Umemsikia MUGABE alichomwambia OBAMA.?

Umemsikia MUGABE alichomwambia OBAMA.?

Nahisi hufikirii vizuri

Hizo sifa za viongozi bora ni zipi na ni nani alikupa au kukufundisha kama sio haohao wazungu?! na unafikiri kwanini hawakuweka hiyo sifa ya hapo kwenye red kuwa sifa ya kiongozi bora.

Unahici tukikukabidhi wewe nafasi ya hao unaowaita sio viongozi bora utaweza kuyafanya hayo yatakayo kupa sifa za kiongozi bora? NI BORA WAO MUGABE NA MUSEVENI WAMEFANYA WANAYOWEZA BADALA Y AKUFANYA WANAYOTAMANI KUFANYA HATA KAMA HWATAWEZA.

Je! Unahici kutowakemea Wazungu kunamfanya kiongozi kuwa Bora, au kunaleta tija kwenye maisha ya Mtanzania,

Sitaki kusadiki kwamba hujui kihistoria na kimwenendo wa hiio dunia sasa wazungu ni watu wa kuturudisha nyuma kwenye nyanja yoyote ile ili tubaki tegemezi. SASA UNASEMA TUSIWAKEMEHE?! Duh

Endelea kumlaumu mzungu kwa kila kitu. Hata ukijisaidia barabarani hilo ni kosa la mzungu.
 
Hujaeleweka mkuu, nenda kajipange halafu ndiyo uje tena......
Hamna cha kujipanga hapa, we have debated this over and over and over, even on the Museven saga.
Waafrika kuwaibia ni rahisi tu, pinga ushoga, utumwa, wazungu, ongelea freemason na vitu vya aina hiyo.
Endeleeni tu kuwaona ni true son of afrika eti kisa wamepinga ushoga, wakati ni majizi makubwa hayaumizwi hata na umasikini wa nchi zao.
 
Bado naona hujasimama vyema..... maana hapa hoja ni kupinga maadili mabovu...... na hilo Mugabe nampa.... big up....
Likija suala la uwizi wao nalo tutajadili hilo kwa kina...... kwenye hili la wa..fi raji.... naomba tuungane kumpa heko Mugabe.....
 
Hata us.enge nalo si jina halisi, msen.ge ni yule passive, yule active ni basha. "Ushoga" unataka kuwajumuisha wote pamoja. Ingawa "shoga" katika Kiswahili ni rafiki wa karibu sana, hususan kwa wanawake.

Hata kiingereza kuna mama mmoja nilikuwa naongea naye, anasema yeye hana tatizo na haya mambo ya gays, tatizo lake ni kwamba wamelichukua hili neno la "gay" ambalo lilikuwa likimaanisha "furaha" na kulipa maana tofauti kabisa.

Akasema "You can't even say " we had a gay old time" anymore without risking being misinterpreted".

Ni kama vile mwanamke wa Kiswahili akisema "huwezi kusema "huyu shoga yangu" bila ya kujistukia kwamba anaweza kutafsiriwa vibaya".

kama ni hivyo basi mabasha waitwe hivyo na wale wengine wase'nge ili kutofautisha neno ushoga!!
 
Siwezi kuwapa heko Mugabe wala Museven kwa sababu wanafanya hivyo kwa nia ovu, watu wengi ukiwemo wewe huwezi kuliona hilo. Nguvu kubwa inayoonyeshwa katika kupinga ushoga ina lengo la kuwazubaisha ili waendelee kuiba na kuzifukarisha nchi zao.

Museven kabla ya hapo alikuwa amesha challengiwa na Obama kwa nini hataki kuachia madaraka kwa waganda wengine, Jamaa ana akili sana, kasaini makusudi, Obama akinyanyua tena sauti yake jamaa atajitetea tu kuwa anamuandama kwa sababu amezuia ushoga, ataendelea kujiibia kiulani tu na kama ilivyo kwa Mugabe, naye atatawala milele.
Bado naona hujasimama vyema..... maana hapa hoja ni kupinga maadili mabovu...... na hilo Mugabe nampa.... big up....
Likija suala la uwizi wao nalo tutajadili hilo kwa kina...... kwenye hili la wa..fi raji.... naomba tuungane kumpa heko Mugabe.....
 
Siwezi kuwapa heko Mugabe wala Museven kwa sababu wanafanya hivyo kwa nia ovu, watu wengi ukiwemo wewe huwezi kuliona hilo. Nguvu kubwa inayoonyeshwa katika kupinga ushoga ina lengo la kuwazubaisha ili waendelee kuiba na kuzifukarisha nchi zao.

Museven kabla ya hapo alikuwa amesha challengiwa na Obama kwa nini hataki kuachia madaraka kwa waganda wengine, Jamaa ana akili sana, kasaini makusudi, Obama akinyanyua tena sauti yake jamaa atajitetea tu kuwa anamuandama kwa sababu amezuia ushoga, ataendelea kujiibia kiulani tu na kama ilivyo kwa Mugabe, naye atatawala milele.

Kwan wewe Obama Umemuona Mungu kwamba kila anachosema ni sahihi? Wewe unafikiri Obama anawapenda waafrika?

Usiwe mjinga, all they say is for their own interests n not yours at all,Huyo unayemuita Obama na wenzie wa magharibi mikono yao imejaa damu za roho na mali za wa africa, they ar killer monsters.

Kama unazijua haki za binadamu nenda deep kwenye imani yako ya kidini then u appeal to God yeye ndio wa kwanza kuforbid this and go against what u call human rights. TO HELL U N UR GOD DAMNED HUMAN RIGHTS.
 
Kama nilivyosema mwanzo.

Pigeni marufuku movies za Hollywood, muziki wa magharibi na nguo zao basi.

Sio mbaki kushadadia kauli za viongozi tu huku hamtengenezi hata pini.

Mpaka chupi watu wanavaa za mtumba, bila kujali zimevaliwa na shoga au la.

Leo nilikuwa nasikiliza wimbo mmoja wa bongoflava Bongoradio.com . Kijana anaongelea jinsi baba hataki utamaduni wa kigeni lakini vijana wanaona ndiyo fasheni ya sasa.

Nikakumbuka maneno yangu niliyoandika hapa kwamba kama Waafrika wako serious kwenye kukataa ushoga, wasiishie kushabikia kauli za magirini tu za viongozi kama Mugabe ambao hawawezi kuongelea uchumi wala siasa kwa sababu wameboronga sana humo, wanaishia kuongelea habari za ushoga.

Waafrika inabidi wajenge mifumo yao ambayo itakuwa hairuhusu ushoga.

Siyo leo unakataa ushoga hapa kesho ndiyo wa kwanza kuagizia series na movies za Hollywood zilizojaa ushoga, na kuvaa mitumba ya "unisex" wanayopenda mashoga bila hata kujijua.

FYI, Kila nchi inachombo cha kuratibu, na kuhakiki hivyo vitu unavyosema kulingana na maadili yao, hata sisi tunacho na kama huna taarifa kuna msanii mmoja mkubwa tu hapa Bongo alitunga filamu yake yenye Maudhui hayo na akaipa jina shoga hicho chombo cha kuratibu kikaipiga chini fasta mno

WE will kill a snake no matter its color, Tutapinga Ushoga na kila kitu if that is what it takes to preserve our diginity.
Na tutafanya kila kitu hata kama kuwakagua makalio stupid! Mungu ibariki TZ, Mungu ibariki Africa
 
Ndugu yangu acha chuki kwa Rais Mugabe na kudhani kuwa Waafrica wanaopinga ushoga ni WAJINGA. Unajidanganya tu. Cavelli Sforva yule mtafiti wa Kiitaliono mwenye asili ya Marekani alishatoa jibu kuhusu tabia za kushiriki mapenzi ya jinsia moja. Ni kupoteza muda na kushabikia "mawazo potofu" ya Wazungu. Homosexuality is not inborn. Kuna "societies" baadhi haya mambo yahajulikani kabisa.

Eti nyie kwa sababu "mnajiona wa-ulaya" ndio mnadhani mbinu ya kuMkosoa Mugabe katika hii issue ya Ushoga ni kupima maendeleo duni ya Zimbabwe na kusema si unaona WATU WAKE WANAKULA PANYA. Hii si sawa hata kidogo.

Unaweza ukadhani "unajuuuuuuuuuua" kumbe haujui jamabo dogo linaloitwa "KUJUA MIPAKA YAKO" kwa jambo fulani.

Mimi naona matokeo ya Umasikini Zimbabwe wala sio kwa sababu Mugabe anapinga ushoga na udhalilishaji wa mapenzi ya jinsia moja. Je akiruhusu mambo yatakuwa sawa?

Kaa chini, jitoe kwenye "kichaka" cha "kudhani u-magharbi ndio suluhisho" fikiri kuhusu utu wako. Mwangalie mdogo wako mtoto wa jirani yako, na jiulize nini unawaza juu yao? Jione upo Africa, jua fedha na maisha ya kitajiri na uhuru uliopitiliza sio furaha ya dunia hii. Usitishwe na ugumu wa maisha ukadhalilisha utu wako. Wewe ni mtoto wa nyumba hii na nyumba hii ni Africa. Africa hatupendezwi na vitendo vya USHOGA kama vile ilivyo rushwa, ukatili, wizi na mmomonyoko wa maadili. Hivi vyote tunavipinga.

Daniel.

Dah! MKuu Sema tu dadaangu ameshaolewa ungejipatia mke bureeeee. Well said GT.
 
Hahahaaaaaa! I hope u wont be calling u r self " MESIAH" one of these comin' dayz bucko.

Mugabe alifanya mapenzi akiwa ndani ndoa na mke wa mtu na kuzaa naye mtoto. Hakuna mtu aliyeonyesha kidole kumwambia kuwa alichofanya sio sawa na maadili ya kiafrika au ya kidini.

Kuna tofauti gani kufanya mapenzi na mke watu, kufanya mapenzi kabla ya kuoana, au kufanya mapenzi ya kijinsia moja? Zote hizo ni dhambi. Na katika vitabu vya dini adhabu ya kupigwa mawe mpaka kufa.
 
Hapo kwenye green cjui kama ukiambiwa thibitisha utaweza, otherwise ni udaku tu na hata kama ni kweli hilo halimzuii mtu kufanya mema eti kwakuwa tu aliwahi kufanya baya hapo nyuma.

Hapo kwenye blue ni vitu viwili tofauti kabisa na kwenye red. Dont get me wrong BUT I doubt your mind kama inashindwa kuona hilo.
 
FYI, Kila nchi inachombo cha kuratibu, na kuhakiki hivyo vitu unavyosema kulingana na maadili yao, hata sisi tunacho na kama huna taarifa kuna msanii mmoja mkubwa tu hapa Bongo alitunga filamu yake yenye Maudhui hayo na akaipa jina shoga hicho chombo cha kuratibu kikaipiga chini fasta mno

WE will kill a snake no matter its color, Tutapinga Ushoga na kila kitu if that is what it takes to preserve our diginity.
Na tutafanya kila kitu hata kama kuwakagua makalio stupid! Mungu ibariki TZ, Mungu ibariki Africa

Sasa mbona vijana wa kiume hawaishi kuvaa "kata k"?

Au hayo nayo ni maadili ya Kitanzania?

Kama siyo, hivyo vyombo unavyovisema vimeshindwa vipi kudhibiti uvaaji wa "kata k" inayovaliwa hadharani na vitawezaje kudhibiti ushoga unaofanyiwa mpaka sirini?
 
Bado naona hujasimama vyema..... maana hapa hoja ni kupinga maadili mabovu...... na hilo Mugabe nampa.... big up....
Likija suala la uwizi wao nalo tutajadili hilo kwa kina...... kwenye hili la wa..fi raji.... naomba tuungane kumpa heko Mugabe.....
Hii ndiyo hasa hoja yangu pia. Yaani hawa wanaompinga wao wanataka tumpinge kwa kila kitu!!!!! Kama kavurunda uchumi anzisha uzi tutamponda huko. Hapa amefanya kitu ambacho kuna watu kimewafurahisha, huwezi kusema kumkubali sio sawa.
 
Mimi msimamo wangu ni kwamba, mambo ya Ngoswe, muachie Ngoswe mwenyewe. Almuradi mtu mzima kaamua kuishi hivyo na hajaingia katika reli zangu, sina sababu ya kujishughulisha na habari za nani analala na nani, wanalala vipi.

Hizi ndizo zile habari za uswahilini za kwenda kuchungulia majaa ya watu nani kala mayai na nani kala dagaa.

Ama kama habari za ku advertise mambo haya, mimi napinga ku advertise mambo ya faragha yote, kwa wote. Kwa hiyo sifagilii "public display of affection" kama kissing kwa mashoga na wasio mashoga. Kwangu zote ni vitu vya private tu.

Kufuatuilia sana mashoga ni unafiki na kukosa kazi.

Kwani kuna mifataki kibao inasambaza UKIMWI kwa makusudi, kwa nini msiifuatilie hiyo nayo?

Kuna mibazazi kibao imezaa watoto bila kuwatunza, kwa nini msiwafuatilie hao nao?

Huyo Mugabe mwenyewe kazaa mtoto na sekretari wake (Grace) nje ya ndoa yake na Sally, na yeye Mkristo, anapata wapi moral authority ya kusema mashoga wakati yeye na wao wote watenda dhambi tu?

[h=1]Mugabe Tells Of Old Secret Affair With Grace[/h]

http://www.zimeye.org/sallys-deathbed-heartache-as-mugabe-revealed-affair-with-grace/
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom