Ulinzi wa Rais Samia alipotua Dar leo

Ulinzi wa Rais Samia alipotua Dar leo

Raisi ana majukumu mengi muhimu kuliko kupoteza muda barabarani kufanya maigizo na 'wanyonge' ambayo hayana faida yoyote kwa nchi.

Hayo ya barabarani ni mambo madogo ya kumalizwa na ma dc,ndiyo maana ya delegation of duties. Siyo sahihi raisi kushughulika na petty issues!
Hizo sio petty issues! Miradi mikubwa ya maendeleo inayogharimu kiasi kikubwa cha fedha na yenye maslahi kwa nchi huwezi kutelekeza kwa watendaji wachache wa serikali na kuwaamini 100% kama wewe ni rais mzalendo! Tunayo experience kubwa ya namna nchi ilivyoongozwa kwa hayo mawazo yako ya 'rais ana majukumu mengi muhimu' mwisho wa siku ndio yale ya ufisadi na ziara za nje zisizo na tija kwa viongozi huku fedha za miradi zikitumika hovyo! Kazi ya rais ni kuwatumikia wananchi na kuwa mfano kwa viongozi wengine.sio kuishi kiboss boss kupanda midege na kutumia ofisi kutanua hali ya kuwa nchi ni masikini.kiongozi bora hujishusha na kuwa karibu na wananchi wake ikibidi kuishi nao ili kujua uhalisia wa maisha yao.
 
Mengi yalizungumzwa kuhusu ulinzi wa Rais Magufuli. Wengi wakakosoa kwamba analindwa na maaskari wanaovaa magwanda ya kijeshi jeshi huku wameshikilia mabunduki makubwa.

Ni viongozi wengi tu duniani hulindwa hivyo. Hata Rais wa Marekani hulindwa na wanausalama wenye mabunduki makubwa na wanaovaa magwanda ya kijeshi jeshi.

Hao huitwa Counter Assault Team. Hao ndo wapiganaji ikitokea Rais anashambuliwa kwa silaha. Wale wanaovaa suti kazi yao si kupigana na adui. Kazi yao ni kuhakikisha rais yuko salama kwa kumkinga [taking the bullet for the president] au kumuondosha kwenye eneo lenye hatari.

Leo Rais Samia katua kwenye uwanja wa ndege Dar.

Chini naweka video. Lakini kabla yake, naweka screenshots za video zinazoonyesha hao watu wa counter assault walikuwepo na mabunduki yao.

Kuna watu walishaanza kusema eti Rais Samia hana walinzi kama hao kama ilivyokuwa kwa Magufuli.

Pia, Rais huwa hajipangii ulinzi wale mwenyewe. Ulinzi wake hupangwa na wataalamu kulingana na vigezo vingi ikiwemo eneo alipo, hali ya usalama wa eneo kwa ujumla, na mambo mengineyo.

Ona huyu na huo mbunduki wake:
View attachment 1742313

View attachment 1742314

Huyu pia ni mwingine akiwa pembezoni kidogo.
View attachment 1742316

Video hii hapa;

Wengine walidai kuwa na warwanda eti..!! Jaman Bongo
 
Au Sio,Me Mwenyewe Nlikuwa Hapo Kama Mlinzi Ni Protocol Tu Hiyo Mkuu,Watu Waheshimu na Kujivunia Ulinzi Tulionao,Mbona Hamzungumzii Mipakani Tulivyojazana Kuwalinda? Au Mna Nini Cha Zaidi Kumzuia Adui 😁 Kama Yupo Basi.

"Ilisikika Sauti Ya Mtu Aliye Nyika"
 
kuna wale walikuaga wanabeba briefcase safari hii hawapo? Ivi zilikuaga zina nini zile?

Wengine wanasema ni bullet proof ikitokea hatari inafunguka , wengine wanasema ilikua ni first aid kit kwakua jiwe alikua anaumwa wengine mara waseme mle kulikua na nuclear codes 😀 wataalam Hebu tujuzeni

Mkuu Generalist nakuomba unisaidie
 
Ulinzi wa raisi wakati mwingine ni swala nyeti,sio lazima uwaone askari wengi wenye sare na mabunduki ndio kiwe kipimo cha ulinzi wake.
 
1617470803367.png
 
JPM alipolindwa na ulinzi Mkubwa shida ilikua wapi? Na Mama yetu akilindwa alindwavyo shida iko wapi?
Watanzania wa JF tufanyeni kazi na Sala. Majungu hayasaidii. Shukuru Mungu wewe huna Mlinzi hata Mmoja zaidi ya Mungu pekee.
 
Usioonekana unamaanisha waganga au?

Waganga hawana mamlaka ya kumlinda mwanadamu aliyeumbwa na Mungu mwenye enzi

"BWANA asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure.​

BWANA asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure.​

Kazi yenu ni bure, mnaoamka mapema, Na kukawia kwenda kulala, Na kula chakula cha taabu; Yeye humpa mpenzi wake usingizi."​


Zaburi 127: 1-2
 
Utofauti ni kwamba Magufuli alihimiza na kuhitaji ulinzi mkali huku Samia Suluhu kapewa tu ulinzi hivyo hawezi kuukataa.
 
kama unausifia utawala wa JK....nina nini cha kujadili na wewe?
Mimi mwenyewe unavo msifia mwenda zake kwa kutokufata katiba na Sheria, kuhatarisha usalama na umoja wa nchi, kuharibu uchumi na uwekezaji na kushangaa kwa kweli maana hata kulinganisha uchumi wa awamu yake na kikwete kuanzia uwekezaji na Mambo ya ajira ni mbingu na nchi
 
Back
Top Bottom