Hatimae nimeamua kuandika kitabu kuhusu mtindo wa maisha ya watu wa mikoa ya Kusini mwa Tanzania

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
15,118
27,112
Wakuu baada ya kupiga kambi Mtwara na Newala nimevutiwa sana na ustaarabu, uungwana na ukarimu wa watu wa kusini mwa Tanzania.

Sasa ninaandika kitabu kuhusu maisha ya watu wa kusini mwa Tanzania. Kitabu kitagusa nyanja zote kuanzia utamaduni hadi shughuli za kiuchumi ikiwa ni pamoja na fursa zote unazoweza kuzipata katika kila wilaya iliyopo katika mikoa ya kusini.

Now naanza kuweka miundombinu ya kuanza utafiti wangu.

Kama kuna jambo unataka nilifanyie utafiti kuhusu maisha ya watu wa kusini tafadhali weka kwenye komenti hapo chini.
 
Mimi hapa mtu wa kusini japo nimezaliwa Dar na kukulia na nimeeenda Mara moja kipindi Niko darasa la pili nikahamia uhamisho wa muda kwa miezi 7 kisha nikarudi Dar mpaka Leo sijawahi kwenda tena nasikilizia mwaka mmoja niende kusalimia InshaAllah ..
 
Mimi hapa mtu wa kusini japo nimezaliwa Dar na kukulia ,na nimeeenda Mara moja kipindi Niko darasa la pili nikahamia uhamisho wa muda kwa miezi 7 kisha nikarudi Dar mpaka Leo sijawahi kwenda tena nasikilizia mwaka mmoja niende kusalimia InshaAllah ..
Unakosa mengi sana. Mimi pia asili yangu ni kusini upande wa bibi mzaa baba. Niliwahi kwenda utotoni pia niliwahi kwenda mwaka 2017 nikaa Mtwara pale siku 3 then nikirudi mjini but kusini kuchele.
 
Mimi hapa mtu wa kusini japo nimezaliwa Dar na kukulia ,na nimeeenda Mara moja kipindi Niko darasa la pili nikahamia uhamisho wa muda kwa miezi 7 kisha nikarudi Dar mpaka Leo sijawahi kwenda tena nasikilizia mwaka mmoja niende kusalimia InshaAllah ..
Miaka kadhaa iliyopita, kuna mtu alitolewa mkoani Tabora na kupelekwa huko Mtwara kishirikina. Mtu huyo, asubuhi moja, alijikuta yuko juu ya mti huko Mtwara bila kutarajia. Hili jambo limekuwa likifikirisha sana, fanya utafiti juu ya jambo hili na utupatie mrejesho (matokeo ya utafiti).
 
Hiyo ni Mpaka Sasa na wengi wao ni Elimu ya darasa la saba
Ila Mtwara mjini sidhani hapo Lindi hata mjini hapajulikani vizuri... Nillifuatilia Mtwara haswa ishu za kielimu hapa town tangu niwe na mpango wa kuhamia 2020 mpaka sasa naona wanaufaulu mzuri yaani madogo wanasoma.

Natoka alfajiri huku jua linawahi kuchomoza, Kumi na moja baada ya sala bodaboda wapo kibao... Tena wanawake ndio wanaenda kwenye shughuli zao.

Kiufupi wanapambana sana....Ila maduka wanafungua saa 2 ...shughuli nyingine haswa shamba mapema.
 
Back
Top Bottom