Ulaji wa Panya mikoa ya Kusini: Safari yangu ya siku 37 ilivyonifungua mambo mengi

Viprealestate

Senior Member
Jan 21, 2014
125
250
Safari yenye takribani kilomita 600+ hadi Mkoani Mtwara wilaya ya Masasi kijiji cha Nangoo napata fursa ya kuifahamu jamii ya watu wa mikoa hii japo kwa uchache.

Nikiwa eneo hilo nilipata fursa ya kufahamu baadhi ya tamaduni za kule, baadhi tu kama vile Unyago na aina ya vyakula ambavyo vipo tofauti na vingine.

Achana na kufanya Upupu kama ni chakula ila hili la ulaji panya lilinivutia zaidi, Panya!! Ukuaji wangu umenikuza nikiamini Panya ni sehemu ya wadudu waharibifu wa kwenye nyumba za watu au mashambani.

Biashara ya kitoweo hiki kule Kusini siyo ya kificho, ni biashara ya wazi inayotembezwa kama bidhaa nyingine tu ya kawaida. Panya wanawekwa kwenye mtungo wa mti au kupangwa fungu kwa idadi fulani na kufungwa na kamba.

UPATIKANAJI NA UANDAAJI WA PANYA
Mwanzo nilidhani ni rahisi tu kupata Panya kwasababu ni kawaida kuwakuta kwenye nyumba zetu za kawaida kumbe la hasha! Siyo kila panya ni kitoweo.

Panya wa Porini Vs Panya wa Nyumbani.

Ikae akilini mwako kuwa kule wametofautisha Panya kwa aina hizo mbili, sasa taarifa ikufikie wale Panya wa Porini ambao kwa kawaida wanapatikana mashambani huko hasa ndio maalumu kwajili ya Kitoweo. Muda wangu wote kule sijashuhudia Panya wa nyumbani wakifanywa kitoweo bali uuliwa na kutupwa kama ilivyo sehemu nyingine.

Panya wa Porini wanapatikana kwenye mashimo huko shamba na kuna utaalamu katika uwindaji wake. Sasa tutazame namna wanaandaliwa Panya hadi kuwa Kitoweo.

Wakishapatikana wanaondolewa uhai wao kwa kupigwapigwa chini, hatua inayofuata ni kuwasafisha/ kuwaandaa kwa kuweka viungo kama chumvi na pilipili kiasi halafu unawabanika jikoni kwa moto wa wastani.

Ni kama tu unavyobanika Kuku au vile wamasai wanavyoweka Nyama kwenye Mtungo na kubanika. Baada ya zoezi hilo hatua inayofuata ni kuwafunga mafungu au kuuza mmoja mmoja tayari kwa kitoweo.

JE, INASHANGAZA?
Hapana bali inavutia, hata mimi mwanzo kila nilipojaribu kuonesha kuwashangaa nao walinishangaa kwanini nina washangaa basi tukawa tunashangaana.

Hoja yao wanasema huo ni utamaduni wao na uheshimiwe ni kitu kilichobadili mtazamo wangu juu yao, wanasema mbona ipo jamii inakula Mbwa kitu ambacho kule kusini siyo utamaduni wao kabisa. Mwingine aliniambia wapo watu wa Mkoa fulani wanakula panzi, bahati nzuri kwao waliamua kukipa thamani kitoweo chao.

FAHAMU
Siyo watu wote wa Kusini wanakula Panya HAPANA, wapo wengine ni tofauti kabisa na hawajawahi kula hata mara moja. Nafikiri hii ni kawaida tu kwenye mambo mengi.

Siku zangu 37 za kuishi kusini nilijifunza mengi sana, watu wake ni wema na wakarimu wanaojali zaidi wageni kuliko wenyewe kwa wenyewe. Huu ni udhaifu toka kwao.

Mwisho.
 

1gb

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
1,986
2,000
Napenda kujaribu kula kitu kinacholiwa na jamii ya watu wa eneo husika ni huluka tu,ndoo maana miaka ile waliniita Mchina.

Ushakula funza wakubwa wakwny magogo na magome ya miti mikavu.

Acha kbsa..

Ni mboga hyo ilikuja na mmisionar alieenda kongo baada ya miezi akaja na madude hayo.
 

Satoh Hirosh

JF-Expert Member
Mar 30, 2021
1,242
2,000
Niongezee nyama kidogo mkuu.

Kwanza kabisa panya hupatikana Kwa wingi kuanzia mwezi wa sita Hadi wa kumi ,kipindi ambacho wakulima wameshavuna mahindi na ufuta mashambani.Panya wanaovunwa kipindi hiko huwa wananona na huwa na mafuta mengi sn Kwa sababu hula mabaki ya vyakula vilivyopo mashambani Kama mahindi,mtama,muhogo na ufuta

Wawindaji wa panya huangalia mashimo yaliyo na njia nyingi zilizo bize,na mashimo ndani ya hayo huwa na panya kuanzia 50 Hadi 100+

Maandalizi:

Panya hupangwa kwenye fimbo ndefu,fimbo moja wanaweza kupangwa hata panya 10 kisha Moto mkubwa huwashwa kisha zile fimbo zenye panya huwekwa kwenye Moto Kwa ajili ya kubabua manyoya

Baada ya manyoya kubabuliwa na kubaki na ngozi laini isiyo na manyoya,Moto unapunguzwa na kubakia Moto wa wastani kisha panya hubanikwa..hatua hii panya huwa wananona na kutoa mafuta mengi sn kiasi cha kumfanya mtu kutokwa na mate Kwa uchu

Baada ya kazi ya kubanikwa kumalizika hutolewa kwenye zile fimbo walizotundikwa na kupangwa mafungu Tyr Kwa kuuza

Mnunuaji wa panya akigika nyumbani anawatoa utumbo kisha huwaunga..kumbuka mapishi ya panya ni tofauti na samaki,panya hawahitaji mchuzi mwingi,mapishi yake ni Kama losti ya maini au nyama

Mboga ikishakamilika inakuwa Tyr kuliwa..tofauti na wakosoaji wengi kwa watu wanaokula panya,nyama ya panya ni tamu sn na mtu yeyote akijaribu Kula panya aliyeandaliwa vizuri hawezi kuacha Kula nyama ya panya

Kuna kisa kimoja cha mwalimu wangu wa geography kutoka kanda Fulani ambaye alikuja kugeuka mlaji mzuri sn wa panya nitakielezea...
 

NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
1,920
2,000
shukrani, umeongea vizuri, we ni kweli umefanya uchunguzi mwenyewe hujakaririshwa.

kuna watu waliokaririshwa basi wao huishia kuiaminisha dunia kuwa panya hawa wa majumbani ndiyo wanaoliwa huko kusini wakati siyo kweli kabisa. pia huaminisha dunia kuwa watu wote wa kusini (lindi na mtwara) wanakula panya, wote! nimefurahi kuona hata wewe umejiridhisha kuwa si kweli, nikienda ndani zaidi ni kuwa ukweli ni kwamba maeneo yenye waumini wengi wasio waislamu km masasi ndiyo yanaongoza kwa ulaji huo wa panya. aina hii ya panya, pia huliwa maeneo fulani ya morogoro

ila nitajaribu kuweka sawa kidogo kama hautojali, ni kuwa si kila eneo la kusini utaona uuzaji wa panya. ni maeneo yale tu wanayopendelea hiyo kitu kama huko masasi. sehemu kama kilwa kamwe huwezi kukuta kitu kama hicho.
 

Satoh Hirosh

JF-Expert Member
Mar 30, 2021
1,242
2,000
Kuna kisa kimoja cha mwalimu wangu juu ya ulaji wa panya..
nimesoma kusini mkoa wa Lindi shule moja inaitwa mahiwa high school

Mwalimu wangu wa geography aliitwa Mr mwazembe jitu la miraba minne kutoka mbeya alibahatika kupata binti wa pale kijijini,.Ruti za shuleni kwenda kijijini Kwa mchumba wake zilikuwa nyingi sn.

Km unavyojua mikoa ya Lindi na Mtwara ulaji wa panya ni kitu cha kawaida sn,Kwa hiyo mke wa ticha alikuwa mlaji mzuri sn wa panya.Km ilivyo kawaida ya wabongo,ticha alidharau sn watu wanokula panya,lkn Yule dada (demu wake) alikuwa mlaji wa panya..siku moja ticha akaamua kujaribu kuonja..asee Radha aliyokutana nayo,kuanzia siku hiyo akageuka kuwa ndiyo kinara wa walaji panya

Ticha akaenda mbali zaidi,akawa na mtu wake maalumu anachukua panya kwa bili,kisha analipia mwisho wa mwezi mshahara ukitoka..
 

Bondpost

JF-Expert Member
Oct 16, 2011
4,419
2,000
shukrani, umeongea vizuri......we ni kweli umefanya uchunguzi mwenyewe hujakaririshwa.

kuna watu waliokaririshwa basi wao huishia kuiaminisha dunia kuwa panya hawa wa majumbani ndiyo wanaoliwa huko kusini wakati siyo kweli kabisa. pia huaminisha dunia kuwa watu wote wa kusini (lindi na mtwara) wanakula panya, wote! nimefurahi kuona hata wewe umejiridhisha kuwa si kweli......nikienda ndani zaidi ni kuwa ukweli ni kwamba maeneo yenye waumini wengi wasio waislamu km masasi ndiyo yanaongoza kwa ulaji huo wa panya. aina hii ya panya, pia huliwa maeneo fulani ya morogoro

ila nitajaribu kuweka sawa kidogo kama hautojali, ni kuwa si kila eneo la kusini utaona uuzaji wa panya. ni maeneo yale tu wanayopendelea hiyo kitu kama huko masasi. sehemu kama kilwa kamwe huwezi kukuta kitu kama hicho.
Hata baadhi ya watu wa njombe wanakula panya hao wa shambani.
 

Wang Shu

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
2,527
2,000
Niliwai kumtembelea rafiki yangu mmoja alinikaribisha ugali mboga panya waliungwa wakauingika haswaa😋😋,bahati mbaya kwake nilimkatalia kula kwa sababu misamamo na imani yangu.
 

Bondpost

JF-Expert Member
Oct 16, 2011
4,419
2,000
Napenda kujaribu kula kitu kinacholiwa na jamii ya watu wa eneo husika ni huluka tu,ndoo maana miaka ile waliniita Mchina.

Ushakula funza wakubwa wakwny magogo na magome ya miti mikavu.

Acha kbsa..

Ni mboga hyo ilikuja na mmisionar alieenda kongo baada ya miezi akaja na madude hayo.
Unajua hata mtu ambaye hajawahi kula ngisi au pweza huwa wanashangaa sana akiona mtu anakula anajinonosa kabisa. Sasa wakishaonja wao hugeuka kuwa walaji wakuu.

Bila kuathiri Imani za watu, Nina washkaji wawili ni waislamu aisee wanapiga mdudu nadhani kwa wiki wanaacha kula siku Moja au mbili tu. Lakini nilifuatilia nikagundua mmoja ya wazazi alibadili dini kwa minajili ya ndoa tu Ila Imani unajua huwezi kuibadilisha sasa watoto wamekuwa katika Imani mchanganiyiko .
 

Satoh Hirosh

JF-Expert Member
Mar 30, 2021
1,242
2,000
shukrani, umeongea vizuri, we ni kweli umefanya uchunguzi mwenyewe hujakaririshwa.

kuna watu waliokaririshwa basi wao huishia kuiaminisha dunia kuwa panya hawa wa majumbani ndiyo wanaoliwa huko kusini wakati siyo kweli kabisa. pia huaminisha dunia kuwa watu wote wa kusini (lindi na mtwara) wanakula panya, wote! nimefurahi kuona hata wewe umejiridhisha kuwa si kweli, nikienda ndani zaidi ni kuwa ukweli ni kwamba maeneo yenye waumini wengi wasio waislamu km masasi ndiyo yanaongoza kwa ulaji huo wa panya. aina hii ya panya, pia huliwa maeneo fulani ya morogoro

ila nitajaribu kuweka sawa kidogo kama hautojali, ni kuwa si kila eneo la kusini utaona uuzaji wa panya. ni maeneo yale tu wanayopendelea hiyo kitu kama huko masasi. sehemu kama kilwa kamwe huwezi kukuta kitu kama hicho.
Safi sn maelezo mazuri
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom