Maisha ya chuoni bila mishe yoyote ni magumu

Street brain

JF-Expert Member
Oct 24, 2022
486
606
Habari wanajf....... Nawasalim kwa jina la jamuhuri ya jf.......
Leo nipo na mada moja ni kuhusu maisha ya chuoni ....
Mimi nipo chuo fulani Ivi apa Tanzania nasoma bachelor of Accountancy with information technology, Nilichagua hiyo programu maana ni kitu napenda na pia napenda kuwa programmer it is my desire and passion.. sikuja kwa bahati mbaya.

Nimetokea diploma nikiwa na awards ya ordinary diploma in Accountancy..

Sasa ngoja nije kwenye hili life la chuo bila kuwa na mishe yoyote kitaa...

Chuoni kuna maisha magumu sana kwa sisi tuliotoka kwenye familia duni na tunaotegemea mkopo na boom kulipa ada, kodi, kula na vitu vingine... Vitu kadhaa ambavyo hufanya wanachuo kuishi maisha magumu chuoni na mwishowe kuingiwa na stress.....

*Kwa mwanafunzi aliye mbali na familia yake na anayetegemea mkopo na boom kuendeshea maisha yake chuoni, changamoto za kiuchumi, mazingira magumu, mifumo dhaifu ya miundombinu, na changamoto za elimu zinaweza kuchangia shinikizo kubwa katika safari yake ya masomo. Kwanza, kiuchumi, kutegemea mkopo na boom kunaweza kuwa na athari kubwa kwa mwanafunzi,
wanaweza kujikuta wakipambana na mzigo wa deni la mkopo ambalo linaweza kuwa kubwa na kuathiri vibaya hali yao ya kifedha hata baada ya kuhitimu. inaweza kusababisha wasiwasi na mkazo wa kifedha, na hivyo kudhoofisha uwezo wao wa kuzingatia masomo yao kikamilifu*...... Haya sasa apa kwenye mkopo wa heslb wakuu ni shida Maana tulio wengi huku bila boom maisha ni magumu sana kwa mfano mara ya mwisho heslb kutoa boom ilikuwa ni mwaka jana mwezi wa 12 sasa apa katikati kwa yule aliyetegemea hilo boom lije lilipe ada na kodi, hapo ndipo shida inaanzia kalipa ada atabaki na asilimia 50 ya boom lote na kama ujuavyo kama ulitegemea boom ni marufuku kukaa hostel sisi huwa tunakaa ghetto ambapo naweza endesha maisha yangu peacefully nikimaanisha nitakuwa na uwezo wa kuset budget yangu vizuri kama kula na vitu vingine kwa mfano..... Mi nakaa Gheto nikihemea mahitaji yangu kama vile
40kg za unga wa dona
1kg ya dagaa ( chakula cha chuo)
Kodi Miezi mitatu (40per month)
6kg za gesi
Ukicheki apo tayari ushabakiwa na kama na 50k ya kuishi nayo sasa mziki unakuja je utatoboa nayo mpaka umalize miezi 3 maana now nipo heslb wanatoa boom
Kwa hiyo ukicheki apo mwanachuo lazima ukonde kidg na yale mawazo yetu tulivyokuwa nayo kuwa hilo boom tutatumia ata kufungua biashara linapoteza mvuto na kupoteza direction sasa unapambania basic needs ambazo nazo ni shida tupu mwishowe ndipo pale boom halijatokea lilishaisha na kulipa madeni ya watu..... Daaah walaaah napaswa kusema chuo hakuna Bata yoyote bali kuna tabu na Karaha na shida tupu... Hustlers uliyepo chuo don't give up wewe ni shujaa.....

Pili, mwanafunzi aliye mbali na familia yake anaweza kukutana na mazingira magumu ya kijamii na kiakili. Kuishi mbali na familia kunaweza kusababisha hisia za upweke na kutengwa, hasa kwa mwanafunzi ambaye hajazoea kuwa mbali na familia yake. Hali hii inaweza kusababisha mzigo wa kiakili na kihisia ambao unaweza kuathiri utendaji wao kitaaluma......... Hili swala wakuu mi nalishuhudia kwa wanangu hapa kuna mabest fulani Ivi kwao wana maisha ya kawaidai ila sasa msela hajui kupika, hajui kufua dadeki blood faken kabisa yaani amekaa kimayai sana.... Ni jirani yangu ghetto apa ila msela hajui kupika ukizingatia hana uwezo wa kula mgahawani kila siku kwahyo inambidi apike tu,,,, dadeki msela amekonda kinoma

Tatu, mifumo dhaifu ya miundombinu katika chuo kikuu kunaweza kuwa changamoto nyingine. Kwa mfano, ukosefu wa huduma bora za malazi, usafiri, au huduma za afya kunaweza kusababisha vikwazo vya kila siku kwa mwanafunzi, na hivyo kumfanya awe na muda mwingi na nguvu kujaribu kumaliza masomo yake. ..... Hili halina shida kwenye chuo mi nilipo labda huko niliokuwa diploma daaah miundombinu mibovu kinoma yaani

Nne, elimu inaweza kuwa changamoto nyingine kwa mwanafunzi huyu. Kupambana na masomo wakati unakabiliwa na changamoto za kiuchumi na kijamii kunaweza kuwa ngumu. Aidha, umbali na familia unaweza kufanya iwe vigumu kupata msaada wa kifamilia katika kujifunza na kukabiliana na changamoto za kitaaluma ........ Sasa wakuu mniambie apa mtu unajua kabisa apa nina kama mwezi sina ata senti kumi mfukoni na katikati ya semester,, assignment ikitolewa unawaza hiyo buku Ya kuprint kazi naitoa wapi daaah chuoni kuna maisha fulani Ivi kama ya story za fiction na non fiction...... Lahaula tumalize tu

La mwisho kabisa wanachuo tunatamani kufanya kazi tukiwa bado vyuoni shida inakuja mitaani napo panakuwa unsupported ukilinganisha na ratiba ya chuoni lakini yote hayo ni masiha tu ya wenye familia duni ambazo haziwezi kumsetia mazingira mazuri mtoto wao ........

Mpaka sitamani ata kuajiliwa serikalini maana nilichoona connection ina matter sana, vipi kuhusu sisi ndiyo wasomi kwenye familia na ukoo wetu yaani sisi ndiyo connection inayotegemewa huko back na no backup ya mjomba wala shangazi..... Yaani ni timbwili tu......

Mwisho kabisa , apa naongea na wanangu wa vyuoni unayechukua certificate, bachelor degree, masters dash life ni gumu sana ukipata space kitaa piga kazi sana, ukienda field show them who you are, soma sana hakikisha haupati chini ya GPA 4.00, tengeneza connection chuoni, maghetoni na mazingira yanayolizunguka, play with matter of chances, usipoteze muda , epuka makundi , epuka ngono tafuta pesa kwanza, jitume kwa kila fursa unayoipata, heshimu kila mtu apo chuoni, ishi peacefully, funga domo lako kama hujakaribishwa kuongea, ishi maisha yako don't fake life ww umetumwa na ukoo,,, kumbuka wewe kwenu ww ndiyo role model na hata kijiji kizima,,,, don't loose time for nothing my man..... kama una tukio lolote kuhusu life la chuo tupia tujifunze.....

Anyway nimeandika mengi sana
NB: KAMA UPO ARUSHA NA UNAKAZI HALALI NICHEKI DM UNIPE HIYO KAZI IWE DAY WORK AU YOYOTE TU HELP ME PLZ NIPO LIKIZO

Wale wazee kucoment shit am sorry
 
Ndugu yangu, kila aliyewahi kuwa mwanafunzi humu, either amemaliza au alifeli, ila aliyepita chuo na ametokea maisha duni walipitia changamoto kede kede. Nakushauri pambana kusoma. Jibane hivo hivo. Utamaliza tu. Ukipata kamishe kakufanya sawa. Ukiona tafrani kausha maana maisha ya chuo bongo na kufanya side hustle unaasilimia 90 za kudondoka.

Okay cha kukusaidia. Jichanganye mjini haswa kwenye maduka ya jumla haya.
Usisahau shule.
Masomo mema
 
Uhakika imechukuliwa hii mkuu
 
Pole sana. Lazima upate kazi. Iwe supermarket, kuuza duka, boda, Bajaj, Uber nk, hata kuchomea vyuma, kufagia, kufyeka, gardening, etc etc
Pambana kijana...
 
Back
Top Bottom