Umemsikia MUGABE alichomwambia OBAMA.?

Umemsikia MUGABE alichomwambia OBAMA.?

MUGABE ni kizazi cha akina NYERERE,NKURUMA,ISACK STEVEN,GAMAL ABEL NASSER,KENYATTA nk,MUSEVEN yeye ni ni wa kizazi cha ukoloni mamboleo,pamoja na mabaya yako yote kwa hili nmpongeza sana,huu sio utamaduni wetu waafrika hii ni laana ya wazungu,tuikimbie
 
Kwa nini hukumu ya mafisadi, wauza unga na hata majangili isiwe ndiyo kifo tena mbele ya umma?
Kwa nini uwe na hasira sana na watu kisa tu wameamua kubadili staili ya kufanya mapenzi, Kiranga amesema, tukiendekeza huu upuuzi mwishowe mtakuja kupiga marufuku hadi katerero.

Wewe unasema wasipopata mtoto ndiyo wauawe, hivi kwani kwenye ndoa ni lazima kupata mtoto?
Walioko kwenye ndoa za mwanaume na mwanamke, wasipopata mtoto nao wauawe?
Ningekuwa mm n mugabe. Ningewaruhusu ndoa zao ila kwa sharti moja tu. N kwamba watakao oana jinsia moja ni kwamba baadaa ya miaka mitatu wawe wameshazaa mtoto mmoja. Kma watakuwa hawajazaa hukumu yao ni kifo tena mbele ya umma...#

Hatutaki ushoga hapa....
 
Wewe Mjuni acha uhuni, usijifanye huoni kinachoendelea hapa. Suala hapa si kuponda ushoga, suala ni kuponda ushoga wakati ambao Marekani inakutaka ukumbatie ushoga kwa mashinikiso. Suala hapa ni nani ana ujasiri wa kupingana na sera na matakwa ya mataifa yenye nguvu. Iwe ni ushoga au ubepari (kipindi kile cha mwalimu), Hoja ya msingi sio kupinga ushoga hususani kwenye hili suala la Mugabe, Narudia tena hoja ya msingi ni uwezo wa kusema hapana mbele ya wanaojiona wakubwa wa hii dunia.

Acheni kupotosha hoja ya msingi!!!


Nimechelewa kuuona uzi huu lakini siwezi kuacha comment hii ipite bila kusema kitu.
Naunganana na wewe kwa asilimia 99.
Copy kwa Kiranga.
 
Tz haina Rais toka 2005 - To Date: Ikulu kuna muigizaji tu! Hata kama Mugabe kwenye baadhi ya mambo hawatendei haki wananchi wale lakini kuna mambo mengine msimamo wake unakuwa nguzo imara sio kama mzee wa tabasamu na kusafiri kila mara. Kuhusu mseveni japo ni dikiteta lakini kuhusu sheria aliyotia saini kwa ujumla inafaa sana hata hapa TZ tungekuwa na Rais jambo hilo lingekuwa muhimu katika nchi yetu lakini ndiyo hivyo Rais hatuna!
Yani haingi akilini kabsa kwa hapa tz kama jamaa hajasaini au hajaingia kwenye makubaliano yoyote dhidi ya ushoga kuna kitu kinaendelea chini ya kapeti maana ushoga umeenea sana hapa bara na zanzibar lakini hakuna kiongozi hata mmoja anaethubutu kukemea haya mambo....!!!
 
Mkuu Kiranga, waafrika tutaendelea kuwa wa mwisho kwa kila kitu hadi kiyama kwa sababu inawezekana kabisa akili zetu zina hitlafu.
Hiyo kauli ina nini cha maana hadi isifiwe?, bora hata angejenga hoja nzuri juu ya huo ushoga anaopinga kuliko kutoa kauli ya kipuuzi tu isiyo na staha, Ni ajabu kwa mpinga ushoga kutaka kuonyesha mfano kwa kuoa mwanaume mwenziye halafu wapinga ushoga wenzie wakashangilia.

Kweli huyu jamaa amewateka akili watu wa kauli za kipuuzi tu zisizokuwa na tija yeyote kwa taifa lake.

Ndugu yangu acha chuki kwa Rais Mugabe na kudhani kuwa Waafrica wanaopinga ushoga ni WAJINGA. Unajidanganya tu. Cavelli Sforva yule mtafiti wa Kiitaliono mwenye asili ya Marekani alishatoa jibu kuhusu tabia za kushiriki mapenzi ya jinsia moja. Ni kupoteza muda na kushabikia "mawazo potofu" ya Wazungu. Homosexuality is not inborn. Kuna "societies" baadhi haya mambo yahajulikani kabisa.

Eti nyie kwa sababu "mnajiona wa-ulaya" ndio mnadhani mbinu ya kuMkosoa Mugabe katika hii issue ya Ushoga ni kupima maendeleo duni ya Zimbabwe na kusema si unaona WATU WAKE WANAKULA PANYA. Hii si sawa hata kidogo.

Unaweza ukadhani "unajuuuuuuuuuua" kumbe haujui jamabo dogo linaloitwa "KUJUA MIPAKA YAKO" kwa jambo fulani.

Mimi naona matokeo ya Umasikini Zimbabwe wala sio kwa sababu Mugabe anapinga ushoga na udhalilishaji wa mapenzi ya jinsia moja. Je akiruhusu mambo yatakuwa sawa?

Kaa chini, jitoe kwenye "kichaka" cha "kudhani u-magharbi ndio suluhisho" fikiri kuhusu utu wako. Mwangalie mdogo wako mtoto wa jirani yako, na jiulize nini unawaza juu yao? Jione upo Africa, jua fedha na maisha ya kitajiri na uhuru uliopitiliza sio furaha ya dunia hii. Usitishwe na ugumu wa maisha ukadhalilisha utu wako. Wewe ni mtoto wa nyumba hii na nyumba hii ni Africa. Africa hatupendezwi na vitendo vya USHOGA kama vile ilivyo rushwa, ukatili, wizi na mmomonyoko wa maadili. Hivi vyote tunavipinga.

Daniel.
 
Ujasiri is overrated, hata Idi Amin alikuwa jasiri lakini mpu.mbavu. Jasiri anayeua maelfu ya raia zake na kusema wazi wazi kwamba ana degree ya violence sio wa kumshangilia.



Generalities are caves for ignorance.Specificity is king.



Kwa kuwa wanataka waafrika wafuate hayo ya kuruhusu ushoga.



Hili nimelisema hapo juu. Mahojiano ya Kikwete na Christian Amanpour yanaonesha hilo wazi. Viongozi wa Afrika wamesha give up ku negotiate mambo kama sovereigns. Kikwete anasema Waafrika watakubali haya mambo tu, ila hawawezi kukubali mara moja, itachukua muda, kwa hiyo wamagharibi wasiwe na shaka sana.



Katika hilo hata huyo Mugabe unayemsifia yumo, sasa nashangaa anasifiwa sana kwa kisa gani.



Kama Mugabe hana cha kupoteza ndio maana anaweza kuongea chochote kile, huwezi kusema ni jasiri.Jasiri ni yule atakaye blast licha ya kuwa na kitu cha kupoteza.



Hili haliondoi ukweli kwamba Mugabe ni chinjachinja anayejisifia kwa uchinjachinja wake waziwazi.



Obviously hunisomi. Nimesema hapo juu kwamba mimi falsafa yangu ni "Mambo ya Ngoswe muachie Ngoswe mwenyewe". Haki ya mashoga ni sawa na haki yako kuwa muislamu, mkristo au straight.

Kwa nini unafikiri mimi naunga mkono kupinga ushoga?

Mimi ninachowalaumu viongozi wa Afrika ni kukosa negotiation skills za ku ensure reciprocity, kwamba Wamagharibi wakitaka tkubali wanayosema wao (ushoga kwa mfano) na sisi tuwape ajenda zetu kwa habari hiyo hiyo ya human rights (ukewenza kwa mfano)

Siojawahi kuunga mkono kupinga habari ya jinsi watu wazima wawili wanavyotaka kujamiiana. Hizo ni habari binafsi zinazopaswa kulindwa na ustaarabu wa faragha katika jamii yoyote ya watu wenye kujiheshimu.

Tukianza kupangiana sheria za ushoga kesho tutaanza kupanga sheria za kukataza katerero, keshokutwa sheria za kupangiana goli ngapi mwanamme anapaswa kupiga, mtondogoo tuta appoint waziri wa kukagua k za wake zetu kama zimezidi kina kilichopitishwa na serikali.

We do not want the government in people's private lives.

It has enough work already in the public sphere.

Mambo ya Ngoswe, muachie Ngoswe mwenyewe.

USHOGA haukubaliki hata uupe jina lolote la kiustaarabu kama unavyofanya wewe kuuficha nyuma ya kimvuli cha haki za binadamu

Sio kila kitu mtu akitakacho au akifanyacho hata kama ni cha kishenzi na kifedhuli kitaacha tu eti kwa sababu ana haki ya kufanya hivyo. Ukiwa na haki haimaanishi ukanyage haki za wengine, Kama wewe ni shoga haimaanishi ujitangaze hadharani kuwa wewe ni shoga ili uharibu watoto wa wengine kimaadili na kiustaarabu.

Kwani kwa akili yako unafikiri TZ hakuna mashoga?!, Je Umeshaona Wanakamatwa na Kushtakiwa? Unahic ni kwanini?

Ni kwasababu wanafanya kwa utaratibu wao wanaoujua wao bila kuhitilafiana na ustaarabu wa wengine wasioamini ushoga na bila kuvunja sheria na haki za wengine napia bila kuhitilafiana na utamaduni tuliolelewa na sheria za imani zetu.

Tuacheni waafrica na ustaraabu wetu, nyinyi mashoga nendeni na ustaarabu wenu huko magharibi.
 
I love you comrade Mugabe. You are my role model. Mpe za uso tu hao hawana lolote. Wenzako wanajikombakomba tu na kutembeza bakuli huku wakitumalizia madini yetu na kampuni yao ya Barrick!!
 
USHOGA haukubaliki hata uupe jina lolote la kiustaarabu kama unavyofanya wewe kuuficha nyuma ya kimvuli cha haki za binadamu

Sio kila kitu mtu akitakacho au akifanyacho hata kama ni cha kishenzi na kifedhuli kitaacha tu eti kwa sababu ana haki ya kufanya hivyo. Ukiwa na haki haimaanishi ukanyage haki za wengine, Kama wewe ni shoga haimaanishi ujitangaze hadharani kuwa wewe ni shoga ili uharibu watoto wa wengine kimaadili na kiustaarabu.

Kwani kwa akili yako unafikiri TZ hakuna mashoga?!, Je Umeshaona Wanakamatwa na Kushtakiwa? Unahic ni kwanini?

Ni kwasababu wanafanya kwa utaratibu wao wanaoujua wao bila kuhitilafiana na ustaarabu wa wengine wasioamini ushoga na bila kuvunja sheria na haki za wengine napia bila kuhitilafiana na utamaduni tuliolelewa na sheria za imani zetu.

Tuacheni waafrica na ustaraabu wetu, nyinyi mashoga nendeni na ustaarabu wenu huko magharibi.

Kama nilivyosema mwanzo.

Pigeni marufuku movies za Hollywood, muziki wa magharibi na nguo zao basi.

Sio mbaki kushadadia kauli za viongozi tu huku hamtengenezi hata pini.

Mpaka chupi watu wanavaa za mtumba, bila kujali zimevaliwa na shoga au la.

Leo nilikuwa nasikiliza wimbo mmoja wa bongoflava Bongoradio.com . Kijana anaongelea jinsi baba hataki utamaduni wa kigeni lakini vijana wanaona ndiyo fasheni ya sasa.

Nikakumbuka maneno yangu niliyoandika hapa kwamba kama Waafrika wako serious kwenye kukataa ushoga, wasiishie kushabikia kauli za magirini tu za viongozi kama Mugabe ambao hawawezi kuongelea uchumi wala siasa kwa sababu wameboronga sana humo, wanaishia kuongelea habari za ushoga.

Waafrika inabidi wajenge mifumo yao ambayo itakuwa hairuhusu ushoga.

Siyo leo unakataa ushoga hapa kesho ndiyo wa kwanza kuagizia series na movies za Hollywood zilizojaa ushoga, na kuvaa mitumba ya "unisex" wanayopenda mashoga bila hata kujijua.
 
and vice versa is also true

To the contrary.

A positive can be proven.

Kama Mugabe kasema maneno hayo, unaweza kuweka video, audio, link to a reputable news source etc.

Hujafanya hilo.

Kama hajasema nitawekaje link kuonesha kwamba hajasema?
 
Kwa kifupi tu viongozi wa Tanzania na Zimbabwe wanaboronga kwa sababu hawana sifa za uongozi wa kutatua matatizo ya wananchi wao. Kukemea wazungu au mitindo ya maisha yao haipo katika vigezo au sifa za viongozi bora. Kwa mtaji huu ujasiri wa Mugabe ni maonyesho ya pembeni tu ambayo hayaongezi ufanisi wa kazi yake kama rais au kuwa kiongozi bora kuliko wale wasiokemea wazungu.

Nahisi hufikirii vizuri

Hizo sifa za viongozi bora ni zipi na ni nani alikupa au kukufundisha kama sio haohao wazungu?! na unafikiri kwanini hawakuweka hiyo sifa ya hapo kwenye red kuwa sifa ya kiongozi bora.

Unahici tukikukabidhi wewe nafasi ya hao unaowaita sio viongozi bora utaweza kuyafanya hayo yatakayo kupa sifa za kiongozi bora? NI BORA WAO MUGABE NA MUSEVENI WAMEFANYA WANAYOWEZA BADALA Y AKUFANYA WANAYOTAMANI KUFANYA HATA KAMA HWATAWEZA.

Je! Unahici kutowakemea Wazungu kunamfanya kiongozi kuwa Bora, au kunaleta tija kwenye maisha ya Mtanzania,

Sitaki kusadiki kwamba hujui kihistoria na kimwenendo wa hiio dunia sasa wazungu ni watu wa kuturudisha nyuma kwenye nyanja yoyote ile ili tubaki tegemezi. SASA UNASEMA TUSIWAKEMEHE?! Duh
 
Mnamsifia mjinga huyo alichukuwa nchi ikiwa first world kaifanya third world na nusu ya wananchi wake wameishia ukimbizini kuwa manamba..poleni kwa ujinga

Ka uelewe uwezi kuwa na rafiki mzungu ata siku moja, walioiua nchi ni wazungu baada ya kuweka vikwazo vya kiuchumi mara baada ya kuwafukuza kwenye mashamba akawapa wananchi wake, mzungu atakaa nawe kwa amani kama unampatia maslai yake na anakonyonya, kama utaki atasababisha ata vita kwa kufadhili waasi ili apate anachokita
 
Fuatilia kwenye comment yangu ya mwanzo mkuu. Nilishasema kama hii ni habari ya kweli.

Mkuu usiangaike, Haijalishi Mugabe amesema kweli au laa, Kikubwa hapa ni kuangalia umadhubuti wa kilichosemwa hata kama mtoa mada ametunga, Kwani sio kweli kwamba Waafrica wengi tunakerwa na ushoga, Na Je! Sio kweli kwamba Uingereza na Marekani wamekuwa wakitulazimisha kukubali ushoga kwa visingizio vya haki za binadamu na kutuwekea vikwazo?

Tuache kujadili event ya Mugabe kusema au kutosema na tujadili issue yenyewe kama ina-make sense au laa.
 
Inastaajabisha sana pale ambapo watu wanashabikia hawa viongozi wa Kiafrika kudai kukataa kuambiwa na nchi za Magharibi namna ya kuendesha nchi zao ilhali hao hao viongozi wa Kiafrika wanasaini sheria zinazowapangia wengine namna ya kuishi maisha yao.
 
Zakumi
Ulichoongea hakina mantiki; matatizo ya kiuchumi katika nchi za Afrika ni matokeo siasa za kibeberu; mfano halisi ni Zimbabwe walijaribu ili kuleta machafuko ya kisiasa; wameshindwa; Afrika wapo viongozi bora wenye lengo la kumkomboa mwafrika! Kwenye siasa huwezi kumridhisha kila mtu hata hapa US wapo wanamuona Obama hafanyi kitu.


Ahsante sana Mkuu! kuna watu shule walienda kujifunza kusoma na kuandika tuu nasio kuelewa kingine chochote, Nahici Zakumi ni mmoja wao.
 
Ngoja nikukubalie kuwa matatizo ya kiuchumi katika nchi za africa ni matokeo ya ubeberu. Katika vitabu vya sifa za kupigana na ubeberu na kuondoa matatizo ya uchumi wa nchi za kiafrika, kukemea mitindo ya maisha ya nchi za magharibi sio sifa ya kiongozi na sio zana ya kupinga ubeberu.

Mitindo ipi? Je walitaja ushoga katika hicho kitabu? tutajie jina nasisi tukakisome.
 
MImi nasikitika sana hii kitu kupewa jina la ushoga wakati jina lenyewe ni Use-nge. Shoga sio jina halisi la hii tabia lazima tuwe wakweli!!
 
"If Obama wants me to allow gays marriage in Zimbabwe,I should marry him first to show the good example"-Robert Mugabe..

Ndio huyu huyu mzee,ambaye alipoulizwa na wanahabari wa Uingereza kuwa kwanini asiachie ngazi ilhali ameshazeeka, aliwauliza kama walishawahi kumuuliza swali kama hilo malkia wao..

Salute kwako uncle mugabe..
Asante sana mzee wa ukweli
 
MImi nasikitika sana hii kitu kupewa jina la ushoga wakati jina lenyewe ni Use-nge. Shoga sio jina halisi la hii tabia lazima tuwe wakweli!!

Hata us.enge nalo si jina halisi, msen.ge ni yule passive, yule active ni basha. "Ushoga" unataka kuwajumuisha wote pamoja. Ingawa "shoga" katika Kiswahili ni rafiki wa karibu sana, hususan kwa wanawake.

Hata kiingereza kuna mama mmoja nilikuwa naongea naye, anasema yeye hana tatizo na haya mambo ya gays, tatizo lake ni kwamba wamelichukua hili neno la "gay" ambalo lilikuwa likimaanisha "furaha" na kulipa maana tofauti kabisa.

Akasema "You can't even say " we had a gay old time" anymore without risking being misinterpreted".

Ni kama vile mwanamke wa Kiswahili akisema "huwezi kusema "huyu shoga yangu" bila ya kujistukia kwamba anaweza kutafsiriwa vibaya".
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom