Asprin
Platinum Member
- Mar 8, 2008
- 68,408
- 96,738
hata mimi nimeishi na kukulia kijijini!mjini nilikuja just by chance!
Hahaha! CHAWOTE village! LOL!
hata mimi nimeishi na kukulia kijijini!mjini nilikuja just by chance!
Tofautisha kati ya kuishi kijijini na maisha magumu , hii chai anasa na kunywa uji wa chumvi hata mijini hayo maisha yapo na watu wanaishi.PJ yale maisha niliyoishi kijijini sipendi mtoto wangu aje hata aguse kabisa
chai ni anasa mojawapo,sanasana uji wa chumvi,kukata kuni kila jmosi,kufuata maji bondeni,afu bado ili uende shule na vihela kidogo inabidi ufanye kibarua cha kupanga nyanya,
ambacho huwa nakimiss kijijini niwapo huku mjini ni ulazi na komoni kwakweli
Mkuu Amoeba
Wewe una uzoefu wa ukweli babaake!
Umenifurahisha hapo kwenye red!
Na kuhusu viatu, hapo mi umenikumbusha raba fulani SIJUI ZA KICHINA, tulikuwa tunaziita DH, sijui ndo Double Hapiness, au nini, lakini ilikuwa ukiwa nazo we ndo mjanja, na kila sikukuu unahakikisha unawapiga bao wenzio kwa kuwa navyo vipya, huku umevalia suruali kitambaa cha KIMPLINI!...huh,what a sweet life!
teh teh, hizo watoto wa mjini waliita dada halima, shamba ziliitwa dada holo! zilikuwepo kabla ya NJUMU, msister duu waligonga redimedi nyekundu zenye vidoa vyeupe na kicheni begani, walifunga mkanda wa lastiki wenye kipepeo tumboni, walivaa viatu vya loso na kuchoma nywele na kuzibana na kibanio cha plastiki chenye alama ya dole.
ahahahah hii imenifurahisha...kuna rubber shoes zilikuwa za Bata tukiziita' rubber mshenzi" we acha ukiwa nazo yaani shuleni ni wewe tu....ah!
Mimi bwana life la village huniambii kitu, mambo ya kuamka asubuhi na kunywa chai na kiporo cha ugali mbona sana tuu, kufua na majani ya mpapai, maswala ya kuoga kijijini si muhimu ki viile, maisha ya kijijini ni peace sana huwa hakuna stress au kuna anaebisha?
PJ mimi nimezaliwa na kusomea shule ya msingi kijijini. Nilianza kutoka kijijini kwa mara ya kwanza baada ya kufaulu mtihani wa darasa la saba na kuchaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari. Huo ndio ulikuwa mwanzo wa kupanda basi na treni.
Watoto wangu huwa nawachekesha kuwa wakati wao naanza kuwavalisha viatu wakiwa bado wanabebwa, mimi nilianza kuvaa kiatu nilipokwenda sekondari. Maisha ya shule ya msingi nilitembea umbali wa karibia kilomita mbili kwa mguu na njia hiyo ilikuwa na changalawe. Unaweza ukapiga picha maisha hayo. Hata kiatu nilichovaa siku ya kusherehekea kumaliza darasa la saba niliazima, suruali nilivaa ya baba ilibidi ipunguzwe ili iweze kunienea. Ni shati tu ndilo mzee alijitahidi akaninunulia mtumba. Kweli ninamshukuru mzee wangu kuniwezesha kufika hatua niliyofikia leo.
Kama mtoto wa kwanza wa kiume nilimsaidia mama kuosha sahani, kuwabeba wadogo zangu mgongoni na kwenda shambani karibia kila siku. Hata kama miaka zaidi ya 30 imepita nayakumbuka maisha hayo. Hata hivyo natamani watoto wangu na wajukuu wasipitie maisha haya.
teh teh, hizo watoto wa mjini waliita dada halima, shamba ziliitwa dada holo! zilikuwepo kabla ya NJUMU, msister duu waligonga redimedi nyekundu zenye vidoa vyeupe na kicheni begani, walifunga mkanda wa lastiki wenye kipepeo tumboni, walivaa viatu vya loso na kuchoma nywele na kuzibana na kibanio cha plastiki chenye alama ya dole.
veryGood,
asante sana PJ
,nimekumbuka mbali sana....binafsi nimezaliwa kijijini,nimesomea primary school kijijini,nimeingia town baaada ya kufaulu std 7.Leo nimesoma post zote,na kukumbuka mbali...zaidi nimegundua kuwa kumbe about 90% ya wanaJF tu wanakijiji....aisee..wakisema kila mmoja arudi alikokuwa akiwa na umri 12years, JF hakutakuwa na mtu,maana vijiji vingi internet ni msamiati.
WanaJF kumbukeni kwenu,pelekeni maendeleo ya kweli vijijini kwenu....si kubaki town mnakula kuku..
Umenikumbusha zazuu..teh teh, hizo watoto wa mjini waliita dada halima, shamba ziliitwa dada holo! zilikuwepo kabla ya NJUMU, msister duu waligonga redimedi nyekundu zenye vidoa vyeupe na kicheni begani, walifunga mkanda wa lastiki wenye kipepeo tumboni, walivaa viatu vya loso na kuchoma nywele na kuzibana na kibanio cha plastiki chenye alama ya dole.
???????????did anyone understand this fella?
???????????did anyone understand this fella?
Umenikumbusha zazuu..