Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,679
- 119,314
Wanabodi,
Bandiko hili ni kufuatia watu fulani humu wenye viherehere na vimbelembele kutaka kuhoji kila kitu sasa wameingilia kuhoji uwezo wa serikali ya JPM kufanya vetting kabla ya teuzi fulani fulani, kumbe hawajui kuwa now days vetting is nothing!. Kinachoangaliwa sasa ni uwezo wa utendaji tuu na uwezo wa ku deliver na sio vetting!. Rais ana mamlaka ya kumteua yoyote kwa position yoyote regardless vetting imesema nini, imefanyika au haikufanyika na kwa mujibu wa katiba yetu, hakuna mamlaka yoyote inayoruhusiwa kuhoji mamlaka ya rais ya uteuzi, wala kuhoji uadilifu wa mteule yoyote wa rais, hata Tume ya Maadili ya Viongozi, ni tume zuga tuu when it comes to wateule wa rais!, hivyo its pointless kulalamikia kwa nini fulani ameteuliwa, au kuhoji uadilifu wa kiingozi yoyote ambaye ni mteule wa rais, kama rais kaona fulani anafaa, who are you kuhoji uadilifu wa mteuliwa yeyote wa rais?!.
Hii ni kufuatia tabia ya baadhi ya watu, wakiwemo wana jf kuhoji kila kitu kinachofanywa na rais wetu na hadi kumuingilia rais katika utendaji wake, ama kwa kujua, ama kwa kutokujua, maana sii wengi wanaojua kuhusu mamlaka ya rais ya uteuzi, inayoitwa " presidential appointment powers", rais anaweza kumteua mtu yoyote, mwenye elimu yoyote, hata ya darasa la saba, kashika nafasi yoyote, bila kuwa sifa zozote, au kwa vigezo vyovyote, bila kuhojiwa na mamlaka yoyote, au mtu yoyote, popote!, who are you kuhoji mamlaka ya rais ya uteuzi au kutaka kumuamuru rais kutengua uteuzi wa kiongozi fulani?!.
Moja ya sifa kuu za jf ni kuelimishana, katika kuelimishana huku, tunajikuta tunasaidiana kwa kuongezeana maarifa kwa mambo watu wasioyajua.
Moja ya sifa kuu za jf ni kuelimishana, kusaidiana na zinapotokea fursa hata kufurahishana. Hivyo hapa hapa naomba kujitolea kusaidia kuelimisha kuhusu Mamlaka ya rais ya uteuzi inayoitwa "presidential appointment powers" ambapo katiba yetu yetu imempa rais wetu mamlaka ya kumteua mtu yoyote kwenye nafasi yoyote, kwa kufuata ushauri, au bila kufuata ushauri wa yeyote, kwa kutoa sababu yoyote, au bila kutoa sababu zozote kwa yeyote na uteuzi huu, hauruhusiwi kuhojiwa na mamlaka yoyote!.
Teuzi za Sifa na Vigezo na Teuzi Ambazo Hazina Sifa wa Vigezo.
Teuzi zote za rais, hufanyika kwa mujibu wa katiba, ila katika teuzi hizo, kuna teuzi za aina mbili, kuna teuzi zinazohitaji sifa na vigezo, na kuna teuzi ambazo hazihitaji sifa wala vigezo. Nafasi za uteuzi zinazohitaji sifa na vigezo, zimeainishwa katika katiba na sifa hizo na vigezo pia zimeainishwa kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni, yaani prescribed kwa kumuelekeza rais atateua watu wenye sifa gani katika nafasi zipi, mfano Jaji Mkuu lazima awe mwanasheria, Mwenyekiti wa NEC lazima awe Jaji Mstaafu, CDF lazima awe ni mwanajeshi, IGP lazima awe polisi, Director wa TISS lazima awe ni "wale jamaa", Msajili wa vyama ni Jaji, CAG mtu wa mahesabu, au wakurugenzi wakuu wa taasisi za umma katika positions za utendaji, lazima wawe na sifa fulani za kielimu na kitaaluma. Baadhi ya teuzi hizi hazifanyiki at presidents pleasures bali rais huzifanya kwa kufuata maelekezo, mfano Jaji Mkuu, ni kwa maelekezo ya Tume ya Majaji, Katibu wa Bunge, tume ya Bunge, na pia zina kitu kinachoitwa " a security of tenure" kumaanisha rais anaweza kuteua tuu not at his pleasure bali kwa maelekezo na akiishamteua hawezi kumfukuza anavyojisikia, not at his pleasure bali kwa utaratibu maalum, hawa ni pamoja na Jaji Mkuu, Gavana wa BOT, CAG etc.
Teuzi za pili ni zile zinazofanyika wholly or totally at the pleasure of the president, yaani rais anazifanya kwa raha zake, anaweza kukuteua leo na kesho kutengua uteuzi wako bila sababu yoyote, just at his pleasure, hizi ni teuzi katika positions za kisiasa, rais anaweza kumteua yoyote, kwa kumuokota popote na bado akawa yuko right. Hivyo hizi kelele za mkuu wa mkoa fulani kufoji cheti, kufoji jina au kutokusoma sekondari, hata ikikutikana yote yanayosemwa kuhusu elimu ya mkuu huyo ni kweli ni elimu ya kuunga unga, ni kweli alifoji cheti, ni kweli alifoji jina bado uteuzi wake unabaki kuwa ni halali, kwa sababu hakuna sifa zozote wala vogezo prescribed kwenye teuzi hizo, na kilichoteuliwa sio jina, wala sio cheti bali ni mtu na ana deliver.
Sifa za Kuteuliwa na Rais.
Sifa kuu pekee za mtu kuteuliwa na rais kuwa mkuu wa wilaya au mkuu wa mkoa au mbunge wa kuteuliwa au nafasi nyingine yoyote ya uongozi na sio ya utendaji, wakiwemo wenyeviti wa bodi mbalimbali ni
1. Kuwa Mtanzania
2. Kutimiza umri wa miaka 18
3. Kujua kusoma na kuandika.
Hivyo rais ana mamlaka ya kumteua mtu yoyote mwenye sifa hizo, kwa kushauriana na mamlaka elekezi, kuwa mkuu wa mkoa, au mkuu wa wilaya, au uteuzi mwingine wowote, hivyo rais yuko very right hata kuteua mtu wa darasa la saba, hivyo hata ikitokea, ikathibitishwa mteuliwa fulani aliishia darasa la saba, bado uteuzi wake ni halali.
Jee Rais Anaweza Kumteua Nani Kwa Sifa na Vigezo Gani?.
Ukiondoa zile teuzi za rais zenye sifa na vigezo, teuzi nyingine zote wakiwemo ma RC na Ma DC, rais anaweza kumteua mtu yoyote bila sifa yoyote wala vigezo vyovyote na hata kichaa, as long as kichaa huyu haokoti makopo, na akawa hajafanya kosa lolote, mfano hai ni mmoja wa wakuu wa mikoa ni kichaa kabisa ila ukichaa wake bado haujaonekana kwa wengi kwa sababu sio ukichaa wa kuokota makopo, but with time wengi mtaushuhudia ukichaa huu, na hata ikitokea pamoja na ukichaa wote huo na bado rais akamuona bado anamfaa, hakuna mwenye mamlaka ya kuhoji ila wenye akili zao watahoji kimoyo moyo utimamu wa mamlaka yake ya uteuzi!.
Kwa vile katiba yetu haikutoa muongozo wowote kuhusu elimu, sifa au vigezo vya uteuzi, hivyo rais yuko huru kumteua yoyote kwa vigezo vyovyote hata kimada wake na sifa kuu ya huyo kimada ni zile huduma!. Rais anaweza kuwateua ndugu zake, jamaa zake, kabila lake, rafiki zake au yoyote kwa sababu yoyote au hata bila sababu yoyote, bado yuko right na hakuna anayeruhusiwa kuhoji.
Taratibu za Rais Kuteua
Pamoja na mamlaka ya rais kuteua, pia katiba imeweka taratibu za kufuata katika baadhi ya teuzi, katika taratibu hizo, pia kuna sheria, taratibu na kanuni. Katika baadhi ya teuzi, kuna teuzi zinaelekezwa kuwa rais atashauriana na fulani, ataletewa mapendekezo ya majina matatu ya kuchagua, etc. Haya yote ni kwa ajili ya ushauri tuu na sii kumlazimisha rais. Anaweza kuletewa mapendekezo ya majina matatu na akayapiga yote chini na kumteua mtu mwingine yoyote alimradi ana kidhi sifa na vigezo vilivyoelekezwa kwenye katiba, sheria, taratibu na kanuni, na akawa hajafanya kosa lolote.
Rais Halazimishwi Kupokea Ushauri Wowote kwa Yeyote, na ana Haki ya Kuupuuza Ushauri Wowote
Rais wetu, ana wasaidizi mbalimbali kuanzia Makamo wa rais, Waziri Mkuu, mawaziri, wataalamu mbalimbali wanaomshauri kwenye kila nyanja.
Katika powers za rais za uteuzi, katiba inampa mamlaka rais kabla ya kuteua baadhi ya watu, atashauriana na fulani, mfano uteuzi wa Waziri Mkuu, rais atashauriana na Makamo wa Rais. Wakurugenzi wa bodi, na wakuu wa taasisi za umma, rais atashauriana na mawaziri husika
Kazi ya washauri wote hawa ni kushauri tuu, na sio kumlazimisha rais kufuata ushauri wao. Hivyo katiba imempa rais mamlaka ya kupokea ushauri wowote, au kutopokea ushauri wowote ikiwepo mamlaka ya kupuuza ushauri wowote na rais akaamua vyovyote yeye mwenyewe na bado yuko right. Mfano kwenye uteuzi wa Kamishna wa Tume ya Kuzuia Madawa ya Kulevya, kanuni zinaelekeza Kamashna ni Ofisa wa Polisi mwenye cheo cha Commisioner na Waziri wa Mambo ya Ndani atapendekeza majina matatu kutoka kwa IGP, lakini Magufuli alipokuta nafasi hiyo iko wazi na hakuna mapendekezo yoyote, alitafuta mwenyewe mtu mwenye vigezo na kumteua.
Hivyo pamoja na hitaji kwa baadhi ya teuzi, rais apelekewe majina na tume za mapendekezo, bado rais anaweza kumteua yoyote, bila mapendekezo kutoka popote na bado rais akawa yuko right, kwa sababu kazi za hizi tume ni mapendekezo tuu, katiba yetu imempa rais wetu mamlaka huru kufikia maamuzi yeye mwenyewe kwa kufuata mapendekezo au bila kufuata mapendekezo yoyote kutoka kwa yeyote na uamuzi wa rais hauhojiwi na mamlaka yoyote!.
Zoezi la Uhakiki wa Vyeti Kwa Watumishi wa Umma.
Zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma, linawahusu waajiriwa wote wa utumishi wa umma, ambao ajira zao, ziliwahitaji kuwa sifa na vigezo vya elimu ya kiwango fulani, ili waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu, lakini zoezi hili haliwahusu wateule wa rais kwa sababu mamlaka ya rais kufanya uteuzi wowote, haukuweka sifa wala vigezo vya rais kuteua, hivyo rais anaweza kuteua hata mtu asiyejua kusoma wala kuandika, na akamuwekea mtu wa kumsomea na kumuandikia, yeye kazi yake ikabaki kusaini kwa saini ya dole gumba na bado rais akawa yuko right.
Waliohitimu Vyuo Vikuu Kwa Majina ya Wengine.
Elimu yoyote ni mali ya yule aliyeingia darasani, akasoma kwa kipindi husika, akafuzu, akahitimu, kuanzishia shule ya msingi hadi Chuo Kikuu, anayeipata elimu ile ni yule mtu aliyehudhuria masomo na kuhitimu, na jina la yule alihudhuria, na kuhitimu ni kitambulisho tuu cha mhitimu yule, anayehesabika kuhitimu ni yule mtu aliyehudhuria masomo na kuhitimi na sio lile jina, jina niutambulisho tuu.
Majina Bandia, Elimu Bandia, Kufoji Jina na Kufoji Vyeti.
Kuna tofauti ya mtu aliyefoji jina akasoma na kufauli kwa majina bandia, na mtu aliyefoji vyeti. Mfano mimi Paskali Mayalla, nilindikishwa shule ya msingi kwa jina la Pasiko Kashinde, nikafeli darasa la saba, au nikazungusha form four, hivyo nikatumia vyeti vya Paskali Mayalla kujiunga chuo kikuu. Nitakuwa nimefoji kujinga chuo kikuu kwa kutumia jina bandia, lakini aliyeingia darasani ni mimi, aliyehudhuria masomo ni mimi na nikahitimu kama Paskali Mayalla, hivyo mwenye hiyo elimu hiyo ya Chuo Kikuu ni mimi in person, regardless natumia jina gani, au nilitumia jina gani, kilichohitimu ni mimi na sio jina, hivyo naweza kwenda kwa wakili yoyote nikatengeneza affidavit ya kubadili jina na kutumia jina lolote, hivyo jina doesn't matter, haijalishi kama nilisoma sekondari au sikusoma, lakini nikaingia chuo kikuu na kuhitimu, mimi ni mhitimu wa chuo kikuu kwa kanuni ya the end justifies the means.
Hivyo nawaomba watu humu jf, msihamanike sana na majina ya watu waliotumia, ama kama walisoma sekondari au laa, as long as waliohitimu chuo kikuu ni wahitimu halali wa chuo kikuu na kuteuliwa kushika wadhifa wowote ni halali, wamesoma kwa kufoji jina na cheti kuingilia tuu chuo kikuu, lakini cheti cha kuhitimu chuo kikuu ni cheti halali kwa jina la kufoji, akiishaapishwa kwa wakili unahalalisha hilo jina la kufoji linakuwa jina halali!.
Paskali.