Uliza chochote kuhusu Rwanda

We niambie mimi nikutumie mpaka pcha na nafasi zao acha blah blah mingi. Swali la pili unajua kikundi cha kitutsi cha ikotany kimeua wahutu wengi kuliko watutsi waliouawa kwenye ile genocide?
Hizo picha sidhani kama sina cha kufanya, kwa sababu wanyarwanda wanachokiangalia ni umhimu wa fulani kwenye nafasi aliyo nayo.
Mtutsi anayesimamia haki, na mhutu anaesimamia wazo la kuua watutsi. Bora nani?

Hao inkotanyi, wawalipe tabasamu wauwaji?
 
Nakataa, kigali kubwa karibia Mwanza, kahama bado sana kuilinganisha na chigali kwa miundombinu mpaka idadi ya watu
Sijui umemaanisha ukubwa gani. Je, Kigali inaanzia wapi, inaishia wapi? Mfano, Mwanza, unajua kutoka Buhongwa, mpaka Kisesa, kuna umbali gani? Hapo ni mjini kati. Maana nikiongelea nje, ntaanzia Usagala, nyuma ya Kisesa sijui mji kwa sasa umefika wapi!
 
Kuna tofauti gani kati ya wahima na watusi?Kingine nikija Kigali sehemu zipi napata watusi wa kwenda hawa wa Benako wamenichosha
 
Tatizo ulilo nalo halina tofauti na kinachoendelea mashariki mwa Congo.

Je, ni nini hasa kinachopelekea kudai kwamba ni wanyarwanda? Unamaanisha uongozi wa nchi yako ni dhaifu kiasi cha kuruhusu hayo? Kwa kifupi, uhamiaji, usalama wa taifa, hawajui wanachokifanya?

Ebu weka akiba ya maneno, nchi haingozwi kama serikali ya mtaa.

Uwepo wao pengine, kama hawana madhala kiusalama, nilihisi ungekuwa faida ya ziada. Wanapolima, wateja ni watanzania. Kila kinachofanyika, ni kwa manufaa ya nchi.

Je, wasiwasi wako, ni kwamba na wao wanapata chance ya maisha?
 
Kuna tofauti gani kati ya wahima na watusi?Kingine nikija Kigali sehemu zipi napata watusi wa kwenda hawa wa Benako wamenichosha
Hahahahahahaha, wahima ni jina wanalopewa wanaoitwa watutsi kwa sasa wapo Uganda. Kama ilivyo, kwa Wanyamlenge, ambao ni wale waliopo DRC.

Watutsi wa kwenda nao, umechoshwa na hao wa Benaco!!! Wale unaochoka nao, ni kwamba hujaamua unataka nini, kwa hiyo, Benaco kwa starehe, hata Kigali ukienda kwa starehe, watakuchosha
 
Hope hujajibu why wanyarwanda kuingia na kuishi Tz ni rahisi si kama mTz kuingia Rwanda na kujitwalia maeneo simply???
 
Ni kweli wanyarwanda wanapenda kuishi TZ?

Ni kweli Ukioa mnywarwanda atapenda azae na mtu wa kwako hata kama mko kwenye ndoa
 
Sema wahima ni wengi hili pori la Nyaishozi mpaka Benaco mbona wao ngozi za soft sana tofauti na watusi wengine nao wajua.Wahima wa Uganda mitaa ya Isingiro,mbarara si ndio wanyankole sio?

Sema vipi nipe list ya club nzuri kigali japo jamaa yangu alinitisha kwamba ukiwa Kigali vijana wengi wa Mr Tall wamejaa kwahiyo chunga sana ni kweli?
 
Umejibu vizuri

Kwa nini Rwanda kuepuka hilo tatizo kwa nini haikuongea na nchi jirani zake wawachukue hao wakimbizi wa Rwanda wawape uraia kama ilivyofanya Burundi kuongea na Tanzania na Tanzania ikakubali kuwapa uraia wakimbizi wa Burundi 250,000 na kuwapa vitambulisho vya taifa ili wawe raia wa Tanzania?
 
Swali kumaliza ukabila Rwanda ili yasijirudie ya Genocide Rwanda imechukua hatua zipi kuhakikisha ukabila hauna nafasi Rwanda?
 
asante kunijuza,bado wanarefusha antena au walishaacha haka ka utaratibu
 
Una chochote unachojiuliza kuhusu Rwanda?

Una chochote unachotaka kujua kiundani zaidi?

Una chochote ulichokisikia na bado umebaki njia panda!!

Iwe jambo la maana, iwe utani, iwe siasa, chochote, uliza utajibiwa hapa hapa.

1. Ni nani ambaye pengine anaandaliwa kumrithi Mr. Tall, akiondoka madarakani?

2. Mfumo wa elimu ya Rwanda ukoje? Kuanzia msingi mpaka vyuo.


3. Mfumo wa matibabu ukoje, huduma za afya zinapatikana kwa urahisi?
Watu wengi wanatumia bima ya afya?
Je serikali inagharamia matibabu kwa baadhi ya makundi ya watu?

4. Rwanda mnachimba madini gani hasa?

5. Kwa nini unasema Rwanda ni masikini wakati mmewekeza mpaka kwenye baadhi ya vilabu vya mpira ulaya (Arsenal, PSG nk..)?

6. Vipi huko Rwanda umeme ni tatizo kubwa? Kuna mgao wa umeme? Vijiji vyote vina umeme?

7. Je huko pia kuna machawa? 😂

Ahsante sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…