Serikali isimamie na kutilia mkazo sheria ya kuzuia ulaji wa KASA ili kuepusha vifo

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Salaam wakuu,

kasa.jpg

Kila mwaka wenzetu Zanzibar wamekuwa wakipata visa vya vifo kutokana na ulaji holela na usio makini wa KASA. Tukiendelea kuendekeza hili suala tutajikuta kila mwaka tunapoteza nguvu kazi nyingi tena za familia moja kutokana na ulaji wa huyu kiumbe.

Ni vyema mamlaka za Zanzibar na Tanzania Bara zikapiga marufuku utumiaji wa kasa kama kitoweo, yeyote atakayebainika kuvua na kutumia kasa basi apewe adhabu kali sana ili iwe fundisho kwa wengine.

Kwa kuanzia, ni vyema mamlaka zikatilia mkazo sheria ya kasa kuwa nyara ya Serikali (Government Trophy) hivyo ni marufuku kuvua na kumtumika kama kitoweo.

Naamini Serikali ikiisimamia sheria hii vizuri, itasaidia kupunguza vifo vitokanavyo na ulaji kasa unaopelekea vifo vya watu hasa familia moja, eneo moja kwa wakati mmoja .

Pia soma
 
Ni kweli inasikitisha tena watoto ndio wanakufa sana wanajua baba kaleta mboga kumbe ameleta sumu
 
Salaam wakuu,

Kila mwaka wenzetu Zanzibar wamekuwa wakipata visa vya vifo kutokana na ulaji holela na usio makini wa KASA. Tukiendelea kuendekeza hili suala tutajikuta kila mwaka tunapoteza nguvu kazi nyingi tena za familia moja kutokana na ulaji wa huyu kiumbe.

Ni vyema mamlaka za Zanzibar na Tanzania Bara zikapiga marufuku utumiaji wa kasa kama kitoweo, yeyote atakayebainika kuvua na kutumia kasa basi apewe adhabu kali sana ili iwe fundisho kwa wengine.

Kwa kuanzia, ni vyema mamlaka zikatilia mkazo sheria ya kasa kuwa nyara ya Serikali (Government Trophy) hivyo ni marufuku kuvua na kumtumika kama kitoweo.

Naamini Serikali ikiisimamia sheria hii vizuri, itasaidia kupunguza vifo vitokanavyo na ulaji kasa unaopelekea vifo vya watu hasa familia moja, eneo moja kwa wakati mmoja .

Pia soma
hapa kinachowaangamiza hawa jamaa zetu ni uroho tu , hakuna kitu kingine uroho ni kitu kibaya sana maana kila mwaka hiyo midudu inawaua lakini hawasikii.
 
Back
Top Bottom