Umemsikia MUGABE alichomwambia OBAMA.?

Umemsikia MUGABE alichomwambia OBAMA.?

Tz haina Rais toka 2005 - To Date: Ikulu kuna muigizaji tu! Hata kama Mugabe kwenye baadhi ya mambo hawatendei haki wananchi wale lakini kuna mambo mengine msimamo wake unakuwa nguzo imara sio kama mzee wa tabasamu na kusafiri kila mara. Kuhusu mseveni japo ni dikiteta lakini kuhusu sheria aliyotia saini kwa ujumla inafaa sana hata hapa TZ tungekuwa na Rais jambo hilo lingekuwa muhimu katika nchi yetu lakini ndiyo hivyo Rais hatuna!
 
Kwani ushoga ni nini?
Mbona wanaume kibao wanawafanya wake zao kinyume na maumbile hamuoni kama ni kitu cha ajabu?
Kuonyesha kuwa waafrika akili zina hitlafu, wanamuona shoga ni muovu kuliko mwizi na hata muuaji.

Mijadala kibao ilishafanyika bungeni kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo ufisadi na vitu kem kem, lakini Wenje alipoibua hoja kuwa chama kimoja cha siasa nchini, itikadi yake inatambua haki za mtu mmoja mmoja wakiwemo mashoga moto uliwaka haijawahi kutokea, Wenje akazuiwa kusoma hadi atoe hicho kipengele. Mwandishi Ezekiel Kamwaga alishawahi kuuliza katika makala zake iwapo ushoga ni mbaya kuliko ufisadi.

Ni ufinyu wa fikra unaoashiria hitlafu katika akili kuamini kuwa ushoga ni jambo baya kuliko yote katika nchi na ni kitu ambacho watawala wanatakiwa kutoa kipaumbele katika kupambana nacho.
blaaah blaaah ushoga haufai mkuu
 
Duh,

Nilivyokuwa namjibu Mjuni Lwambo nilikuwa sijakusoma mkuu.

Sasa napitia posts za karibuni naona kwamba kumbe hili swali la authenticity ya hii habari si langu tu, kuna wengine wameliona.

Hatuwezi kupewa habari tu tukaimeza nzima nzima bila kuichunguza kama ni ya kweli au vipi.

Nimegoogle combinations kadhaa za hii habari sijaona lolote zaidi ya vi blog, vi website vya wanaija na twitter/ facebook.

Kama hii habari si ya kweli, itadhihirisha jinsi watu walivyo rahisi kuamini mambo bila kuthibitisha.

hata mimi nilivyoiona hii habari nikaiona ni ya uongo kabisa na nikajaribu kupitia statement za Mugabe on Gay marriage hamna kitu kama hii
 
Tz haina Rais toka 2005 - To Date: Ikulu kuna muigizaji tu! Hata kama Mugabe kwenye baadhi ya mambo hawatendei haki wananchi wale lakini kuna mambo mengine msimamo wake unakuwa nguzo imara sio kama mzee wa tabasamu na kusafiri kila mara. Kuhusu mseveni japo ni dikiteta lakini kuhusu sheria aliyotia saini kwa ujumla inafaa sana hata hapa TZ tungekuwa na Rais jambo hilo lingekuwa muhimu katika nchi yetu lakini ndiyo hivyo Rais hatuna!

Uraisi ni Taasisi Mkuu.
 
hata mimi nilivyoiona hii habari nikaiona ni ya uongo kabisa na nikajaribu kupitia statement za Mugabe on Gay marriage hamna kitu kama hii

Watu humu ndani wanatoka povu kama wamemshuhudia akitamka!

Hata kama Mugabe ni Mropokaji Mzuri kidiplomasia hii haipo.
 
Mugabe awe ni "trapeze artist" au jina lolote utakalopenda kumpa, kumbuka kwamba inahitaji ujasiri kutoa kauli kama hiyo kwa kiongozi wa taifa kubwa kama Amerika

Ujasiri is overrated, hata Idi Amin alikuwa jasiri lakini mpu.mbavu. Jasiri anayeua maelfu ya raia zake na kusema wazi wazi kwamba ana degree ya violence sio wa kumshangilia.

Watu namaaniha watu

Generalities are caves for ignorance.Specificity is king.

Nimeona ukiongelea hicho kitu wamagharibi waige au waruhusu mila za kiafrika kwa lipi wanalotaka kutoka kwetu?

Kwa kuwa wanataka waafrika wafuate hayo ya kuruhusu ushoga.

na hata kama lipo viongozi wetu wameshindwa kufanya wamagharibi kujua msimamo wetu na tunanufaikaje na wao kupata hicho wanachokitaka kutoka kwetu.

Hili nimelisema hapo juu. Mahojiano ya Kikwete na Christian Amanpour yanaonesha hilo wazi. Viongozi wa Afrika wamesha give up ku negotiate mambo kama sovereigns. Kikwete anasema Waafrika watakubali haya mambo tu, ila hawawezi kukubali mara moja, itachukua muda, kwa hiyo wamagharibi wasiwe na shaka sana.

Wanachofanya ni kuhakikiha wanaendelea kupata/kunufaika zaidi na rasilimali za waafrika huku wakiendelea kutuletea mambo yao hata kama yanapingana na desturi na mila za kiafrika.

Katika hilo hata huyo Mugabe unayemsifia yumo, sasa nashangaa anasifiwa sana kwa kisa gani.

Kikwete alichekacheka alipoulizwa kuhusu ushoga licha ya kujua ukweli kwamba sio utamaduni wetu, alijua fika vitu gani anaweza kuvikosa kwa jibu lake. Mugabe tayari ana vikwazo vya kiuchumi ndio maana anaweza kuongea chochote kwa taifa lolote hasa wamagharibi, hana cha kupoteza kutoka kwao.

Kama Mugabe hana cha kupoteza ndio maana anaweza kuongea chochote kile, huwezi kusema ni jasiri.Jasiri ni yule atakaye blast licha ya kuwa na kitu cha kupoteza.

Hujaona mtu hata akiwa bwana mdogo kama ana uwezo watu wanamuogopa kumkosoa hata pale anapokosea kisa watakosa msaada wake?

Hili haliondoi ukweli kwamba Mugabe ni chinjachinja anayejisifia kwa uchinjachinja wake waziwazi.

Unafikiri ni kiongozi gani wa Afrika ambaye ameshatatua matatizo ya nchini kwake angestahili kutoa hiyo kauli ya kupinga ushoga? Kwa sababu Mugabe kwa mtazamo wako hana credibility kisa uchumi mbovu na mauaji ya wananchi wake.

Obviously hunisomi. Nimesema hapo juu kwamba mimi falsafa yangu ni "Mambo ya Ngoswe muachie Ngoswe mwenyewe". Haki ya mashoga ni sawa na haki yako kuwa muislamu, mkristo au straight.

Kwa nini unafikiri mimi naunga mkono kupinga ushoga?

Mimi ninachowalaumu viongozi wa Afrika ni kukosa negotiation skills za ku ensure reciprocity, kwamba Wamagharibi wakitaka tkubali wanayosema wao (ushoga kwa mfano) na sisi tuwape ajenda zetu kwa habari hiyo hiyo ya human rights (ukewenza kwa mfano)

Siojawahi kuunga mkono kupinga habari ya jinsi watu wazima wawili wanavyotaka kujamiiana. Hizo ni habari binafsi zinazopaswa kulindwa na ustaarabu wa faragha katika jamii yoyote ya watu wenye kujiheshimu.

Tukianza kupangiana sheria za ushoga kesho tutaanza kupanga sheria za kukataza katerero, keshokutwa sheria za kupangiana goli ngapi mwanamme anapaswa kupiga, mtondogoo tuta appoint waziri wa kukagua k za wake zetu kama zimezidi kina kilichopitishwa na serikali.

We do not want the government in people's private lives.

It has enough work already in the public sphere.

Mambo ya Ngoswe, muachie Ngoswe mwenyewe.
 
Nyie viongozi wenu ambao hawajafanya hiyo mismanagement mbona mnakula shida tu kama wao? Mzungu sio rafiki yako hata siku moja, atakunyonya na atakudharau na shida zako utabaki nazo pale pale. Ni heri ya Mugabe, wanakula shida lakini hakuna manyanyaso ya wazungu. Fullstop

Kwamba mzungu (reductivism again, the west is more than "mzungu", Obama si mzungu, Erick Holder si mzungu) si rafiki yako hakumaanishi Mugabe aliyeua raia zake 20,000 na kutamba waziwazi kwamba ana degree ya violence ni rafiki yako.

Waafrika wengine wako quick kulaumu wazungu, lakini mweusi mwenzao kama Mugabe ataua na kufilisi, lakini kwa sababu ni mweusi tu na anajua kujificha nyuma ya pazia la "them against us" anapata a pass kufanya anachotaka.

Kwa waliouawa na Mugabe, is it any consolation kwamba aliyewaua ni mweusi mwenzao?
 
Waafrika kama kweli mko serious na kukataa ushoga na cultural imperialism pigeni marufuku movies za magharibi, pigeni marufuku nguo za magharibi, pigeni marufuku muziki wa magharibi, pigeni marufuku internet.

Anzisheni mifumo yenu yenye maadili ya kiafrika mnayoyataka.

Otherwise mtapiga kelele sana kumshangilia Mugabe (kwa habari ambazo hata hajazisema!) wakati mnaangalia shows za Hollywood zilizojaa LGBT themes na subtle sympathy.

Mtajikuta nyie mnapiga kelele wakati watoto wenu wanaoangalia haya mambo na kufuatilia wataona ndio mambo ya kisasa.

Ndiyo maana jibu la Kikwete kwa Amanpour in a way, ingawa halikuwa smart, lilikuwa na admirable candor (labda kwa sababu Kikwete is not smart/ confrontational enough to duck and deflect kama Mkapa na Mugabe). Waafrika hawawezi ku fight haya mambo, it is only a matter of time kabla hayajakubalika Afrika. I have to agree with Kikwete on that even though the answer was not statesmanlike, especially the tepid answer to the follow up question.

As long as hatu make content tunayo consume, basi hata mass psychology yetu itakuwa dictated na wengine, kwa mfano Hollywood.

Angalia vijana wanavyovaa kata k utaona jinsi gani hata kama Obama akinyamaza kuhusu ku force issue ya gay rights, Hollywood itamfanyia kazi yake.

Kwa hiyo hii focus nzima ya kuangalia viongozi na kusahau popular culture iko misguided.

Hawa hawa wanaomsema Obama na kumshangilia Mugabe ndio hawa hawa watakaoshangilia shows na movies za Hollywood zilizotengenezwa na the Hollywood gay crowd na kujazwa a disproportionate level of gay scenes.

I have noticed that there is a dramatic increase in gay/ lesbian sympathetic scenes in Hollywood movies/ shows. Are you guys going to boycott those too or just blabber hypocritically?

Nenda Facebook na Instagram uangalie watoto wa Kiafrika wanavyoshindana kujifanya Wamarekani.
 
Obviously hunisomi. Nimesema hapo juu kwamba mimi falsafa yangu ni "Mambo ya Ngoswe muachie Ngoswe mwenyewe". Haki ya mashoga ni sawa na haki yako kuwa muislamu, mkristo au straight.

Kwa nini unafikiri mimi naunga mkono kupinga ushoga?

Mimi ninachowalaumu viongozi wa Afrika ni kukosa negotiation skills za ku ensure reciprocity, kwamba Wamagharibi wakitaka tkubali wanayosema wao (ushoga kwa mfano) na sisi tuwape ajenda zetu kwa habari hiyo hiyo ya human rights (ukewenza kwa mfano)

Siojawahi kuunga mkono kupinga habari ya jinsi watu wazima wawili wanavyotaka kujamiiana. Hizo ni habari binafsi zinazopaswa kulindwa na ustaarabu wa faragha katika jamii yoyote ya watu wenye kujiheshimu.

Tukianza kupangiana sheria za ushoga kesho tutaanza kupanga sheria za kukataza katerero, keshokutwa sheria za kupangiana goli ngapi mwanamme anapaswa kupiga, mtondogoo tuta appoint waziri wa kukagua k za wake zetu kama zimezidi kina kilichopitishwa na serikali.

We do not want the government in people's private lives.

It has enough work already in the public sphere.

Mambo ya Ngoswe, muachie Ngoswe mwenyewe.

I salute you brother, hasa hapo kwenye bluu. Thanks
 
Nyie viongozi wenu ambao hawajafanya hiyo mismanagement mbona mnakula shida tu kama wao? Mzungu sio rafiki yako hata siku moja, atakunyonya na atakudharau na shida zako utabaki nazo pale pale. Ni heri ya Mugabe, wanakula shida lakini hakuna manyanyaso ya wazungu. Fullstop

Kwa kifupi tu viongozi wa Tanzania na Zimbabwe wanaboronga kwa sababu hawana sifa za uongozi wa kutatua matatizo ya wananchi wao. Kukemea wazungu au mitindo ya maisha yao haipo katika vigezo au sifa za viongozi bora. Kwa mtaji huu ujasiri wa Mugabe ni maonyesho ya pembeni tu ambayo hayaongezi ufanisi wa kazi yake kama rais au kuwa kiongozi bora kuliko wale wasiokemea wazungu.
 
Nashangaa kwanini watu hawahoji kwanini Obama atuamulie misimamo ya ushoga kwenye nchi zetu matokeo yake wanamshambulia Mugabe kwa kauli yake (Kama ni ya kweli).

Mugabe ana matatizo yake, haimaanishi apingwe kwa kila kitu kwa sababu ameshindwa kutatua matatizo Zimbabwe.

Katamka lini na wapi hiyo kauli Mugabe?

Fuatilia kwenye comment yangu ya mwanzo mkuu. Nilishasema kama hii ni habari ya kweli.
 
"If Obama wants me to allow gays marriage in Zimbabwe,I should marry him first to show the good example"-Robert Mugabe..

Ndio huyu huyu mzee,ambaye alipoulizwa na wanahabari wa Uingereza kuwa kwanini asiachie ngazi ilhali ameshazeeka, aliwauliza kama walishawahi kumuuliza swali kama hilo malkia wao..

Salute kwako uncle mugabe..

MUGABE AMKUMBUKA NYERERE: Rais Mugabe wa Zimbabwe amewalaumu viongozi wa Afrika kwa kushindwa kumuenzi Mwl Nyerere kwa mchango wake wa ukombozi Barani Afrika.
 
Maelfu ya watu wa Zimbabwe wamehudhuria sherehe rasmi za siku ya kuzaliwa Rais Robert Mugabe.

Bwana Mugabe ambaye ameongoza nchi tangu mwaka wa 1980, alipeperusha mabofu 90 katika uwanja wa michezo wa Marondera, mashariki ya Harare.

Rais Mugabe, ambaye amerudi punde kutoka Singapore kwa matibabu, alisema ajisikia mzima na kijana kama mtoto wa miaka 9

Aliuambia umati kuwa ushindi aliopata kwenye uchaguzi wa mwaka jana ulishangaza nchi za magharibi zinazomlaumu.

Sherehe hiyo inakisiwa kugharimu dola milioni-moja na hivyo kuzusha malalamiko katika nchi ambayo ina matatizo ya kiuchumi.
 
Activister wewe pigiliwa tu hakuna nouma; sisi tunafuata mafundisho; kama hufahamu Quran na Biblia vimekataza hiyo michezo yenu ni wazi game imekukolea
 
Last edited by a moderator:
"If Obama wants me to allow gays marriage in Zimbabwe,I should marry him first to show the good example"-Robert Mugabe..

Ndio huyu huyu mzee,ambaye alipoulizwa na wanahabari wa Uingereza kuwa kwanini asiachie ngazi ilhali ameshazeeka, aliwauliza kama walishawahi kumuuliza swali kama hilo malkia wao..

Salute kwako uncle mugabe..

huyo ndio komrade Mugabe.
 
Kwa kifupi tu viongozi wa Tanzania na Zimbabwe wanaboronga kwa sababu hawana sifa za uongozi wa kutatua matatizo ya wananchi wao. Kukemea wazungu au mitindo ya maisha yao haipo katika vigezo au sifa za viongozi bora. Kwa mtaji huu ujasiri wa Mugabe ni maonyesho ya pembeni tu ambayo hayaongezi ufanisi wa kazi yake kama rais au kuwa kiongozi bora kuliko wale wasiokemea wazungu.
Zakumi
Ulichoongea hakina mantiki; matatizo ya kiuchumi katika nchi za Afrika ni matokeo siasa za kibeberu; mfano halisi ni Zimbabwe walijaribu ili kuleta machafuko ya kisiasa; wameshindwa; Afrika wapo viongozi bora wenye lengo la kumkomboa mwafrika! Kwenye siasa huwezi kumridhisha kila mtu hata hapa US wapo wanamuona Obama hafanyi kitu.
 
Ngoja nikukubalie kuwa matatizo ya kiuchumi katika nchi za africa ni matokeo ya ubeberu. Katika vitabu vya sifa za kupigana na ubeberu na kuondoa matatizo ya uchumi wa nchi za kiafrika, kukemea mitindo ya maisha ya nchi za magharibi sio sifa ya kiongozi na sio zana ya kupinga ubeberu.
 
mimi huwa najiuliza kwa nini races nyingine like wazungu, waarabu, wachina wahindi etc wakimiliki mali Africa ni right...lakini hawatoi nafac kwa waafrica kumiliki mali nchi zao.................??????????????????
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom