Unakumbuka breakup yako ya kwanza?

Unakumbuka breakup yako ya kwanza?

Nilimpenda kweli, ni story ndefu, alikuwa mmanga hawa wa ki-Oman, ndugu zake hawakunitaka na waliloamini ni kwamba ningemuharibia masomo yake na hatimae maisha yake.

Katika harakati za hapa na pale ikatokea safari ya kimasomo kwenda nchi flani hivi, nlifanya yote yaliyowezekana akawemo safarini maana mimi nlikuwa na nafasi tayar, alinishkuru sana for that lakini alikuwa kuungana na kukubaliana na matakwa ya ndugu zake kwamba aachane nami. Kipindi cha rehearsal kilikuwa ndio kipindi cha kutuweka karibu but she always avoided me. I was never happy at school na kila safari ilivyokaribia ndivyo hakunielewa ba kujaribu kuji-distance from me.

Siku ya safari ikafika, ndege yetu saa nne asubuhi mpaka saa mbili hajafika. I started worrying na nkataka kugoma pia, kama haendi nami sitokwenda, fikra zangu ziliniambia ndugu zake wamemzuia. Around saa mbili na nusu alitokea, nlikumbatiana na kaka yake aliemsindikiza na akaninong'oneza kuwa he believes I will protect his sister. I gave him my words that she was in a safe hands.

Mmanga yule hakutaka kuongea nami mpaka tulipofika Amsterdam alipopata matatizo na suitcase yake. She was crying and calling me "my love". I had some courage and strength to do whatever I had to ili vitu vyake vyote tupate kusafiri navyo.

In Norway, she gifted me her ............

We enjoyed our time, and she promised me that she will be mine no matter what.

As we reached Tanzania, out of the flight, she pulled me, hugged me, kissed me and said it was over between us. And it wa

Sweet love story
 
Yule ms*nge aliniacha jumapili ambayo jumatatu yake tulikuwa na test...sababu yake mammmae zake nikachafua CV ya kuzungusha ile paper (nilipata zero)

Nilikuwa siwezi kula
Siwezi kulia japo natamani kulia lakini machozi hayaji
Nilikuwa mchekaji mzuri lakini siku hizi sicheki kabisaaaa

Popote ulipo ama kama unasoma hapa ujue tu nakuchukia kuliko kawaida!!!na kwa taarifa yako ninae baby mpya nampenda sanaaaaaa

#povu

Halafu bado nakupenda
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 povu kama lote
 
My first breakup!
He was truly my first love, tulipendana mpaka familia zetu walijua. Akitumwa dukani lazima aniite nimsindikize, nikitumwa mimi lazima nimpitie anisindikize, ndio alinifundisha kupenda mpira maana alipenda sana football na hata shuleni alikuwa mchezaji wa kutegemewa.!

Tulipata misuko suko sana, tulitoka familia zinazofanana (yeye kwao alikuwa mtoto wa kambo mi kwetu nililelewa na mamdogo) manyanyaso na masimango tuliyopitia kwny maisha yetu yalikuwa yanafanana na kutuweka karibu zaidi..

Nilimbadilisha kwny vingi sana, pombe aliacha, akawa anaenda kanisani ( wakati hata alikuwaga haendi) hadi kwny semina za mwakasege tukawa tunaenda wote...

Baadae akawa ananikwepa bila sababu, simu yangu akawa anapokea kwa shida baadae hakupokea kabisa! Nikawa namtafuta bila mafanikio, nikamtumia dada yangu aongee nae lkn alimjibu tu mwambie nitamtafuta! Mwaka ukakatika sijamuona. Nakumbuka siku ile ilikuwa harusi ya bro wangu akaja ameongozana na mdada nisiyemfahamu. Kumbe ndio mchumba wake! Niliumia kupita maelezo. Dada yake ndo kaniambia mbona huyo mchumba wake na nyumbani wanamjua karibu wanafunga ndoa! Maumivu niliyoyapata Mungu tu ndo alijua. Nilikuwa nashinda nalia tu ndani, chakula hakipiti. Nikaenda kwao kuongea nae akawa hataki kabisa kuonana na mimi. Basi nikakubali kishingo upande nikaendelea na maisha yangu.

Baada ya miaka kadhaa nimerudi kutoka visiwani nikashangaa ananipigia simu tuonane. Nikaenda kumsikiliza ndo ananiambia kilichotokea kwamba baba yake alimwambia aoe mwanamke kutoka kabila la kwao na si vinginevyo ili kumtii baba yake akaamua kufuata maagizo " but u are my first love T, u still the best woman i ve ever had, please forgive me for all the sleepless nights and th pains i ve caused. Am so sorry and know that i still love u so much!" Hayo ndo maneno aliniambia and by then hayakuwa na muhimu maana alishaoa na mimi kuolewa.
 
Poleeeee
 
Ile msg ya Naona tuachane tu aisee nilihisi Gizaa flani hivi nikataka kuzimia..!! Sikuweza kuongea na mtu yani nililia kama mtoto ila mama akajua tatizo aisee alinitia moyo na kunipa shule kuhusu wanawake yani toka siku ilee mwanamke hawezi isumbua akili yangu hata Kama Nimpende vipii... akizingua namuacha dak sifuri kitu kingine siwezagi Kumbembeleza mwanamke kabisaa.
Mtt wa mama sio?,hivi kweli mwanaume umeachwa na dem unaenda kumlilia bi mkubwa wako are you serious!?,...
 
Inauma sana,
Aliniambia ana maongezi muhimu na familia yangu akaniomba niwape taarifa na kuwasisitiza mama na ndugu zangu wawepo siku ya kikao. Nilijitahidi sana kuandaa mazingira mazuri ya kufanyia kikao bila kujua naandaa panga la kunichinjia! Niliachwa mbele ya ndugu zangu.
Sitaisahau siku ile,
Mama watoto popote ulipo Mungu akubariki na akupe umri mrefu na mafanikio wewe na mwanetu, najua ipo siku ukweli utaujua na Mungu atakurudisha mikononi mwangu hata kama itapita miaka 20.
#Evln
Dah!,alitaka akuue na presha nin?
 
We nae uliendekeza mapenzi ya kishamba/ ya kizungu wakati wewe ni mbongo tu! Kwanini usingepiga chini tokea tu ulipojua kuwa ndugu zake hawakupendi!
Alijidai eti ana mapenzi ya kweli[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Daah kuna kaka nilimpenda mno na alikuwa anajua bhasi bhana wee! Alikuwa ananitesa hatari eti sababu nampenda,
ila nilijikaza baada ya kuchoka na mateso niliamua kumuacha nikakaa wiki sijawasiliana nae hakuamini akapiga simu kuuliza kweli ' L' wiki nzima unakaa bila kuwasiliana na mpenzi wako!

Nikamjibu sina vocha, (maana nisipo piga mimi hapigi) ,
ikaenda akawana anapiga akijisikia hata baada ya siku 2,3 lakini moyoni mwangu nikasema huyu simtaki tena sikuwahi kumpigia tena.

kuna siku alipiga alilalamika mno nimebadilika sijui nini na nini sikumpa majibu yakueleweka najidai nipo bize, ikaenda ikaenda akipiga simu sipokei akachoka akapotezea.

Japo niliumia sana mapigo ya moyo yalikuwa yanaenda si kawaida
Kwa maumivu yale Aisee! Siruhusu tena mapenzi yanitese kiasi kile.
UNAJITAMBUA [emoji122][emoji122][emoji122]
 
Sijawahi teswa na breakups sababu sijawahi achwa

Otto
Kina j watatu
Sunday
G
Elvin
Brayo
Yahya

Mnisamehe tu kwakweli

Ila mpenzi wa Sasa naomba usije niumiza maana nakupenda Hadi najisahau
Hao uliowataja ndio uliwatosa?
 
Hapa ndo nilithibithisha kua mapenzi ni yanauma,
Maumivu nilioyapata sijawai kuyapata tena na naomba yasijieudie, yan huumwi sehemu yoyote ya mwili lakini unaona dunia iko juu chini,
Kwa mara ya kwanza nikashindwa kula.
Chozi linatoka, lecture hazipandi.

Sikua mpenzi wa nyimbo ila nilijikuta nawafahamu kina Bruno Mars, Celine dion, ibra nation, Adele na wengine wengi.
Nilikua nikiangalia picha yake au nikiangalia call history nalia. Sema nilikua najikaza watu wasinione dhaifu.
Hakika haya mambo yasikie. Kwa ambae hayajamkuta hawezi kuelewa hii hali
Yes i remember it was too childish
 
Nilipogundua anataka kuniacha nikamuwahi akajifanya bado ananipenda kumbe ananilia timing anifanyie suprise ya kuniacha, siku anataka kukamilisha mpango wake nilimtandika makofi hatosahau maishani

Yaani nikipiga upande huu narudia upande wa pili ndo nahesabu kofi moja.
@Jembekillo alikula makofi mangapi?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Daah uzi umenikumbusha mbali sana. 1st love aliniacha baada ya yeye kuingia form 5, alijitangulia darasa moja. Sikuumia sana at first, badala yake nikapambana sana ili na mimi niende advance pengine angerudisha moyo. Nilihisi pengine anahitaji mtu aliyejitambua.

Siku matokeo ya form 4 yametoka tu na nimefaulu nikamrukia hewani. Looooh asalaleeee, baada ya mazungumzo akanitxt move on dude, mi moyo wangu upo kwa mtu mwingine. Daaah niliumia sana, nikachana kadi, barua na kuchoma moto picha zake zote.

Mwaka huu kati kati nilikuja kuonana baada ya muda mrefu, akanipa stori nyingi kuwa kapitia kutendwa sana hapa katikati and lastly akaja kuomba nimuoe. Impossible, nikamwambia na mimi ni wale wale tu nikishapita sikurudii tena, bora utafute mwingine.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119]
 
Back
Top Bottom