Uonevu dhidi ya Mbowe: Viongozi wa dini toeni kauli ya kitume

Yaani hata sio jambo la kucheka, bali ni aibu kwa taasisi zetu za usalama kufanya igizo la kitoto kama hilo. Halafu unakuta ni watu wazima na wengine wazee wanafanya huo utoto. Watu wanahitaji katiba mpya, watu wa usalama wako usingizini wanasubiri kuagizwa na wanasiasa kutunga tuhuma za kitoto, na wanalipwa mshahara!
Hivi viongozi wa kisiasa huwa haiwezekani kuwa magaidi?

Kwani gaidi huwa anatakiwa kuwa na rangi gani na anatakiwa atokee wapi ndio tuamini kuwa ni gaidi?
 
Uzi huu ni mahsusi kwa viongozi wetu wa kiroho (maaskofu na mashehe)

Hakuna Mtanzania (wakiwemo viongozi wa serekali wenyewe) asiyejua kuwa kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya kubambikwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe ni nia ovu ya kutaka kumkata makali katika adhma yake ya kupigania haki kwa watu wote hapa nchini kwetu.

Kwa ajili ya muktadha tu.

Mbowe ni mzazi.

Mbowe ni kiongozi wa siasa anayeheshimika barani kote Africa and beyond.

Mbowe ni mfanyabiashara mwadilifu - vinginevyo angekuwa tayari amebambikiwa makosa ya uhujumu uchumi siku nyingi

Baba yake Mbowe alipigania uhuru wa nchi hii, hivyo Freeman ni mtu ambaye damu yake imeshikamanishwa moja kwa moja na uhuru wa Tanganyika / Tanzania

Mbowe ni mtoto wa kiroho wa baba wa taifa Mwalimu JKN (Mungu amrehemu)

Viongozi wetu wa kiroho simameni mhesabike. Tunajua mnajua tunajua mnajua tunajua kwamba Mbowe anaonewa na serekali. Sababu za kuonewa kwake sihitaji kuzirudia hapa kwani zipo well documented.

Haya mambo ya kuonewa na kunyanyaswa chini ya serekali ya CCM ni suala la zamu. Usiponyanyaswa leo, ipo siku yako huko mbeleni inakuja - bila kujali wewe ni mtumishi wa Mungu au la. Anaweza kuja kutokea kiongozi mwingine wa hovyo zaidi kuliko hawa waliopo sasa kwa utashi wake tu akaitumia katiba hii kuwasulubu ninyi viongozi wa kiroho. Hahitajiki nabii kuliona hili likija huko mbeleni.

Kwa sababu sasa wamejitokeza watu jasiri walioamua kusimama kwa niaba yetu, hakuna wakati muafaka mwingine zaidi kwenu viongozi wa kiroho kupaza sauti zenu ili Mungu akapate kutenda kupitia kwenu haki ipate kutamalaki katika taifa letu alilotupa Mungu mwenyewe, sawasawa na maandiko matakatifu katika Biblia (Zaburi 7:11)

nakumbuka nshaletaga uzi apa nkiuliza kwann chadema mnamuona mbowe kama Goddes meanwhile kuna mambo yanayojulikana maeneo ya hai ambayo msingependa kuyaskia
 
Mnalia lia nini sasa kuomba haruma si mlisema mnatatumia wembe ule ule kumnyoa rais.
Kuna watu wiki chache kabla ya tarehe 17 March walikuwa wanasema hivi hivi. Mungu hataniwi!
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Waitoe kauli gani ?!!!

Hivi Kuna IMANI KUBWA zaidi ya USALAMA ,UTULIVU NA AMANI YA WATANZANIA?!!!

#NchiKwanza
#KaziIendelee
 
Kuna watu wiki chache kabla ya tarehe 17 March walikuwa wanasema hivi hivi. Mungu hataniwi!
Mungu anaingiaje hapa yaani mnamtisha Rais akijibu mapigo mnakimbulia kwa Mungu, msitishe watu suala la kufa kila nafsi itaonja mauti, kwa hiyo Rais akifa Chadema ndiyo mtapewa dola akili matope.
 
Shehe ponda na askofu bagonza

Hao huwa wanatoa matamko wao binafsi, mara zote huwa hawana backup ya mabaraza...

Ndio maana unaona Sheikh Ponda amekuwa akikamatwa mara kadhaa, yule Askofu Mwamakula naye kashawahi wekwa lupango...

Wenye nguvu ya kuongea na kusikika ni lazima wawe baraza kama Bakwata, TEC n.k
 
Hivi viongozi wa kisiasa huwa haiwezekani kuwa magaidi?

Kwani gaidi huwa anatakiwa kuwa na rangi gani na anatakiwa atokee wapi ndio tuamini kuwa ni gaidi?
Zama zimebadilika boss, propaganda alizofanya mahita miaka 20 iliyopita hazina tija miaka hii. Hao vyombo vya dola wamkamate aliyejiunganishia bomba la mafuta na sio huo utoto wanaofanya. Nyie ndio mnasababisha wazungu wanatuita manyani. Tunahitaji katiba mpya, huu utoto mwingine bakini nao na hayo mazee yanalipwa pesa za bure kutunga mambo ya kipuuzi.
 
Mkuu hebu punguza hasira naona unachuki kubwa sana moyoni, tulia kisha jibu swali la sivyo na wewe utakuwa unaendeleza utoto huo huo unao ulalamikia hapo.

Nimekuuliza.

Viongozi wa kisiasa haiwezekani kuwa magaidi?

Gaidi anapaswa kutoka wapi ili ndio tuweze kuamini kuwa yawezekana akawa gaidi?
 
Nasema hivi, acheni siasa za kitoto tafadhali. Wanaume wazima mnashindwa kufanya mambo ya maana mnaendekeza utoto, mnaujua ugaidi au mnadhani mnaongea na watoto wadogo? Hivyo vyombo vya dola vimtaje aliyejiunganishia bomba la mafuta, sio kupoteza fedha za umma kwa mambo ya kipuuzi.
 
Back
Top Bottom