kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 17,409
- 17,014
Wakuu ukiachilia mbali wazazi wako kijijini, hivi ulishawahi kuwafanyia watu wa kijijini kwenu kwa ujumla? Umewakumbukaje wewe binafsi?
Mara zote kwenu halisi ni kule ulikozaliwa au kukulia wewe au wazazi wako. Mara nyingi asilimia kubwa ya watu wamezaliwa na kukulia vijijini na kujikuta wako mjini ukubwani kutokana na masomo, kutafuta maisha au kuletwa na ndugu na jamaa. Hata wale wachache ambao wamezaliwa mijini lakini wazazi au babu na bibi zao wanapatikana vijijini.
Bahati mbaya maisha ya vijijini yana changamoto nyingi hasa kutokana na maisha yao kutegemea zaidi maliasili za kilimo cha kutegemea mvua, ufugaji, uvuvi, uchimbaji, na mazao ya misitu. Huduma za kijamii kama ajira, usafiri, nishati, maji, matibabu, malazi, masoko na elimu ni haba na duni. Hii inasababisha watu wengi hasa vijana wasipende kuishi vijijini hivyo kulazimika kujisogeza kwenda mjini kwenda kujaribu bahati zao kimaisha na kujikuta tuko mjini wewe na mimi kwa kuzaliwa ama kwa kuhamia ukubwani.
Sasa wewe leo uko mjini kwenye fursa nyingi, lakini wako ndugu na jamaa zako ambao bado wako kijijini kwenu.
Je, wewe uliyeko mjini leo hii umewakumbuka na kuwafanyia nini wale wanavijiji (watoto, vijana, wazee) wa nyumbani kwenu kwa manufaa ya jumla ya wanakijiji?. Mfano, mimi niliwahi kugharamia kuweka kalafati kwenye njia inayongia shuleni ambayo ilikuwa tatizo kwa watoto kwenda shule wakati wa mvua nyingi.