Kevzy
JF-Expert Member
- May 23, 2026
- 969
- 1,696
Wanajukwaa hamjambo
Dunia Ina vitu vingi tunavyovitumia kama chakula na binaadamu tupo na mzio/aleji wa vitu na vyakula mbali mbali na huwa ukila chakula husika ambacho una mzio/aleji nacho uenda usiweze kuinjoy chakula au inaweza kukupelekea kupata ugonjwa fulani, au au au au
Binafsi sili kuku, sio kuku tu ni kuku ambaye ajaandaliwa vizuri, uzuri wa hapa ninaouongelea ni kuondoa shombo yote kwenye nyama ya kuku, ikaushwe vizuri hio nitakula vizuri tu niliona kwenye KFC, huwa naweza kula zile wings zilee zilizokauka kau kau nikilaga haziniletei shida, nikila yale mapande ya KFC ambayo hayajakauka vizuri huwa inanipelekea kuchefuka, kichefu chefu na nisipowahi kitu cha uchachu kama ndimu, au kitamu zaidi kama pipi au sukari huwa natapika, na kuku hata wa kuandaliwa nyumbani huwa ananishindaga, wanawake wananiulizaga ukinioa Kwa hivyo tutakuwa hatuli kuku, jibu lao ni kuwa utaenjoy yaani utakula kuku kila siku ambayo unataka tu, shida zangu hazitakusumbua
Turudi kwenye mada ya bangi, nilikuwa najaribu kuiangalia bangi Kwa mfano huu wa mzio/aleji yaani nilikuwa naona bangi Ina nafasi hii ya mzio/aleji kwamba ukitumia then ukaona kichwa chako hakiwi kawaida na inakuletea shida mpaka kugombana na watu au kuwa kama chizi mitaani Kwa Nini? Usiachane nayo
Sababu Kuna watu wakitumia bangi huwa wanaenjoy na kujihisi Raha/furaha na mpaka kufanya meditation na kutatua shida zao za kimaisha/kidunia , kwanini usiwaachie hawa watumie kama starehe na kuyainjoy maisha ya bangi
Naona shida Kwa ndugu yangu mmoja hivi, yeye bangi haumtaki , baadhi ya rafiki zake wengi wanatumia bangi lakini haiwaathiri ila yeye inamfanya anakuwa kichaa, yaani kiufupi bangi haimtaki kabsa yaani inamfanya anakuwa chizi kabsa so nimeona nije na uzi huu kuwa bangi ni kama chakula kama unahisi au unaona una mzio/aleji nacho usile achana nacho maana kitakuletea madhara
Huyu ndugu yangu bangi ilimchanganya miaka Fulani hivi, alirudi nyumbani akiwa na mawenge analia anaongea vitu ambavyo havieleweki, tukampeleka hospital akapata tiba na kupata mapumziko baada ya mwezi akarudishwa nyumbani akiwa yupo poa
Na aliambiwa asitumie bangi tena kwani itamletea madhara kwani haimtaki, jamaa aliendelea kuvuta bangi, mawenge yakawa yanamrudia tena, kupiga makelele , kuongea vitu visivyoeleweka, home wakajua amerogwa, wakaniamuru nimpeleke kijijini Kwao alipozaliwa baba yake , nikampekeka , kule alikuwa anatibiwa ki Mila na desturi , tiba asili, na wao walisema huyu hajarogwa ila bangi hazimtaki ,
Ni sawa tu walivyosema hospitalini, kweli alipata tiba na mapumziko Kwa miezi sita , akapona na huko kwao walisema kabsa kuwa huyu hatakiwi kuvuta bangi tena na ikitokea akavuta anakuwa chizi wa kuokota chakula najalalani na kula kabsa, yaani imepita miaka 10 Sasa hivi jamaa alirudia bangi na kile walichosema kwao ndio kinamtokea anaokota chakula majalalani na anakuja, siamini ninachokiona aisee yale yale waliyosema kwao jamaa yamemrudia
Nimejifunza mengi Sana kupitia ndugu yangu huyo, na nasisitiza bangi ni kama chakula ambacho una mzio/aleji nacho ukihisi au kuona akikufai achana nacho kitakuletea madhara
Asante