Ni kigezo gani hutumika na viongozi wa kitaifa kutoa pole kwa familia iliyoondokewa na mpendwa wao?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
876
4,101
Pale unapotokea msiba wapo ambao viongozi utoa pole kupitia mitandao ya kijamii, ipo misiba Mhe Rais utumia barua ya Ikulu nk

Napenda kufahamu ili Mhe Rais atoe pole kwa kupitia akaunti yake ya kijamii anapaswa kuzingatia vigezo gani?

Je, anapotumia barua rasmi ya Ikulu kutoa pole utumia vigezo gani?

Je, uzingatia wingi wa marehemu? Itikadi ya kisiasa au nafasi katika nchi na jamii? Utumia aina ya kifo au njia gani umwongoza Rais kutoa pole ndani ya nchi na hata nje ya nchi.

Tujuzeni wajuzi wa mambo ili tuweze kuelewa na kuacha kutumia standards zilizopo kumkumbusha kiongozi wetu pale anapopitiwa.
 
Anayefanya hayo siyo Rais Bali ni taasisi.

Sasa Kwa akili yako unadhani Rais ndio aliwaalika kina Mwijaku Kula futari Ikulu?
 
Back
Top Bottom