Ulishawahi kupata stress?

Ulishawahi kupata stress?

Pata muda wa kuitafakari hii hali yako na tamani kuitatua sasa ,usijipe mawazo kupitiliza sana jambo likienda ndivyo sivyo kubali ndiyo dunia ndugu ,ukijifunza kuzikubali changamoto zako nakuona ukiondokana na hii hali .

Ila zaidi sikushauri kujitenga punde uwapo na stress si nzuri kwa afya yako ya akili ,Dr MIN-min uko wapi ,una client huku .

Pole sana .
Asante daktari, ntalifanyia kazi hili jambo🥰
 
Stress kukaa nayo ni siku 1 tu.
Nikishalala . nikiamka nishaizoea.

Na kila kitu kingne ntafanya kama kawaida na pengne watu wa karibu hata mwenza asigundue.

If you can’t control it, don’t let it control you.
Na If you can control it, take action.

Sheria yangu iko simple.

Usikae ndan sasa shem. Pigia shost wako mmoja. Toka nenda bar. Ukaonje ladha ya serengeti apple. 😁😁😁😁. Kabia labla kazur kale kakakuliwaza.
Asantee shem! Nitajitahidi kufata ushauri wako! Pombe hapana, kuna kipindi niliziendekeza nikawa nakata Hanson’s kubwa na sili😅 bora saiz niko kwenye kujifungia ndani..
 
Chanzo cha stress ni nini Fedha ? Ajira Mahusiano? Ugonjwa? Hasara kwenye biashara? Fear of Unknown? Umefirisika kwenye biashara ,Pressure kwa marafiki? Pressure kwa familiy members wategemezi ? Unaweza jichunguza hata ukienda hospital ujue wapi pakuanzia

Mimi pia nilikuwaga nadhani na dalili za depression lakini kila nikipata kibunda tu nakuwa normal kabisa na furaha juu zikiisha naboeka narudi kujifungia ndani najitenga hasira etc
 
Chanzo cha stress ni nini Fedha ? Ajira Mahusiano? Ugonjwa? Hasara kwenye biashara? Fear of Unknown? Umefirisika kwenye biashara ,Pressure kwa marafiki? Pressure kwa familiy members wategemezi ? Unaweza jichunguza hata ukienda hospital ujue wapi pakuanzia

Mimi pia nilikuwaga nadhani na dalili za depression lakini kila nikipata kibunda tu nakuwa normal kabisa na furaha juu zikiisha naboeka narudi kujifungia ndani najitenga hasira etc
Same situation! Ila kuhusu chanzo, stress ikiwa ya biashara,kazi, mahusiano au familia zote na-act same! So haijalishi ni upande upi!
 
Binafsi nikiwa na huzuni inaniletea sonona sijui huwa ni kwanini najisikia hivi, kitu kikinikosesha raha kabisa nawaza sana mapigo ya moyo yanaenda kwa kasi kila nikifikiria upya!

Mbaya zaidi inanipelekea nakosa hamu ya kula, hata nikila naonja onja tu,napata homa ya ghafla, sijisikii kuongea na watu,sitaki mtu anipigie simu, sijisikii kwenda kazini na hata nikienda sijisikii kuongea na watu ni tumbo joto tu, nataka kukaa mwenyewe chumbani ata siku mbili hadi 3! Natamani chumba kisiwe na mwanga uwe wa mbali sana! Nakaa tu ndani na siwezi kufanya chochote! Sitamani kuoga, kula sebleni wala kupika japo itanilazimu sometimes😩

Hivi na nyie mnapitia hii hali mkiwa na stress au ni mimi tu?🥺
Hiisshhh. Mbona mbaya sana hii.
Mengine uliyoyataja hapo ni symptoms za migraine. Vyema ukaendq hospital. Migraine sio ya kuichkulia poa ujue
 
Mnaagua tu, hamjui lolote 🤪
20260204_182915.jpg
 
Back
Top Bottom