Unakumbuka nini miaka ya 90's kushuka chini?

Unakumbuka nini miaka ya 90's kushuka chini?

Nakumbuka sekeseke la Idd Amin mjomba walipelekwa vitani kijogoo ndiyo nina mwaka mmoja tangu nihitimu elimu ya msingi niliogopa sana tena na tunaambiwa Amin anakula binadam ndiyo kabisa eti vilema wanapelekwa mtoni chakula cha mamba nakumbuka kuchunga mifugo n k
 
Rehema ya Maulana Mola wangu!
 
Nakumbuka mwaka 1985 tukiwa darasa la 6 Muhimbili Primary school na akina Dj Bonny love na Kibonde, alikuja Mwl. Nyerere shuleni kwa shuhuli ya mwenge. Tukaambiwa usipoimba wimbo wa taifa utakufa.. hiyo bidii ya kukariri huo wimbo sitakaa nisahau..
 
Nakumbuka majina kama lunyamila, Thomas kipese, Goerge masatu, Duwa Said, Damian Kimti, Akida Makunda,Sanifu Lazaro.
 
Itifaki izibgatiwe,

Kuna mambo nmeyakumbuka wkt wa miaka 90's kuja 80's, kwanza kulala ilikuwa saa12 ukionekana nje umeumia. Sukari haikuuzwa dukani tulikuwa tunapanga foleni kununua sehemu fulani zinaitwa ugawaji. Tv mnatizama jumapili tu na ukiwa na TV lazima iwe na kibali.

Wewe unakumbuka nini?
Nakumbuka baba alikua anapanga nizaliwe
 
Back
Top Bottom