Umemsikia MUGABE alichomwambia OBAMA.?

Umemsikia MUGABE alichomwambia OBAMA.?

Mosi, tunarudi pale pale kuwa unaamini kile unachojua wewe ndio ukweli. Eti huwezi kusema!!! Kwa mujibu wa nani?? Wewe?!!. Pili, naomba unithibitishie hiyo kauli kwenye nyekundu hapo au na wewe ndio kama huyu jamaa na Mugabe wake?
Hiyo ya kuuliza ni kwa mujibu wa nani nimeijibu katika posti yangu #140 , hilo la Saudia kuwatengea wanawake mji wao ni kweli, hiyo habari imeandikwa sana na magazeti na hata humu JF imo, usishabikie tu kuzuia mitindo ya mavazi bila kujua repercussions zake.
 
Hili suala la ushoga limepamba moto miaka ya karibuni. Mugabe yupo madarakani kwa zaidi ya miaka 30. Kama yeye ni kiongozi mahiri basi angetatua matatizo ya wananchi wake kabla suala ushoga alijaanza.
Hawezi kutatua kitu, na anajua ili waafrika waendelea kumuona, simba wa Afrika, kidume, mzalendo, shujaa na heshima nyingine nyingi asizozistahili ni kuponda tu ushoga, as simple as that, you win Africans.
 
Kabla ya kwenda mbali kwenye kuuliza ni binafsi kwa tafsiri ya nani, naomba nikuulize, wewe unaona kuwa mapenzi ni suala la public?
Tunajuaje kwamba hiki ni sahihi na hiki sio sahihi?, au hiki ni public na hiki ni private?, tafsiri ni ya nani?, naomba nitumie kiingereza.

There are universal fundamental principles to define things which are obtained due to intuitive judgements, ndio maana tunasema, kila mtu anao uhuru wa kuwa na maoni na mtazamo wake lakini hakuna mtu mwenye haki ya kuwa na ukweli wake peke yake.
Andika kiswahili twende vizuri. Tatizo lenu mnafikiri kama wazungu halafu mnadhani kwamba mna suluhu za matatizo ya waafrika!!!
 
Hawezi kutatua kitu, na anajua ili waafrika waendelea kumuona, simba wa Afrika, kidume, mzalendo, shujaa na heshima nyingine nyingi asizozistahili ni kuponda tu ushoga, as simple as that, you win Africans.
Wewe Mjuni acha uhuni, usijifanye huoni kinachoendelea hapa. Suala hapa si kuponda ushoga, suala ni kuponda ushoga wakati ambao Marekani inakutaka ukumbatie ushoga kwa mashinikiso. Suala hapa ni nani ana ujasiri wa kupingana na sera na matakwa ya mataifa yenye nguvu. Iwe ni ushoga au ubepari (kipindi kile cha mwalimu), Hoja ya msingi sio kupinga ushoga hususani kwenye hili suala la Mugabe, Narudia tena hoja ya msingi ni uwezo wa kusema hapana mbele ya wanaojiona wakubwa wa hii dunia.

Acheni kupotosha hoja ya msingi!!!
 
Wapi nimewananga Waafrika? Kivipi?

Kuhoji source za habari sijaanza leo, utasemaje najidai nimeliona hilo?

Post ya kwanza, ile niliyoitoa kabla ya kuhoji uhakiki wa habari hii, ilihusu habari ilivyopokelewa hapa JF, which is a fact regardless of the veracity of the news.

Baada ya kusema watu wanakuwa sidetracked kuacha kuangalia mambo muhimu kwa habari za ushoga, nikazama zaidi kuanza kuangalia kama hata hizo habari zenyewe ni za kweli au zimepandikizwa tu, katika jibu langu kwa Mjuni Lwambo.

Ningesema "Mugabe mpuuzi sanan kwa kutoa kauli hii" ungeweza kusema kwamba nimeikubali kauli kwamba imetolewa na Mugabe, which is far from the case.

Nimeobserve tu kwamba waafrika wengine wanapenda sarakasi zaidi ya maendeleo. Kitu ambacho wewe kwa kichwapanzi chako huwezi kutofautisha kati ya waafrika wengi na waafrika.

Kuhusu mimi kutokukosea hiyo ni inferiority complex yako tu.
"Inferiority Complex"??!! Endelea kuota....(Unajiona ukoo juu sana eeh?!!!!!)

Turudi kwenye mada. Ngoja nikupe mfano wa kawaida kabisa labda utaelewa, Chukulia una baba ambaye ni bazazi haswa, kuacha hela ya msosi nyumbani ni majanga pamoja na kuwa anakulimisha, saa nyingine anakupiga na pengine akinunua chakula anakusimanga. Kwa upande mwingine kuna bazazi jingine mtaani tuliite Bzk lina nguvu sana kiasi kwamba likiamua linamlawiti yeyote bila ridhaa yake hata kama yeye na familia yake yote watapinga. Sasa chukulia kwamba imefika kipindi imeshazoeleka kiasi kwamba kila mtu anaogopa kupinga na huyu Bzk anafanya anachotaka bila upinzani.

Kwa maana hiyo basi siku yoyote Bzk anaweza kugonga mlango wenu na kutaka huduma ya 0713 kutoka kwako wewe Kiranga, chukulia kuwa hupendelei wala hutaki kusikia hizi habari (kwa kifupi huwezi hata kufikiria kufanyiwa hivyo). Lakini kwa nguvu alizonazo Bzk unajua kuwa akigonga mlango na kuomba mzigo lazima utatoa japo hupendi. Bahati nzuri kwako au mbaya kwa Bzk, baba yako ambaye naye ana ubazazi wake anatangaza hadharani kuwa, nyumbani kwake hawezi kuruhusu Bzk afanye chochote na akijaribu ama zake ama za Bzk. Wewe Kiranga hutamshangilia baba yako japokuwa ni bazazi?

Kama hutamshangilia baba yako kwa mfano huu hapo juu basi, ninakubaliana nawe kuwa wanaoshabikia hii habari hawako sahihi.
 
Kwa hiyo kutohadaiwa ni kukubaliana na kile unachofikiri wewe kuwa ni sahihi??!!!

Kutohadaiwa ni vile uonavyo wewe.

Kama wanawake wanamuunga mkono wewe unashangaa nini??

Nashangaa wao kumuunga mkono!!

Umeambiwa kuwa wanawake wote ni lazima waunge mkono uvaaji wa vimini??!!

Hapana, sijaambiwa.

Kwani kama unaona kuvaa chupi barabarani ni sawa, kuna tatizo gani mwingine akiona si sawa??

Kama suala ni la kuona (maoni) tu basi sina tatizo endapo mwingine akiona tofauti na nionavyo mimi.

Tatizo langu ni pale huyo mwingine anapoamua kupandikiza hayo maoni yake kwa wengine na kuwataka wayafuate.

Iweje utake watu wote wawe na maoni kama yako??

Nimetaka wapi?
 
"Inferiority Complex"??!! Endelea kuota....(Unajiona ukoo juu sana eeh?!!!!!)

Turudi kwenye mada. Ngoja nikupe mfano wa kawaida kabisa labda utaelewa, Chukulia una baba ambaye ni bazazi haswa, kuacha hela ya msosi nyumbani ni majanga pamoja na kuwa anakulimisha, saa nyingine anakupiga na pengine akinunua chakula anakusimanga. Kwa upande mwingine kuna bazazi jingine mtaani tuliite Bzk lina nguvu sana kiasi kwamba likiamua linamlawiti yeyote bila ridhaa yake hata kama yeye na familia yake yote watapinga. Sasa chukulia kwamba imefika kipindi imeshazoeleka kiasi kwamba kila mtu anaogopa kupinga na huyu Bzk anafanya anachotaka bila upinzani.

Kwa maana hiyo basi siku yoyote Bzk anaweza kugonga mlango wenu na kutaka huduma ya 0713 kutoka kwako wewe Kiranga, chukulia kuwa hupendelei wala hutaki kusikia hizi habari (kwa kifupi huwezi hata kufikiria kufanyiwa hivyo). Lakini kwa nguvu alizonazo Bzk unajua kuwa akigonga mlango na kuomba mzigo lazima utatoa japo hupendi. Bahati nzuri kwako au mbaya kwa Bzk, baba yako ambaye naye ana ubazazi wake anatangaza hadharani kuwa, nyumbani kwake hawezi kuruhusu Bzk afanye chochote na akijaribu ama zake ama za Bzk. Wewe Kiranga hutamshangilia baba yako japokuwa ni bazazi?

Kama hutamshangilia baba yako kwa mfano huu hapo juu basi, ninakubaliana nawe kuwa wanaoshabikia hii habari hawako sahihi.

An excessive amount of irrelevant hypotheticals.
 
Kutohadaiwa ni vile uonavyo wewe.

Nashangaa wao kumuunga mkono!!

Hapana, sijaambiwa.

Kama suala ni la kuona (maoni) tu basi sina tatizo endapo mwingine akiona tofauti na nionavyo mimi.

Tatizo langu ni pale huyo mwingine anapoamua kupandikiza hayo maoni yake kwa wengine na kuwataka wayafuate.

Nimetaka wapi?
Hata kuvaa chupi ni kulazimisha wengine waone uchi wako hata kama hawataki, kumbuka sizungumzii kutazama nazungumzia kuona!!!!
 
Hata kuvaa chupi ni kulazimisha wengine waone uchi wako hata kama hawataki,

Kwanza, kama umevaa chupi wengine watauonaje uchi wako?

Pili, kinachodaiwa kupigwa marufuku Uganda si utembeaji uchi. Ni uvaaji wa nguo fupi.

Tatu, katika kuona kwa macho hakuna kulazimishana maana macho ni yako na una hiari ya kuyafumba na kuyafumbua. Hivyo huna hoja hapo unless uje na habari za watu kufumbuliwa macho yao kwa nguvu ilhali wameyafumba kwa sababu hawataki kuona kitu au jambo.

kumbuka sizungumzii kutazama nazungumzia kuona!!!!

Tofauti ya kutazama na kuona ni nini?
 
Kwanza, kama umevaa chupi wengine watauonaje uchi wako?

Pili, kinachodaiwa kupigwa marufuku Uganda si utembeaji uchi. Ni uvaaji wa nguo fupi.

Tatu, katika kuona kwa macho hakuna kulazimishana maana macho ni yako na una hiari ya kuyafumba na kuyafumbua. Hivyo huna hoja hapo unless uje na habari za watu kufumbuliwa macho yao kwa nguvu ilhali wameyafumba kwa sababu hawataki kuona kitu au jambo.

Tofauti ya kutazama na kuona ni nini?
Moja achana na uchi, hata mapaja kama watu hawatopenda kuona unaweza kuwaingilia kwa kuwalazimisha kuyaona. Pili kuona si hiyari, kuona ni pale ambapo umetupa macho upande fulani katika hali ya kugeuka au kugeuza shingo au huta kuelekeza uso mbele yako. Katika hali hiyo chochote ambacho jicho lako litakutana nacho litaona upende au usipende. Kwenye kutazama ni tofauti kidogo, hapo ndipo hiyari inapokuja. Ni ile hali unajua kabisa unageuza shingo kwa madhumuni ya kupata taswira ya kitu fulani, kama vile unavyoamua kuangalia runinga. Kwa mfano, unatembea wewe na dada yako, kwa bahati upepo mkali unavuma na kumfunua dada na wewe wakati huohuo ulikuwa unaangalia upande, hapo utakuwa umeona, lakini ukiamua kuendelea kumwangalia dada yako kwa kuwa bado yuko uchi basi unakuwa unatazama.
 
Moja achana na uchi,

Dalili za kushindwa hoja hizi! Mambo ya uchi umeyaleta mwenyewe halafu sasa unanambia niachane nayo. Unaanza kuhaha na kubadili magoli. Hamna shobo. Twende hivyo hivyo tu.

hata mapaja kama watu hawatopenda kuona unaweza kuwaingilia kwa kuwalazimisha kuyaona.

Kama wapo ambao hawatopenda kuona vivyo hivyo tupo ambao tunapenda kuona mapaja. Wasiopenda, kama nilivyosemaa (andika) awali wana hiari ya kutoangalia. Wanaweza wakafumba macho, wakageuza vichwa kuangalia mengine, au hata kuinamisha kichwa kama hawana kingine cha kutazama.

Pili kuona si hiyari, kuona ni pale ambapo umetupa macho upande fulani katika hali ya kugeuka au kugeuza shingo au huta kuelekeza uso mbele yako. Katika hali hiyo chochote ambacho jicho lako litakutana nacho litaona upende au usipende.

Sasa ukigeuza shingo na kwa bahati mbaya ukaona kitu ambacho hakikupendezi machoni ya nini tena kuendelea kuangalia? Si ugeuze tu shingo yako kwingine. We vipi wewe?

Kwenye kutazama ni tofauti kidogo, hapo ndipo hiyari inapokuja. Ni ile hali unajua kabisa unageuza shingo kwa madhumuni ya kupata taswira ya kitu fulani, kama vile unavyoamua kuangalia runinga.

Unavyoamua kutazama runinga au kuangalia runinga? Unaanza kujichanganya mwenyewe kwa maneno yako!!

Kwa mfano, unatembea wewe na dada yako, kwa bahati upepo mkali unavuma na kumfunua dada na wewe wakati huohuo ulikuwa unaangalia upande, hapo utakuwa umeona, lakini ukiamua kuendelea kumwangalia dada yako kwa kuwa bado yuko uchi basi unakuwa unatazama.

Unachofanya sasa ni kutenganisha unywele tu!!
 
Moja achana na uchi, hata mapaja kama watu hawatopenda kuona unaweza kuwaingilia kwa kuwalazimisha kuyaona. Pili kuona si hiyari, kuona ni pale ambapo umetupa macho upande fulani katika hali ya kugeuka au kugeuza shingo au huta kuelekeza uso mbele yako. Katika hali hiyo chochote ambacho jicho lako litakutana nacho litaona upende au usipende. Kwenye kutazama ni tofauti kidogo, hapo ndipo hiyari inapokuja. Ni ile hali unajua kabisa unageuza shingo kwa madhumuni ya kupata taswira ya kitu fulani, kama vile unavyoamua kuangalia runinga. Kwa mfano, unatembea wewe na dada yako, kwa bahati upepo mkali unavuma na kumfunua dada na wewe wakati huohuo ulikuwa unaangalia upande, hapo utakuwa umeona, lakini ukiamua kuendelea kumwangalia dada yako kwa kuwa bado yuko uchi basi unakuwa unatazama.

Ngoja mimi nikubaliane na wewe. Je hao wanawake wakishavaa mavazi kwa kutumia vigezo vyako wanapatiwa haki zao za kimsingi za kibinadamu au kutambuliwa mchango wao katika jamii?
 
Si ndiyo hicho!!!.
Mimi sijapotosha chochote, unachosema ndicho ninachosema, hoja kuu hapa ni kuonekana unawapinga wakubwa wa dunia, basi.
Mugabe alishasoma saikolojia ya waafrika, huhitaji kuumiza kichwa. Sema tu hapana kwa wanachosema wazungu, bila kujali hiyo hapana inawasaidiaje wananchi wako, you win Africans, utaonekana kidume. "Kambishia Obama"
Mugabe ataendelea kung'ang'ania madaraka na kuifukarisha nchi, huku yeye na familia yake wakiishi maisha mazuri.
Wewe Mjuni acha uhuni, usijifanye huoni kinachoendelea hapa. Suala hapa si kuponda ushoga, suala ni kuponda ushoga wakati ambao Marekani inakutaka ukumbatie ushoga kwa mashinikiso. Suala hapa ni nani ana ujasiri wa kupingana na sera na matakwa ya mataifa yenye nguvu. Iwe ni ushoga au ubepari (kipindi kile cha mwalimu), Hoja ya msingi sio kupinga ushoga hususani kwenye hili suala la Mugabe, Narudia tena hoja ya msingi ni uwezo wa kusema hapana mbele ya wanaojiona wakubwa wa hii dunia.

Acheni kupotosha hoja ya msingi!!!
 
Waafrika wengi kuwapoteza lengo ni kazi rahisi sana.

Watajie habari za wakoloni, wazungu, utumwa, new world order, ushoga, maadui wa nje, maadui wa ndani, wasaliti, waliokosa uzalendo etc etc.

Utawaibia mabilioni kwa mabilioni huku wanakupigia makofi.

Wengi wanataka waigizaji na vitongozi.

Hawataki viongozi.

Sasa mtu kama Mugabe baada ya mauaji yote na economic mismnagement aliyoifanya Zimbabwe naye ni wa kusifiwa?

Kisa?

Kawatongoza waafrika masikini vizuri na kujipa image ya mpinga wazungu!

Wanaomsifia Mugabe wanajua jinsi gani alivyoua wa Ndebele?

Someni Gukurahundi

http://en.m.wikipedia.org/wiki/Gukurahundi

Wewe unafikiri kila kinachoandikwa juu ya viongozi wa Africa( wanaopingana na wazungu) ni kweli bila kujua wakat mwingine ni trick za wazungu kuharibu utawala wa waafrika, ndo mana unaambiwa akili za kuambiwa changanya na za kwako: au ulitaka kuona mapandikizi wa kizungu watutawale ili kusave interests za wazungu?
 
Let's get specific, generalities are caves for ignorance.

Mugabe aliafiki a systemic killings of 20,000 Ndebele au ni propaganda za west tu?

Mismanagement ya uongozi wa Mugabe imesababisha superhyperinflation Zimbabwe au ni propaganda za wamagharibi tu?

Halafu kusema "wazungu" kuna betray racism. The west need not be "wazungu".

The president of rge US is Mr. Obama, not a mzungu. The Attorney General is Eric Holder, not a mzungu.

Is this the kind of reductivism I have to deal with?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom