Sungusia Rais TLS, Kulishitaki Gazeti la Mwanahalisi. Awataka Wanachama wa TLS kushiriki mijadala ya maamuzi, wasiishie kulalamika mitandaoni

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987

Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika - y yThe Tanganyika Law Society (TLS), Wakili Harold Sungusia tarehe 19 Januari 2024 ametoa ufafanuzi, ambapo amefafanua mambo mbalimbali kuhusu uongozi wake ikiwemo tuhuma zinazungumzwa dhidi yake.

Sungusia ambaye anashika Madaraka ya Urais tangu alipochaguliwa Ijumaa, Mei 12, 2023 ameanza kwa kueleza kuwa anatarajia kulifikisha Mahakamani Gazeti la Mwanahalisi kudai fidia kwa kile alichokiita kuchafuliwa na chombo hicho cha habari.

Anasema “Suala la kwanza ninaloenda kuzungumzia ni Marekebisho ya Sheria katika Sekta ya Sheria.

“Kumekuwa na madai Wanachama wetu hawakushirikishwa na wengine wanataka tugomee huo mchakato.

“Ukweli ni kuwa tulipata taarifa kuhusu Muswada wa Sheria ambao unarekebisha Sheria mbalimbali, ambapo tuliusoma kwenye mitandao ya Bunge.

“Tulipata nakala halisi Septemba 10, 2023 tukatoa maelekezo kuwa Wanachama wote wapelekewe na waweze kutoa maoni yao kwa Sekretarieti ili yaratibiwe na yapelekwe katika Kamati husika, baada ya kurekebishwa yapelekwe kwenye Govern Council kwa ajili ya kupelekwa Bungeni.

“Septemba 14, 2023 tukafanya mkutano lakini Wanachama walishiriki kwa uchache, bahati mbaya tunapotangaza masuala yanayohusu haki zetu wanaojitokeza ni wachache kama ilivyokuwa.

“Ilikuwa ni kikao cha online na walioshiriki siku hiyo ni Wanachama 26 tu, orodha ya majina yao tunayo.

“Sio kwamba wapo bize, hapana, ila ni maamuzi tu, unajua watu ni wepesi sana kulalamika lakini hawashiriki katika hatua za awali, ikitokea Sheria kandamizi inapitishwa ndio wanakuwa wa kwanza kulalamika.

“Septemba 16, 2023 Kamati yetu ya Sheria ilikaa na kupitisha mapendekezo yaliyopatikana kutoka kwa Wanachama na kutengeneza Bango Kitita ambalo liliwasilishwa kwenye Baraza la Uongozi mnamo Oktoba 9, 2023.

“Interest yetu TLS tulitaka kuona angalau kuwe na uchaguzi kila baada ya miaka miwili au mitatu, tukaomba kama inawezekana mwaka mmoja mmoja ubadilishwe kwa kuwa uchaguzi una gharama na ndani ya mwaka mmoja ni vigumu kufanya maendeleo.

“Oktoba 10, 2023, TLS iliandaa mdahalo kuhusu adhabu ya Kifo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Sheria, tukamueleza kiu yetu TLS kuona muda wa miaka miwili au mitatu unarekebishwa na mambo mengine hayafai kwenye muswada, yaondolewe, akasema amesikia kilio chetu atafanyia kazi.

“Oktoba 17, 2023 tulipewa taarifa kuwa Kamati ya Bunge inasikiliza huo Muswada ili wadau waweze kupeleka maoni.

“Tukatuma ujumbe kwenda Bungeni ukiongozwa na Makamu wa Rais, kikubwa yalipelekwa maazimio ya kuongeza muda tu.

"Hivyo, unaposikia mitandaoni kuwa Viongozi wa TLS wamesaliti, hawajachukua hatua, wamenyamaza ni mambo ambayo hayana ushahidi na ya kutunga.

“TLS tulishiriki ili tusipate Sheria mbovu lakini ikumbukwe kuwa sisi sio watungaji wa Sheria na sisi sio Wabunge.

Hivyo, anaposimama mtu anasema TLS imepitisha muswada wenye masharti ya kibaguzi huyo ni mtu ambaye hapaswi kuwa Mwanasheria, inakuwaje Mwanasheria hujui mchakato wa utungaji wa Sheria unavyokuwa.

“Ni hatari sana Mwanasheria msomi kutoa hoja ambazo haziendani na taaluma ya Sheria. Kabla hujaandika kwenye mtandao jifikirie, hicho unachokiandika wenzako wanakuona, natamani nidhamu ya Sheria iwe na hadi kama jamii inavyotuchukilia. Tusifanye vitendo vya kudhalilisha taaluma ya Sheria.

"Pili, katika suala la Muswada unaohusu Sheria ya Marekebisho ya Sheria uliorekeisha TLS Act, sisi Baraza la Uongozi tulitenda haki kwa kusimamia misingi inayosimamia misingi ya Wanachama na kuhakikisha hakuna tulipoacha gape.

“Tumefanya kila tunachoweza kukifanya na sasa jopo letu linatarajia kusimamia kesi ya kupinga vifungu korofi, sisi kama taasisi hakuna kitu mbacho tunaweza kufanya zaidi ya hapo, sisi tunafuata utawala wa Kisheria.”
 
Back
Top Bottom