Mimi msimamo wangu ni kwamba, mambo ya Ngoswe, muachie Ngoswe mwenyewe. Almuradi mtu mzima kaamua kuishi hivyo na hajaingia katika reli zangu, sina sababu ya kujishughulisha na habari za nani analala na nani, wanalala vipi.
Hizi ndizo zile habari za uswahilini za kwenda kuchungulia majaa ya watu nani kala mayai na nani kala dagaa.
Ama kama habari za ku advertise mambo haya, mimi napinga ku advertise mambo ya faragha yote, kwa wote. Kwa hiyo sifagilii "public display of affection" kama kissing kwa mashoga na wasio mashoga. Kwangu zote ni vitu vya private tu.
Kufuatuilia sana mashoga ni unafiki na kukosa kazi.
Kwani kuna mifataki kibao inasambaza UKIMWI kwa makusudi, kwa nini msiifuatilie hiyo nayo?
Kuna mibazazi kibao imezaa watoto bila kuwatunza, kwa nini msiwafuatilie hao nao?
Huyo Mugabe mwenyewe kazaa mtoto na sekretari wake (Grace) nje ya ndoa yake na Sally, na yeye Mkristo, anapata wapi moral authority ya kusema mashoga wakati yeye na wao wote watenda dhambi tu?
Mugabe Tells Of Old Secret Affair With Grace
Mugabe Tells Of Old Secret Affair With GraceÂ-|Â-ZimEye