666 chata
JF-Expert Member
- Mar 14, 2013
- 1,688
- 3,816
Wakuu kwema!
Huyu Rafiki wa zamani tulipotezana miaka mingi kidogo, enzi za chuo chuo miaka ile mwamba akisomea moja ya fani ya Engineering pale DIT. Miaka hiyo tukiongelea future jamaa alikuwa akijiweka katika nafasi kama tisa hivi za juu za nchi vile akiamini uinjinia utakapo mweka.
Juzi nipo chimbo moja hapa mjini, namkuta yeye ndio mpishi mkuu wa eneo hilo, akiwauzia watu supu na vyakula vingine, kavaa nguo zile za ki chef, nilishtuka ila sikujisikia vibaya maana pesa inatafutwa bwana! Ikabidi tuzungumze na nijue what happened? Chief Engineer imekuwaje kuaje mpaka uwe chef cooker?
Mwamba alistuka lakini akawa mkweli tu mzee na vile tumeshakuwa watu wazima, akasema ni mchakato tu wa maisha, ila aka kazia 'anachosikitika kitu alichokisomea hajawahi kukifanyia kazi, miaka minne yote aliyosomea uinjinia imepotea bure tu na sasa anafanya kazi ambayo hata kama angeishia darasa la saba angeifanya tu'.
Anasema, maisha yalikuwa magumu kweli kweli, kazi hakuna so akaomba kazi ya u dj bar flan sababu alikuwa anapenda sana muziki. Baadaye kwenye u dj kukawa kugumu basi akaona kuna bar imeanzishwa maeneo jirani yake akaomba kazi pale wakampa chaka la jiko, na amekuwa akihama toka bar flan kwenda nyingine na sasa ndo kabobea hapo kwenye karia ya majiko.
Maswali ya kujiuliza, hivi watu hua wanazingatia kweli muda walioupoteza kwenye masomo yao? Kweli hustles zile zimeenda bure? Wanazingatia mamilioni waliyoyalipa vyuoni kwa ajili ya icho walichokuwa wanakisomea? au shida ni kwamba watu wengi walienda kusomea vitu ambavyo sio kusudi lao ambalo Mungu aliliweka ndani yao so degree zao zinakua ni gabage?
Watoto wetu tunawaandaa vp na tunawaambia vipi kwamba baba ako mimi usinione ni chef mimi nina degree ya uinjinia. So hatuwezi kuwa ving'ang'anizi kwenye vile tulivyovisomea kwa miaka mingi na kulipia fedha nyingi?