Ungependa kiongozi gani aje Jukwaani kutoa majibu na ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayoendelea nchini?

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,014
Habari wadau,

Jamiiforums imekuwa sehemu ya wanachama kushiriki kutoa maoni yao, kuelezea kero zao na kupata ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali nchini, nafasi inayowawezesha kufanya maamuzi mkiwa na taarifa sahihi na zenye ubora. Wapo viongozi wachache kama Dkt. Gwajima D ambao wamekuwa wakitoa ufafanuzi mara zote wanapohitajika.

Kama mkipata nafasi ya upendeleo ya kuletewa viongozi kwa siku maalum kwa lengo la kuwahoji na kutolea ufafanuzi wa kero mbalimbali hapa Jukwaani ungependa kiongozi gani awe wa kwanza na kwasababu gani?

1708429800208.png
 
Binafsi ninahitaji hizi idara mbili zije kuniweka sawa

Moja ni Mamlaka ya maji - Maji sasa hivi ni anasa, vilio vinazidi mtaani. Mtaani kwangu mwezi wa tatu hatujui maji ya DAWASA.

Idara ya Tanesco; Hawa nimechoka na ahadi zao, nina biashara yangu inayohitaji uhakika wa umeme lakini nashindwa kufanya biashara kutokana na kutokuwa na umeme wa uhakika.

Nyongeza nataka kusikia mamlaka inayohusika na sukari. Vitisho vimekuwa vingi kuliko uhalisia mtaani, mwisho wa siku wafanyabiashara wa rejareja wanaishia kukamatwa kwa kuuza bei ambayo itawapa faida.
 
Aje Mama mwenyewe atuambie sababu hasa ya maisha kuwa magumu kupitiliza mtaani. Yaani hela haina kabisa thamani! Halafu mbaya zaidi hata ukiipata, haitulii mkononi; unakuta imekwisha! Shida iko wapi?

Mzunguko wa hela mtaani unakatisha tamaa! Vitu bei juu! Uchumi umerudi mikononi mwa watu wachache!! Hii ni hatari aisee. Mama aangalie vizuri. Nahisi kuna sehemu kunavuja kwenye kapu lake la uchumi.
 
1. Umeme Waziri Dotto.
2. Ukosefu wa Usd Waziri wa fedha.
3. Kuuzwa bandari zetu Mama mwenyewe
4. Wageni kupata uteuzi Mama mwenyewe
5. Katiba mpya Mama mwenyewe
6. Wazanzibari kumiliki ardhi Tanganyika Mama mwenyewe.
7. Wazanzibari kupewa ajira Tanganyika Mama mwenyewe
8. Ukosefu wa sukari Mama mwenyewe
9 Wazanzibari kutawala Tanganyika Mama mwenyewe.
10. Utendaji duni wa mawaziri,makatibu wakuu,wakuu wa mikoa na wilaya, jeshi la polisi rushwaa hasa kitengo cha usalama barabarani. Mama mwenyewe
11. Utendaji mbovu wa Bunge na Mahakama Mama mwenyewe
 
Sioni Kama tunahitaji ufafanuzi kuliko tunavyohitaji huduma na bidhaa Sawasawa na mahitaji. Ufafanuzi hauwezi kuleta Sukari na wala sio suluhu ya mgao wa umeme. Ufafanuzi hauwezi kushusha gharama za maisha.
 
1. Umeme Waziri Dotto.
2. Ukosefu wa Usd Waziri wa fedha.
3. Kuuzwa bandari zetu Mama mwenyewe
4. Wageni kupata uteuzi Mama mwenyewe
5. Katiba mpya Mama mwenyewe
6. Wazanzibari kumiliki ardhi Tanganyika Mama mwenyewe.
7. Wazanzibari kupewa ajira Tanganyika Mama mwenyewe
8. Ukosefu wa sukari Mama mwenyewe
9 Wazanzibari kutawala Tanganyika Mama mwenyewe.
10. Utendaji duni wa mawaziri,makatibu wakuu,wakuu wa mikoa na wilaya, jeshi la polisi rushwaa hasa kitengo cha usalama barabarani. Mama mwenyewe
11. Utendaji mbovu wa Bunge na Mahakama Mama mwenyewe
Maswali yako mengine mbona tayari Lucas mwashambwa alishayatolea ufafanuzi? Fuatilia nyuzi zake.
 
Tungependa kumwona Mchengerwa na TAMISEMI yake.
Kuna mambo mengi tunaona yanaenda kombo kwenye wizara yake, uwenda yeye atakuwa na majibu yetu.
Moja ya mambo yanayoleta sintofahamu Kwa wananchi ni matamko yake yasiyotimilika
mfano,

1. Agizo Halmashauri kuzipa muda Fulani kumaliza malipo ya ajira mpya Kuna raia Hadi Sasa chenga pesa zimeliwa.
2. Ajira mpya za afya na elimu kutangazwa January na February 2024 chuma hiyo inapepea yaonesha ni ulongo.
3. Mifumo yote ya kiutumishi online ni usumbufu aifanyi kazi

Na mengine mengi akija tutamuuliza
 
Jukwaani ungependa kiongozi gani awe wa kwanza na kwasababu gani?
Kiongozi wa TANESCO aje atoe maelezo kuhusu suala la umeme, kwanini umeme unakatwa masaa 12 mpaka 13/14 bila kutoa taarifa yoyote yenye mashimo nini kinaendelea na hii ni mpaka lini?

Maana tuliambiwa mwisho trh 16 Mwezi wa 2 umepita Jana trh 19 wamekata kuanzia asubuhi mpaka usiku bila taarifa yoyote yaan masaa 14 TANESCO wamekata umeme, sasa nini kinaendelea aje atoe maelezo yaliyojitosheleza sababu haswa ni nini za kutukatia umeme kikatiri namna hii? Mtu unakaa masaa 14 huna umeme
 
Spika wa Bunge la Tanzania,aje atueleze kwanini anasimamia wabunge wasiowajibika kwa wanakura wake
 
1. Umeme Waziri Dotto.
2. Ukosefu wa Usd Waziri wa fedha.
3. Kuuzwa bandari zetu Mama mwenyewe
4. Wageni kupata uteuzi Mama mwenyewe
5. Katiba mpya Mama mwenyewe
6. Wazanzibari kumiliki ardhi Tanganyika Mama mwenyewe.
7. Wazanzibari kupewa ajira Tanganyika Mama mwenyewe
8. Ukosefu wa sukari Mama mwenyewe
9 Wazanzibari kutawala Tanganyika Mama mwenyewe.
10. Utendaji duni wa mawaziri,makatibu wakuu,wakuu wa mikoa na wilaya, jeshi la polisi rushwaa hasa kitengo cha usalama barabarani. Mama mwenyewe
11. Utendaji mbovu wa Bunge na Mahakama Mama mwenyewe
Pengine pote sawa ila kwenye bunge mama hausiki

Ubovu wa Bunge umetengenezwa na awamu ya tano labda kama hukuwa nchini kipindi cha uchaguzi
 
Back
Top Bottom