Labda leo niwape mkasa mmoja wa mwanafamilia mmoja huko kwetu. Huyu ni babu yangu, yaani ni mjomba wa baba yangu.
Huyu Mzee (Apumzike Salama) alikuwa ni mtumishi wa serikali tatu alipomaliza darasa la 12 (nakumbuka alikuwa akipenda kunitajia kiwango cha elimu yake akimaanisha elimu ya Form Four). Na akiwa kazini alifanikiwa kukutana bintinwa kichaga wa maeneo ya Mengwe pale Rombo. Mzee huyu ni mzaliwa wa mkoa wa Pwani. Hapa kuna mchanganyiko wa tamaduni mbili tofauti.
Walifanikiwa kupata watoto watatu na wote ni wakiume. Huyu babu yangu alikuwa Muslamu kwa dini yake na mkewe ni Mkristo wa Roman Catholic. Na wale watoto watatu walikuwa na majina ya Kiislamu ila wakaja kupewa majina ya kikristo na kubatizwa ili wawe wanaenda kanisani. Kifupi mwanamake alikuwa na nguvu ma ushawishi kwenye familia.
Nakumbuka wakati nasoma elimu ya upili hulo Kusini mwa Tanzania, pale nyumbami kwao Kigogo, Dar es Salaam palikuwa ni kambi yangu kwa ajili ya kwenda tuition za Mchikichini kwa sababu nyumbani kwetu ni mbali na Dar es Salaam.
Sasa ukifika pale, swali la kwanza utaulizwa unakaa siku ngapi. Pili yule mama atakupa masharti ya kuishi pale ndani. Na wakati huo kuna vijana wengine walikuwa wanakuja likizo kutokea Moshi na hawakuwa wakipewa masharti kama sisi WACHEZA VIGODORO. Na kama yule Mzee akikupa posho ya kupanda dala dala, ni lazima mama atakuuliza ulipewa kiasi gani. Na kuna muda alutaka posho ile ipitie kwake. Yule Mzee alikuwa anampatia posho ya kunipa mimi na baadaye angeniita chemba ili aniongeze yeye maana mkewe alikuwa anapunguza ile posho ya kunipa mimi.
Vikwazo hivi havikuwapo kwa wale wageni wa kutoka Moshi. Siku za mwisho wa wiki hawa vijana wangelala hadi muda wanaoutaka na wasiulizwe na mtu yeyote, ila sisi tulitakiwa kuamka asubuhi sana na kwenda mto Msimbazi kukata majani kwa ajilinya mbuzi, kurudi kufanyanusafi wa ndani, na mwishowe atawapa nguo za vijana wake watatu ili zifuliwe. Na baada ya hapo utapewa chai ya rangi ukae pembeni unywe ili yeye, watoto na nduguze wakae sebuleni wakinywa maziwa. Hatukuruhusiwa kutumia sebule tuliyoisafisha muda mfupi uliopita.
Yaani tukiwa tunaenda pale, anamwambia mdada wa kazi kutoka kwao apumzike kwa maana sisi tulikuwa tumefika. Na kweli ugali maharage utakaokula pale ni lazima uulipie muda so mrefu.
Ubaguzi huu haukuwa kwetu tu, ulimfikia hadi Mama mzaa mumewe. Yaani pale unaaweza kukuta Mama wa mwanamke na Mwanaume wamekutana kwa pamoja nyumbani kwa watoto wao ila kunakuwa na treatments mbili tofauti kwa wazazi hawa. Na ilifikia siku hadi Mama wa Mwanaume alichezea makofi mpaka akavunjwa mkono. Hii ilisababisha ndugu wengine wa Mwanaume wasuse kuwa wanakwenda pale. Kifupi jamaa alitengwa na familia yake.
Mbaya zaidi aliwakataza wale watoto wasiwe wanaenda kwa ndugu zao kule Pwani. Likizo walikuwa wanaenda Moshi na akwa anawaambia huku ndiyo kwenu.
Basi yule Mzee akawa anaishi kwa kutengwa na mwisho alistaafu. Baada ya muda akapata shida ya kupooza mwili. Nilisikia kuna muda alitengwa kwenye chumbanchabuani akijisaidia humo humo ndani. Ndipo siku moja nikapanga safari kutoka mkoani ninapofanya kazinna kwenda kumuona MSELA wangu. Nilimkuta na hali mbaya sana. Kwa maneno yake mwenyewe alikuwa akilalamika na akilia kuwa mkewe na watoto wake walikuwa wakimtembezea kichapo wakati akiwa na hali ile ya kupooza mwili. Kiukweli nilitokwa na machozi. Nilikaa pale na nikamtoa pale uani ili jifanye usafi kwenye chumba alichokuwa akiishi. Kilikuwa kichafu sana. Mzee alifarijika sana kwa mimi kwenda kumuona. Nilipomuaga jioni kuwa naenda zàngu, alilia sana na akaniambia nirudi tena kumuangalia.
Ilifikia muda waliamua kumuhamisha kutoka Dar es Salaam na kumpeleka Kibaha - Misugusugu ambapo walikuwa na shamba maeneo hayo na mifugo. Mke na watoto waliendelea kuishi Dar es Salaam na kumuacha kule akiangaliwa na mfanyakazi wa kike.
Mwaka wa juzi yule Mzee alifariki akiwa na mfanyakazi tu pale shambani. Watoto wote walikuwa makazini kwao Dar es Salaam na wengine Dodoma.
Sasa ikafikia muda wa mazishi, yule mama wa kichaga akawa anataka ndugu wa marehemu wawepo kwenye msiba, ila ndugu wengi walikataa kwenda. Mimi nilisafiri kutoka mkoani na kwenda Kibaha kumsindikiza MSELA wangu. Nakumbuka alinivusha pakubwa sana wakati wa kutafuta elimu alikuwa na msaada mkubwa sana.
Yule Mama aligoma mumewe asizikwe kwenye shamba lao walilotafuta pamoja, alizikwa kwenye makaburi ya Waislamu.
Wakati wa uhai wake, Mzee alifanikiwa kuwekeza kwenye mashamba na nyumba zilizopo Morogoro, Tanga na Pwani. Hakuna mtu anaweza kujua nini kiliendelea baada ya kifo chake.
Hapa tupate dunzo kidogo. Wazee wetu walikuwa na maana kubwa sana kutufundisha kuoana na mke au mume mnayefanana tamaduni. Hii michezonya kuokotana na kuanza maisha bila ya kujuana, mwisho wake huwa ni mbaya sana.
Na huu ndiyo ukawa mwishonwa MSELA wangu. (R.I.P)