Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,232
- 113,610
Mengi yalizungumzwa kuhusu ulinzi wa Rais Magufuli. Wengi wakakosoa kwamba analindwa na maaskari wanaovaa magwanda ya kijeshi jeshi huku wameshikilia mabunduki makubwa.
Ni viongozi wengi tu duniani hulindwa hivyo. Hata Rais wa Marekani hulindwa na wanausalama wenye mabunduki makubwa na wanaovaa magwanda ya kijeshi jeshi.
Hao huitwa Counter Assault Team. Hao ndo wapiganaji ikitokea Rais anashambuliwa kwa silaha. Wale wanaovaa suti kazi yao si kupigana na adui. Kazi yao ni kuhakikisha rais yuko salama kwa kumkinga [taking the bullet for the president] au kumuondosha kwenye eneo lenye hatari.
Leo Rais Samia katua kwenye uwanja wa ndege Dar.
Chini naweka video. Lakini kabla yake, naweka screenshots za video zinazoonyesha hao watu wa counter assault walikuwepo na mabunduki yao.
Kuna watu walishaanza kusema eti Rais Samia hana walinzi kama hao kama ilivyokuwa kwa Magufuli.
Pia, Rais huwa hajipangii ulinzi wale mwenyewe. Ulinzi wake hupangwa na wataalamu kulingana na vigezo vingi ikiwemo eneo alipo, hali ya usalama wa eneo kwa ujumla, na mambo mengineyo.
Ona huyu na huo mbunduki wake:
Huyu pia ni mwingine akiwa pembezoni kidogo.
Video hii hapa;