Ukweli kuhusu Jane Urassa - mke aliyeuawa kwa risasi 💔

Ukweli kuhusu Jane Urassa - mke aliyeuawa kwa risasi 💔

Baba yake aliwahi kuua mtu?

Hebu fungua uzi uyaelezee kwa kina, kuna kitu hakiko sawa kwenye huo ukoo wa mwanaume..!!

Itabidi turudi kama zamani, kabla ya kuolewa na kuoa kuna umuhimu wa kuchunguza familia za waoaji. Kimasihara unajibebea bomu kama huyo bwana Kweka….!!
Watoto wake ni the same linapokuja suala la mwanamke na mali kwanini Jane aliandika majina yake na ya watoto kwenye hio hati kinyume na makubariano? Kwanini asiandika majina yake na mumewe na ya watoto yote kwa pamoja au unahisi angefanya hivyo angepigwa risasi? Yaan mwanaume atafute kwa jasho halafu mwishoni mti ule aliokua anaupalilia kila siku umetoa kivuli kikubwa cha watu kukaa chini na kujipatia kivuli panapokua na jua kali then wale watu aliowaandalia kivuli wanamfukuza kwenye mti alioupanda na kuuhangaikia kwa muda mrefu yaan wanamtenga ungekua wewe ungechekelea? Muwe mnajiuliza mara 77
 
Kosa la mwamba ni kujenga nyumba kwenye kiwanja Cha mwanamke alafu mwanamke akataka kumu exclude kwenye hati ya nyumba

Kweka akafanya aliyoyafanya

Daah!!.
Kama walikubaliana basi mali zote zilikuwa zao, isingekuwa katika makubaliano mwamba angenunua kiwanja sehemu nyingine na akajenga ila naona ni ulaghai wa mwanamke
 
Hoja hiyo wanairuka wanakimbilia mbele, kwanini talaka itoke na majina ya mama na watoto Baba akawekwa pembeni? Maana hapo ndio tatizo lilipoanzia ukianza ooooh sijui alimvumilia tu, ooh ndoa ilikuwa imeisha zamani, bila hilo swali kujibiwa bado unakuwa unaruka ruka
Hilo swali hakuna wa kulijibu na wanaogopa hata kuliangalia maana wanajua hio ndio source ya tatizo lenyewe wewe mtu ahangaike then baadae unamtoa kwenye mali zake yaan mimi nijenge nyumba kisha wewe uje ujiandike jina lako na la watoto na mimi niliehangaika kuijenga usiku na mchana unaniweka wapi? Majina inabidi yaingie yote Baba, Mama na Watoto ingawa kiutaratibu inatakiwa yasome majina ya Baba mwenye nyumba wanawake wasio na nidhamu kwa waume zao tu ndio hung'ang'ania majina yasomeke ya kwao
 
Kwenye hati ndio msingi wa tatizo, na wengine wanasema huyo mwanamke ametishiwa kuuawa muda mrefu inaonekana ni mkorofi pia na mbinafsi ndio maana mwisho wa siku kapata alichokitaka
 
Baba yake aliwahi kuua mtu?

Hebu fungua uzi uyaelezee kwa kina, kuna kitu hakiko sawa kwenye huo ukoo wa mwanaume..!!

Itabidi turudi kama zamani, kabla ya kuolewa na kuoa kuna umuhimu wa kuchunguza familia za waoaji. Kimasihara unajibebea bomu kama huyo bwana Kweka….!!
Ndio baba wa mwanaume aliua,

Mi kufungua uzi ni mtihani na sijui kupangilia story,

Kingine hapo kwa mwanaume, (last born) urithi wa huko kwao alimuuzia kaka yake, na vilevile alitaka kununua hiyo nyumba ya bunju,

Kikwazo kikubwa ilikuwa kiwanja alinunua mwanamke baada ya mwanaume kukataa kila kiwanja alichopelekwa akisema ni porini,, miaka hiyo
Mwanamke akaona mume hamnazo akaamua kulipia kiwanja kwa jina lake na pesa yake, kidogo kidogo akaanza ujenzi, mwanaume nae akaunga kwenye kujenga, baada ya muda mwanaume akataka kupauza hapo ndipo shida ilipoanzia, akatafuta hati kwa njia za panya akapata hati isiyo halali, wakafikishana mahakamani,
Ndipo mwanamke akafatilia hati halali akaandika majina ya watoto na yeye mwanamke km msimamizi ili kumuwekea ngumu mwanaume aliyetaka kuuza, na ilitoka siku za karibuni kabla ya kifo chake,

Kuna kipindi mwanaume aliugua kansa ni mwanamke huyohuyo alimuuguza mpaka kupona,

Mwanaume alipoteza kazi akamuharibia na mwanamke akapoteza kazi, mwanamke akaendelea kukomaa kwa kukopa na kufanya vibarua tofauti tofauti, alikuwa na kiwanja dom, na kigamboni ana nyumba, hii ilimkera mwanaume maana aliona mke ana nguvu ya kiuchumi kumzidi, na tunawajua hawa wenzetu wanavyokuwa wakizidiwa na mwanamke.
 
Mi namuombea japo kaua lakini watoto kukosa wazazi mimi huwa inaniumiza sana
Masuala ya mauaji kama haya makandokando mengi sana - mikosi, laana kwenye koo, n.k.
Roho ya uuaji - katika ulimwengu wa roho haiji kirahisi rahisi.
Wenye busara walipoweka kuua bila ya kukusudia waliona mengi.

Ninachosikitika zaidi ni pale ndugu watakapitka kufuja mali. Ni vigumu sana ndugu kujali hao watoto.
 
Mmmh kwanini atoke jela my dada na ameua?
Alee hao watoto ambao alimuua mama yao ndani ya nyumba waliyokuwemo 😭

Na kabla hajaua alishamtishia mkewe kwamba atammaliza mpaka akahama nyumba?

Ni kweli, huku kwenye ndoa kunahitaji kujishusha sana, na kamdomo inabidi kupunguza.
Nafikiri wachaga swala la kujishusha kwenye mali, hawana!

💯 💯 📌
Hiyo kutishia kuua na kuua ni kesi nyingine maana dhamira ya kufanya hiyo kitu alikuwa nayo na akaja kuikamilisha. simuungi mkono lakini nikiwa na uzoefu kidogo wa haya mambo ndio maana naona akija kuweza kutoka aje alee familia yake.
kweli kaua lakini kuna mengi sana hatuyajui, na watoto hawa nakwambia huyo baba hawatamchukia niko hapa labda kama huyo baba kabla ya hicho kitendo alikuwa na matendo maovu.

Mi binafsi namuombea kwa sababu,
sisi waafrika wengi wetu tunatengeza maisha ya sasa hivi tukiwa hai! asilimia 90 hatutengenezi kesho ya watoto kesho ambayo mtoto atakuwa na uhakika wa malazi na elimu pamoja na huduma nyinginezo.
Nakwambia hao watoto wanaenda kuishi maisha ya manyanyaso, masimango, dharau. tusi la makosa ya baba yao na mama yao itakuwa ndio tusi lao maisha yao yote. Nimeona picha za watoto bado wadogo sana ni watoto wanaohitaji full time care nani atafanya hivyo???
Hao ndugu msiba ukiisha wape wiki mbili tu kama uko nao karibu utaniambia story nyingine tofauti kabisa.

Huyo kaka kafanya kosa kubwa mno bila kuangalia madhara yake!
na Kansa sio tiketi ya kifo kuna muda Mungu huwa anafanya maajabu yake sema kaharibu kila kitu.

Wanaume zetu wajifunze sana kuzuia hasira zao maana matokeo ya hasira yanakuja kubebwa na watoto wao.
 
Masuala ya mauaji kama haya makandokando mengi sana - mikosi, laana kwenye koo, n.k.
Roho ya uuaji - katika ulimwengu wa roho haiji kirahisi rahisi.
Wenye busara walipoweka kuua bila ya kukusudia waliona mengi.

Ninachosikitika zaidi ni pale ndugu watakapitka kufuja mali. Ni vigumu sana ndugu kujali hao watoto.
Kweli kabisa
 
Watoto wake ni the same linapokuja suala la mwanamke na mali kwanini Jane aliandika majina yake na ya watoto kwenye hio hati kinyume na makubariano? Kwanini asiandika majina yake na mumewe na ya watoto yote kwa pamoja au unahisi angefanya hivyo angepigwa risasi? Yaan mwanaume atafute kwa jasho halafu mwishoni mti ule aliokua anaupalilia kila siku umetoa kivuli kikubwa cha watu kukaa chini na kujipatia kivuli panapokua na jua kali then wale watu aliowaandalia kivuli wanamfukuza kwenye mti alioupanda na kuuhangaikia kwa muda mrefu yaan wanamtenga ungekua wewe ungechekelea? Muwe mnajiuliza mara 77
Kwahiyo kuua ni solution ya kutatua tatizo?

Aliyemtuma akajenge kwenye kiwanja cha mwanamke nani?

Haya sasa kapata faida gani zaidi ya kujiumiza yeye mwenyewe kisaikolojia na kimwili ( maana sasa hivi anaishi gerezani na magereza ya Tanzania si unayajua?)

Watoto wake walioshuhudia baba yao akimuua mama yao kawasababishia trauma za kipuuzi..!! Na upendo na ile bond ya baba na watoto haitokuwepo tena..!!

Watoto wake kawaacha yatima kwa uzembe wa sekunde 1 ya kufyatua risasi kwa hasira za kijinga..!!

Shida yenu wanaume hamkubali kuachika..!!
Nyie mnataka muache sio kuachwa..!
 
Hapa kuna tatizo zaidi ya nyumba.
Kuna kila dalili ya usaliti katika ndoa ambao ulipelekea chuki kati yao na kila mmoja kudai haki kwenye nyumba.....kwanini wanandoa walio ishi zaidi ya miaka 18 amabao wanawatoto 4 wagombanie nyumba? hapa lazima kuna usaliti umeingia.

Usaliti ndani kwa wanandoa au wapenzi limekuwa janga kubwa sana ambapo wahanga wakubwa wamekuwa wanawake.
Wanawake mlioko kwenye ndoa au mahusiano chukueni tahadhari, either ubaki kwenye mahusiano ukiwa mwaminifu ukishindwa kuwa mwaminifu jitoe haraka sana usisubiri kifo.
 
Mara zote huwa nasema huku ndani, mwanaume kukosa akili ndio chanzo cha matatizo mengi kwenye ndoa sababu kuanzia kwenye uchaguzi wa mwanamke wa kuishi nae mwanaume unatakiwa kumsoma huyu mtu atakuja kubadilika au la

Hapa bwana Kweka alikosa akili tokea mwanzo kwa kukubali kujenga kwenye kiwanja cha mwanamke maana ndio makosa yalipoanzia
Kujenga kwenye kiwanja cha mwanamke wa kichaga
 
Kwamba kiwanja alinunua mke kabla ya ndoa, na baada ya ndoa mume akakiendeleza Kwa asilimia Mia moja. Kwa hiyo umiliki wa hiyo nyumba kwa mujibu wa sheria ya ndoa unakuwaje?
 
Hapa kuna tatizo zaidi ya nyumba.
Kuna kila dalili ya usaliti katika ndoa ambao ulipelekea chuki kati yao na kila mmoja kudai haki kwenye nyumba.....kwanini wanandoa walio ishi zaidi ya miaka 18 amabao wana watoto 4 wagombanie nyumba? hapa lazima kuna usaliti umeingia.
Inawezekana
Usaliti ndani kwa wanandoa au wapenzi limekuwa janga kubwa sana ambapo wahanga wakubwa wamekuwa wanawake.
Wanawake mlioko kwenye ndoa au mahusiano chukueni tahadhari, either ubaki kwenye mahusiano ukiwa mwaminifu ukishindwa kuwa mwaminifu jitoe haraka sana usisubiri kifo.
Unataka kusema wanawake kwenye ndoa wanachepuka zaidi ya wanaume 🤔?
 
Kuna majitu humu ni majinga.. sikupata kufikiria hata humu JF kuna mabumunda kiasi hiki... majitu yanatetea ujinga sijui ni stress za maisha ama nini...

Huyo ch0k0 aitwae Kweka kwanini amuue huyo dada, kwanini utoe bastola una shoot mtu kikatili kichwani? hao ndio aina ya watu kama wale polisi walioua 29 Oct, ni aina ya watu ambao ni wa hovyo... kutoa uhai wa mtu kwao si kitu..

Huyo dada hajafanya kosa lolote kustahili kuuawa kama jambazi ama muuaji... kisa nyumba? hivi nyumba ni kitu cha kukufanya utoe uhai wa mtu?

Katika kitu sipendi ni uonevu, na naapa huyo dada angekuwa ndugu yangu, huyo muuaji ningemchinja kama kuku nipelekwe jela, nisinge hangaika kum shoot, ningechinja kama kuku, Ana bahati huyo mshenzi alijipeleka polisi maana anafahamu nini kingempata.... huyo mbwa angeji shoot na yeye, unaua mtu halafu unakimbiza korodani zako polisi... yeye si kidume , yeye ana hasira sana, basi angeji shoot..... mbuzi kabisa...
Hata mimi napata ukakasi sana na watu wanaotetea haya mauaji.
Kwenye tatizo lolote, solution haiwezi kuwa violence.

Tuache kujichukulia sheria mkononi, kuonea wale tunaofikiri tuna mamlaka au uwezo zaidi yao na tujifunze kuregulate emotions zetu!
 
Mbona tunaambiwa kiwanja walipewq kama zawadi ya Harusi wakati huo ?

pamoja na yote , jamaa kachafua familia snaa

Mfano sisi tulishakataa mwanaume home aliekuja kuposa mtoto yetu. Kwenye vetting tuliyofanya tulibaini baba ya huyo mwanaume alimuua mama yake mzazi kwa kumkata na mapanga…. Ni machame huko huko ukoo wa Mushi
Tulimkataa huyo jamaa

Kuna familia hao watoto wakiingia watakataliwa sana hasa familia zinazofanya vetting vema

History repeats … tunaamini hivo

Ukirudi nyuma kwenye ukoo wa kweka back then huenda sio tukio la kwanza kwao

That is why kuoa muhindi ni zaidi ya vetting za kuwa TISS kuepukq ujinga kama huu

THAT IS why hukuti huu ujinga kwa familia za wahindi

Vetting ni muhimu sana wazee - kuna familia nyingine sio kabisa kuruhusu kijana wako kuingia
Sahihi mkuu, historia hujirudia. Ni hatari sana mtu kuoa hao mabinti, na hata baba yao angetangulia mbele za haki kwa hila za mwanamke, basi hata mabinti nao wagekuwa na hayo maisha ya kutanguliza wanaume zao.
 
Back
Top Bottom