Nakumbuka JKT Bulombola 1980 wenzetu wapo front line halafu tunawapongeza, nakumbuka Mugabe anapata uhuru tunaimba kumsifu (najuta), nakumbuka kupanga foleni kununua sukari kwa kutumia kadi ya meneja wa kijiji, kg. moja tu basi. Nakumbuka kulala guest kwenda kuchukua mshahara halafu unaambiwa muda umeisha inabidi ulale siku mbili na nauli umekopa kwa meneja wa kijiji. Nakumbuka Katambuga au Arusha to Moshi unachagua ile nzuri ya tyre za East Africa ambazo baadaye kiwanda kiliuzwa na Makonde, nakumbuka nipo Moro Sokoine amefariki baada ya wahujumu uchumi, mmoja wao alikuwa RPC wa Moro, watu wake walishangilia saana siku hiyo sababu Kantabula alikuwa amefukuzwa kazi na Nyerere mhanga namba moja. Nakumbuka kutumia nguo za kuzikia kusitiri watoto kama nepi. Hakukuwa na nepi nchini tulizifua vizuri na kuzipamba sababu shuleni enzi zetu tulisoma needlework hivyo tulijua jinsi ya kupendezesha vitu. Siwezi maliza yote hayo yanatosha.