Umeishi Kijijini? ...Mimi Nimeishi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umeishi Kijijini? ...Mimi Nimeishi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by PakaJimmy, Dec 5, 2009.

 1. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #1
  Dec 5, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Mwana jamvi,

  Wewe binafsi umeshawahi kuishi kijijini?

  Ninaposema kuishi kijijini ninamaanisha kuwepo huko, kushiriki majumuiko mbalimbali, sherehe na kazi zote za uzalishaji za huko.

  Nia ya swali langu ni kujaribu kujua hasa wakati tunapojadili masuala kama ya kumkomboa mkulima(peasant), au asilimia 80 ya watanzania kuishi vijijini, tunaongea kwa uchungu na kujua kiukweli maisha ya vijijini yalivyo?

  Pia tunaongelea KILIMO KWANZA,ambapo kwa kiasi kikubwa kinatekelezwa vijijini.

  Usikute watu wanajiita Mzee Mwanakijiji, Ng`wana Madaso, au Balantanda, kumbe wamezaliwa, kukulia, na kusomea mijini, na hawajaonja pepo ya kijiji!. Nina shaka na watu kama Bluray, Firstlady, Kigogo,bht na wengine, kama wanajua jembe, kama si kuliona kwenye nembo ya sisiemu!

  Mimi binafsi nimezaliwa, kukulia, na kusomea kijijini.
  Nimechunga mbuzi na kondoo, nikaokota kuni msituni ,na kucheza dimbadimba! Nimetembea pekupeku kwa kadiri ya muongo mmoja, thats me!

  Umeishi kijijini, na una kisa chochote? tupe basi!
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Dec 5, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  PJ mie nashindwa kujibu hapa cause haya maisha nashindwa nisemeje
  ila nimefurahishwa sana na wewe ..unajua hali halisi iliyoko vijijini
  nitakuwa huko kijijini kwa muda wa mwezi mzima ..nitakupa update
   
 3. Lily Flower

  Lily Flower JF-Expert Member

  #3
  Dec 5, 2009
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 2,555
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mie hata cjui nisemeje all I know is mjini, nimezaliwa mjini, nimekulia mjini, nimesomea mjini, ninaishi mjini, respect to you PJ cause you it all vya kijijini na vya mjini, mie cku nikienda sijui itakuaje I pitty my self.
   
 4. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #4
  Dec 5, 2009
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  Mimi bwana life la village huniambii kitu, mambo ya kuamka asubuhi na kunywa chai na kiporo cha ugali mbona sana tuu, kufua na majani ya mpapai, maswala ya kuoga kijijini si muhimu ki viile, maisha ya kijijini ni peace sana huwa hakuna stress au kuna anaebisha?
   
 5. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #5
  Dec 5, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  PJ yale maisha niliyoishi kijijini sipendi mtoto wangu aje hata aguse kabisa
  chai ni anasa mojawapo,sanasana uji wa chumvi,kukata kuni kila jmosi,kufuata maji bondeni,afu bado ili uende shule na vihela kidogo inabidi ufanye kibarua cha kupanga nyanya,
  ambacho huwa nakimiss kijijini niwapo huku mjini ni ulazi na komoni kwakweli
   
 6. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #6
  Dec 5, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Sina hakika kama kuzaliwa na kukulia kijijini halafu ukahamia na kuishi mjini kunakufanya uwe na uelewa mzuri wa kijiji. Kuna watu walihamia mjini wakiwa na miaka zaidi ya 25 na sasa wanadai hata lugha zao za asili wamezisahau. Labda kama unaendelea kuishi kijijini hadi sasa ila kama ulishahama huko baada ya kupata kazi na kuanza kutembeza EPA +ufisadi mjini inawezekana memory ilishakuwa-deleted. Kwa hiyo mtu anaweza kuzaliwa mjini then akaishi kijijini akiwa mtu mzima na kuelewa vizuri maisha hayo kuliko wale ambao walizaliwa vijijini lakini wamesha-mutate na kuwa alienated.
   
 7. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #7
  Dec 5, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  -PJ hukukosea,nami nimeishi kijijini,nimezaliwa na kukulia huko.Shle ya msingi nimesoma na kumalizia kijijini,bahati nzuri kijijini kwetu kumekuwa na shule ya sekondari muda mrefu so hata elimu ya sekondari nimesomea kijijini kwetu(O-level) baada ya hapo sasa A-level ndo nikaenda kusoma mjini.

  -Nayakumbuka sana maisha ya kijijini mkuu,nikianza na shule nakumbuka jinsi tulivyokuwa tukiamka asubuhi na mapema kwenda shule kuwahi NAMBA(tulikuwa tukihesabiwa asubuhi),baada ya kuhesabu namba tulikuwa tukikimbia mchakamchaka kisha tunarudi shule kwa ajili ya kufanya usafi(kufagia) na ilikuwa ni lazima kwa kila mwanafunzi kwenda shule na Ufagio,usipokuwa nao ni viboko kwa kwenda mbele.Baada ya usafi kengele ilipigwa kwa ajili ya ukaguzi wa usafi na gwaride(nakumbuka nilikuwa Band Master),kila Alhamis na Jumatatu tulikuwa twafanyiwa ukaguzi wa nguo.Baada ya ukaguzi na gwaride tuliingia darasani

  -Pia nakumbuka wakati wa breki ya saa 4 asubuhi tulikuwa tukila Vibama,Mihogo ya kuchemshwa au ya kukaanga,togwa na wengine tulikuwa tukienda shule na mahindi ya kukaanga(wenyewe tuliita BISI).Pia nakumbuka kipindi cha baridi tulikuwa tukichoma majani na kuanza kuotea Moto(ilikuwa tukiingia darasani ni harufu ya moshi mpaka basi)...Pia kila mwezi tulikuwa tukifanya zoezi la kupika msosi ili kuyafanyia kwa vitendo yale tuliyokuwa tukijifunza katika somo la Sayansi Kimu(Maarifa ya nyumbani)

  -Kwa kijijini ikifika kipindi cha kilimo ilikuwa ni noma hasa,maana ilikuwa kila Ijumaa tunaenda kwenye mashamba ya shule(mashamba ya Pamba,Alizeti na Karanga),na Jumamosi tunakwenda kwenye shamba letu(la nyumbani) so ilikuwa hakuna cha kupumzika weekend wala nini.Jumapili ni kanisani kama kawa na nilikuwa sikosi(nilikuwa mtumishi wa kanisani)

  -Kipindi cha likizo tulikuwa tukikitumia zaidi kwa kwenda porini kuwinda na mbwa,tulikuwa tukiwinda wanyama wadogowadogo kama Sungura,Pimbi,Simbilisi,na wakati mwingine hata Swala...Pia wakati mwingine tulikuwa tukienda shamba kulinda ndege wasishambulie Mpunga..Pia tulikuwa wataalamu sana wa kutega ndege kwa kutumia mitego tuliyokuwa tukiita ya mwanja(ya mviringo hivi) kwa ndege wadogo na pia tulikuwa tukitega miteo ya kufyatuka(Fyatua) kwa ajili ya ndege aina ya KWALE..Ilikuwa raha kwa kweli kuishi kijijini....Sisi hatukuwa na tuisheni wala nini so likizo ilikuwa ikiisha kwa kufanya shughuli hizi tu

  -Pia ilikuwa tukitoka shule jioni baada ya kula na kupumzika tunaenda mtoni/kisimani kuchota maji,na tukifika huko mtoni ilikuwa ni kuogelea mpaka basi(nakumbuka rafiki yangu wa karibu mnoo niliyekuwa nikisoma naye darasa moja alifariki tukiwa twaoga naye mtoni mwaka 1987 R.I.P Sadiq,mimi mwenyewe nilinusurika kufa maji karibu mara 3 lakini nilikuwa sikomi maana ndo ilikuwa starehe yetu ya kijijini hiyo)

  -Nakumbuka nyakati za usiku bibi alikuwa akituhadithia hadithi na wakati mwingine sisi wenyewe tulikuwa tukipeana hadithi mbalimbali..Pia nyakati za usiku watoto tulikuwa tukijikusana na kuanza kuimba nyimbo mbalimbali(wakati mwingine na wakubwa walishiriki kuimba) na wakati mwingine tulikuwa tukicheza mchezo wa KOMBORELA(nakumbuka kuna jamaa alikuwa akaijifanya mbabe ba mnjanja sasa kuna siku tukiwa twacheza komborela tukapanga tumfanyizie tukaondo mpira wa chandimu uliokuwa ukitumika kuokolea tukweka JIWE halafu tukamtegea yeye ndo aende kutuokoa basi alitoka spidi huyo akaenda kulipiga lile jiwe akidhani ni mpira,aliumia sana,mguu ulivimba sana aisee).

  -Nakumbuka Radio ndo ilikuwa kiburudisho pekee cha kijijini so nilikuwa msikilizaji mzuri sana wa RTD enzi hizo hasa vipindi vya muziki,kipindi cha mama na mwana(tyulikuwa na klabu yetu ya mama na mwana),vipindi vya mchezo wa redio vya akina Jangala,akina mzee Jongo na kile cha Pwagu na Pwaguzi

  PJ umenikumbusha mbali sana mkuu wangu,sasa hivi najona kama niko kjijini kwetu TINDE,Shinyanga..Ubarikiwe sana mkuu
   
 8. F

  Future Bishop Member

  #8
  Dec 5, 2009
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 75
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  PJ mimi nimezaliwa na kusomea shule ya msingi kijijini. Nilianza kutoka kijijini kwa mara ya kwanza baada ya kufaulu mtihani wa darasa la saba na kuchaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari. Huo ndio ulikuwa mwanzo wa kupanda basi na treni.

  Watoto wangu huwa nawachekesha kuwa wakati wao naanza kuwavalisha viatu wakiwa bado wanabebwa, mimi nilianza kuvaa kiatu nilipokwenda sekondari. Maisha ya shule ya msingi nilitembea umbali wa karibia kilomita mbili kwa mguu na njia hiyo ilikuwa na changalawe. Unaweza ukapiga picha maisha hayo. Hata kiatu nilichovaa siku ya kusherehekea kumaliza darasa la saba niliazima, suruali nilivaa ya baba ilibidi ipunguzwe ili iweze kunienea. Ni shati tu ndilo mzee alijitahidi akaninunulia mtumba. Kweli ninamshukuru mzee wangu kuniwezesha kufika hatua niliyofikia leo.

  Kama mtoto wa kwanza wa kiume nilimsaidia mama kuosha sahani, kuwabeba wadogo zangu mgongoni na kwenda shambani karibia kila siku. Hata kama miaka zaidi ya 30 imepita nayakumbuka maisha hayo. Hata hivyo natamani watoto wangu na wajukuu wasipitie maisha haya.
   
 9. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #9
  Dec 5, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  USIPATE SHIDA DARKCITY

  Kama una wazo hilo ni zuri sana, anzisha thread ya hivyo kwaajili ya watu waliohamia kijijini, nayo itapata washabiki walioyaishi maisha hayo, WEENGI TU!
   
 10. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #10
  Dec 5, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Kwakweli bwana FB umenifurahisha sana, hasa hapo kwenye RED...DUu,.. ama kweli usione vyaelea vimeundwa!
   
 11. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #11
  Dec 5, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Duh jamiiforums ina mambo mengi mazuri ya kujifunza na kupata uzoefu.

  PJ,nimekupata mimi bahati mbaya/nzuri nimezaliwa mjini nimesoma mjini na ninaendelea kuishi mjini ingawa siku hizi kila mwisho wa wiki natia timu kijijini[si kijiji walichozaliwa wazazi].Uzoefu wangu wa kijijini ulikuwa ni wakati wa likizo hasa mwisho wa mwaka nilikuwa naenda kijijini kuwasalimia Babu na Bibi.Bahati nzuri kijiji chetu kilikuwa kimepiga hatua kubwa hasa zile huduma muhimu kama maji na umeme vilikuwa ni kitu cha kawaida kwa familia zenye uwezo.

  Tangu mwaka jana nimekuwa nikisafiri kila mwisho wa wiki katika kijiji nilichoamua ndiyo yakapokuwa makao yangu makuu siku za usoni,sijui labda kuishi kwangu mjini muda mrefu kumenifanya nitamani kuishi kijijini.

  Uzoefu wangu mdogo wa maisha ya kijiji nilichoamua kiwe makazi yangu ni kama ifuatavyo.
  [1] Maisha kwa ujumla ni magumu sana hasa huduma muhimu kama hospitals,barabara,umeme,maji na nk.
  [2] Mzunguko wa fedha ni mdogo ukilinganisha na mjini.Ukienda na note ya tsh 10;000/= unaweza kupata matatizo ya kupata huduma.

  [3] Hali ya watoto ni mbaya sana,wengi wao bado wanaenda shule umbali mrefu tena bila viatu.

  [4] Wanakijiji wengi ni wakulima wanaotumia jembe la mkono kitu ambacho kinawafanya waendelee kuwa maskini.Ardhi ya kutosha ipo ambayo kama wangeitumia vyema ingeweza kuwakomboa wanakijiji wengi.

  Kwakuwa muda si mrefu nitaweka makazi yangu kijijini nadhani niataendelea kupata uzoefu.

  Naomba kuwasilisha.

   
 12. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #12
  Dec 5, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180

  Mkuu Ngongo,

  We ni Mchaga nini, maana hawa watu ndo zao kukimbilia Moshi kila mwisho wawiki, na ni kweli kwamba vijiji vyao vingi vina maendeleo makubwa(lo!..just for fun!)

  Kweli Mkuu umejaribu kuonyesha kwa kuainisha, uzoefu mzuri sana wa maisha ya vijijini, na nadhani ukiambiwa suala la pembejeo kwa Mkulima, angalau unaelewa asaidiweje huyu mtu!

  Nakutakia kila laheri pindi utakapohamia huko kijijini, najua utabadilisha kwa kiasi kikubwa mtazamo wa KILIMO KWANZA!...All ze best Mkuu.
   
 13. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #13
  Dec 5, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280

  Heshima kwako PJ.

  Mkuu Kilimanjaro hakuna ardhi ya kutosha kwa mtu mwenye mawazo yangu siwezi kwenda kubanana na kwenye eka mbili tatu.Nimeenda kwa wazigula si unajua wenzetu wana ardhi kubwa yenye rutuba kibao.

  Niko kwenye maandalizi ya kuboresha kwanza kabla sijaamia,kuna vitu kama umeme na maji na mazao ya kudumu ni muhimu kwanza kufanya kabla ya kuhamia.

  Mkuu PJ tusisubiri ardhi yetu ivamiwe na wakenya ndiyo tuanze kupiga kelele,tuanze kuifanyia kazi sisi wenyewe.Mkuu mimi niko Arusha ardhi ipo lakini ni ghali sana huwezi kununua labda uwe na fedha za EPA.Ningependa kubaki Arusha lakini bei ya ardhi imenikimbiza watu kama kina mheshimiwa Kimaro ndiyo wanaweza kununua.
   
 14. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #14
  Dec 5, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145


  Nimezaliwa kijijini Kwimba, nimeishi kwa ujumla vijiji vingi vya mkoa wa mwanza au kanda ya ziwa, Ukerewe-Kagunguri, Bukongwa,Nansio,murutunguru, mkasiska , kazilankanda,Bwangija. Nyamahande,Bugorola. Geita,Buselesele,Sengerema Nyehunge,kahunda, Nkome,Uzizinza,Itabagumba. Magu,manangwa,misasi,manangwa,nyanguge,misungwi,inonelwa, yanii nikiaja huku msoma majita kisorya, tarime, ikoma, nikija shy usiseme huko ma kahama kote nime kaaaa sio ati kupita tuuu, Dodoma huko Bahi,Bihawana,kondowa, Arusha,Moshi jamani
  Kuwepo huko nipo na niana mpango wa kwenda kulima kazilankanda huko mama yangu aliacha mashamba mengi sn,kweli ukerewe kuna njaaaa ntarudi huko kwa wajomba zangu, ingwa mbunge wetu huko Getrude Mongera ajitahidi sn kwa kilimo ktk kuwapa wan ukerewe Elimu ya kilimo na Uvuvi

  Hapo kweli kwahitajika nguvu ya ziada na sio porojo tuna maeneo makubwa sana kwa kilimo hata ufugaji ni swala la fund,kujipanga na elimu, tuaje siasa fitna na tuwe na siasa za kuinua uchumi wa kilimo haswaaaaa  Hiii ni kauli mbiuuu au twataka kupotezea watanzania kwa kujifanya ati siasa yawajali sn watanzania 80% ya wakulima???? wakati twasoma tulikuwa na Kauli ya "Kilimo ndio Uti wa Mgongo" Hii Kauli ilipotelea wapi na akina nani waliipotezeaaaa?? Je ilikuwa na mafanikio au laaaah? Tulikuwa na Majineli huko Kanda ya Ziwa ya ki operate vyema tu mashirika ya Umma eg Shireku, Moshi na Arusha vilipotelea wapi??? Viwanada 12 Mwl.JKN aliviacha kwishaaaaa faster Tena Nakumbuka Mwatex na Mutex jamaniii watu walichuma hela pale usipaime i was there wapwa nilikuwa najionea kwa macho yangu.

  Ili tukwamke sasa twahitaji dhamila ya hali ya juuu na kujikita kwa Kilimo huko Tarime wao sasa wananchi wana wana jikita kwenye migodi kwa wingi je Hiki Kilimo kwanza kitawaingiaje? twaitaji mbinu makiji kuwarudisha kwa Kilimo as soon as possible,

  Mikakati ya Masoko,pempejeo,kodi ndogo,ruzuku,elimu na mipangiro ilio swafi kwa maslahi ya nchi, wakulima wa nchi zilizo endelea ni matajiri kweli kweli.
  Wajisemee wao hapo chachaaa   
 15. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #15
  Dec 5, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Jethro,

  Mchango wako nauheshimu sana.

  Kweli sina neno lakuweka hapo zaidi, maana ukekuwa muwazi sana.
  Nina ndugu yangu alisoma chuo cha ualimu hapo mahali panaitwa Murutunguru, kumbe ushakanyagakanyaga maeneo yote hayo na kulijenga Taifa!..huh!

  Hakika we Mkuu ni mfano mzuri wa mabaki ya sera nyoofu za Mwalimu za Ujamaa na Kujitegemea, pamoja na Azimio la Arusha la kuondoa Ubepari!

  Nimeshawishika kutafuta mabandiko yako mengine!
   
 16. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #16
  Dec 5, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Umeniacha hoi pale juu kwenye RED!..Kama mlikuwa mnaruhusiwa hadi kwenda na TOGWA shuleni, kweli mlifaulu ku'customize maisha kwa kinyumbani haswaa!, yani its so interesting and funny.

  Actually, historia yako na ya walio wengi tulioishi vijijini inafanana mno katika kila nyanja, tofauti inakuja kwenye mazao mliyokuwa mkilima, kwa mfano kwetu mimi PAMBA haipo, na kwa macho yangu sijawahi kuiona physically!

  Hapo kwenye kazi, sisi, ilifikia wakati tulipata Mwalimu Mkuu aliyezinduka na kuwa Fisadi wa Enzi hizo, ambapo alianza kutulimisha mashamba ya raia kijijini, kwa ujira mdogo sana, na akidai hela hizo zinaingia kwenye mfuko wa EK=Elimu ya Kujitegemea! Tulikwenda hadi misituni kukata fito za kusimamishia nyanya na yeye akazipeleka MJINI kwenda kuzitafutia soko!

  Amakweli zilikuwa zama za aina yake!

  Kuhusu REDIO TANZANIA, nimekuelewa vizuri sana, maana ulishatundika thread nzuri sana ya ZA KALE, ambapo mimi bila kusita nilikupa THANKS YA TOKA MOYONI!.

  Nakuheshimu sana Mkuu Balantanda kwa kuongea kweli tupu!
   
 17. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #17
  Dec 5, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145


  Kwakweli Mpwa pare Murutunguru nimesoma ile shule ya mazoezi karibu na Chuo cha Ualimu in 80's na upande mwingine kulikuwa na chuo cha CCM sikuhizi imekuwa ni secondary i was there in March. Kwakweli maisha ya kule yamehalibika kutokana na kutokuwa na usimamiaji sanifu wa kilimo kwani ile Jineri ya pale imebakia majengo na vipuli vyote vimeharibikia hapo majengo yalikuwepo mazuri sana ila kweli ukiwa kiongozi yakupoasa uwe na upeo wakulitizama Taifa unaloliongoza kwa miaka 10 na zaidi ijayo litakuwa wapi. na ni murutunguru hapo karibu na sokoni ndipo MB Getrudi Mongera kazaliwa lakini nenda sasa ukajioneee ni Nyumba ya baba yake ilikuwa inajengwa na ndio nzuri pale kijijini kwa eneo lile ingwa kuna tax siku hizi na rami umbali fulani tokea nansio mjini na itakatikia njiani, Ukerewe ni kubwa sana Ianstahili kuborsha na kuitwa mkoa.

  Mpwa nawe huwa unamichango mizuri sana na mpiganaji safi ktk kutaka kulijenga Taifa hili upya.

   
 18. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #18
  Dec 5, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na mimi nimezaliwa na kukulia kijijini. nimesoma hadi darasa la saba kijijini. kuanzia hapo nimekuwa naishi mijini, nimefanya kazi dar na biashara dar, na nchi jirani (zambia na kenya) na kwa sasa naishi nje ya bara la afrika kwenye mji mkubwa labda zaidi ya mara 200 ya dar.

  ukweli kijijini ukikuta mtu ana pengo ujue ni kwa ajiliya ugomvi au ajali. matumizi ya sukari ni kidogo sana unaweza kumaliza mwaka hujaonja ladha ya sukari.

  enzi zetu tunachunga ng'ombe na mbuzi maporini ilikuwa kawaida kurudi nyumbani na sungura pori tuliowaua kwa kuwafukuza na mbwa, samaki tuliowavua kwa ndoana mabwawani au mboga za majani zinazotambaa kwenye vichaka na kutatua tatizo la kitoweo nyumbani. vyote hivi vilikuwa vingi tu

  wakati wa kilimo tulikuwa tunaanza kulima saaa 9 usiku na kumaliza saa 5 asub na wakati wa mbalamwezi tulikuwa tnalima usiku kucha kwa ng'ombe.

  tv yetu kijijni ilikuwa wazee wenye busara na hadithi nzuri. karibu kila siku tulilala sio chini ya saa sita usiku kutgemeana na wingi wa magogo ya kuota moto tuliyokusanya siku hiyo

  tulipokuwa vijana wakubwa (wakati wa balehe) tulilia kisu kwa uchu kuliko vijana wa siku hzi wanvyolilia simu za vigajani. mzee akigoma kukufanyia suna unajichapa mwenyewe kwa mkono yako halafu unakwenda kumwonyesha ajue kuwa wewe ni mwanume.

  wakati wa sherehe tulicheza usiku kucha pamoja na dada zetu tuukiwalinda badala ya kuwabaka na walikuwa salama bila mimba wala magonjwa ya zinaa wala kuharibiwa bikira zao hadi wanapoolewa. kulikuwa na maadili si mchezo

  kijana wa kike na kiume alinunliwa kiatu alipokuwa akitoka jandoni ili kumtangaza rasmi kuwa yu tayari kuoa au kuolewa, kabla ya hapo asahau

  umenikumbusha mbali sana mkuu,

  yako mengi nitaendelea baadaye
   
 19. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #19
  Dec 5, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145


  Teh teh mama na mwana jamani mnakumbuka hata huko hadithi ya Adili na Nduguze mwaikumbuka nilikuwa siikosi na yule bibi mwenye sauti ya kutisha.

  Mwakumbuka Mikingamooo??
  Na mikingamo ndicho kipindi kilichokuwa chawaacha hoi wazeee wetu ile usiku shutuma wazi wazi, wazee wetu walikuwa na hali jojo.


   
 20. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #20
  Dec 5, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kwanza kabisa hii thread imekuwa nzuri sana kwa upande wangu. Kwa hli tu kwanza nimechapa PJ na Senks ya ukweli kabisa ikiongozwa na furaha ya moyo wangu. Mimi pamoja na kutokwa na umri mkubwa kama Balantanda alivyoeleza hapo juu ila nimeishi kijijini na kuna mambo mengi sana ambayo nayakumbuka ambayo leo hii uko vijijini hayapo tena na uku mijini ndio kabisa hakuna.

  Mimi nakumbuka wakati nasoma shule ya primary nilivyokuwa naenda peku peku na hata Bibi akijitutumua na kuninunulia viatu kwa sababu most of pupils walikuwa hawavai viatu basi unakuta nilikuwa na vivua na kuviweka kwenye mfuko wa Malboro ambao ndio ulikuwa umebeba daftari zangu. Pia nakumbuka jinsi ambavyo tulikuwa tunaenda kuchunga ng'ombe na mbuzi maeneo ya msituni, hapa nakumbuka kuna siku mbuzi walipotea uko msituni wakati tunatandaza kabumbu na watoto wengine, nakumbuka siku hii kwasababu kipigo niichoenda kukipata kilinifanya niuchukie mpira kabisa.

  Pia nakumbuka wakati naanza kidato cha kwanza shule ambayo nilikuwa nasoma ilikuwa about ten kilometres kutoka kijijini kwetu. Sasa kimbembe kilikuwa wakati wa kurudi jioni manake nakumbuka tulikuwa tunakatiza vijiji viwili kufika shuleni basi washikaji wa kijiji kimoja walikuwa wachokozi sana hasa wale ambao hawakupata nafasi ya kwenda sekondari, basi ilikuwa lazima kila wiki ngumi zipigwe baina ya wanaotoka shule na wale wa mtaani, nakumbuka kuna binti mmoja shule ilimshinda kabisa mpaka wazazi wake wakampeleka shule ya ufundi.

  Jamani kijijini kuna alot of things which are good actually na ambayo yanahitaji kukumbukwa na kuenziwa, hapo sijataja nyumba ambazo tumekuwa tunaishi n.k

  Thanks PJ for this useful thread
   
Loading...