Ulaji wa Panya mikoa ya Kusini: Safari yangu ya siku 37 ilivyonifungua mambo mengi

Mkuu nilichokieleza ni kweli kabisa

Kuna sehemu mkoa wa Lindi panya wanakula vizuri Tu..au naongopa mkuu Viprealestate
 
Na hata hvyo namtumbo inapakana na wilaya ya tunduru si masasi wilaya ya masasi inapakana na wilaya ya NANYUMBU ambayo makao yake makuu yapo m MANGAKA

Huyo jamaa n muongo anatulisha matango pori

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Satoh Hirosh yupo sahihi panya wanaliwa sana hata mkoa wa Lindi maeneo yenye wakristo wengi.
 
Yule sio panya... Tuelewane hapo kwanza. Kuanzia Wayao, Wamakua, Wamatumbi, Wamakonde na makabila mengi ambayo nimekutana nayo wanakula huyo kiumbe. Na walaji wengi ni wakulima.

Shida yenu vijana ni kubisha tu hata kama kitu hukijui. Mie ni mkulima na nimelima maeneo hayo na siku hizi makabila yamechanganyika sana tofauti na zamani. Kusini yote nimevuruga sijui utaniambia nini. Nimelala sana maporini, naomba nisiongee sana sababu naweza kuta nabishana na mtu ambae anaifahamu kwa kupitia google. Na hao unaosema ni waislamu sana wa kusini huko wanagonga kitimoto kama hawana akili nzuri hususani ya kitomoto pori.

Unabishana na mtu ambaye yupo Mtandi sahizi akiwa ametoka Kibo muda huu.
 
Nadhani mtoa post anawazungumzia Ndezi ambao nahisi kama jina lingine ndio Panya pori. Na kuna mdau amezungumzia wale wanaokula wadudud kwenye magamba ya miti, wadudu wale wanaitwa Sondo.

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Umeishi lakini hujalima..... Watu wanaokula hawa viumbe huwa ni wakulima na sio majumbani.

Ila watu mnashangaza hapa, yawezekana mnadhani viumbe hawa wanauzwa mabuchani. Tembeeni mashambani huko muone watu wanakula vitu gani.

Mie nimeshuhudia wati wakila chatu Mafia sehemu wanaita Utende. Jiulize ni kina nani waliokua wakila hao chatu? Usije ukasema waburushi sijui hawali nimekaa miaka 8 huko sijaona. Suala la kuona ni binafsi sana.

Hata huko Meatu, Shinyanga, Kibiti, Mwanza, Morogoro, Mwanza wanakula hawa viumbe na kote nimeshuhudia watu wakila. Ukitaka kuona show ya hayo mambo tembelea wakulima.
 
Nilikula panya Lusaka tena downtown kabisa wanauzwa kwenye masinia a wale wadudu jamii ya washa washa watam balaa
 
Kama ni hao wa shambani hata mi nimekula sana utotoni huko mkoani. Kuna mwingine panyabuku, kuna mnyama makazi yake ni chini kwa chini anapendelea sehemu mliyolima viazi vitamu na haoni mchana (jina lake kwa kiswahili sijui, najua kwa lugha yangu tu)
 
Nilikula panya Lusaka tena downtown kabisa wanauzwa kwenye masinia a wale wadudu jamii ya washa washa watam balaa
hata hao jamii ya washawasha nimekula, kuna funza wanene wa kwenye miti nimepiga, ndege fulani wana rangi nyeupe na nyeusi hawaliwi kule mkoani mimi nimepiga, paka anayetembea usiku tu anakula kuku nimepiga, hao panzi ndio sana tu.
 
Hebu nieleze vizuri hapo kwenye UPUPU kuwa msosi .
Kuna upupu wa porini(unawasha) na upupu tunaita wa nyumbani(hauwashi),huu wa nyumbani sasa ndio unaoliwa,unapandwa(mbegu zipo)shambani na kuvunwa ukikomaa na kukauka.Unapikwa na kumwagwa maji mara kadhaa then unachunwa maganda yake na kupikwa tena mpaka uive,hapo unakua tayari kwa kuliwa.Unaweza kula kama ulivyo kwa kunyunyuzia chumvi kama chipsi kavu au unaweza kuungaaka na viongo vingine kama nyanya na vitunguu then ukala au ukafanya mboga.Mostly upupu unatumika kama kifungua kinywa na ni biashara nzuri sana wilaya ya masasi(kuuza upupu usiopikwa kwa wapikaji,kuuza upupu uliopikwa kww walaji)

Ule wa porini kuna baadhi wanauandaa pia na kula,maandalizi yake si ya kitoto,unaweza chomoka ulimi ukikosea.
 
Mwazembe ni Mnyiha, Wanyiha wanakula panya pia. Labda ticha mwanzon alikuwa anavunga tu.
 
Aliyepo huko anitumie pua,masikio na miguu ya panya.Ntamtumia na ya kutolea.😝😝😝😝😝
 
ajabu yake, wanakula sana panya lakini panya wewe hawaishi. hata hivyo, siwadharau kwasababu katika maisha yangu ilishawahi kutokea sehemu fulani nilipokuwepo wanakula panya, na nilikula hadi nikawazoea kama chakula cha kawaida kabisa. wala sio kitu cha ajabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…