Binafsi nawapenda sana wanyarwanda kwa sababu ya wanamshikamo sana kuliko hata watanzania, japo napenda sana Wanyarwanda kwa sababu ya ukalimu wao na vile walivyo wazalendo wa nchi yao. Sijawahi kuona mnyarwanda asopenda nchi yake . Hongereni sana .Fauka ya hayo nina vimaswali kidogo hivi,
1. Mapema mwaka 2017 tulisikia katika vyombo vya habari wanajeshi zaidi Ya 800 waliachishwa na August 2024 tukasikia maafisaa 216 wamefukuzwa Kutoka RDF bila kutolewa sababu za kufukuzwa baada muda mfupi tukasikia Tena M23 imeanzisha mapambao dhidi ya Jeshi la Congo huko Goma . Kutokana na hali hiyo;
Je, ni kweli kwamba Jeshi la Rwanda linatoa support kwa M23?
Je, wanajeshi waliofukuzwa Huko Rwanda ndio hao M 23?
Ili nchi ipate Maendeleo ni muhimu sana kudumisha amani na majirani zake ili kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya kufanya biashara , je, kwa nini Rwanda hawapendi kudumisha amani na usalama dhidi ya Congo, Rwanda, Burundi, Uganda?
Ntakujibu mimi kama mimi sijibu kwa niaba ya serikali:
1. Wanajeshi ni ibinadamu kama wengine. Jeshini,kosa vyote, siyo nidhamu. Rwanda bila kujali una cheo gani, ukilalamikiwa, hasa na raia, na kweli ukakutwa na hatia, ndo imeisha hiyo. Kwa hiyo, wanajeshi kufukuzwa kazi ni jambo la kawaida.
Jeshi la Rwanda kusupport M23 ndo sijui. Kilichopo labda kama kuna mwanajeshi, inasemekana waliweka mbinu za kiusalama(Security measures) kulinda mipaka ya nchi. Inasemekana zinaweza kuwa ndani au nje ya mipaka.
Lakini pia, kumbuka M23 ni wanyarwanda wa Congo, ambao uraia wa Congo waliupata kutokana na mipaka ya wakoloni. Hivyo,kuoana na kuzaliana na kutembeleana, kulibaki pale pale.
N nadhani mpaka sasa kinachowachanganya wengi, ni kutofautisha wanajeshi wa Rwanda na wa M23 ukiacha uniform. M23 wanaongea kinyarwanda. Sawa na masai wa Kenya na Tanzania. Ukiambiwa tofautisha, sidhani kama unaweza.
M23 ni watu waliokimbia mauaji dhidi ya watutsi huko miaka ya 1995 na kuendelea. Wapo wanaume, na watoto wao.
Kwa sababu wengine walikuwa ndani ya jeshi la serikali, baada ya kuona serikali imekalia kimya mauaji hayo, waliamua kusaliti jeshi lao na kujiunga.
M23 ya leo ni muungano wa makundi tofauti tofauti, yaliyokuwa na nia ya kupigania haki za watu wao waliokuwa wakiuliwa huko mashariki mwa DRC.
Kwenye swala la kudumisha amani, bado sijakubaliana na wewe kwa kauli hiyo:
Nianze na Uganda: Katika vita vya pili vya Congo, Rwanda na Uganda walikiwasha, na inasemekana Uganda ilipoteza sana, ikahapa kulipiza kisasi kwa kuivvamia Rwanda. Rwanda haikuwa na namna, lazima ijilinde
Kuhusu Congo: Machafuko yote unayoyaona, yameanza baada ya interahamwe kukimbilia Congo. Walipokuwa huko, walijipanga na kuivamia Rwanda, mara kadhaa, na walifanikiwa,na kila mara,waliua. Serikali ya Rwanda ilikuwa ikiomba DRC iwachukulie hatua, ilishindikana. Na ndo kikawa chanzo cha wahutu hao, kuyavamia makazi ya watutsi huko DRC, na kuanza kuwaua na kuchoma nyumba zao. Mpaka leo hii, wakimbizi wa mambo hayo, wapo Rwanda na Burundi, na nahisi Tanzania wanaweza wakawepo.
Kuhusu Burundi, mzozo ulianzia hapa: 1994 wakati wa mauaji dhidi ya watutsi, kuna wakimbizi wa kihutu walikuwa nchini Rwanda. hawa walisaidia Interahamwe za Rwanda kuua watusti. Badae serikali ya Rwanda ikatoa list ya watu hao, wakamatwe na washitakiwe, serikali ya Burundi ikauchuna. Ambapo utasikia kuna watu walihusika na kutaka kupindua serikali mwaka 2015, wakakimbilia Rwanda, na yenyewe ikakumbushia. Sasa mtihani ukawa hapo. Burundi tuliokuomba uwashughulikie, ulikataa. Leo hii, unataka tukupe unaowataka wewe. Haikuwezekana na kuanzia hapo, mahusiano yakaharibika.
Pia, kwa sasa, FDLR inasaidiwa na serikali ya Congo. Hivyo yeyote anayesaidia jeshi la Congo, ni mshirika kuisaidia FDLR.
Burundi ikiwa mstari wa mbele. Hapo hayo mahusiano mazuri yatatoka wapi?
Lakini pia, kumbuka, Burundi ndo ilifunga mipaka, siyo Rwanda.
Navyosikia, vitu vinavyoendelea huko kijeshi, si mchezo. Ukifuatilia, FDLR mafunzo ni polii la Kibila upande wa Burundi. kwa maana, inawaunga mkono. Mahusiano mazuri yatatoka wapi!
Navyosikia, iwe hao wa Kibila au waliopo DRC, wanapata dose ya uhakika, na hakika kila mtu anajua aliefanya hivi atakuwa ni furani.
Kwa sasa, Burundi imeomba poo. Viongozi wa kidiplomasia wana vikao, ngoja tuone kitatokea kitu gani. Hapa M23 ndo inaenda kupakana na Burundi, ambayo ndo wanajeshi wake walikuwa wanaua ndugu zao. M23 na Burundi ujirani utakuwa wa style gani?