Unakumbuka nini miaka ya 90's kushuka chini?

Unakumbuka nini miaka ya 90's kushuka chini?

tapatalk1.jpg
Nimekumbuka hii picha
 
Mimi flaire ambazo zilikuwa soro kipindi cha seventies. Hizo zilikuwa za mabitoz kumbuka kamanyola wakati huo unaliza watu, Moro jazz, Tabora Jazz na Vijana jazz. Zilikuwa nyingi nashangaa sasa wanasema wanamziki wasiimbe siasa wakati siasa tuliisoma kwenye music.
Hahahaaaaaaa uchochezi kwa magu
 
Nakumbuka miaka ya 90's ukipewa hela hata kama ni mwezi wa kwanza unaitunza hadi krismasi au mwaka mpya ndio utumie,,,na usiponunuliwa nguo mpya hiyo krisimasi ni bifu kubwa na wazazi....
 
Nakumbuka mwaka 1985 tukiwa darasa la 6 Muhimbili Primary school na akina Dj Bonny love na Kibonde, alikuja Mwl. Nyerere shuleni kwa shuhuli ya mwenge. Tukaambiwa usipoimba wimbo wa taifa utakufa.. hiyo bidii ya kukariri huo wimbo sitakaa nisahau..
 
Nakumbuka JKT Bulombola 1980 wenzetu wapo front line halafu tunawapongeza, nakumbuka Mugabe anapata uhuru tunaimba kumsifu (najuta), nakumbuka kupanga foleni kununua sukari kwa kutumia kadi ya meneja wa kijiji, kg. moja tu basi. Nakumbuka kulala guest kwenda kuchukua mshahara halafu unaambiwa muda umeisha inabidi ulale siku mbili na nauli umekopa kwa meneja wa kijiji. Nakumbuka Katambuga au Arusha to Moshi unachagua ile nzuri ya tyre za East Africa ambazo baadaye kiwanda kiliuzwa na Makonde, nakumbuka nipo Moro Sokoine amefariki baada ya wahujumu uchumi, mmoja wao alikuwa RPC wa Moro, watu wake walishangilia saana siku hiyo sababu Kantabula alikuwa amefukuzwa kazi na Nyerere mhanga namba moja. Nakumbuka kutumia nguo za kuzikia kusitiri watoto kama nepi. Hakukuwa na nepi nchini tulizifua vizuri na kuzipamba sababu shuleni enzi zetu tulisoma needlework hivyo tulijua jinsi ya kupendezesha vitu. Siwezi maliza yote hayo yanatosha.
Shikamoo mkuu.
 
Wajukuu zangu

Mnanikumbusha mbali kweli kweli.
Kipindi hicho nakumbuka ndo tulikuwa tunapigania uhuruu.
 
Mi nilikua naburudika na video za kina Shokosugi, Bruce Lee na kina Jimmy Kery.
Bila kuwasahau akina Charles Bronson ,Fred Williamson, Clint Eastwood, bud Spenser.
 
Power mabula, power ilanda, power bukuku....stanley mabesi super ninja, iraq hudu, habib kinyogoli....athuman digadiga, black moses, baucha......
Pia akina jitu lishibalo, power ten by ten , super ngedere, kokoliko, jitu la miraba minne,
 
Nakumbuka majina kama lunyamila, Thomas kipese, Goerge masatu, Duwa Said, Damian Kimti, Akida Makunda,Sanifu Lazaro.
Bea Simba, malota soma, DEO njohole, Nico njohole, Raphael Paul, RAMADHANI Lenny , DEO mkuki, peter tino, gebo peter, MOHAMED mwameja, kichochi lemba, HAMISI kinye, zamoyoni mogella.
 
Back
Top Bottom