Umeishi Kijijini? ...Mimi Nimeishi

Umeishi Kijijini? ...Mimi Nimeishi

Mwana jamvi,

Wewe binafsi umeshawahi kuishi kijijini?

Ninaposema kuishi kijijini ninamaanisha kuwepo huko, kushiriki majumuiko mbalimbali, sherehe na kazi zote za uzalishaji za huko.

Nia ya swali langu ni kujaribu kujua hasa wakati tunapojadili masuala kama ya kumkomboa mkulima(peasant), au asilimia 80 ya watanzania kuishi vijijini, tunaongea kwa uchungu na kujua kiukweli maisha ya vijijini yalivyo?

Pia tunaongelea KILIMO KWANZA,ambapo kwa kiasi kikubwa kinatekelezwa vijijini.

Usikute watu wanajiita Mzee Mwanakijiji, Ng`wana Madaso, au Balantanda, kumbe wamezaliwa, kukulia, na kusomea mijini, na hawajaonja pepo ya kijiji!. Nina shaka na watu kama Bluray, Firstlady, Kigogo,bht na wengine, kama wanajua jembe, kama si kuliona kwenye nembo ya sisiemu!

Mimi binafsi nimezaliwa, kukulia, na kusomea kijijini.
Nimechunga mbuzi na kondoo, nikaokota kuni msituni ,na kucheza dimbadimba! Nimetembea pekupeku kwa kadiri ya muongo mmoja, thats me!

Umeishi kijijini, na una kisa chochote? tupe basi!

Kuchota maji umbali wa km 10 au zaidi, kula matunda mwitu (Sungwi, Lade, mbelembeo n.k), kuamka asubuhi sana kuswaga ng'ombe kwa kulima, Palizi kama kawa mpaka saa 7 mchana na ukipoozea na uji wa chumvi! Bila kusahau kona ya malividavi kumsubiri demu mida ya saa 2 usiku hadi saa 3 usiku bila ya mafanikio chini ya miti na siku unampata utakapomlaza hapataota nyasi
 
PJ kaka, mimi naenda sana 'ushagoo' usinipimie (ila sikai sana a few days), ila kiukweli maisha ya kule si mchezo yataka moyo....kulima siwezi kwanini nidanganye kwanza huko hata hii kilimo kwanza yenyewe sioni kama ni applicable, maji kama almasi, watu wameharibu mazingira utadhani hakuna serikali!!!
 
uzuri wa kijijini mamisosi unlimited halafu natural.. ukisikia tu njaa unajisevia chochote tena cio kutoka kwenye frij toka mtini original/shambani
R u serious mkuu?
Nimezunguka vijiji vingi sana kujaribu kuona uhalisi wa dhana hii ya kujisevia kila kitu tena bila kutumia pesa kwa vile kila kitu - vyakula na mboga hupatikana shambani.Nilishangaa nilichokiona!
 
Kuchota maji umbali wa km 10 au zaidi, kula matunda mwitu (Sungwi, Lade, mbelembeo n.k), kuamka asubuhi sana kuswaga ng'ombe kwa kulima, Palizi kama kawa mpaka saa 7 mchana na ukipoozea na uji wa chumvi! Bila kusahau kona ya malividavi kumsubiri demu mida ya saa 2 usiku hadi saa 3 usiku bila ya mafanikio chini ya miti na siku unampata utakapomlaza hapataota nyasi

We kimbweka ni hatari sana....du!, umenifurahisha mbaya mkuu!
Mi nakumbuka wakati ninakaa nyumba ya pamoja na wazazi, baadhi ya marafiki zangu walikuwa na ghetto, kwahiyo ilikuwa ukipata mrembo unamwomba jamaa ghetto, then unaenda kurekebisha tabia huko ndani, na most of times ilikuwa mkimalizana mnaondoka bila hata kurudishia fresh mablanketi na shuka la jamaa!
 
PJ kaka, mimi naenda sana 'ushagoo' usinipimie (ila sikai sana a few days), ila kiukweli maisha ya kule si mchezo yataka moyo....kulima siwezi kwanini nidanganye kwanza huko hata hii kilimo kwanza yenyewe sioni kama ni applicable, maji kama almasi, watu wameharibu mazingira utadhani hakuna serikali!!!

Kumbe ndo maana ukaitwa bht!!!....ok...ok...!

Una bahati sana kwamba mdogo wangu XPIN anaishi town maisha yote!

Ungekuwa naniliu wa mtu kama mimi,..oooh, nakwambia ungejifunza jembe bila kupenda, maana kwetu kule heshima ya mwanamke inakuja kwa kupitia jembe tu, na si kuwa na nanihino kuubw kama ilivyo kwa wanawake wa mjini..lol!
 
Mkuu heshima mbele! Nafanya kazi mjini sikatai, ila naishi kijijini boko! Kule migomba kama moshi, ng'ombe kama kawa, kuku wa kienyeji wa kufa mtu! Jembe hapa ni nyumbani kwake.LOL!
 
Kumbe ndo maana ukaitwa bht!!!....ok...ok...!

Una bahati sana kwamba mdogo wangu XPIN anaishi town maisha yote!

Ungekuwa naniliu wa mtu kama mimi,..oooh, nakwambia ungejifunza jembe bila kupenda, maana kwetu kule heshima ya mwanamke inakuja kwa kupitia jembe tu, na si kuwa na nanihino kuubw kama ilivyo kwa wanawake wa mjini..lol!

PJ ntake radhi Iribini kuishi kijijini Boko na mimi wapi na wapi??? afu mi si naniliu wa Iribini
 
.......Nimezaliwa mjini na kukulia mjini, wazazi wangu ni makabila mawili tofauti, hivyo nimeweza kwenda vijijini kwao wakati wa likizo nilivyokuwa mdogo na hivi sasa.

Kijiji alichotoka mama yangu hakipo tofauti sana na mjini , sema tu hakuna maghorofa makubwa kama haya ya hapa posta.

Kijiji hicho huduma zote za msingi kama maji, umeme, zahanati na shule nzuri zipo. Raha ya kijiji hichi ni mazingira, kina mazingira mazuri na hali ya hewa nzuri kuliko Dar. Upande wa vyakula ndio usiseme, unapata chakula natural tena kwa bei nafuu.

....Kijiji cha pili nilichoenda ni upande wa my daddy, sasa hichi ndio kijiji halisi, maana nyumba kwanza zipo mbali mbali na nyumba ipo katikati ya mazao.Kama umesafiri kwa basi kwenda huko, sehemu ilipo stand ya bus hadi ufike kijiji ni mbali kweli kweli, utatembea hadi utalia kama ni mtoto.Nadhani hichi kijiji hakina tofauti sana na baadhi ya vijiji vingi viliyopo hapa nchini.

....... Mie bado tu napenda kwenda kijijini, hata kijiji kiweje maana nyumbani ni nyumbani. Japo wazazi wote wapo hapa Dar, ila nikipata likizo tu lazima nitie timu kwenda kijijini kusalimia wanaukoo na kupata fresh air.
 
Maskini hawezi msaidia maskini mwenzake
Mkulima hawezi msaidie mkulima mwenzake
Mfanyakazi hawezi msaidia mfanyakazi mwenzake

kuna haja ya kubadilisha kwa makusudi kabisa na kutengeneza mchanganyiko wa kijamii ile watu wa vijiji watambue umuhimu wa "ubora wa Maisha"

Kijijini kwetu hakuna tatizo la umaskini ila kuna tatizo la watu kutojua umuhimu na ubora wa maisha..sioni mantiki ya mwanakijiji mwenye ekari kumi na ng'ombe hamsini kuishi maisha duni (shelter sehemu anayolala, chakula anachokula, usafiri anaotumia, usafi wake wa mwili e.g. kuoga, kufua nguo etc) kupita muuza magazeti Dar anayeisha chumba kimoja tandika nafikir urban poverty is too critical than rural poverty

isipokuwa watu wa mjini wanafahamu umuhimu wa ubora wa maisha kama vile kuoga, kuvaa nguo safi, kulala eneo na sehemu nzuri (kitanda na godoro) vijijini mtu analala ovyo ovyo..japo ana ng'ombe..

Nimeishi kijijini siwezi kuishi kama nilivyoishi zamani lazima nipa-improve sana.

Ustaadhi nina swali kwako. Kule nyumbani Pemba, kuna mtu anaweza kuwa na ng'ombe hamsini kweli? Ni mfano tu!
 
umenikumbusha mbali pakajimmy... haya maisha yana utamu wake kwa kweli.
 
hapa ndio tutawajua watu wanaoyajua maisha ya viijijini vizuri.
Balantanda na PakaJimmy nimekubali uzoefu wenu. The Boss nadhani hapa kimya...
 
leo wajameni mmenikumbusha miaka 9/10 iliyopita...nimezaliwa mjini na kukulia mjini lakini likizo nyingi tu hadi za high school nilikuwa naenda kijijini, wakati mwingine nakaa kule mwezi mzima

nakumbuka kutwanga mahindi kwenye kinu hadi kuyakoboa tukitaka kula makande, siku ya kula wali tunatwanga mpunga mpaka kupata mchele kudadadeki!

kufua nguo mtoni kwenye mawe na kuzianika kwenye majani, maji kuchota kisimani au mtoni umbali wa zaidi ya kilometa moja tena sio tambarare ni milima na mabonde na ndoo kichwani kwa kwenda mbele....

nakumbuka tukiamka asubuhi tunaenda shamba kuchimba magimbi, na kukata mikungu ya ndizi...magimbi yanachemshwa kwa breakfast, ndizi kwa lunch mchana...overall maisha ya kule ni magumu lakini yana raha zake kwa kwelli...

kilimo kwanza kule ni kaaazi kweli kweli, watu hawana elimu ya ukulima bora wala hawana pesa/pembejeo, miundo mbinu hakuna, ardhi kubwa ni mapori yasiyofikika....kila niiki imagine kilimo kwanza cha kuwasaidia wakulima wa sehemu kama ile naona kama ni ndoto za alinacha...time will tell.
 
PJ mie nashindwa kujibu hapa cause haya maisha nashindwa nisemeje
ila nimefurahishwa sana na wewe ..unajua hali halisi iliyoko vijijini
nitakuwa huko kijijini kwa muda wa mwezi mzima ..nitakupa update
..Nina imani update yako haitakuwa na uhalisia wa huko kijijini..nikikuangalia tu sidhani kama unaweza kuweza kuweka mtungi wa maji kwenye hizo rasta zako za kimasai, wala hutaweza kusafisha meno yako kwa mswaki wa mti na kipande cha mkaa au urekebishe menu kwenye jiko la kuni au kunywa maji ya kisimani bila ya kuchemsha wakati jana lunch time nilikuona na kichupa cha maji ya mlimani unajivinjari.Utaweza kulalia kitanda cha kamba weye???...So tunasubiri simulizi zako za kuchonga!!!
 
kwamba tumetoka kule tulikokuwa kupitia msaada wa Elimu.

Hakika tuna kila sababu ya kuwashukuru wazee wetu, na pale tupatapo hela ya sukari tusiwasahau[/QUOTE]

Kweli kaka PJ hapo umenena!!!!
 
..Nina imani update yako haitakuwa na uhalisia wa huko kijijini..nikikuangalia tu sidhani kama unaweza kuweza kuweka mtungi wa maji kwenye hizo rasta zako za kimasai, wala hutaweza kusafisha meno yako kwa mswaki wa mti na kipande cha mkaa au urekebishe menu kwenye jiko la kuni au kunywa maji ya kisimani bila ya kuchemsha wakati jana lunch time nilikuona na kichupa cha maji ya mlimani unajivinjari.Utaweza kulalia kitanda cha kamba weye???...So tunasubiri simulizi zako za kuchonga!!!

Hahahaaa:

Laligeni, mbona unamwona kwa mashaka sanahuyu dada FL1?
Usiwaone hawa wadada wazuri hapa mjini(especially wale wa 25+), wengi wao ni wa vijijini. Wakifika huko wanabadilika by 180degrees na kuwa wakulima.
Mi naamini FL1 atatusimulia vyema kabisa yanayojiri vijijini, japo si kwa accuracy ya 98%
 
Wazazi wangu wote ni wa-shamba, nimezaliwa shamba, nilipotimiza miaka mitano nilichukuliwa na mjomba wangu mpenzi aliyekuwa admin wa sehemu flan na kupelekwa mjini maalum kwa ajili ya KUSOMA, shule ya msingi ilikuwepo kijijini kwetu kwa muda mrefu kidogo, lakini mpaka mm nafikisha umri wa miaka mitano historia ya kufaulisha ilikuwa ni mwanafunzi mmoja tu (ambaye ndiye mjomba wangu), kulikuwa na tetesi kuwa waalimu walikuwa WAKIUZA majina ya wanafunzi waliofaulu kwa watu wa vijiji vya jirani!

Pamoja na kuondoka village nikiwa na miaka mitano, mjomba wangu alihakikisha kuwa tunaenda kjjn kila likizo. Mambo yalitofautiana kutokana na msimu weyewe, nilichukia sana kipindi cha masika, kwani ilikuwa ni kilimo kwa kwenda mbele, unaamshwa saa kumi usiku kwaa ajili ya kwenda KUTUPIA (kupanda mbegu) wakati wakubwa wakilima kwa jembe la kukokotwa na ng'ombe (plau), unaambiwa hesabu raundi tatu halafu utufuate nyuma na mbegu, basi mwanaume unahesabu raundi SITA, mahindi yakija kuota yapo mbalimbali kama meno ya kibogoyo! Hiyo kitu inaenda kazi mpaka saa sita mchana (hapo hakuna chai wala uji, kama mnapanda karanga bahati yako, unakula mbegu tu, nakumbuka bibi alikuwa anatia majivu ya kinyonga ili tusile mbegu, lakini ngoma ilikuwa inafikichwa na kwenda kinywani. Mkitoka hapo mida ya saa sita mnaanza safari ya mguu saa nzima kurudi home, mnafika mnakunywa uji, mnapumzika robo saa mnakula ugali, mnachukua majembe ya mkono kwenda kupalilia, hiyo ngoma mpaka jua lizame, raha pekee ni kualika watu wengi kusaidia kulima, basi anachinnjwa n'gombe mzima nyama inacchemshwa bila kuungwa , na bonge la ugali. hali inakuwa hivyo siku zote isipokuwa jumapili tu

Likizo za kiangazi nilizifurahia sana,ilikuwa ni kipindi cha mavuno, mnaenda shambani asubuhi kurudi jioni, lakini hakuna njaa kwa sababu matango, karanga, matikiti maji, viazi, na miwa kibao shambani, basi mnavunaa jioni mnapakia kwenye mkokoteni wa kuvutwa na ng'ombe (wenye wanaita TELA). Habari ya maji ilikuwa inasumbua kidogo, sisi familia yetu hapo kjjn ilikuwa na uwezo, kwa hiyo suala la maji tulikuwa tukichukua TELA letu usiku wa saa tisa wakati hakuna foleni kisimani, kisima chenyewe kilikuwa umbali wa saa moja hv porini, basi huko mnakutana na taa za wachwawi na milio ya fisi tu, tunajaza pipa zetu tatu tunarudi zetu home.

Pamoja na tabu nyingi kijijini kuna burudani tosha, hasa mambo ya ngomani, harusini (hakuna kadi na mahudurio ni muhimu kama msibani), au gulioni kuchagua kaundasuti mpya za KIMPRINI na viatu vya TAFU baada ya mauzo ya mazao.
 
Pamoja na tabu nyingi kijijini kuna burudani tosha, hasa mambo ya ngomani, harusini (hakuna kadi na mahudurio ni muhimu kama msibani), au gulioni kuchagua nguo mpya na viatu vya TAFU baada ya mauzo ya mazao.

Mkuu Amoeba

Wewe una uzoefu wa ukweli babaake!
Umenifurahisha hapo kwenye red!

Na kuhusu viatu, hapo mi umenikumbusha raba fulani SIJUI ZA KICHINA, tulikuwa tunaziita DH, sijui ndo Double Hapiness, au nini, lakini ilikuwa ukiwa nazo we ndo mjanja, na kila sikukuu unahakikisha unawapiga bao wenzio kwa kuwa navyo vipya, huku umevalia suruali kitambaa cha KIMPLINI!...huh,what a sweet life!
 
..Nina imani update yako haitakuwa na uhalisia wa huko kijijini..nikikuangalia tu sidhani kama unaweza kuweza kuweka mtungi wa maji kwenye hizo rasta zako za kimasai, wala hutaweza kusafisha meno yako kwa mswaki wa mti na kipande cha mkaa au urekebishe menu kwenye jiko la kuni au kunywa maji ya kisimani bila ya kuchemsha wakati jana lunch time nilikuona na kichupa cha maji ya mlimani unajivinjari.Utaweza kulalia kitanda cha kamba weye???...So tunasubiri simulizi zako za kuchonga!!!

Na bado mengi hujayasema: Kwenda porini na shoka kutafuta kuni. Kuchunga ng'ombe na mbuzi, kule kwetu kuna kuchuma kahawa, kutoa mbolea kwenye zizi na balaa kubwa kuliko vyote kulima shamba zaidi ya heka mbili kwa jembe la mkono! Mwanakijiji acha aitwe mwanakijiji. Ukimwona mwanakijiji anakunywa bia na nyama choma mpigie makofi mara tatu! Anastahili!
 
hata mimi nimeishi na kukulia kijijini!mjini nilikuja just by chance!
 
Back
Top Bottom