CHADEMA: Tujadili Utayari wa Kutawala Nchi 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA: Tujadili Utayari wa Kutawala Nchi 2015

Discussion in 'Great Thinkers' started by Mchambuzi, Aug 10, 2012.

 1. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Kilichonipa hamasa ya kuja na mjadala huu ni kauli ya Mwenyekiti wa Chadema (Taifa), Freeman Mbowe, aliyoitoa hivi karibuni ambapo alitamka (nanukuu):

  "Iwapo CCM itashinda uchaguzi mwaka 2015, basi nitajiuzulu Siasa."

  Ifikapo mwaka 2015, CCM itakuwa imetawala Tanzania kwa miaka 54 mfululizo. Kwa Mtanzania aliyeajiriwa, huu ni umri wa kustaafu na kujipanga kula pensheni. Umri huu pia unalingana na wastani wa maisha ya mtanzania (life expectancy). Kwa kila hali, miaka 54 ni miaka mingi sana. Katika mazingira ya kisiasa, jambo hili sio rahisi kutokea katika nchi yoyote ile inayofuata mfumo wa vyama vingi, hasa katika nyakati hizi za demokrasia ya kiliberali (liberal democracy), soko huria (free market) na utawandawazi (globalization).

  Utawala wa CCM kwa miaka zaidi ya hamsini (50) umeambatana na uwepo wa ‘amani' na ‘utulivu', suala ambalo ni moja ya mafanikiio makubwa ya kisiasa kwa CCM. Lakini ni vizuri tukaambiana ukweli – hatuna utulivu Tanzania bali uvumilivu. Vinginevyo kama alivyotamka Nyerere mwaka 1987, ipo siku bomu litalipuka kwani kufaulu kwa CCM kisiasa kunaenda sambamba na kufeli katika nyanja za kiuchumi na kijamii. Kwa mfano, pamoja na kuishi katika mazingira ya amani na utulivu, Mwanakijiji wa Tanzania amekuwa mvumilivu sana kusuburi pengine ipo siku ahadi za TANU wakati wa harakati za uhuru zitatimizwa. Vinginevyo, maisha ya mwanakijiji leo sio tofauti sana na yale ya 50 iliyopita. Isitoshe, tofauti na enzi za Ujamaa, leo wageni wale wale tuliowafukuza kutokana na kuiba rasilimali zetu wanapokewa kwa mikono miwili; wizi wa fedha za walipa kodi ni umeongezeka; matumizi ya rasilimali za nchi yanafaidisha wachache zaidi; tofauti ya kipato baina ya walio nacho na wasio nacho imekuwa kubwa zaidi; dira na mwelekeo kama taifa havipo tena; na hakuna dalili zozote kwamba hali hii inaweza kubadilika katika muda mfupi na wa kati ujao. Ndio maana hata viongozi wengi wa CCM wanakiri chini kwa chini kwamba ‘The Country is Suffering From CCM Fatigue'. Huu ndio msingi wa kauli ya Freeman Mbowe!

  Kuna tofauti kubwa baina ya "Doing the Right Things" na "Doing things Right", na ili ufanikiwe, nilazima kufanya yote mawili. Chadema has been doing the right things ambayo ni kutumia kikamilifu mapungufu ya CCM kujijenga kisiasa. Lakini tatizo linakuja kwenye "doing things right" – ambapo, mbali na kutumia mapungufu ya CCM, kuna umuhimu wa kufanyia kazi viambato (ingredients) vinavyoiwezesha CCM kuwa na mafanikio ya kisiasa. Ushindi wa Chadema utatokana na umahiri wake kufanyia kazi mambo kuu tisa kama ifuatavyo:


  1. CCM ndio iliyoongoza mageuzi ya kiuchumi (political reforms) Tanzania;
  2. Umiliki na Udhibiti wa Vyombo Vya habari;
  3. Uchumi Mkubwa Wa CCM;
  4. Ujamaa Bado ni Relevant (unaendana) na Maisha ya Wengi Vijijini;
  5. CCM imejenga Coalition na Taasisi zote nchini zenye nguvu kiuchumi, kijamii na kijeshi;
  6. Katiba ya Sasa ya nchi inaipa CCM nguvu kubwa kisiasa;
  7. Mbinu za upinzani zinazotumiwa na Chadema Hazipo Consistent na Coherent;
  8. Tanzania inakabiliwa na Udhaifu mkubwa wa Civil Society; na
  9. Political Culture ya Tanzania ina matatizo.
  1. Uongozi wa Mageuzi ya Kisiasa
  Tume ya Nyalali ilikusanya maoni yaliyoonyesha kwamba watanzania wengi walipendelea nchi iendelee na mfumo wa chama kimoja. Lakini CCM ikaamua kuruhusu maoni ya wachache ndio yatawale. Ni dhahiri kwamba suala la vyama vingi lilikuwa haliepukiki lakini mkakati wa CCM wa kuhakikisha mageuzi ya kisiasa hayatokani na nguvu ya umma bali CCM na serikali yake imekijenga sana chama hasa vijijini kwani nimetembea maeneo mengi na kushangazwa na maoni ya wengi kwamba wanachofanya chadema ni "shukrani ya punda ni mateke". Katika nchi nyingi maskini, chaguzi kuu zilifanyika muda mfupi baada ya umma kufanikisha kuleta demokrasia ya vyama vingi, hivyo kupelekea vyama vingi tawala kuanguka na kupotea katika medani za siasa. Nchini Tanzania, mbali ya kuruhusu vyama vingi kinyume na matakwa ya wengi, CCM pia ilijiwekea muda wa kutosha (miaka mitatu) kujiandaa kabla ya kuitisha uchaguzi wa vyama vingi. Hili ni jambo la kwanza la Chadema kulifanyia kazi.

  2. Umiliki na Udhibiti wa Vyombo Vya Habari
  Sina haja ya kujadili hili sana kwani lipo wazi, lakini muhimu hapa ni mambo mawili: kwanza ni ile sheria ya mwaka 1976 ambayo hadi leo bado inatumia na madhara yake yapo wazi; pili, ni kwamba muundo na utaratibu wa ufanyaji kazi wa Wizara ya Habari haujabadilika sana na ule enzi ya kimoja. Wizara hii kwa kiasi fulani bado ni extension ya idara ya propaganda na uenezi ya CCM. Chadema ina waziri kivuli wa Habari ambae he/she is supposed to do "things right" in that regard.

  3. Uchumi Mkubwa wa CCM
  Hili lipo wazi kwa Chadema, kwa mfano, katika ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2000, chadema iliazimia kurudisha mali zote za CCM serikalini kwa hoja kwamba mali hizi ziligharimiwa na watanzania wote chini ya mfumo wa chama kimoja. Iwapo hoja hii ina mashiko kisheria, basi kosa linakuja pale Chadema inapoliweka hili kama ahadi nyakati za uchaguzi badala ya kulishughulikia kama chama cha upinzani. Isitoshe, tofauti hii ya kiuchumi baina yake na CCM inachangia sana Chadema kutofanikisha malengo yake za kisiasa. Kupitia rasilimali hizi, CCM pia inafaidika sana na ‘political branding'. Siasa ni bidhaa kama nyingine sokoni, kwahiyo wananchi wanapoona au kusikia ‘brands' kwa mfano ‘CCM kirumba', au maeneo kuitwa "CCM Makao" etc, brand awareness kupitia macho, masikio na memory, haina utofauti mkubwa na ile ya bidhaa nyingine sokonikama Vodacom, CRDB n.k. Isitoshe, kuna watanzania wengi ambao wanaamini kwamba Chadema haistahili kuongoza nchi kwa sababu bado haina fedha. Hii ni imani potofu na ni muhimu kwa chadema kuanza kutoa elimu kwa umma kwamba chama chochote cha siasa kikipewa ridhaa na umma kuongoza nchi, uwezo wake kufanikisha malengo ya kuendeleza taifa unatokana na fedha za walipa kodi na kwamba hivyo ndivyo CCM imekuwa ikifanikiwa kutawala.

  4. Ujamaa Bado ni Relevant (unaendana) na Maisha ya Wengi Vijijini
  Itikadi ya Ujamaa imebakia kuwa nadharia, kwani kivitendo, CCM inatekeleza sera za soko huria zinazoendekeza ubepari na elements zote zinazoendana na mfumo huo. Lakini pamoja na hayo, bado Ujamaa unaendana na maisha ya asili aliyokuta mkoloni vijijini. Ndio maana TANU ilipata wafuasi wengi walioamini kwamba lengo kuu la TANU ni kumuondoa mkoloni na kuwarudishia wananchi utamaduni na maisha yao ya awali. Hali hii pia ilichangia sana Nyerere kuamua kufuata sera ya Ujamaa mwaka 1967 kwani Tanganyika huru ilikuwa dominated zaidi na vijiji vilivyosheheni wakulima wadogo wadogo waliokuwa wanaishi katika umaskini uliopindukia. Mazingira haya provided "excellent material and social basis for Ujamaa to flourish" – kwani dhana ya Ujamaa iliakisi maisha halisi ya walio wengi; lakini pia malengo ya sera ya Ujamaa na kujitegemea yaliendana na ndoto za wananchi wengi.

  Tatizo lililopo sasa ni kwamba - Chadema haijafanikiwa kuja na itikadi ambayo wananchi wengi (wale waliounga mkono TANU) wanaweza kuikubali kama ndio mbadala wa kweli wa sera ya Ujamaa. Ni muhimu kwa Chadema kujipanga mapema na kurekebisha itikadi yake ya sasa ili iendane na uhalisia wa maisha ya watanzania walio wengi, lakini muhimu zaidi, iendane na ndoto ya watanzania hawa kwani kwa ujumla, hali zao na ndoto zao hazipishani sana na zile za enzi ya TANU na uhuru (1950s-1960s), na uliberali kama sera na itikadi, ambayo hata Chadema inaifuata, na pia CCM kuitekeleza kwa miaka zaidi ya 20 sasa, ni chanzo kikubwa cha umaskini Tanzania.

  5. CCM imejenga Coalition na Taasisi zote nchini zenye nguvu kiuchumi, kijamii na kijeshi.
  Kwa mfano, sekta binafsi (wafanyabiashara); majeshi ya ulinzi na usalama; vyama vya ushirika; watumishi wa umma; mashirika ya umma n.k. Tukianza na sekta binafsi, sekta hii ni muhimu sana katika kusaidia Maendeleo ya vyama vya siasa na sio kwa Tanzania tu, bali hata mataifa makubwa. Ingawa sekta hii haikupewa nafasi wakati wa mfumo wa chama kimoja, Tanzania huru ilikuwa na tabaka hili ambalo liliwezeshwa na mfumo wa kikoloni, hasa wahindi. Sasa ili waendelee na shughuli zao katika mazingira ya Ujamaa, wengi wao walitegemea kulindwa na baadhi ya viongozi wa TANU/CCM, ambao kwa kumzunguka Nyerere, walianza kuwa washirika wakubwa wa wafanyabiashara, hasa katika wizi wa rasilimali za umma. Mfumo wa vyama vingi ulipoingia mwaka 1992, na pia sekta binafsi kuhalalishwa, sehemu kubwa ya wafanyabiashara hawa ilikuwa tayari loyal kwa CCM, hivyo ikawa vigumu kwa vyama vipya vya siasa kujenga mahusiano na kada hii.

  Kumekuwa na kelele nyingi kwamba CCM imenunuliwa na wafanyabishara, lakini lazima tukubaliane kwamba hakuna chama cha siasa kinachoweza kufanikiwa bila kuwa na uhusiano wa karibu na wafanyabiashara. Hata Chadema ikipata mwanya huo, ni muhimu ifanye hivyo, ili mradi iwe katika mazingira transparent, incorrupt na yanayozingatia taratibu zilizopo. Isitoshe, ni sahihi nikisema kwamba bila ya Chadema kuwa na viongozi kadhaa wenye uwezo mkubwa wa kifedha, isingefanikiwa kufika ilipo leo.

  CCM pia ilishajijenga kwenye vyombo vya ulinzi na Usalama, kwa mfano, ilikuwa ni kawaida kwa viongozi wa juu wa jeshi kuwa wajumbe wa halmashauri kuu ya taifa (NEC) na Kamati Kuu (CC); vyombo ambavyo hadi leo vina maamuzi ya juu katika nchi yetu. Nafasi hizi pia walipewa viongozi wa taasisi za umma (mfano NBC, NIC/Bima); viongozi wa vyama vya wafanyakazi; viongozi wa vyama vya ushirika n.k; Pamoja na mabadiliko ya kutenganisha siasa na utumishi wa umma, majeshi ya ulinzi na usalama n.k, CCM bado ina mkono mrefu katika taasisi hizi, hasa kupitia mamlaka ya uteuzi ya Rais.

  6. Katiba ya Sasa ya nchi inaipa CCM nguvu kubwa kisiasa
  Jambo hili tayari linaeleweka lakini nitalijadili kidogo. Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 msukumo wake mkubwa ulikuwa ni muungano wa CCM na ASP (1977), kwani kabla ya muungano wa vyama hivi viwili, Tanzania haikuwa na katiba rasmi bali ya mpito kwa miaka karibia kumi tatu: 1964 – 1977. Katiba ya Tanzania (1977) ilitungwa ili kuhalalisha ufalme wa CCM. Moja ya mambo muhimu yanayopiganiwa katika michakato ya katiba mpya katika nchi yoyote ni "Democracy/democratization of the the society." Maana rahisi ya democratization ni - mabadiliko ya sheria/kanuni/taratibu za msingi za kuongoza mwenendo na utawala wa nchi husika. Katika mchakato unaoendelea wa kupata katiba mpya Tanzania, ni muhimu chadema ikaelewa mambo mawili:

  i. Kwanza ni kukumbushana tu kwani tayari linajulikana: there has to be a compromise baina ya nini CCM inataka kiwepo/kisiwepo ndani ya katiba mpya na nini Chadema pamoja na wadau wengine wa demokrasia wanataka kiwepo/kisiwepo ndani ya katiba mpya. Ni vigumu kushawishika kwamba Chadema (na upinzani kwa ujumla) itafaidika na mchakato huu kuliko CCM, hasa ikizingatiwa kwamba uteuzi wa wajumbe wa tume husika kwa kiasi kikubwa una mkono mrefu wa CCM. Pia ni vigumu kuelewa kwanini mwanazuoni incorrupt and sober katika masuala ya sheria ya katiba, Professor Issa Shivji ambae anaheshimika kimataifa katika fani hiyo, hakuteuliwa kwenye tume ya Warioba.

  ii. Pili, pamoja na Chadema kufanikiwa kuwa sehemu ya historia ya katiba mpya, wasijisahau na kudhania kazi ndio imekwisha kwani kazi ndio kwanza imeanza. Siasa za katiba mpya zitatawala sana uchaguzi wa 2015, hasa suala la muungano. Mwisho wa siku kutakuwa na referendum, hivyo na suala muhimu kuzingatia ni kwamba – bado Chadema haina uhakika wananchi wengi wataegemea upande gani kuhusu masuala mbali mbali katika referendum kwa maana ya – hatujui masuala yepi yatapata kura nyingi za NDIO au HAPANA. Sasa, iwapo leo chadema tayari wana misimamo ya wazi kuhusu masuala fulani fulani, halafu baadae, aidha kwa uhalali au kwa kuchakachua, referendum ikatoa matokeo kwamba wananchi wengi wapo upande tofauti na msimamo wa Chadema, haya yatakuwa ni maafa makubwa sana kwa Chadema kwa 2015 and beyond.

  7. Mbinu za upinzani zinazotumiwa na Chadema Hazipo Consistent na Coherent
  Kwanza Chadema wanastahili pongezi kwa kuonyesha ukomavu wa kisiasa kwa kuwa politically active majira yote, tofauti na zamani ambapo kilikuwa ni chama cha msimu wa uchaguzi tu. Lakini pamoja na mafanikio haya, bado Chadema kinaonyesha udhaifu mkubwa kwenye mbinu inazotumia kuendesha siasa za upinzani. Mbinu za Chadema kwa kiasi kikubwa hazina consistency (uthabiti) na coherence kwani zinabadilika mara kwa mara. Hili ni tatizo, hasa pale chama kinapokuwa hakina mvuto unaotokana na itikadi bali masuala ya mpito (mfano ufisadi) au mvuto wa wapiga kura unaotokana na personalities za viongozi kadhaa. Katika mazingira ya namna hii, umma (hasa wenye uelewa mdogo wa mambo), unaofuatilia siasa za chadema unaishia kuchanganyikiwa, huku ukizidi kuwa vulnerable na propaganda za vyama vingine vinavyoishambulia Chadema.

  Yapo masuala ambayo chadema huwa na msimamo kama chama, lakini huwa inatokea mara nyingine individual leaders wanasimamia mambo ambayo mara nyingine yanapishana na mtazamo wa chama, au wa viongozi wengine. Kuna mifano kadhaa:

  · Kwanza, Upinzani wenye utiifu na uaminifu kwa CCM – kuna nyakati viongozi wa Chadema huwa wanahubiri sera mbadala wa CCM huku wakiendelea kukitambua CCM kama ni chama halali chenye kuendesha serikali halali.

  · Pili, Upinzani wa kuasi – Mara nyingine Chadema huonyesha umma kwamba chama kimejenga disloyalty na utawala wa CCM, lakini unakuta sio viongozi wote wanaoshikamana katika misimamo kama hii. Kwa mfano mwaka 2010 wabunge wa chadema walipotoka bungeni kukacha hotuba ya Rais Kikwete kufungua bunge, Zitto hakushiriki.

  · Tatu, Upinzani dhidi ya muundo wa kisiasa (hasa katiba ya nchi) – Chadema wamekuwa wanapinga vipengele vingi vya katiba ya sasa, hasa vinavyohusiana na mapungufu ya current political system (mfano suala la muungano n.k), huku wakiendelea kuitambua serikali iliyopo madarakani kwamba ni halali kwa mujibu wa katiba ya nchi iliyopo sasa.

  · Nne, Upinzani dhidi ya Itikadi ya CCM, lakini bila ya kutoa dira na itikadi mbadala iliyo practical – Chadema wamekuwa wanapinga sera nyingi za CCM bila ya kutoa itikadi na dira mbadala kwa Ujamaa; mpaka sasa hawana itikadi yenye kusisimua na kuvutia wananchi walio wengi (vijijini) – [rejea mjadala wangu wa awali kuhusu relevance ya Ujamaa katika vijiji vya leo Tanzania].

  Ni muhimu nisisitize kwamba tatizo sio mbinu hizi za upinzani bali the inconsistency na incoherence katika hilo.

  8. Tanzania inakabiliwa na Udhaifu wa Civil Society

  Leo, watanzania wengi wanaishi kama ndugu, hasa wakati wa shida, lakini hawana ‘associational life', hata kwa standard za bara la Africa. Nitafafanua.

  • Demographics:
  Watanzania wengi wanaishi pembezoni mwa nchi (vijijini) huku wachache wakiishi katika maeneo machache ya miji. Vile vile, watanzania wanaishi kwa kutapakaa ovyo na katika makundi madogo madogo (rejea sababu za kuanzishwa kwa vijiji vya Ujamaa). Kwa mfano, wingi wa idadi ya watu kwa kilometa za mraba (population density per square kilometer) ni ndogo sana ikifananishwa na nchi nyingi za Africa, na pia zote za maziwa makuu. Kwa mfano, Kwa Tanzania, wakati population density ni (49); Kenya ni (76); Uganda ni (182); Rwanda ni (473); na Burundi ni (411). Tanzania pia inakabiliwa na hali duni ya miundo mbinu, hivyo kuzidi kufanya 'associational life' kuwa ngumu zaidi. Kwa mfano, ‘social interaction' baina ya jamii mbalimbali Tanzania upo chini sana; interaction za namna hii zipo limited kwenye maeneo ya miji au kwenye major highways watu wanapokuwa safarini. Matokeo yake ni kwamba inawia vigumu kwa watanzania wengi to engage in any meaningful collective action to promote or defend a particular cause or idea, kwa mfano to organize wananchi for a political cause.

  • Social Capital:
  Kama tujuavyo – umoja ni nguvu, na utengano ni udhaifu. Hii ndio dhana ya social capital, lakini kwa maana nyingine rahisi zaidi, social capital ni mtaji unaotokana na umoja, ushirikiano na pia hali ya kuaminiana baina ya watu waliounda kundi fulani kwa nia ya kufanya kazi kwa pamoja ili kufanikisha malengo waliyojiwekea. Tofauti enzi za Ujamaa, leo Social Capital Tanzania ipo very weak. Kwa mfano, jamii ya kitanzania haiaminiani tena, iwe katika mazingira ya maisha kwa ujumla wake, au mahusiano ya uongozi/uanachama. Chanzo cha tatizo hili ni kukithiri kwa rushwa, utapeli, ubinafsi, utamaduni wa kulindana, kutokuwepo kwa rule of law, mmomonyoko wa maadili etc. Tatizo hili limekithiri zaidi baada ya uongozi wa CCM kuvunja Arusha la Arusha mwaka 1992.

  9. Na Mwisho ni tatizo la Political Culture Tanzania.

  Kila jamii inaongozwa na values, norms na ethics – ambazo husaidia kutoa mwongozo juu ya mwenendo au tabia za kuzingatiwa katika mazingira ya siasa (political behavior), hasa mahusiano baina ya viongozi na wananchi. Historia ya nchi yetu inaelezea vizuri sana jinsi gani viongozi wengi wa kimila walivyokuwa na maadili mema kabla ya ukoloni na jinsi gani hali ilivyoanza kubadilika baada ya kuja mkoloni, hasa kutokana na sera yake ya ‘divide and rule'. Huo ndio ukawa mwanzo wa kuporomoka kwa maadili yetu ya uongozi hadi leo.

  Baada ya uhuru, makabila mbali mbali yalikuwa yameshakuwa polluted na corrupted na ukoloni. Ili kuepuka madhara mengi zaidi, Nyerere alitumia mbinu mbalimbali ili kuondoa tofauti zetu kwa misingi ya ukabila, udini, ukanda na badala yake kujenga jamii yenye kuheshimiana kama binadamu, hali ya umoja, undugu, na usawa. Lugha ya Kiswahili pia ilikuwa muhimu katika kufanikisha lengo hili. Sera Ujamaa ilitupatia itikadi na dira inayoeleweka, na pia maadili ya uongozi, hivyo baadhi mapungufu ya utamaduni wa Kiswahili hayakuweza kujitokeza sana wakati wa ujamaa (tukumbuke kila kabila/utamaduni una faida na mapungufu yake), hivyo tulifanikiwa kujenga political culture bora, juu ya utamaduni wa kiswahili, bila matatizo makubwa. Lakini tatizo ni kwamba hatukuwa tumejiandaa kwa siku za mbeleni:

  Kwa mfano, yale yote Nyerere aliyojitahidi kuyadhibiti (hasa suala la ukabila katiak uongozi/siasa), yameanza kushamiri kwa kasi kubwa ndani ya jamii yetu. Leo hii masuala ya uongozi na siasa yametawaliwa sana na misingi ya Ukanda, Ukabila na Udini. Nje ya fedha, ni vigumu kwa Mtu kufanikiwa kupata uongozi bila ya vigezo hivi vitatu (pamoja na fedha). Inawezekana baadhi ya watu wasikubaliane na mimi katika hili, lakini pengine mifano midogo itasaidia. Kwa mfano, katiba ya sasa ya Tanzania inaruhusu mtanzania yoyote kwenda kugombea nafasi yoyote ya uongozi katika sehemu yoyote ya Tanzania – bara na visiwani. Lakini sote tunajua ukweli kwamba ukiachilia maeneo machache ya mijini, ni vigumu kwa watanzania wa maeneo mengi ya Tanzania kumchagua mtu bila kwanza ya kuangalia vigezo vya ukanda, udini au ukabila.

  Hata katika ngazi ya urais, hali ni hiyo hiyo. Kwa mfano, wengi tumeshasikia kauli kwamba Rais ajaye mwaka 2015 hatatokea kanda fulani; Vile vile kwa miaka mingi, kuna sumu iliyosambaa kwamba Rais wa Tanzania kamwe hatatokana na makabila matatu: (1)Wachaga, (2) Wanyakyusa na (3) Wahaya. Pia, katika siku za hivi karibuni, tumesikia wanasiasa kadhaa wakiapia kwamba rais ajaye 2015 lazima atoke mkoa fulani etc etc. Tumeanza kujenga na kulea tatizo kubwa sana katika jamii yetu; ukosefu wa ushindani wa kisiasa kwa njia ya itikadi, ukosefu wa dira na mwelekeo kama taifa, na uchaguzi wa viongozi unaofuata vigezo vya personalities za wagombea (badala ya misimamo yao), haya yote yanazidi kuimarisha mizizi ya ukabila, udini na ukanda.

  Ni vigumu kwa sasa kubaini masuala la udini, ukabila na ukanda yata ‘play out' vipi katika siasa za CCM na Chadema 2015. Kitakachoweza kutokea ni kwamba – viongozi kutoka dini au makabila fulani wataanza kuunda makundi yatakayo exploit tofauti zilizopo kihistoria kwenye jamii – tofauti za kiuchumi na kielimu, kwani zipo jamii nyingi ambazo zinahisi historia ya nchi na utawala wa CCM haujawatendea haki.
  Uwepo wa ombwe la itikadi utasababisha ushindani wa CCM na Chadema mwaka 2015 utawaliwe na siasa chafu sana. Ni dhahiri kwamba Sera za CCM na Chadema hazipishani sana - wote wanaunga mkono (kwa kujua au kutojua) kumnyonya mkulima ili kufaidisha nchi tajiri, and in return kupata fedha (AID), lakini muhimu ili vyama vyao viendelee kuwa in good books na wakubwa wa dunia yetu (tofauti na Nyerere aliyepingana na upuuzi huu); ndio maana katika hali ya leo, wahisani sasa wanakabiliwa na democracy fatigue, kwani wanajua kwamba uwepo wa CCM au Chadema Ikulu hautakuwa na utofauti wowote mkubwa kkwenye interest zao. Kikubwa wanajali zaidi uwepo wa amani ili strategic interest zao zisipate madhara, hasa vitega uchumi.

  Vinginevyo ni muhimu Chadema ikafanya marekebisho ya maana kwenye itikadi yake, kwani nje ya uchovu wa wananchi na CCM, nje ya agenda ya serikali ya CCM kutokuwa na maamuzi magumu kutatua matatizo ya nchi, na pia nje ya agenda ya ufisadi, Chadema haina ammunition ya kutosha kisera kuitoa CCM magogoni. Hivi karibuni, chadema imekuwa ikifananishwa na TANU, jambo ambalo ni la kheri kwa Chadema. Lakini ili Chadema iwe TANU iliyokamilika, inahitaji ije na ‘new and a radical orientation' inayo challenge dhana ya soko huria (hasa mapungufu yake), na ambayo inahimiza umuhimu wa umiliki wa mageuzi (ownership of reforms kwa wananchi), badala ya sasa ambapo mageuzi yanafuata mtindo wa ‘Top – Down" (badala ya bottom – up). Ni muhimu na ni lazima wananchi wahisi kwamba kuna chama ambacho kina nia ya kuwashirikishwa katika kila hatua ya mageuzi i.e. a bottom up and participatory process (badala ya top – down), kwani tangia mwaka 1985 Tanzania ilipoachana na mfumo wa Ujamaa, wananchi wamekuwa wanatengwa na kuachwa wapigane vikumbo kivyao vyao na nguvu za soko (market forces). Hili linahitaji kubadilika na ndio kete kuu ya Chadema 2015 itakayowaletea mafanikio yenye mashiko zaidi mbali ya vita dhidi ya ufisadi ambayo sio mwarobaini (panacea) ya matatizo ya wananchi walio vijijini. Tukumbushane tu kwamba CCM enzi za ujamaa ilijitahidi sana kuzuia ufisadi lakini hiyo haikutosha kumletea mabadiliko mwananchi wa kijijini.

  Ni mambo haya tisa ambayo nadhani yakifanyiwa kazi na Chadema, basi yatazidi kujenga mazingira ya utayari kwa Chadema kushika madaraka ya nchi 2015 – kwani mbali ya "doing the right things", pia watakuwa wametekeleza dhana ya "doing things right"
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Tatizo CHADEMA deep down hawaamini wanachukua nchi; bado wako bize kuikosoa serikali badala ya kujiandaa kuongoza vizuri
   
 3. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Dr. Slaa alikosea sana alipotamka mwaka jana mbele ya vyombo vya habari kwamba:

  "Kazi kubwa ya Chadema ni kokosoa mapungufu ya CCM, lakini CCM ikiweza kurekebisha yote tunayoyakosoa, basi tutaishiwa hoja".

  Dr. Slaa hakutakiwa kutamka hayo kwa nafasi yake.
   
 4. s

  step Senior Member

  #4
  Aug 10, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 190
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Good comments, nafikiri ni vizuri kuwa more strategic wananchi wameanza kubadilika na chama ni lazima kianze matayarisho ila hakuna aliyekamilifu by 100% tuendelee kukijenga chama.
   
 5. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Hao ni CDM wazee wa kucheza na maneno, CCM ikishinda Mbowe atasema alimaanisha uchaguzi wa ubunge wa Hai!!!
  Slaa si alisema hagombei Urais 2015 kwa sababu atakuwa mzee, lakini sasa tayari swala la uzee halipo anajiandaa kwa kinyang'anyiro!
   
 6. Godlisten Masawe

  Godlisten Masawe Verified User

  #6
  Aug 10, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 739
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hacha kupotosha wewe; Dr slaa/Mbowe/Zitto/Mnyika/Lissu au kiongozi yeyote wa juu wa CDM anapoikosoa serikali ya ccm huwa wanataja sera/njia mbadala ya kufanikisha hilo jambo, kwa maana iyo watakapopata ridhaa ya wananchi watatumia hizo sera/njia mbadala kuongoza nchi ktk kufikia maendeleo yenye tija kwa kila mwananchi (sio sasa JK anasema wingi wa magari dsm ni maendeleo).

  Kwa faida; rejea michango ya Zitto/Mbowe/Lissu/Mnyika bungeni aposhauri serikal ibuni vyanzo vipya vya mapato (apartment/gest/kupunguza misamaha ya kodi ktk makampuni ya madini) badala ya kung'ang'ania kila siku kupandisha kodi ktk bia na sigara.
   
 7. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #7
  Aug 10, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Unajua maana ya kupotosha?

  Kwanini mnaumizwa na any criticisms hata kama zipo constructive? Dr. Slaa Mwenyewe inasemekana baadae hakupenda jinsi alivyoitoa kauli yake.

  Nakushauri kwamba kabla ya kuja na hoja, jaribu uwe unafanya utafiti, pia uwe una digest issues na kuzitafakari objectively (not subjectively) kabla ya kujibu hoja. Vinginevyo katika hili, kidogo unatoka nje ya mada. Pia kumbuka - you are entitled to your own opinion but not to your own facts.
   
 8. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #8
  Aug 10, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Mchambuzi,

  Ukiichambua vizuri mada yako si haba, hoja zimo. Ila naona kama umechanganya mambo mengi sana pamoja. Yaani umelundika vitu vingi ktk kapu moja. Kwa mada hii ungeweza kuwa na mada nyingine ziszopungua tatu zenye kujitosheleza vizuri.

  Sijui kama itawezekana kwa sasa kurekebisha; ila naona shida kuchangia nusu nusu na pia naona shida kuchanganya mambo!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. T

  Temple Member

  #9
  Aug 10, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 34
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 15
  Mchambuzi nakubaliana na wewe, lakini that is too theoretical.

  (1). umeshindwa kutambua wananchi wana mawazo gani kuhusu itikadi za ki- TANU.
  (2) Ni rika gani linathamini itikadi hizo unazo shauri, fahamu kuwa CHADEMA inatumia Vijana kama mtaji wake. Je! ni kweli vijana watashawishika kwa hizo sera zako? No .
  (3) Fanya utafiti vizuri tawala za nchi nyingi za kiafrika hazitolewi/ haziangushwi kwa wananchi kwa kushiba sera bali hoja. CHADEMA wakifuata ushauri wako itawachukua ten years kueleweka.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. mwana wa mtu

  mwana wa mtu JF-Expert Member

  #10
  Aug 10, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 220
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Well said Mchambuzi.

  Nafikiri kungekuwa na uwezekano, katiba mpya (kama kungekuwa na mazingira mazuri ya kutumia nafasi hii: ikiwemo kutumia udhaifu kuwa Serikali ilikuwa haijajipanga kwa mchakato husika;)ingeweza kuwa mwokozi mkubwa!lakini kwa mwenendo wa mambo, sidhani kama Wariona na timu yake watakuwa mwarobaini.

  Na pia Shivji kutokuwemo ni kati ya faulo zilizochezwa na wenye 'utawala' in favour of them.

  Hata hivyo, kumbuka kuwa itafikia mahali, of all the situations ulizosema may not apply kwa watu kuchoka....hapa ndipo changes hutokea regardless ya nini!refre, mapinduzi ya Ufaransa, kuondolewa wakoloni Afrika..na hivi sasa yaliyotokea Misri, Libya, Syria na kwingineko.

  Lakini pia hujaangalia CCM wanavyoandaa anguko lao kwa mambo ambayo wengi wanayasahau kuyaona: shule za kata (uwingi wa wasomi hata kama wanapata zero, lakini ni chachu ya mabadiliko), mitaala ya elimu, matatizo makubwa ya wafanyakazi katika kila nyanja..na hata hayo maisha magumu uliyoyasema!

  Nafikiri THE TIME IS COMING..AND THE FREEDOM is around the corner...naamini hivyo.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #11
  Aug 10, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nimefurahishwa sana na mawazo yako ila lengo "objective" haiko wazi na mapendekezo yako hayaashirii mwelekeo wa kupata mwendelezo.

  1. Kwa hali ya mambo ilivyo, tukubali tupo kwenye "evolution" mambo yanajitokeza, yanajiendesha na kuleta matokeo bila shinikizo. Tofauti na "revolution" mambo yanajitokeza, yanajiendesha na kuleta matokeo kwa shinikizo. Ndiyo maana kauli ya amani na utulivu haitatoka mdomoni mwa CCM hata kwa kumwaga damu. Ni kweli CDM na "wapinzani" wote hawana rasilimali ya kuikabili CCM, ila wanachokifanya kinatosha kwa sababu kina matokeo ya kuwashirikisha wananchi kidhamira kuliko kimatokeo.

  2. Itikadi ziko mbili tu kwa msingi wa kufaidika na rasilimali. Hapa CCM na CDM zimejitenga wazi. Namna ya kuzalisha hawatakiwi watofautiane, ila kwa sasa CCM wako "inefficient" kwa kukosekana kwa lengo la uzalishaji, CDM wananyoosha kidole kuonyesha mapungufu na kutuambia kuwa CCM wadokozi na hawatufaidishi. Hili pamoja na hali ngumu ya maisha tunalipokea na kujiwekea matumaini ya mabadiliko. Nataka kusema misingi ya itikadi haina sababu ya kutofautiana bali usimamizi na mgawanyo wa ngawira ya rasilimali ndilo suala kubwa.

  3. Ni kweli inaonekana CCM imejizatiti sana na vyombo vya dola na taasisi nyingine; ukweli niuonavyo mimi kwa uzoefu, CCM inadhani inafaidika kumbe si kweli. Hivi vyombo na taasisi ndizo zinafaidika kwa kila hali, mimi binafsi naamini hizi ndizo zitaiteketeza CCM. Dalili zote ziko wazi hakuna kitu nyeti cha CCM kisichojulikana na CDM. Vyanzo ni hivyo vyombo na taasisi. Maana yake kwa wenye akili ni kwamba CCM imeporwa madaraka ya utawala kwa hiyo hata uchaguzi uliokuwa unaipa ushindi CCM usio kauli ya wapiga kura uko hati hati. Ushahidi upo kila mahali.

  4. Ukizingatia hoja yangu ya kwanza mimi naona hakuna mjadala wa Utayari Wa Kutawala Nchi 2015, kilichopo ni kuwa wewe na mimi tujiulize je tunataka mabadiriko?

  i. Tunahitaji sisi tutoe kauli ya mabadiriko kwenye sanduku la kura. Hapa nina maana kwanza yaje mabadiriko ya utawala na uongozi halafu tusawazishe mashimo ya CCM ndipo tuendelee na "full" ukombozi.

  ii. Tukikumbusha maumivu tuliyonayo kuhusu tulivyotendwa na CCM ni hatari na mbaya sana; hapa ni kusonga mbele kuondoa magugu kidogo dogo bila pupa. Hapa kama ni kweli tuje na maana moja ya amani na utulivu, uvumilivu ita jina lo lote. Ninachokijua ni kuwa kwa wanaotaka mabadiriko CCM ni tayari Shetani, ila CDM ni mkombozi mbadala bila kujali udhaifu wake. Yaani hata kama hawatatufikisha tunakotaka lakini atutoe tulipo.

  iii. Miundo mbinu ya kuelekea kwenye mabadiriko kama unavyokiri hapo juu halikuwa na halitakuwa jukumu la CCM. CDM ni lazima watumie miundombinu iliyopo. Hawajatutangazia na si vizuri watutangazie ngazi mbali za mikakati yao, inatosha kuamini kuwa kwa sasa wanastahili kupewa jukumu la kuongoza mabadiriko.

  iv. Mikono ya CCM inanuka kila aina ya maovu kwa wananchi, hususan suala la raslimali ambazo wanafaidi, bila ujumbe wa kutufahamisha maovu hayo (ambayo CCM hawajitetei) fursa ya mahitaji ya mabadiriko inakuwa haiko wazi. Kwa bahati nzuri kwa CDM tunawaelewa CDM. Sikubaliani na wewe kwa kutuona sisi wanavijiji hatuielewi CDM; ni kinyume chake nyinyi watu wa mijini ni wasaliti wakubwa kwa sababu nyie si ajabu mnafaidika kiasi fulani tofauti na sisi tunavyopigika.

  Kwa utaratibu wa mabadiriko unavyoendelea sina uhakika wa lengo la mada yako kwamba haitafuti mikakati ya CDM. Ila mimi binafsi nawaamini CDM kwa mikakati yao kwa lengo langu moja tu NIMECHOSHWA NA CCM NAHITAJI MABADIRIKO
   
 12. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #12
  Aug 10, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Mchambuzi, umeleta sredi ambayo kama Watanzania tungekua watu wa kujadili hoja za manufaa kwa taifa letu,ingepata wachangiaji wengi.

  Kama kuna kipindi viongozi wa chama changu CDM wanapaswa kujadili mambo ya msingi nchi yetu itaongozwa vipi baada ya 2015 ni sasa! Hizi stori za watu kutafuta urais,binafsi zinakwaza sana. Siyo wakati wake sasa, tujenge chama! Kikichukua dola kionyeshe tofauti.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. J

  JF-MBUNGE JF-Expert Member

  #13
  Aug 10, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 422
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mchambuzi nakubaliana na wewe..lkn ninaushauri wa ziada CDM kabla ya kuwaza kutawala lazima wawatolee uvivu mapandikizi kwao..maana bila kuwatolea uvivu hawawezi shika dola.

  Nawashauri watafute kura 100 za wanachama CDM JF za kuwashinikiza viongozi wao Mbowe na Slaa wahudhurie mdahalo humu kisha watoe onyo kali kwa wale wote wanaosaliti chama kwa kuacha kukijenga chama na kujijenga wao.

  Hii itawasaidia viongozi wao pia kuwatoa nduli wanaoharibu chama chao ambacho wananchi tunaamini wanania ya dhati kuleta maendeleo. Mie sio CDM lkn nachukia sn vijana iwe wa CCM au CDM sijui NCCR ambaye anacheza siasa za mbimnu ya kuwanyonya wananchi nachukia sn.

  CDM mdharau mwiba????.........................
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #14
  Aug 10, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  sio kweli. hayo ni maoni yako tu, kutokana na unavyoona wewe. hiyo analysis hapo juu isikutishe, hizo ni mbwembwe tu za kujaribu kuwababaisha wavivu wa kufikiri. hivi wewe unaamini hakuna watanzania wenye uwezo wa kuiongoza hii nchi tofauti na hiki kikundi cha mafisadi kilichopo madarakani sasa hivi???????sitaki kuamini wewe ni mvivu wa kufikiri kiasi hicho. nakushauri uwe na amani, IAMINI CHADEMA, IPO TAYARI SANA. HEBU WAAMBIE CCM, WAACHIE NCHI LEO HALAFU UONE.
   
 15. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #15
  Aug 10, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  lakini Dr.slaa hakuyasema hayo kwa bahati mbaya, wanajua udhaifu wa chama cha magamba kuwa kadri unavyowakosoa ndivyo wanavyozidisha makosa ujue jinsi walivyozeheka, hiyo inasaidia kuwajulisha wananchi kuwa magamba wanatupeleka ndiko siko, hivi wasipowakosoa watakuwa wanafanya siasa gani?
   
 16. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #16
  Aug 11, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Naona kama hizo dhana mbili zinapingana, mwanzo umesema kuwa Chadema inaweza kuongoza kwa ridhaa tu bila pesa baadae umesema Chadema kimefika kilipofika kutokana na viongozi kadhaa kuwa na uwezo wa mkubwa wa kifedha.
   
 17. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #17
  Aug 11, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 25,601
  Likes Received: 16,559
  Trophy Points: 280
  Mchambuzi ukiniuliza na mawazo gani kuhusu kesho ya Nchi yangu, naweza kukujibu hivi:

  Nafuu hata Paka awe raisi lakini siyo kiongozi yoyote toka CCM sababu CCM wote hawana uwezo wa kusema Hapana.Hakuna Rais wetu dhaifu wala msaidizi wake hakuna, wote walio CCM wanasubiri ni namna gani apate uongozi ili afilisi zaidi.

  Ile dhana ya vyama vya upinzani vitaleta vita imepitwa na wakati, iangalie Zambia, Malawi mbona vinavyotawala leo ni vilivyokuwa vyama vya upinzani?

  Watanzania tuondoe woga,tuone uchungu na Maliasili zetu tubadilishe mtawala ili hata anayekuja awe mwoga ajue kesho yake ipo kwenye hatihati.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #18
  Aug 11, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  CDM hawahitaji kuzama sana katika itikadi za TANU.VIjana hawaijui TANU, na TAnu haikuwa perfect kihivyo.Ila kuna vifaida vidogo vidogo na kujihusisha nayo , pamoja na vitu fulani ambavyo ni universal vilivyokuwepo katika TANU.

  Kukimbilia sana TANU ni kuwapa CCM comfort zone.Kwani watapunguza nguvu kwa kusema kuwa ni ya TANU, halfu warudi sema kuna ni ya CCM kwa vile ilizaliwa katika TANU.Sasa inabidi pawe na New creations.Ili CDM waseme kuwa wana nia na mshikamano kama TANU ila wanafanya Mambo makubwa kuliko TANU.
   
 19. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #19
  Aug 11, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Ni sawa tu kwani the very vocation of intellectuals is to theorize reality and thereby understand it better.
  Bado nina amini kwamba TANU ilifanikiwa kutokana na kuungwa mkono na wanavijiji ambao walichoshwa na mfumo wa kikoloni ambao uliingilia tamaduni zao na mazoea ya maisha yao kwa ujumla; Ndio maana nia ya Nyerere ilikuwa ni kwa jamii yetu kuanza upya kwa kurudia pale pale mkoloni alipotukuta. Sidhani kama utakataa kwamba maisha ya wengi vijijini leo hii yapo katika hali ile ile kwa miaka 50. Ndio maana nadiriki kutamka kwamba ndoto za mwanakijiji wa leo ni zile zile kama enzi ya TANU; Unapotoa hoja kwamba siwezi ongelea mawazo ya mtanzania kuhusu TANU ki-itikadi, jaribu kutomwangalia mtanzania wa mjini au aliye nje ya nchi, bali mtanzania wa kijijini na maisha yanayomzunguka kwani upesi utabaini kwamba tangia wakati wa ukoloni hadi leo, maisha yake ni yale yale na ndoto zake ni zile zile kwani serikali ya sasa inafanya yale yale, tofauti ni kwamba aliyepo ikulu ni mtu mwenye ngozi kama yao (nyeusi); vinginevyo serikali ya CCM inatekeleza matakwa yale yale ya nchi tajiri kama ilivyokuwa wakati wa mkoloni - kama ilivyokuwa wakati wa ukuloni, mwanakijiji produces for export bila faida yoyote ya maana kwake; mwanakijiji produces food for the urban elites bila faida yoyote ya maana; and I am sorry to say this: Chadema wataenda kuendeleza haya haya Ikulu.

  Kwa ufahamu wako, Vijana wanashawishika na itikadi ipi au sera zipi za Chadema? Au kwa lugha nyingine, ni kitu gani vijana wanachoona kina mvuto kwao kuhusu chadema? Tuzungumzie vijana wa mjini na wa vijijini. Kwa maoni yangu – vijana bado wanatafuta itikadi ya kuiamini, huku wakiwa na uchovu na itikadi ya Ujamaa ya CCM ambayo haijatekelezwa. Chadema inawapa matumaini lakini ni kwa sababu tu haijaingia ikulu bado. Vinginevyo mimi naamini kabisa kwamba itikadi ya Social Democracy ndio mkombozi wa vijana, but kwa bahati mbaya hakuna chama chenye kuzingatia hili.

  You might have a valid point. Lakini naomba nikuulize: Je kwanini imechukua miaka 15 (1995-2010) kwa chadema kuwa na nguvu kwenye umma, kiasi cha kupelekea kuaminiwa kwamba Chama kipo tayari kuchukua madaraka ya nchi 2015? Je, kuna strategy maalum ambayo Chadema walikuwa wanaitumia consistently? Kwani hoja yako inaashiria kwamba kuna mkakati maalum ambao Chadema waliuweka miaka 15 iliyopita na ndio umezaa matunda leo. Ningependa kujua hili kwani binafsi sina taarifa yoyote na badala yake nadhani mafanikio ya Chadema yametokana na Chama kufanikiwa ku link umaskini wa wananchi na ufisadi, wakati ukweli wa mambo ni kwamba ufisadi explains only a fraction of the story – kwanini watanzania maskini. The bigger story ni sera zinazoshinikizwa na mataifa matajiri, sera ambazo hata chadema wataenda kuzitekeleza Ikulu kama CCM inavyofanya sasa. In short, we talk of development but we do not own our development agenda!
   
 20. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #20
  Aug 11, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Unachoshindwa kuelewa hapa ni kwamba TANU ilitoa ahadi ya kuwakomboa watanganyika kisiasa na kiuchumi, ilifanikiwa kisiasa lakini imeshindwa kuwakomboa kiuchumi.

  Watanzania wanahitaji the second independence kwani the first one chini ya TANU haikukamilika. Ni bahati mbaya tu CCM ya sasa inahusishwa na TANU lakini ukweli ni kwamba hizi ni taasisi mbili tofauti kabisa, kwa mfano, TANU haikumkomboa mzanzibari. Mtu anaetatizwa na Chadema kufananishwa na TANU basi sio muelewa wa matatizo ya watanzania.

  Pengine itasaidia iwapo tutaita chama kilichoikomboa tanzania kwa jina lingine lisilohusiana na CCM ndipo itaeleweka vizuri kwanini changamoto za TANU na Chadema ni zile zile.
   
Loading...