Umewahi kula papa? Mara ya mwisho lini?

Umewahi kula papa? Mara ya mwisho lini?

Omary mkali bingwa kabisa chuchu sound band aliwahi kuimba.

Papa mkubwa = PAPA
Papa mdogo je = KIPAPA

Eh, kwaheri
 
Mi sikumbuki lini ni kama mwaka Sasa. Kinachonifanya nsipende sana ni shombo yake.dizaini naifananisha na mk*j*..Ina shombo Kali nisamehewe😒
Pili ni chumvi nyingi sana.

Mie asili yangu ni pwani,hiyo ni kitu pendwa kule.wanapenda kavu au na muhogo.mhogo wa nazi au ugali wake wanaita bada.
Na pia kuunga mchuzi lazima bamia na nyanya chungu.

Mara ya mwisho kula papa ni lini?
Jamii yenu inakula?View attachment 3597452View attachment 3597453View attachment 3597454View attachment 3597455
Chumvi ni kutokana imekaushwa na kutumiwa chumvi kuifanya isiharibike si kwamba nyama yake ina chumvi. Hii ni chumvi ya kuwekwa. Hiyo nyama inachemshwa na kukaushwa ndiyo maana ipo hivyo
 
Tupe utofauti wake
Papa analiwa na kupikwa au kukaangwa akiwa mbichi au kubanikwa..
Ng'onda samaki yyte mkubwa au hata mdogo hukaushwa na kuwekewa chumvi ili kuliwa baadae akiwa mkavu..

Wavuvi wa Majarife\Nyavu chumvini wakikuta Jodari au Fulusi nk.wamekaa sana kwenye nyavu na teyari wamevunda.Hao samaki hawatupwi..Walitayarishwa na kuhifadhiwa kwa Chumvi\ Juani wawe Ng'onda. Kipindi cha Kusi samaki wanapoadimika Papa\Nguru\Ng'onda walitumika sana.
 
Binafsi sijawai kula hao papa, nguru ila nasikiaga wanadaresalama wakisema n'gonda Huwaga na harufu Kali sana akivunda JE? Kuna ukweli wowote
 
Back
Top Bottom