye manukato ambayo humtambulisha katika ulimwengu wa roho kama wake. Ndio maana mwanamume akilala na mwanamke mwingine, pale arudipo kwa mkewe, mke hupata hisia kwamba amesalitiwa, sababu katika ulimwengu wa roho mwanamume atakuja na harufu tofauti na ile aliyopuliziwa na mkewe. Mwanamke hutambua hilo kabisa katika roho.

Kwa hiyo kiroho mwanamume huwa na muunganiko na mwanamke wa pili na kusababisha vita katika ulimwengu wa roho. Nafsi ya mke na nafsi ya mwanamke tofauti hupambana kutafuta umiliki wa huyu mwanaume. Ndipo matatizo ndani ya ndoa huanza. Kwa sababu mwanamume amekuwa na harufu tofauti ya manukato, mwanamke hukereheka kila waingilianapo, na ndipo nafsi yake hutafuta harufu nzuri kwingineko, nayo huja kwa jina la kulipiza kisasi. Ukweli ni kwamba tayari kuna mpasuko katika roho, hivyo furaha ya ndoa haipo tena. Kisasi hiki ni matokeo ya ugomvi kwenye ulimwengu wa roho.

Ni vema kufahamu kuwa nguvu ya hisia itokayo kwa mwanamume ni copy yake yeye mwenyewe!! Kwa hiyo kufanya mapenzi na mwanamke ni kuhifadhi kopi kwake inayoungana na mwanamke kufanya mwili mmoja. Mwanamke ataishi na hiyo nakala ambayo ni wewe maisha yake yote kama hatochukua hatua sahihi.

Reproductive energy

Hii ni nguvu kubwa kabisa kwa mwanadamu. Ni muhimu kufahamu kuwa mambo yote huanzia kwenye ulimwengu wa roho kisha hudhihirika katika mwili. Kwa hiyo, mwanamume humwaga shahawa kwa mwanamke ambaye naye hutoa maji maji na yai ili kukamilisha uumbaji. Shahawa na majimaji ya ukeni hutokana na nguvu ya hisia.

Agano la bikra

Emotional energy hufua nguvu hii katika ulimwengu wa roho kisha baada ya kuungana katika nafsi hudhihirisha matokeo kwenye mwili kwa kumwaga shahawa na kutoa majimaji. Ndio maana pasipo hisia hakuna mapenzi. Hili ni jibu pia kwa waliobakwa, utagundua kuwa hujeruhiwa Kwa sababau hakuna majimaji yaletwayo na emotion. Lakini tangu kale ilikuwa mwanamume akimbaka binti bikra amekuwa mke wake halali . Hata Mungu katika kumbukumbu la torati aliagiza mwanamume akimbaka bikra na amuoe!! Why? Kwa sababu amefunga agano la maisha (bikra) na binti huyo, tena hana ruhusa kumwacha.

Kumbuka kuwa yai atoalo mwanamke halina uhusiano na emotional energykwa sababu hata asipokuwa na hisia za mapenzi litatoka tu kwa majira yake. Kwa maana nyingine nguvu hii ya uumbaji hutokana na ulimwengu wa roho, hivyo tendo la ndoa sio la kimwili, bali mwili ni uthibitisho wa nje tu kwamba nafsi zimeungana. Wala sio kanisa au msikiti unaounganisha ndoa, bali ni Mungu mwenyewe kwa njia ya damu ya Agano amwagayo mwanamke, ambapo mwanamume huchinja mnyama wa sadaka (bikra) kisha hujinyunyiza damu hiyo uumeni na kumwaga nyingine kwenye madhabahu. Ushuhuda huu huonyeshwa kwa wazeewa mji kwamba agano la ndoa limefungwa. Kumbe kitendo cha mke na mume kuendelea kujamiiana ni kulifanya upya agano, renewing of the covenant, damu humwagika mara moja tu kwenye agano la maisha. Ndio agano la bikira hilo!!

Inaendelea.......


**************************************
SEHEMU YA PILI
**************************************

Mapenzi na wengi
Mwanamke akifanya mapenzi na wanaume wengi huhifadhi copy zao ndani yake. Hata pale ajapoolewa zitamsumbua sana, kwani mwanamume wa awali akitaka mchezo, kopi yake iliyo ndani ya mwanamke huamka na kuutiisha mwili. Hujikuta dhaifu mno asiyeweza kujizuia kuutoa mwili wa mumewe kwa mwanamume mwingine. Ukitaka kuamini hili ongea na mwanamke, pale aonapo picha ya mpenzi wake wa zamani, au akipigiwa naye simu asikiapo sauti, au wakikutana ghafla hata kama ni baada ya miaka mingi kupita, hisia za awali huamka ndani yake. Unahitaji juhudi ndogo tu kulala na mwanamke huyu tena kwa sababu tayari kuna kivuli chako moyoni mwake.

Sasa mfano binti asiyeolewa akifanya mapenzi kwa mara ya kwanza, huweka agano la maisha na huyo mwanamume. Ndio maana wanawake wengi wako radhi kumvulia nguo mwanamume aliyewatoa bikira wakati wowote akitaka mchezo, hata kama wameolewa. Huwa kama kondoo aliye machinjioni akisubiri kisu tu kipite shingoni. Nguvu ya agano la damu hutenda kazi.

Lakini binti huyu kadri anavyoendelea kutembea na wanaume mbalimbali hujiwekea ndani yake copy zao na kusababisha machafuko katika ulimwengu wa roho. Nafsi yake huwa na muunganiko na nafsi mbalimbali za wanaume, hivyo hata kama ataolewa, ni vigumu mno kwa mume wake kumtuliza nafsi mwanamke huyu, kwa sababu wameungana kimwili lakini kiroho sio mwili mmoja . Mwili mmoja ni pale nafsi mbili huru zinapoungana na kuwa nafsi moja. Ni vigumu sana kwa mwanamke huyu kudumu kwenye ndoa kwa sababu nafsi yake inaambatana na waume mbalimbali. Ni kwamba mwanamume mmoja kati ya wengi amejitwika mzigo wa kuuhifadhi mwili wa mwanamke huyu hali nafsi ikiwa na mafungamano mengi.

Mambo haya husababisha ndoa kuyumba na hivyo migogoro haitoisha kamwe. Tayari kuna muunganiko wa nafsi mbalimbali ambazo zina haki sawa ndani yenu. Ndio maana nasema ndoa sio jibu la mzinzi. Kwamba akioa au akiolewa ataacha!! Wala kwenda kanisani sio jibu hata kidogo. Kumbuka mwili ndio uendao kanisani, lakini roho yaweza kuwa mbali mno.

Hili pia ni jibu kwa wanawake wanaolalamika kuachwa na wanaume waliowatarajia kuwaoa. Mahusiano huwa matamu mpaka pale wanapofanya mapenzi, ndipo vurugu huanza, sababu tayari kuna muunganiko na wanaume wengine. Emotion energy za wanaume waliotangulia kuhifadhi ndani ya mwanamke zinapambana na energy ya mwanamume huyu mpya na kuvuruga mahusiano.

Siri ya mafanikio kwenye ndoa

Kuna wadau walianza kupinga hata kabla ya kusikia nini kinasemwa. Haya tuendelee...

Mungu alipowaumba Adamu na Eva aliwabariki kwa baraka ambazo NDIZO NGUVU za kuitawala dunia. Tusome:

Mwanzo 1

²⁷ Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
²⁸ Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.


** Hebu tuzitazame kwa kina hizi baraka:
1. Zaeni - tendo la ndoa
2. Mkaongezeke - tendo la ndoa
3. Mkaijaze nchi - tendo la ndoa
4. Na kuitiisha; kwamba mkisha tekeleza hayo mtaitiisha nchi,mtaitawala na kuwa himaya yenu. Zingatia hizi alama (;) kwamba maneno yanayofuata yanafafanua kuitiisha kwa jinsi gani. Kwa kutawala majini, angani na nchi kavu.

Hizo ndizo baraka alizopewa mwanadamu, lakini umegundua nini? Baraka hizo zimefungwa kwenye ndoa . Kwamba huwezi kuzaa ama kuongezeka pasipo tendo la ndoa. Hapo ndipo ilipo nguvu ya barakahizo.

Kumbukumbu la Torati 8
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹ Amri hii ninayokuamuru leo mtaishika kuitenda, mpate kuishi na kuongezeka, na kuingia katika nchiile ambayo Bwana aliwaapia baba zenu; nanyi mtaimiliki.


** Tazama kwa umakini, Mungu anarudia ahadi ile ile ya Adam na Eva kwa wana wa Israeli.

1. Mpate kuishi - tunatengeneza uhai kwa tendo la ndoa
2. Kuongezeka - kuijaza nchi
3. Kuingia katika nchi
4. Kuimiliki - kuitiisha

Kumbe kuishika amri ya Bwana kunapelekea baraka zake maishani mwetu. Tena mbele kidogo Tu aliendelea kuweka wazi:

⁷ Kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yuakuingiza katika nchi nzuri, nchi yenye vijito vya maji, na chemchemi, na visima, vibubujikavyo katika mabonde na milima;

** Hapo kuna maana nzito mno katika roho. Nikusihi weka akika neno hili nitalielezea hapo chini, lakini kwanza tuone hili:

¹⁷ Hapo usiseme moyoni mwako, Nguvu zangu na uwezo wa mkono wangu ndio ulionipatia utajiri huo.
¹⁸ Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lakealilowapa baba zako, kama hivi leo.


** Mungu ndiye atupaye nguvu za kupata utajiri. Waendao kwa wachawi hupata nguvu zao huko, kwa sababu hawaelewi zilipo nguvu za Mungu. Agano la Mungu ni kumrejeshea mwanadamu umiliki wa dunia, ilivyokuwa kwa Adamu na Eva. Nguvu ya agano hili imo katika emotions. Kama vile Adamu alivyofunga agano hili kwa kutoa bikra ya Eva, ndivyo mwanamume anavyofunga aganohili kwa kutoa bikra ya binti.

Sasa tuangalie kuhusu hiyo aya tuliyoiacha hapo juu:

⁷ Kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yuakuingiza katika nchi nzuri, nchi yenye vijito vya maji, na chemchemi, na visima, vibubujikavyo katika mabonde na milima;

Aya hii (vijito, chemchemi, visima) imeelezewa vema hapa:

[Mithali 5[/B]
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁵ Unywe maji ya birika lako mwenyewe, Na maji yenye kububujika katika kisima chako.


** Hapa moyo wa mwanamke umefananishwa na birika, au tanki (cistern), ambamo mwanamume huhifadhi nguvu zake za hisia (emotional energy). Halafu tena sehemu zake za siri zimefahamishwa na kisima kinachobubujisha maji ambamo mwanamume humwaga mbegu zake humo na kuburudika.

Kwa hiyo, mwanamume anapaswa kunywa maji aliyohifadhi mwenyewe ndani ya birika ambalo ni mwanamke (emotions). Hii ni nguvu aiwekayo mwanamume ndani ya mwanamke. Kumbe mwanamke humpenda mume kwa kadri anavyokeza ndani yake hisia zake. Lugha nyepesi, utavuna ulichopanda. Mwanamke pia HATAKIWI KATU kuingiza nguvu nyingine tofauti na mumewe, kwani kufanya hivyo ni kuleta vurugu katika roho. Biblia inamwasa mwanamume kuwa anywe maji ya birika lake mwenyewe , sio kwenye birika la jumuiya. Kwamba mtu ambaye ameshaitoa nafsi yake kwa wanaume wengine, wakaweka hisia zao ndani yake, wakamwacha. Ndio maana wanawake wengi hutembea na majeraha ya kuachwa na wapenzi wao wa kale, kisha huingia kwenye mahusiano mapya wakiwa na SURA ZA WANAUME waliowajeruhi. Ndizo hadithi za wanaume wote wako hivyo.

Kisha mwanamume na anywe maji kutoka kisima (sehemu za siri)chake tu, yaani kujamiiana na mkewe tu. Katika nguvu za hisia, anywe katika birika alilojaza, kimwili sasa anywe katika kisima chake tu. Kutembea na wanawake wengi ni kutawanya nguvu zako hovyo, hivyo utapata taabu sana maishani, labda ujisalimishe kwa shetani full time. Kumbuka hizi ndizo nguvu zikupazo KUMILIKI juu ya nchi, hivyo ukizitumia hovyo huwezi kamwe kumiliki kwa mpango wa Mungu.

¹⁶ Je! Chemchemi zako zitawanyike mbali, Na mito ya maji katika njia kuu (Street)?
¹⁷ Yawe yako mwenyewe peke yako, Wala si ya wageni pamoja nawe.


** Chemchemi ni nguvu ya hisia ndani ya mwanaume. Chemchemi haipaswi kukauka, nayo hutoa maji na kujaza kwenye birika lake (mke) daima. Kumbukumbu kumbuka chemchemi hapa ni FOUNTAIN, yaani yale mapambano ya mji yanayotoa maji kisha kumwaga kisimani na kurudi tena. Mfano kwenye jengo kubwa nje wameweka sanamu la samaki akitoa maji mdomoni kisha yakamwagika bwawani alipo samaki huyo kufanya pambo zuri. Hiyo ndio fountain au chemchemi inayosemwa hapa. Kwamba mwanamume anatoa emotional energy kama maji hayo nayo yanahifadhiwa kwa mkewe, kisha hurudi kwake tena na mzunguko huendelea. Fountain haimwagi maji hovyo mtaani, kwani ni yake tu na bwawa (birika) lake (mke).

“Should your fountains be dispersed abroad, Streams of water in the streets?”
— Prov 5:16


Mito ya maji ni shahawa ambazo hutoka kama uthibitisho wa hisia katika mwili. Huwezi kumwaga maji kwenye njia kuu (street - kjv) kila mtu anapita anajisevia tu. Yaani wewe unagawa nguvu zako hovyo kwa wanawake wageni wanaopita mtaani?

Sasa ni makosa kutoa hisia zako kwa wanawake wa mbali nawe zaidi ya mkeo. Tena usiruhusu kumwaga shahawa zako hovyo kwa uzinzi kwani ni nguvu zako mwenyewe, zihifadhi mahali ambapo utakuwa ukizichota tena na tena ili kupata nguvu zaidi. Tena mkiunganisha nguvu zako za chemchemi na nguvu za kisima cha mkeo kuimiliki nchi.

¹⁸ Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe umfurahie mke wa ujana wako.
¹⁹ Ni ayala apendaye na paa apendezaye; Maziwa yake yakutoshe sikuzote; Na kwa upendo wake ushangilie daima
.

** Hapo ndipo zilipo baraka za Mungu, kwenye chemchemi yako. Ndipo zilipo nguvu zako kutoka kwa Mungu zikupazo utajiri. Ni hapo palipo na furaha ya mke wa ujana (bikra) kwa sababu ni mke wa agano lako.

Inaendelea........ View attachment 1531300**************************************
SEHEMU YA TATU
**************************************

Malaki 2
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁴ Lakini ninyi mwasema, Ni kwa sababu gani? Ni kwa sababu Bwana amekuwa shahidi kati ya wewe na mke wa ujana wako, uliyemtenda mambo ya hiana, angawa yeye ni mwenzako, na mke wa agano lako.
¹⁵ Hakuna mtu mmoja aliyetenda hivi, ambaye alikuwa na ufahamu kidogo. Au je! Kuna mtu mmoja atafutaye mzao mwenye kumcha Mungu? Kwa hiyo jihadharini roho zenu; mtu awaye yote asimtende mke wa ujana wake mambo ya hiana.
¹⁶ Maana mimi nakuchukia kuachana, asema Bwana, Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake kwa udhalimu namchukia, asema Bwana wa majeshi; basi jihadharini roho zenu, msije mkatenda kwa hiana.


** Ukimtenda bila uaminifu mkeo basi elewa unajifungia baraka za Mungu juu yako. Ukiwa mchepukaji Mungu hawezi kamwe kukusikiliza ukimwomba kwa sababu analikumbuka agano lako kwa mkeo. Tena mara mbili Mungu anasisitiza JIHADHARI ROHO ZENU, kwa maana mambo yote huanzia rohoni kisha tunayatimiza katika mwili. Mungu amekupa NGUO SAFI isiyo mawaa, mke wa ujana wako, kisha wewe unaichafua kwa udhalimu, kwa kumtenda vibaya mkeo, Mungu asema wazi kuwa anakuchukia!! Mtu awaye yote asimtende mkewe kwa hiyana (treacherously).

1 Petro 3

⁷ Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.


** Hapa wengi wamepatumia kama silaha ya kuwachapia wanawake. Lakini ni nini hasa kusudi la aya hii?

Wanaume ishini na wake zenu kwa BUSARA (according to knowledge). Sio hii tusemayo akili mkichwa, ama umfiche mkeo mambo yako, si kweli kabisa. Tena aya inasema UKIMPA HESHIMA(honour). Hii ni heshima itokayo kwa Mungu ambayo ndiyo iliyobeba BARAKA ZENU:

1 Mambo ya Nyakati 29

¹² Utajiri na heshima hutoka kwako wewe, nawe watawala juu ya vyote; na mkononi mwako mna uweza na nguvu; tena mkononi mwako mna kuwatukuza na kuwawezesha wote.


** Kwa hiyo hii ni heshima ya kiungu ya kumtendea mke kwa kadri ya Agano la ndoa. Kwamba usiwe na mafungamano ya nafsi na wanawake wengine, kwanini? Kwa sababu mwanamke ni KAMA CHOMBO (kilicho baharini) KISICHO NA NGUVU (a WEAKER vessel), hakiwezi kuhimili dhoruba kubwa, hatimaye husombwa na upepo kokote uendako.

Mfano: mume ni kama boti yenye injini na mke ni kama mtumbwi wenye injini. Pamoja na kuwa vyote vina injini, uwezo wa kuhimili dhoruba umetofautiana. Lakini kwa kuwa mnakuwa safari moja mkienda kituo kimoja (mmekuwa nafsi moja) mnaamua kuungana, boti ikivuta mtumbwi (miili yenu ni kama boti na mtumbwi). Sasa ikitokea mume kutaka kufanya mambo binafsi, itambidi kufungua mtumbwi na kuendesha boti kwenda atakako. Wakati huo mtumbwi utakuwa peke yake katikati ya bahari. Ni heri kama bahari haitochafuka , iendelee kuwa na mawimbi madogo madogo ambayo mtumbwi unaweza kuyahimili. Lakini kama ikitokea dhoruba basi ni rahisi sana kutwaliwa na mawimbi na kusombwa kokote kule. Ndiyo ilivyo kwa mke pia akiamua kuwa na mambo binafsi.

Kama utamletea dhoruba mkeo ndani, aweza kushindwa kuhimili na hivyo akasombwa na ushauri wa mashoga zake, au akapitiwa na wanaume waviziaji nk. Ieleweke kwamba sisi sote mume na mke ni wadhaifu, ila mwanamke ni dhaifu zaidi (weaker). Unapofanya uzinzi unaleta mkanganyiko katika ulimwengu wa roho, unafungua vifungo vya ndoa, hivyo kunapelekea mke naye sababu ya UDHAIFU WAKE kujikuta akitii mwili na kwenda kuzini nje.

Si hilo tu, ukimtendea mambo yasiyofaa, ni rahisi mno kwa mwanamke kuanguka majaribuni kwa sababu uimara wake unategemea sana wewe umemweka vipi rohoni mwako. Je, ni nafsi moja nawe, au ni kama kijakazi wako? Ni jukumu lako kama mume kuziba hilo gap la udhaifu kwa kumjaza emotions katika birika lake ndipo utavuna matunda yako.

Hivyo basi, ili kuona matokeo chanya ya maombi yenu, ni lazima MUWE NA NIA MOJA, mkiongozwa na dhamira safi. Sio habari ya kuvumiliana tu, ni lazima muwe na roho safi msio na lawama mbele za Mungu, hapo ombeni lolote kwa jina la Yesu, Mungu atajibu. Ni ajabu watu wanapenda tu kupatana na washitaki wao ili wakatoe sadaka, huku wakisahau kuwa WAKE ZAO NDIO WASHTAKI NAMBARI MOJA . Hawapatani na wake zao bali hukimbilia kupatana na marafiki na watu wengine, wanawadharau wake zao waliobeba baraka zao. Kwa jinsi hii maombi mengi mno yamezuiliwa sio na Mungu, bali na mke ama mume. Wamekuwa mwili mmoja lakini wenye nia tofauti, mke ana kinyongo, mume anadharau, kisha wanamlilia Mungu awape baraka. Mungu huitazama ndoa kama nafsi moja ndani ya miili miwili, hivyo iweni wenye nia moja. Inawezakana vipi?

Msitafute kuridhishana ninyi kwa ninyi bali tafuteni kumridhisha Mungu !! Maisha yenu yawe kwa kusudi la kumpendeza Mungu, hiyo ndio iwe nia yenu, nanyi hamtopishana katika jambo lolote. Ukichunguza kwa makini, migogoro yote ni juu ya mambo ya kidunia lakini Mungu ni Yeye yule. Mfano wakati mke anataka kujenga kwanza, mume anataka gari la kurahisisha mizunguko. Lakini wote hawatofautiani kuhusu Mungu. Hata migogoro ya kidini ni mambo ya namna hiyo, wengine wanasema Mungu anaponya, wengine wanasema haponyi, wengine wanasema Mungu anaishi mbinguni wengine wanasema yupo hapa hapa duniani nk. Lakini Mungu ni Yeye yule na Neno lake ni AMINI.

Tena hapa tunazidi kuona heshima ipi anayostahili mke wa ndoa? Hebu soma hapa ili usijezuiliwa maombi yako tena:

Mithali 5

³ Maana midomo ya malayahudondoza asali, Na kinywa chake ni laini kuliko mafuta;
⁴ Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga; Ni mkali kama upanga wa makali kuwili.


⁸ Itenge njia yako mbali naye, Wala usiukaribie mlango wa nyumba yake.
Usije ukawapa wengine heshima yako, Na wakorofi miaka yako;


** Epuka kabisa kucheza na malaya, ukatoa heshima anayostahili mkeo kwa kahaba. Mpe heshima yako mkeo tu (emotion & reproductive energy). Hii ndiyo heshima inayosemwa hapa, sio kumwita honey, baby, mrembo, barafu wa moyo nk. huku ukiishi katika uzinzi. Mpe NGUVU ZAKO kwani yeye ni hazina yako, nawe ujapompa hutapungukiwa kamwe, bali zitakurudia wakati wa uhitaji. Kiendacho kwa kahaba hakurudi, hicho hupotea milele.

Itaendelea............

¹⁰ Wageni wasije wakashiba nguvu zako; Kazi zako zikawa ndani ya nyumba ya mgeni;
¹¹ Nawe ukaziombolea siku zako za mwisho, Nyama yako na mwili wako utakapoangamia;
¹² Ukasema, Jinsi nilivyochukia maonyo, Na moyo wangu ukadharau kukemewa;


** Usiwape wanawake wageni nguvu zako, emotins, wasijekufanya mateka wakajinufaisha kwa nguvu zako. Wanawake hawa ndio waendao kwa waganga kusudi kuwanasa wanaume wapumbavu, kisha huzichukua nguvu zao za kiroho na kuzitumia kujinufaisha wenyewe. Kama huamini tazama jinsi wanavyochukua shahawa za mwanamume mzinifu na kuzipeleka kwa waganga, kwani hapo mganga huipata nafsi ya huyu mjinga. Kisha humfanya mateka. Ndoa ya mwanamume huyu hugeuka kaa la moto kwa sababu sorce ya ndoa (nafsi) iko mateka, mkewe hubaki kutapatapa asijue la kufanya.

Itaendelea......


*************************
SEHEMU YA NNE
*************************

NGUVU YA SOULTIE (si wawili tena)

Mke na mume wakiwa sawa mbele za Mungu, muunganiko wao hutengeneza nafsi moja. Kwa hiyo mbele za Mungu kila jambo linalofanywa na mkono wa kushoto ni lilelile linalokubalika na mkono wa kulia. Huwezi kusema mkono wa kushoto unataka kufungua mlango huku mkono wa kulia unapinga. Sababu ni kuwa viungo vyote source yake ni moja tu, ila tofauti ni uwezo wa majukumu. Mwingine atasema mkono wake wa kushoto una nguvu, mwingine atasema mkono wa kulia, lakini mwili ni mmoja.

Anayeamrisha mkono wa kulia ndiye huyo huyo anayeamrisha mkono wa kushoto. Kwa hiyo, nafsi inayomwongoza mke ndio hiyo hiyo inayomwongoza mume. Tofauti na aina ya majukumu na si kukinzana kwa amri. Sasa kama ndivyo, wawezaje mkono kupeleka maombi yake kwa siri kwenye ubongo pasipo mkono wa kulia kufahamu? Ndivyo ilivyo kwa mke na mume. Mke awezaje kumlilia Mwenyezi Mungu pasipo mume kujua? Mume naye awezaje ikiwa nafsi yao ni moja? Ndio maana tunaongelea KUWA NA NIA MOJA ili kuweza kupeleka hoja za nguvu.

Mke na mume wakishibana mmoja akipata tatizo, wote wanaumia, mmoja akiugua wote huwa wagonjwa, mke akipata mimba mume anapata kichefuchefu nk. Hiyo ndio nguvu ya soul tie.

Nguvu ya tendo la ndoa

Tendo la ndoa ni muunganiko wa mwili na roho kati ya mke na mume ambao tayari ni nafsi moja. Hili ni tendo la kukumbuka tukio la uumbaji ambapo Mungu aliumba mtu mume akampulizia roho moja ambayo ilikuwa ni Adam na Hawa. Baada ya kuwatenganisha ndipo tukawa mwanamke na mwanamume tofauti. Sasa roho ya mke hutafuta kuirudia roho ya mwanamke ili kukamilisha nafsi. Hili ni somo zuri sana ambalo huweka wazi namna Mungu alivyofanya uumbaji wake na kujua asili ya mvutano wa kimapenzi. Tuendelee na mada....

Umewahi kujiuliza ni kwa vipi binti akampenda mvulana kiasi hata wazazi wakiingilia kati kuwatenganisha hutishia kujidhuru? Wengi wanasema binti ama mvulana kachanganywa na mapenzi. Ukweli ni kuwa kuna jambo lililofanyika katika ulimwengu wa roho. Kama sio ushirikina umetumika kuiteka nafsi, basi ni soul tie. Ndipo wanaume wengine hutamba kabisa, huyu binti hata akija kuolewa hana ujanja juu yangu, nitalala naye kila ninapotaka, halafu kweli inakuwa hivyo!! Hawa wanaweza kutengana kadri wanavyozidi kuingiza nafsi nyingine ndani, kisha mahaba haya hubaki kama kumbukumbu nzuri akilini mwao (wanajenga hali ya emotional blur).

Je umewahi kuona mwanamume, kwa sababu ya wingi wa mali zake akaamua kupora mpenzi wa mtu mwingine na kumfanya mke? Huyu ni mjinga kabisa asiyeelewa ni jinsi gani utajiri wake utatumika kumlea huyu kijana mwenye soul tie!! Kile kivuli kilichomo ndani ya mwanamke huyu kitakuwa kikiamka mara kwa mara na kumwamuru asimzuie kitu mwenza wake (aliye rohoni). Mume bandia hugeuka mshika mapembe huku maziwa akifaidi mwingine. Nguvu ya soul tie hupofusha hata mke yuko tayari kuvunja ndoa yake na kuharibu maisha mazuri anayoishi na mume bandia kwa sababu ya msela mmoja!! Hiyo ndiyo soul tie, jihadhari usijeingia kwenye mtego huo hatari!!

Hatari ya soul tie

Sasa hakuna jema lisilo na madhara. Tayari tushaona jinsi gani muunganiko huu unaweza kupelekea hata ndoa kuyumba. Lakini si hayo tu, soul tie ni nguvu ya hatari pia kama wapenzi wawili hawatakuwa na kujizuia.

Mwanamke ndiye aliyebeba sura yote ya mwanamume ndani yake, hivyo aweza kutumia mwanya huo kumuumiza mwanamume. Mfano mwanamke aweza kujiapiza kuwa, kama umeingiza tupu yako ndani yangu, ukakojoa humu, basi hutokuwa na amani hata ukipata mwanamke mwingine yeyote. Mwanamke huyu kama kweli ulimkuta katika ujana wake akakushiba, basi mwanamume utaishi kwa kutangatanga bila malengo. Utashangaa haudumu na mwanamke yeyote yule.

Au umewahi kusikia wazazi hulaani? Basi jambo hili wengine huliona kama masimulizi lakini lipo kabisa!! Mama anapokubeba tumboni mwake miezi tisa akakuzaa, basi ujue kivuli chako hubaki ndani yake. Ndio maana mtoto hata awe mvuta bangi, jambazi sugu, teja nk kwa mama atabaki kuwa MTOTO BORA kabisa. Akiwekwa ndani mama atampigania atoke, akiwa na shida yoyote mama aweza kugombana na ndugu wengine ili wamsaidie. Ndio maana ni kutokuwa na maarifa kuanzisha biashara changa halafu ukaweka ndugu zako wa damu waisimamie, kwani siku wakiihujumu, ukawapeleka polisi ili warejeshe walichoiba, mama huapa kutembea uchi kama hujawatoa. SOUL TIE!!!

“Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye; Bali mwana mpumbavu ni mzigo wa mamaye.

Mithali 10:1


Baba husimama na mwana mwenye hekima, kwa sababu ndio sifa yake. Hana mambo ya soul tie na watoto, lakini mtoto akiwa mpumbavu tu, baba hajishughulishi naye katu. Mama ndio ataanza kuhangaika mara polisi, mara kwa mjumbe nk.

Sasa mama ili amlaani mwanae huvua nguo na kubaki utupu, kisha humwonyesha uchi wake huku akimwapia, mfano, kama nilikubeba tumboni mwangu miezi tisa, nikashikwa uchungu nikakunya, ukapitia hapa kwenye uchi wangu,....... Hapo mama anaamuru kivuli cha mtoto kilichobaki tumboni mwake ambacho ndicho huleta muunganiko na mwanaye. Jambo hili hutimilika kabisa, hasa kama umemtendea jambo baya na kumsononesha.

Itoshe sasa kusema kuwa, iko sababu kwa nini sio vema hata kidogo kuoa/kuolewa kwenye familia ambayo mama ndio kila kitu. Watoto huwa na muunganiko wa hatari na mama yao, kiasi kwamba lazima atayumbisha ndoa za wanaye vibaya sana!

Kwa upande wa wanaume, hicho kitu ni nadra sana, kwani mtoto wa kike akiwa karibu mno na baba, hata jamii hutilia shaka kwamba huenda ni wapenzi. Lakini hata wakiwa karibu sana basi sio rahisi baba kuingilia ndoa za wanaye, hii ni sekta ya wamama. Mara nyingi ukiona baba anaingilia kati ugomvi wa kawaida tu baina ya binti na mumewe huwa kuna shaka huenda aliwahi kumwingilia akaweka nafsi yake humo. Yaani mpaka binti anageuka agent wa baba kwamba kila mkipishana kauli kidogo tu anampigia simu, na baba naye anakuja kufoka na kutoa vitisho vingi kwa mume. Vinginevyo itakuwa ni kiburi cha nje kama utajiri, kazi nzuri aliyonayo, nafasi yaje serikalini nk.

Kwa upande wa watoto wa kiume, mara baba huwa anasimama upande wa muolewaji, na hii ndio hekima. Ni aibu kubwa kukuta baba na mwana wanamchangia binti mwolewaji kumshambulia kwa matusi. Lakini ni jambo la kawaida mama na Mwana kumvaa binti kwa na sababu kubwa ni mama kuwa rubani wa familia na hivyo watoto wamelelewa hivyo. Mtoto aliyelelewa vyema, hata kama mke amekosea vipi hawezi kamwe kusimama na mama yake wakimtukana na kumpiga. Mwanamume huyu atafanya kila linalowezekana kumtuliza mama kisha atatafuta jinsi ya kusuluhisha mambo. Soul tie inamfanya mama aamini kuwa ana haki ya kuendesha maisha ya wanaye pia na watoto nao wanaamini mama ana wajibu huo!!

Kuishi kama mapepo

Kwa kawaida mapepo huzunguka huku na kule na kukivaa chochote kilichotoa nafasi. Ndivyo alivyo mwanamume ambaye anatembea na wanawake mbalimbali na kuwatenda na kuondoka. Atajiona anaishi sawa lakini kwa sababu ya laana ya wadada aliowaumiza, mambo mengi yatakuwa yanavurugika yakikaribia kufanikiwa. Atakuwa hana kituo maalum, hata wakati akiona mambo yanakaribia kuwa safi ghafla yanaharibika.

Mbaya zaidi ni pale mtu anapofungamana na pepo (spirit). Mfano jini mahaba, haya humvaa mtu mzinzi ama aliyeacha roho yake isiwe na kinga yoyote na kisha kufunga naye soul tie kiasi kwamba hakuna jambo atakalofanya litafanikiwa bila kuliomba na kulitolea kafara. Mwanamke ama mwanamume mwenye pepo wa ngono hawawezi kuwa na ndoa imara. Hata wakifunga ndoa hazidumu, ama waweza kufunga ndoa ikawa kila mimba inaharibika, maana yake yanachukua hizo mimba. Soul tie na mapepo ni hatari zaidi.

Itaendelea........ [/B][/B]

Mahusiano kati ya watoto na wazazi

Baba ana uhusiano wa mwalimu na mwanafunzi kwa watoto wake. Anawafunza na kuwatiisha pale wanapokosa utii. Ndio maana ni rahisi tu kwake kushika bakora kumuadibisha mtoto. Mahusiano ya mtoto na baba hupitia kwa mama kwani ndiko kumehifadhiwa kivuli cha baba na mtoto pia. Mama akisema kwa baba ni rahisi kueleweka na pia akimwambia kitu mtoto ataeleweka kiurahisi. Sasa uelewe ni kwa nini mtoto anaumia sana mama akiteseka kuliko ilivyo kwa baba. Mtoto atakufa kwa ajili ya mama, mama naye kwa ajili ya mtoto. Kwa hiyo kiunganishi kati ya baba na mtoto kiroho ni mama.

Mama yeye anawabeba wote, baba na mtoto. Ndio maana mke hawezi kuona mume ana tatizo akatulia, yuko radhi hata kutumia mali za kwao kutatua tatizo hilo. Hapa ndipo wengi hudhani mwanamke ni mjinga, si kweli. Mwanamke ni emotional being. Mume akimjaza mke emotional energy basi atamtumia huyo atakavyo. Kilicho cha mwanamke ni chake pia. Hapa ndipo wanaume walioharibika akili hutumia kuwaingiza hata wanawake wenye kuwa na msimamo kwenye mambo ya hivyo kama uvutaji bangi, ulevi, mapenzi kinyume na maumbile nk. Mwanamke atafanya kumfurahisha mume, lakini ukweli ni kwamba anaifurahisha nafsi yake mwenyewe kws saba wamekuwa nafsi moja!!

Watoto wa kambo

Nadhani iko wazi sasa, baba hana shida kwa mtoto wa kambo kama ilivyo kwa mtoto wake mwenyewe. Akioa mke mwenye mtoto, ujue tu kwamba KAOA MKE. Ameungana na mke, hivyo kivuli chake hutembea humo. Mapenzi kwa mtoto wa kambo yatatokana na emotional energy iliyo ndani ya mwanamke. Hivyo ana nafasi ya kumtendea mtoto wa kambo kama vile ni mtoto wa viuno vyake mwenyewe.

Mama kwake ni tofauti kabisa. Hana connection yoyote na mtoto wa kambo. Ndio maana asilimia kubwa ya wanawake huwatendea kwa ukatili watoto wa kambo. Watoto hawa huwa na muunganiko na mama zao wa kuwazaa, hivyo baba ni kama mlezi tu sawasawa na mama wa kambo. Ukiona mama wa kambo anamlea vema mtoto, basi ujue alikuwa katika maadili bora kabisa au hofu ya Mungu imo ndani yake. Lakini pia kama amempenda kweli mume wake, emotional energy yaweza kumfanya ampende mtoto pia, ingawa hili ni mara chache sana.

*********************
SEHEMU YA TANO
*********************

UFANYE NINININI

Ni kweli kabisa kwamba hakuna aliye mkamilifu kati yetu wanadamu. Sote kila wakati tunaingia dhambini. Wako ambao wakiona neno dhambi wanawaza dini tu, lakini dhambi ni nini?

“Whosoever committeth sin transgresseth also the law: for sin is the transgression of the law.
1 John 3:4


Kwa hiyo, uasi dhidi ya sheria ndio maana ya dhambi. Mungu alipoiumba dunia, aliweka na sheria zake, lakini kwa sababu ya uasi dhambi iliingia duniani. Kwa hiyo wanadamu wote hujikuta tukitenda dhambi ama kwa kujua ama kwa kutokujua.

Mpango wa Mungu ni mwanamume na mwanamke waingiliane wakiwa ni wanandoa, sio nje ya hapo. Lakini kwa sababu ya mazingira, wakati mwingine tunajikuta tumeingia kwenye tendo la ndoa nje ya ndoa. Biblia inasema hivi:

1 Yohana 3
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁴ Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi.
⁵ Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake.
⁶ Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua.


⁸ atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi
.

Yesu Kristo alikuja ili kuikabili nguvu ya dhambi ambayo msingi wake mkuu ni ulimwengu wa roho. Hivyo basi hata vifungo vya kiroho vinafunguliwa katika yeye. Damu yake hubatilisha maagano yote, kwa vile nguvu yake ni katika roho.

Ili kujitoa katika mtego huu mbaya, yakupasa kumkiri yeye kuwa ndiye pekee awezaye kukufungua na kukusafisha kabisa uwe mpya. Ndio maana Biblia inasema:

Yohana 8
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
³² tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.


³⁶ Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.


Mtaifahamu kweli, kweli gani? Kweli ni lile kusudi la Mungu kwa mwanadamu. Yale maisha aliyoikusudia aishi siku zake hapa duniani. Kwa hiyo mpango wa Mungu ni mtu awe na mke wake mmoja tu na asitembee nje ya ndoa ili nguvu yao ya uumbaji izunguke kati yao na hivyo waweze kuitawala na kuitiisha dunia.

Unapoijua kweli hii, ni jukumu lako kuchukua hatua ili kumpa nafasi Kristo aingie ndani yako na kuzivunjavunja nira za shetani ili uwe huru kweli kweli.

Mwanadamu ni kiumbe cha kiroho

Tangu kuumbwa kwake mwanadamu ni roho iliyovikwa mwili. Ndio maana ni makosa kuruhu kuongozwa tokea nje. Kufanya hivyo kunaua nguvu ya roho na ndio chanzo cha kuingizwa kwenye utumwa. Unapotazama mwanamke ukamtamani, maana yake umekubali kuongozwa na matukio,mambo ya nje, yanaulisha moyo wako. Ukioewa rushwa ukapokea maana yake tukio la nje limekuwa na nguvu kuliko roho yako. Ukivutiwa na fuesta maana yake umeyahesabu matendo hayo kuwa ni yenye faida kwako, lakini jiulize,roho yako inanufaika na nini? Yote hayo ni matendo ya mwili ambayo huichafua roho. Sasa kama wewe ni kiumbe wa kiroho,wawezaje kuvipiga vita vya kiroho iwapo mwili wako hauko kwenye msimamo mmoja na roho yako?

Tena twajua kuwa Munguni Roho, hivyo imetupasa kumtafuta katika roho ili tuyashinde ya rohoni. Kumbe ili kutoka kwenye vofungo hivi, mwanamke au mwanaume yampasa kuifufua roho yake ambayo imekufa kwa sababu ya tamaa za mwili. Sasa roho yako haifufuki kwa kuwekea mikono, bali ni kwa kuamini pasipo shaka kwamba Kristo aweza kukutoa huko. Ukishaamini, jutia makosa hayo, raha moyo wako, lia machozi ya uchungu mbele za Mungu. Hakika atakusikia.

Hizo ni hatua za awali, hatua kubwa kabisa, funga na kuomba. Hatua hii inapofanywa kwa dhamiri safi ndiyo bomu la kiatomiki. Hakuna uchawi au nguvu za giza zitasimama mbele yako. HILI NI DHAHIRI KABISA. Tatizo hapa kuna watu hushinda na njaa wakaita funga.

Mathayo 12

²⁹ Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake.


Kusudi la kufunga ni kuua mwili ili roho iinuke na kuchukua uongozi. Nguvu ya mwili ni chakula, ndio maanabaada ya shibe, mawazo ya anasa huinuka kwa nguvu. Ukiunyima mwili chakula kwa muda, nguvu ya dhambi huondoka kabisa. Roho ikiinua Mungu anaingia kusafisha yote na kukuweka huru kabisa. Kufunga ni kutangaza kifo, kwamba unakufa katika dunia na kufufuka ufalme wa Mungu. Unajua mwili ili kuruhusu roho ikuongoze, nayo sio roho yako tena, bali Roho Mtakatifu huchukua nafasi na kuanza kukuongoza.

Mungu anaongea hata sasa. Nimepingwa na wadau wengu sana humu kuhusu hili, lakini itoshe tu kusema,haya sasa Mungu anasema nami kwa njia mbili, kupitia Mwana (mafunuo ya neno lake) na kupitia ndoto na maono. Haya yamekuwa maisha yangu ya kila siku kadri anavyoona inanifaa.

Zaburi 25

⁶ Ee Bwana, kumbuka rehema zako na fadhili zako, Maana zimekuwako tokea zamani.
Usiyakumbuke makosa ya ujana wangu, Wala maasi yangu,. Unikumbuke kwa kadiri ya fadhili zako, Ee Bwana kwa ajili ya wema wako
.

Mungu ni mwenye rehema, ukimtumainia atafuya makosa yako wala hawezi kuzikumbuka dhambi za UJANA wako. Wewe omba neema iliyokuja na Kristo ikufunike na damu yakeikusafishe kabisa.

¹² Ni nani amchaye Bwana? Atamfundisha katika njia anayoichagua.
¹³ Nafsi yake itakaa hali ya kufanikiwa; Wazao wake watairithi nchi.
¹⁴ Siri ya Bwana iko kwao wamchao, Naye atawajulisha agano lake.


Wako ambao hata wakifunga hawajui waombe nini. Ni kupoteza muda bure pale unapofunga halafu unakaa kwenye tv kuwatazama isidingo au kina bongo muvi wakisifia ngono na upuuzi kama huo. Tumia muda wako kusoma neno la Mungu na kuomba. Kama hujui jinsi ya kuomba fungua vitabu vya zaburi, mfano Zaburi ya 20, 21, 25 ni sala nzuri sana. Ukisoma kwa kumaanisha Mungu atakuonekania na nira zako zikaanguka mara.

Baada ya hayo, kama huna ndoa, ACHA MTEGO WA KUZUNGUKA MAKANISANI kutafuta ndoa. Ujinga wa kwenda kwa mhubiri kisa katangaza eti kama umetafuta mume ukakosa, utafungamanishwa na mapepo. Dumu katika kuomba na kufunga mara kwa mara huku ukiulisha moyo wako kweli yake. Kwa majira yake atakuinulia mtu akufaaye, tena Mungu hakawii. Atakujibu kwa ndoto nawe utamshangaa Mungu. Kuchukua hatua kama inavyoitwa siku hizi, ukijaribu kujilengesha, ni kiashiria mojawapo kuwa humwamini Mungu. Sasa hapo ndipo penye subira ya watakatifu. Pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu. Tena kumbuka mambo yote huanza katika ulimwengu wa roho kisha yakadhihirika katika mwili. Ukianza kujipitisha huku na huko hata kama ni Makanisa,haina tofauti na wale wajioitishao kwenye mabaa na vijao vya wanaume. Hizo ni njia za kimwili kabisa, lakini Munguni Roho.

Amini kuwa Kristo akikusafisha, basi ya kape yote yamepita nawe umekuwa mpya, damu yake imekuwa mbadala wa damu ya bikira. Usiyarudie tena maisha ya kwanza bali dumu katika kweli yake. Usihangaike kutafuta mume au mke, kwa sababu Yeye azijua haja za mioyo yetu hata kabla hatujaomba. Kwa nini basi anasubiri tuombe? Ili kuonyesha imani kwake, wala si kwamba hajui. Wewe hangaikia KUUTAFUTA KWANZA UFALME WA MUNGU NA HAKI (RIGHTEOUSNESS) YAKE. Ukiupata huo umepata vyote. Usijibane kutafuta kakitu kamoja ambako nika kupita tu. Mtafute Mungu maadam anapatikana, mwite maadam yu karibu.


Yeremia 15
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁹ Kwa sababu hiyo Bwana asema hivi, Ukirudi, ndipo mimi nitakapokurejeza, upate kusimama mbele zangu; nawe ukitoa kilicho cha thamani katika kilicho kibovu, utakuwa kama kinywa changu; nao watakurudia wewe, bali hutawarudia wao.
²⁰ Nami nitakufanya kuwa kama ukuta wa boma la shaba juu ya watu hawa; nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, ili nikuokoe, na kukuponya, asema Bwana.
²¹ Nami nitakuokoa na mkono wa watu wabaya, nami nitakukomboa katika mkono wao wenye kutisha.


Hao waliikufunga watajaribu kukurudia wewe, lakinikwa kuwa Bwana yuko pamoja nawe hutowarudia kamwe. Mungu atakuzingira na kukulinda, kwani nguvu za kiroho haziondoki hivi hivi. Ndio maana ni lazima kumtanguliza Mungu mbele akupigie vita vyako.[/i][/b


Maya Angelou, Africa Tanzania, dumbi, LOGARITHM, Sergei Lavrov, LOVE U JF, korino, Mshuza2, park don, Surya, big-diamond, Mwanamena, Tajiri wa Magomeni, dudupori, Bubolwa Chura, Patra31, Depal, alumn, Ed Kawiche, Sexless, The 13, Avriel, Styles
yna2, ngebo, iMind, HoneyBee, Will jr, gbmm, True Believer, Saint Anne[/i][/B][/B]
 

Nyenyere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
14,243
10,090
Relationship between Mafanikio and dhambi (ya uzinzi).
Nasubiri hayo mashudu, utanisamee kwa kukupinga kabla ya mada yenyewe kuandikwa.
Haitakufaa, fuata thread nyingine ussipoteze muda na bando lako albure
 

big-diamond

JF-Expert Member
May 23, 2009
408
493
Relationship between Mafanikio and dhambi (ya uzinzi).
Nasubiri hayo mashudu, utanisamee kwa kukupinga kabla ya mada yenyewe kuandikwa.
Japo tunavamia kabla ya Mada, ila wacha tubwabwaje,

Iweje Masikini anapozini na tajiri ,utajiri haumfuati masikini?

Nimesoma boarding tangu form 1, suala la nyeto ni kama vile hakuna mwanafunzi ambae hajapitia huko, leo tuna vibanda vyetu na vi terios kid vyetu.

Nami nasubiri hoja zako.

NB: Kwa maisha ya sasa ukibahatika kuoa bikira basi ukae kijijini, vikija mjini vinakuwaga vicheche zaidi ya kuku wa kienyeji...Mtazamo tu
 
56 Reactions
Reply
Top Bottom