Unakumbuka nini miaka ya 90's kushuka chini?

Unakumbuka nini miaka ya 90's kushuka chini?

  • Siku za Jumapili ilikuwa mwisho saa nane mchana kuendesha gari, vinginevyo, lazima uwe na kibali.
  • Bia zilikuwa adimu, tukienda bar tulikuwa tunanunua crate nzima na kuweka chini ya meza.
  • Bia kama zikitoka TBL ni brand hiyo hiyo kwa hiyo ukienda bar huna chaguao: Crown au Safari.
  • Upungufu mkubwa wa bidhaa kama Colgate na sabuni za kuogea.
  • Sukari ilikuwa inapatikana kwa ration, lazima uwe na kadi kutoka kwa mjumbe ndio upate sukari.
  • n.k.
 
Nakumbuka VIJANA wote na WAZEE wanaume tunavaa CHUPI aina moja VIP tu...tena chupi hizo hazikawii KUKATIKA ukaishtukia IPO TUMBONI
 
download.jpg

sisi matozi wa enzi hizo tulikua tunamsikiliza Flavor flav (public enemy)
vanilla_ice.jpg
na Vanilla Ice
 
Ni kwamba asili ya neno daladala ni wakati wa Mwl Julius Nyerere wakati shilingi tano likuwa sawa na dollar moja ya kimarekani hivyo shillingi tano ikawa inaitwa dala na wapiga debe enzi hizo walisema dala -dala-dala kumaanisha kuwa nauli ni dala moja(gwala/shilingi tano) na ndipo lilipoibuka neno daladala.
kamba hiyo ..sio kweli...Sh 7 =1US dollar 1960s sio 80 au 90

daladala ilitokana na nauli sh sh 5. ni kitambo Sana Kama umehadithiwa mm nilikuwepo
 
Nakumbuka tu maisha yalivyokuwa matamu, muziki wa Keith sweet, Joe Thomas, Boys to men, Back street boys, Tevin Campell, na wengine wengi.. muziki mzuri.
 
Nakumbuka JKT Bulombola 1980 ..
Umenikumbusha ya JKT, mwaka 1976 Makutupora kuruta tulivyokuwa tunachangishana na kununua mbuzi kwa 5,000/- w/end na kumchoma. Pia ilikuwa shida kunywa chai asubuhi ya moto ili kuwahi foleni. Mwenzetu mmoja akisingizia kuumwa hakuamka asubuhi. Alipokurupushwa na afande alisema anaumwa. Kuliuzwa ni nini akajibu "mine is a serious problem". Afande kusikia hivyo akatuamrisha kumpeleka haraka mwenzetu zahanati akatibiwe "ini"
 
Sisi tulikuwa tunaimba maserure mara oho likatokea joka wee hakuna cha serule wote tulikimbia, baada ya hapo tukaambiwa turudi combania. Ila magonjwa yalikuwa mengi Pseudomonas, Pendulum na mengi tu halafu maafande wanasema hehehe hayo yaliua shangazi wangu nenda kwa matron.
 
Nakumbuka wimbo wa" we are the world "(Au U. S. A- AFRICA) mwaka 1985 ulioimbwa ili kuchangia baa LA njaa barani afrika. Wimbo uliimbwa na wakali wa muziki wakina Michael jackson, Leonel Richie.,Diana Rose. Nilikuwa form one mawenzi Sec. Moshi. Siwezi kuandika yote bora niishie hapo.
Mkuu huo wimbo ni wa mwaka huo!!! mi nimekuja kuuona 94, miaka hiyo nlikuwa najua michael na thriller
 
Mkuu huo wimbo ni wa mwaka huo!!! mi nimekuja kuuona 94, miaka hiyo nlikuwa najua michael na thriller
Mkuu! Ulivuma Sana mwaka 1985.nakumbuka nilikuwa form one. Tulikuwa tunauandika kwenye daftari then tunafanya mashindano ya kupita mbele ya darasa na kuimba.
 
Napakumbuka Magot kulikuwa na Dj mmoja mkali sana akiitwa Young millionare.
huyu aliitwa jacob osungu. nyuma kidogo alikuwa mtangazaji rfa. na baadae kupitia simu ya msikilizaji alikubaki kuwahi kutumia jina hilo. na anamilki music centre mitaa ya mwanza nahisi ni stend sina hakika alitaja rwagasore au tanganyika. namkubali na ni shabiki wake hasa kwenye nyimbo za zamani
 
Back
Top Bottom