Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 Oct 2011

Aghakhan hawawezi ku-detect Malaria!!!! Aghakhan hawawezi ku-detect Sinusitis!!! Aghakhan wana thermometers za homa tu!!!

Aghakhan!!!...
mkuu hili ni jambo la kushangaza. tena malaria yenyewe si wadudu watatu ni wadudu 150 hata mwanafunzi wa siku moja tu kwenye maabara atawaona kwenye kipimo hata kama ni ile darubini ya zamani! Anyway ndio hospitali zetu hizo.isije ikawa hata muhimbili nao wamekosea manake nao hawaaminiki baada ya kupasua kichwa badala ya mguu!
 
Dua zetu zote zipokelewe. Na hatua zote, njia zote ulizopitia ni mapenzi na usimamizi wa Mwenyeezi Mungu. Yupo pamoja nawe na atakuponya tu.
 
Zitto,
Pole sana, tambua kuwa binadamu wote huwa na maradhi na hupata maradhi. Inategemea tu ni aina ya maradhi gani.

Hivi sasa jambo muhimu ni kuendelea na matibabu na kupata mapumziko ya kutosha hasa utakaporudi nyumbani.

Tatizo linawalowakabili viongozi wengi na hasa wanasiasa waadilifu na wapiganaji wa kweli ni kuwa na munkari wa kufanya kazi nyiingi kwa wakati mmoja na bila kupata muda mrefu wa kupumzika.

Hali hii inaweza kukuletea madhara zaidi. Ukitoka kwa surgery tumia muda mrefu kupumzika zaidi hata ya muda waliokupangia madaktari. At the end of the day you are the one who will strenghthen your health or weaken it.

Kumbuka kuwa watanzania wote wenye mapenzi mema na uzalendo wa nchi yao, wako nyuma yako.

Pole sana zitto, tunakuombea na utakuwa salama.

Julius Mtatiro,
30.10.2011.
 
bora kamanda umeliona hilo, NAPE ajitokeze walu na yeye atoe pole
 
Kila la heri kaka mkubwa. Aghakhan wameshawahi kusababisha dogo wa rafiki yangu kupoteza maisha kwa kumchelewesha wakitibu wasichokifahamu
 
tENA AGHAKAN BEI ZAO ZIKO JUU MNO!! nA TENA UKIENDA PALE NA BIMA YA AFYA NDIO BEIZ ZAO ZINAZIDISHWA KARIBU MARA TATAU YA BEI YA KAWAIDA!

INABIDI ICHUNGUZWE HASA KATKA BEI WANAMLIPISHA MTU MWENYE BIMA YA AFYA TUSIPOKUWA MAKINI HII HOSPTILA ITAIFILIZI BIMAYA AFYA TUTARUDI KULE!!!!!!!

Kwani hao AGHA KHAN walijuaje kwamba kuna pesa zinatolewa "BIMA YA AFYA" kwa ajili ya wafanyakazi? Tatizo liko kwetu waswahili hatajali watanzania wenzetu, michoro yote ya kulazimisha wafanyakazi kwenda Agha Khan inasukwa na watu wa BIMA YA AFYA wakishirikiana na watoa huduma za afya kwa kudanganywa na kitu kidogo TU. At the end of the day wanao faidika ni watoa huduma za afya, ukiangalia bill zao utashangaa sana.

Mtu unajiuliza hivi mbona hata hapo Agha Khan madaktari walio wengi wanatoka Muhimbili, sasa inakuwaje shirika la UMMA linashindwaje kuwapeleka wafanyakazi wagonjwa wanaolipiwa na "BIMA YA AFYA" kwenda Muhimbili wakalipa hela kidogo kwenye uduma za kulipia, badala yake wanakwenda kuwanufaisha watu wasiyo jali huduma za wagonjwa wanacho jali zaidi ni PESA - na wakishindwa pale utawasikia wanasema mpeleke Muhimbili when its too late, hili Hospitali hiyo ya Taifa ilahumiwe kwa kusababisha vifo. Hivi vitu siyo vyakudhalau, tunapashwa kuwa macho sana, mis-diagnosis iliyotokea kwa Mh. Kabwe inaweza kutokea kwa mtu yeyote pale, nilisha sema humu familia yangu imekwisha pata zahama hizi mara nne - hii hawezekani hikawa bahati mbaya, kuna tatizo pale.
 
Ahsante kwa taarifa. Mungu azidi kumtia nguvu na amponye haraka mpambanaji wetu. Taifa hili linamuhitaji sana zitto na mchango wake sikuzote nitauheshimu.

Tunamwombea apone haraka
 
Umesaidia saana saana kuliondoa taifa katika taharuki ya imani potofu kwamba sasa viongozi wetu wanaugua kwa mkono wa mtu.
 
God has to be fair to the united republic of TZ, we dnt wana lose ZITTO at this age and time.
 
Wana JF,
Hii ni email kutoka kwa Mh. Zitto Kabwe. Nimeona ni vyema niiweke hapa ili tuweze kujua kwapamoja hali yake inavyoendelea.
Nawasilisha,
Nice 2

Ndugu zangu,

Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kuniwezesha muda huu kuwa na nguvu za kukaa katika kiti na kuweza kuandika haya machache kwenu. Nawashukuru sana Wanamabadiliko kwa salaam zenu nyingi za pole mara mliposikia ninaumwa na kulazwa hospitalini. Najua hamkuwa na taarifa kamili za kuumwa kwangu na kwa kweli suala la kuumwa ni suala la mtu binafsi (hata kwa mtu mwenye dhamana ya kiuongozi wa umma japo umma nao una haki ya kujua kinachomsibu kiongozi husika).

Mwanzo

Nilianza kupatwa na maumivu ya kichwa usiku wa siku ya Ijumaa tarehe 20 jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili kutoka Jimboni tayari kwa kazi za Kamati za Bunge ambapo Kamati yangu ilikuwa imekwishaanza kazi wiki hiyo kwa kupitia mahesabu na utendaji wa Mamlaka za Maji nchini.

Kama kawaida yangu niliona maumivu hayo makali kama ni sehemu tu ya uchovu wa ziara za Jimboni na safari za mara kwa mara nilizofanya kuinigilia ziara za Jimboni ikiwemo kuhudhuria Mdahalo wa Umeme na Mkutano wa Uwekezaji Kanda ya Ziwa Tanganyika.

Hivyo nililala na nilipoamka kichwa kilikuwa kimepona na hivyo nikahudhuria kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma katika Ofisi ya Bunge mpaka saa saba mchana.

Siku ya Jumapili saa kumi na moja jioni nikiwa katika Hoteli ya Southernsun nilipatwa na homa kali ghafla. Nilikatisha mkutano niliokuwa nao na kuamua kurejea nyumbani, lakini nilishindwa kuendesha gari na hivyo kumwomba Dereva wa Mhe. Mhonga anifuate ili anisadie kunifikisha nyumbani.

Nilipofika nyumbani kwangu Tabata, homa ilizidi kupanda na hivyo kuamua kwenda Hospitali mara moja. Nikapelekwa Agakhan Hospital na nikapata huduma.

Nilipochukuliwa vipimo ilionekana sina malaria wala homa ya matumbo na pia hawakuweza kuona sababu ya homa ile namna ile (maana ilifikia degree 40).

Walituliza homa, nikapewa Panadol na baadaye nikaruhusiwa kurudi nyumbani mnamo saa tano usiku. Nilipoamka siku ya Jumatatu nikaenda kazini kuongoza Kikao cha Kamati ya Bunge ambapo tulikuwa tunashughulikia Hesabu za Bodi ya Utalii na Benki ya Posta Tanzania.

Nilipita Agakhan kupata majibu ya ziada na kuambiwa nipo sawa ila nipumzike nisifanye kazi kwa siku kadhaa na nitakuwa sawa.

Hali kubadilika

Siku ya Jumanne niliamka nikiwa salama, kichwa kikiuma kwa mbali lakini sio vya kutisha. Nikawajulisha wajumbe wenzangu wa kamati kuwa sitakwenda kazini na wao waendelee na kazi.

Hata hivyo ilipofika saa sita kamili nilianza kutetemeka mwili mzima na homa kuwa kali sana huku kichwa kikiniuma sana sana sana!

Dada zangu wakamwita Driver na kunikimbiza Hospitali ya Agakhan. Wakarejea vipimo vilevile na matokeo yakawa yaleyale. Joto lilifika degree 39.8 Hivyo wakanipa dawa za kupoza homa na maumivu ya kichwa kwa drips na sindano kadhaa.

Siku ya pili hospitalini nikafanya vipimo zaidi ikiwemo ultra sound na vyote kuonekana sina tatizo lolote. Niliendelea kuwepo Hospitali na kwa kweli hali ilikuwa inatia moyo sana kwani nilipata nguvu na hata kuweza kuzungumza, homa ilikuwa imepungua sana.

Pamoja na kwamba Mganga Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Waziri wa Masuala ya Bunge na Daktari wangu binafsi kuwataka waangalie upya vipimo vya malaria, madaktari wa Agakhan waliwahakikishia viongozi hawa na Daktari wangu kwamba hawajaona Malaria na hivyo wanaendelea na uchunguzi wa 'a trigger' ya homa kali niliyokuwa napata.

Hali kuwa Mbaya

Usiku wa siku ya Jumatano Hali ilikuwa mbaya sana. Joto lilipanda tena kufikia 40 na kichwa kuuma zaidi. Nilikuwa kama ninatwangwa kwenye kinu kwa kweli. Nilikuwa natetemeka sana. Ilikuwa taharuki kubwa sana katika chumba nilicholazwa.

Wageni waliokuwa wamekuja kunijulia hali wakati hali inabadilika ilikuwa ni pamoja na Ndugu Murtaza Mangungu na Mohamad Chombo ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya POAC, walishauri mara moja nihamishwe Hospitali kupelekwa Muhimbili.

Muda si mrefu kupita Waziri Lukuvi na Katibu wa Bunge walifika, wakaafiki na nikahamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na kwa hali niliyokuwa nayo nikalazwa katika Chumba wanachokiita Mini-ICU. Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Mama Blandina Nyoni alikuwepo Hospitalini tayari.

Usiku huo huo nilifanyiwa vipimo upya. Full Blood picture pamoja na BS. Vile vile kufuatia malalamiko kuhusu maumivu ya kichwa ikaamuliwa kuwa nifanyiwe CT Scan usiku ule.

Ikaonekana nina wadudu wa Malaria 150 na mara moja nikaanza matibabu. Namshukuru sana Daktari kijana Dkt. Juma Mfinanga kwa umahiri mkubwa aliouonyesha tangu nilipofika pale Mini ICU.

Asubuhi ya siku ya pili nikapata majibu ya tatizo la maumivu ya kichwa. Nimekuwa nasumbuliwa na kichwa kwa miaka zaidi ya Kumi sasa na katika kipindi hicho mara nne nilipoteza fahamu na kuanguka (Mara ya kwanza mwaka 2000 nikiwa Jijini Mwanza nikielekea kwenye Mkutano wa Vijana wa National Youth Forum, Mara Pili Mjini Dodoma katika mkutano kama huo mwaka 2001 lakini ilikuwa usiku, Mara ya tatu Nikiwa chumbani, Hall II mara baada ya kutoka *Prep, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2002 na mara ya Nne Bungeni siku ya kupitisha Muswada wa Madini 2010 kufuatia wiki nzima ya Kamati na Mjadala wa Bunge (Ndugu Katulanda anakumbuka siku hii kwani yeye ndiye niliyemkamata njiani kunikimbiza Zahanati ya Bunge).

Tatizo lililogundulika ni SINUSITIS, ambayo tayari imekuwa sugu. Daktari Bingwa wa magonjwa haya Dkt. Kimaryo akanieleza kwa kirefu juu ya tatizo hili na kuniambia suluhisho ni 'surgery' na pale Hospitali ya Taifa hawafanyi hiyo operesheni. Akashauri niletwe India ambapo kuna Daktari mpasuaji wa ugonjwa huu. Nikakubali.

Baada ya kuwa Malaria imedhibitiwa kwa kufikia nusu ya 'dozi' nilopewa na wadudu kuonekana kutokomea, Ofisi ya Bunge ikaandaa safari. Nimefika India. Nimebakiza sindano mbili ili kumaliza 'dozi' hiyo na tayari nimefanyiwa taratibu zote kwa ajili ya 'surgery' hiyo.

Sijafa

Uvumi ulienezwa nimekufa. Kwa kupitia kwenu ndugu zangu Wanamabadiliko, napenda Watanzania wenzangu wajue mimi ni mzima wa Afya. Nimepata maradhi kama Binadamu mwingine yeyote anavyoweza kupata na namshukuru Mungu kwamba ninapata matibabu mazuri kabisa.

Shukran
Nawashukuru sana Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili chini ya Prof, Mwafongo kwa juhudi kubwa walioonyesha katika kunihudumia. Naishukuru Ofisi ya Bunge kwa Kutimiza wajibu wao kwangu kama Mbunge, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya kwa kuonyesha upendo wa hali ya juu na watumishi wote wa Wizara ya Afya, Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Slaa kwa ufuatiliaji wa karibu wa Afya ya Naibu wake, Wabunge wajumbe wa Kamati ya POAC, Dkt. Alex Kitumo, ndugu, jamaa na marafiki zangu wote.

Nawapa pole wananchi wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kwa uvumilivu mkubwa hasa kufuatia uvumi mbalimbali ulioenezwa, pia Watanzania wengine kwa uzito huo huo.

Nitawajulisha kwa lolote Mungu akipenda. Ninaendelea na matibabu na hali yangu ni nzuri

Ndugu yenu

Zitto

Tuko pamoja katika sala.
 
hapa ndipo huwa namkubali Zitto. anatoa habari wakati muafaka na si kuwaaacha watu waanze kubuni. Zitto ni mwanasiasa wa kisasa anajua information is power. amejitofautisha na wanasiasa wengine ambao wako India ambao sisi ndio tunawalipia gharama za zmatibabu lakini hatujui wanaumwa nini! Big up ZZK

Jamani yaani Agakhan hawawezi kubaini malaria wakati ndipo panapotegemewa? Twafwa

Well said,umenikumbusha current waziri wa afya Kenya Prof Anyang ambaye alibainika kuuguwa prostate cancer na akaamua to go public, kitendo ambacho kimewafungua macho wengi juu ya ugonjwa huu/ unatibika ukiwahiwa mapema.
 
Pole sana mheshimiwa Zitto kwa ugonjwa ulioupata. Jambo la kumshukuru Mungu ni kwamba umegundulika una huo ugonjwa ambao unatibika.
Mie binafsi nimewahi kupatwa na ugonjwa kama huo ambao ulinitesa kwa kipindi cha miaka kama kumi hivi. Nimewahi kupoteza fahamu mara kadhaa na ikawa inatafsiriwa kwamba nina Kifafa.
Namshukuru sana Dr Edwin wa hospitali ya Muhimbili aliyegundua tatizo langu na kulimaliza kabisa. Nina miaka mitatu sasa sina hilo tatizo kabisa. Hivyo ninaimani kwamba na wewe utarejea katika hali yako ya kawaida na kuendelea na ujenzi wa taifa. Sote tunakuombea upone haraka!
Wana JF,
Hii ni email kutoka kwa Mh. Zitto Kabwe. Nimeona ni vyema niiweke hapa ili tuweze kujua kwapamoja hali yake inavyoendelea.
Nawasilisha,
Nice 2

Ndugu zangu,

Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kuniwezesha muda huu kuwa na nguvu za kukaa katika kiti na kuweza kuandika haya machache kwenu. Nawashukuru sana Wanamabadiliko kwa salaam zenu nyingi za pole mara mliposikia ninaumwa na kulazwa hospitalini. Najua hamkuwa na taarifa kamili za kuumwa kwangu na kwa kweli suala la kuumwa ni suala la mtu binafsi (hata kwa mtu mwenye dhamana ya kiuongozi wa umma japo umma nao una haki ya kujua kinachomsibu kiongozi husika).

Mwanzo

Nilianza kupatwa na maumivu ya kichwa usiku wa siku ya Ijumaa tarehe 20 jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili kutoka Jimboni tayari kwa kazi za Kamati za Bunge ambapo Kamati yangu ilikuwa imekwishaanza kazi wiki hiyo kwa kupitia mahesabu na utendaji wa Mamlaka za Maji nchini.

Kama kawaida yangu niliona maumivu hayo makali kama ni sehemu tu ya uchovu wa ziara za Jimboni na safari za mara kwa mara nilizofanya kuinigilia ziara za Jimboni ikiwemo kuhudhuria Mdahalo wa Umeme na Mkutano wa Uwekezaji Kanda ya Ziwa Tanganyika.

Hivyo nililala na nilipoamka kichwa kilikuwa kimepona na hivyo nikahudhuria kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma katika Ofisi ya Bunge mpaka saa saba mchana.

Siku ya Jumapili saa kumi na moja jioni nikiwa katika Hoteli ya Southernsun nilipatwa na homa kali ghafla. Nilikatisha mkutano niliokuwa nao na kuamua kurejea nyumbani, lakini nilishindwa kuendesha gari na hivyo kumwomba Dereva wa Mhe. Mhonga anifuate ili anisadie kunifikisha nyumbani.

Nilipofika nyumbani kwangu Tabata, homa ilizidi kupanda na hivyo kuamua kwenda Hospitali mara moja. Nikapelekwa Agakhan Hospital na nikapata huduma.

Nilipochukuliwa vipimo ilionekana sina malaria wala homa ya matumbo na pia hawakuweza kuona sababu ya homa ile namna ile (maana ilifikia degree 40).

Walituliza homa, nikapewa Panadol na baadaye nikaruhusiwa kurudi nyumbani mnamo saa tano usiku. Nilipoamka siku ya Jumatatu nikaenda kazini kuongoza Kikao cha Kamati ya Bunge ambapo tulikuwa tunashughulikia Hesabu za Bodi ya Utalii na Benki ya Posta Tanzania.

Nilipita Agakhan kupata majibu ya ziada na kuambiwa nipo sawa ila nipumzike nisifanye kazi kwa siku kadhaa na nitakuwa sawa.

Hali kubadilika

Siku ya Jumanne niliamka nikiwa salama, kichwa kikiuma kwa mbali lakini sio vya kutisha. Nikawajulisha wajumbe wenzangu wa kamati kuwa sitakwenda kazini na wao waendelee na kazi.

Hata hivyo ilipofika saa sita kamili nilianza kutetemeka mwili mzima na homa kuwa kali sana huku kichwa kikiniuma sana sana sana!

Dada zangu wakamwita Driver na kunikimbiza Hospitali ya Agakhan. Wakarejea vipimo vilevile na matokeo yakawa yaleyale. Joto lilifika degree 39.8 Hivyo wakanipa dawa za kupoza homa na maumivu ya kichwa kwa drips na sindano kadhaa.

Siku ya pili hospitalini nikafanya vipimo zaidi ikiwemo ultra sound na vyote kuonekana sina tatizo lolote. Niliendelea kuwepo Hospitali na kwa kweli hali ilikuwa inatia moyo sana kwani nilipata nguvu na hata kuweza kuzungumza, homa ilikuwa imepungua sana.

Pamoja na kwamba Mganga Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Waziri wa Masuala ya Bunge na Daktari wangu binafsi kuwataka waangalie upya vipimo vya malaria, madaktari wa Agakhan waliwahakikishia viongozi hawa na Daktari wangu kwamba hawajaona Malaria na hivyo wanaendelea na uchunguzi wa 'a trigger' ya homa kali niliyokuwa napata.

Hali kuwa Mbaya

Usiku wa siku ya Jumatano Hali ilikuwa mbaya sana. Joto lilipanda tena kufikia 40 na kichwa kuuma zaidi. Nilikuwa kama ninatwangwa kwenye kinu kwa kweli. Nilikuwa natetemeka sana. Ilikuwa taharuki kubwa sana katika chumba nilicholazwa.

Wageni waliokuwa wamekuja kunijulia hali wakati hali inabadilika ilikuwa ni pamoja na Ndugu Murtaza Mangungu na Mohamad Chombo ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya POAC, walishauri mara moja nihamishwe Hospitali kupelekwa Muhimbili.

Muda si mrefu kupita Waziri Lukuvi na Katibu wa Bunge walifika, wakaafiki na nikahamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na kwa hali niliyokuwa nayo nikalazwa katika Chumba wanachokiita Mini-ICU. Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Mama Blandina Nyoni alikuwepo Hospitalini tayari.

Usiku huo huo nilifanyiwa vipimo upya. Full Blood picture pamoja na BS. Vile vile kufuatia malalamiko kuhusu maumivu ya kichwa ikaamuliwa kuwa nifanyiwe CT Scan usiku ule.

Ikaonekana nina wadudu wa Malaria 150 na mara moja nikaanza matibabu. Namshukuru sana Daktari kijana Dkt. Juma Mfinanga kwa umahiri mkubwa aliouonyesha tangu nilipofika pale Mini ICU.

Asubuhi ya siku ya pili nikapata majibu ya tatizo la maumivu ya kichwa. Nimekuwa nasumbuliwa na kichwa kwa miaka zaidi ya Kumi sasa na katika kipindi hicho mara nne nilipoteza fahamu na kuanguka (Mara ya kwanza mwaka 2000 nikiwa Jijini Mwanza nikielekea kwenye Mkutano wa Vijana wa National Youth Forum, Mara Pili Mjini Dodoma katika mkutano kama huo mwaka 2001 lakini ilikuwa usiku, Mara ya tatu Nikiwa chumbani, Hall II mara baada ya kutoka *Prep, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2002 na mara ya Nne Bungeni siku ya kupitisha Muswada wa Madini 2010 kufuatia wiki nzima ya Kamati na Mjadala wa Bunge (Ndugu Katulanda anakumbuka siku hii kwani yeye ndiye niliyemkamata njiani kunikimbiza Zahanati ya Bunge).

Tatizo lililogundulika ni SINUSITIS, ambayo tayari imekuwa sugu. Daktari Bingwa wa magonjwa haya Dkt. Kimaryo akanieleza kwa kirefu juu ya tatizo hili na kuniambia suluhisho ni 'surgery' na pale Hospitali ya Taifa hawafanyi hiyo operesheni. Akashauri niletwe India ambapo kuna Daktari mpasuaji wa ugonjwa huu. Nikakubali.

Baada ya kuwa Malaria imedhibitiwa kwa kufikia nusu ya 'dozi' nilopewa na wadudu kuonekana kutokomea, Ofisi ya Bunge ikaandaa safari. Nimefika India. Nimebakiza sindano mbili ili kumaliza 'dozi' hiyo na tayari nimefanyiwa taratibu zote kwa ajili ya 'surgery' hiyo.

Sijafa

Uvumi ulienezwa nimekufa. Kwa kupitia kwenu ndugu zangu Wanamabadiliko, napenda Watanzania wenzangu wajue mimi ni mzima wa Afya. Nimepata maradhi kama Binadamu mwingine yeyote anavyoweza kupata na namshukuru Mungu kwamba ninapata matibabu mazuri kabisa.

Shukran
Nawashukuru sana Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili chini ya Prof, Mwafongo kwa juhudi kubwa walioonyesha katika kunihudumia. Naishukuru Ofisi ya Bunge kwa Kutimiza wajibu wao kwangu kama Mbunge, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya kwa kuonyesha upendo wa hali ya juu na watumishi wote wa Wizara ya Afya, Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Slaa kwa ufuatiliaji wa karibu wa Afya ya Naibu wake, Wabunge wajumbe wa Kamati ya POAC, Dkt. Alex Kitumo, ndugu, jamaa na marafiki zangu wote.

Nawapa pole wananchi wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kwa uvumilivu mkubwa hasa kufuatia uvumi mbalimbali ulioenezwa, pia Watanzania wengine kwa uzito huo huo.

Nitawajulisha kwa lolote Mungu akipenda. Ninaendelea na matibabu na hali yangu ni nzuri

Ndugu yenu

Zitto
 
Mh. Zitto sisi wana mabadiliko na watanzania wote kwa ujumla tunamuomba Mwenyezi Mungu azidi kukulinda na kukusimamia ili upone hara na urudi nyumbani.Tunakuhitaji haraka kabla ya kikao cha bunge maana ukiwa pale mbele na mh. Lissu michango yenu ni muhimu.Pia unahitajika maana ule muswada wa katiba mpya ndio utawasilishwa.GET WELL SOOOOOOOOON ZITTO ZUBERY KABWE.
 
Ndugu Kazi ndiyo kipimo cha utu,sina shida yoyote na daktari huyo.Hata hivyo hapo chini nimekubandikia tena,ugonwa huo kuwa cronic unaweza kujulikana kwa dalili na si lazima muda kama unavyodai hiyo miaka 10.Dalili za cronic sinusitis ni hizo hapo chini...

Isipokuwa mtiririko huo wa kutibu ni wa cronic sinusitis,na hizo hapo juu ni dalili zake.Kwa hiyo miaka 10 hajawahi kupatiwa tiba yoyote ya sinuistis zaidi ya ile ya malaria.

Kwahiyo miaka 10 alikuwa anajuwa kuwa ni cronic sinutis?Jibu la wazi ni "no"
Nadhani daktari aliassume kuwa nyakati hizo Zitto alijuwa ni sinusitis inamsumbua.

Kiutaratibu,surgery huwa ni option ya mwisho.

Nakubaliana na hoja kwamba tuboreshe idaya zetu za afya na vitendea kazi.However sikubaliani na wewe kuhusisha miaka kumi ya kuuguwa kwake na cronic sinutis.Kitaalamu wanasema ina last 12 weeks despite treatment attempts...

Na hizo treatment attempts hazikuwa za sinusitis,for 10 years hakujuwa,ama hawaku i diagnose.Na kwa mujibu wa Zitto,dalili ambayo ameitaja na inaendana na maelezo ya ugonjwa huu ni headache peke yake.Mengine hatujui.Inawezekana alipatwa na homa iliyosababishwa na sunsitis.Sasa sijui hiyo sinusitis ina uhusiano gani na malaria.Ndipo hapo sometimes ni kuchanganyana tu.
Ndugu Mushi!
Rudia maelezo yangu ya awali swali langu kwako kwani ktk hiyo miaka kumi aliyokuwa anasumbuliwa na hilo tatizo Mheshimiwa Mbunge alienda kutibiwa muhimbili au Hospitali nyingine ambazo ni consultant hospitals eg. kcmc na bugando,kutokana na maelezo yake mwenyewe ni hapana na huko kwenye hizo hospitali ndiyo kuna madaktari bingwa washauri(Consultant Specialists).Na nilipoweka kigezo cha miaka kumi ni kwamba ktk hiyo miaka kumi ambayo ameishi na hilo tatizo bila ya kutibiwa limepelekea kuleta complication ikiwemo kuathiri mfumo wake Nasal Sinus drainage na Surgery to improve the drainage of the sinus is the only option.Wewe unaweka mabandiko ya maelezo ya Chronic Sinusitis lkn unachosahau ni kwamba huna matokeo ya ugunduzi wa vipimo vya dakari aliyeamuona Mh. Zitto na kuona tatizo lilipofikia ni lazima afanyiwe operesheni.Na wala findings za kitaalamu ikiwemo CT -SCAN wewe na mimi hatuna lkn mimi naelewa na Science ya huo ugonjwa ni unapokuathiri kwa hizo siku kadhaa hata kama hukutibiwa unaweza ukapata nafuu lkn baadae ukarudia tena na kila unaporudia tenana tena unaathiri mfumo wa drainage kwenye hizo sinuses yaani Frontal Sinus,Ethmoidal Sinuses ,Maxillary Sinus na mara nyingine kuziba na unapoziba ndiyo unapozidisha Intracranial Pressure na moja ya sign ya hilo kipanda kichwa (Persistent severe headache) ambayo haisikii dawa .Lingine anaweza akawa na nasal polyps ambayo inapelekea kuziba(block)mfumo na inategemea ukumbwa hiyo polyp nayo surgery inahitajika kuiondoa ili kufungua mfumo wa drainage wa pua.Sasa hayo ni maswala ya Zitto na daktari wake kama wataona ni vyema kutumegea ,kwani ni uamuzi wa mgojwa kuanika kwa undani kinachomsibu.
 
Ni kweli kabisa akirudi aangalie namna ya kujenga uwezo yeye kama change agent.
Hii ni changamoto kuuubwa tunapoazimisha miaka 50 tangu uhuru. Jamani Sinusitis ni ugonjwa wa kawaida sana. Kwa lugha nyepesi ni kwamba kamasi zinakuwa zimeingiliwa na bacteria/virusi. Mara nyingi hao vijidudu hushambulia kwenye chanzo cha hifadhi ya hizo kamasi (sinus)ambazo ziko kulia na kushoto kwa pua sambamba na matundu ya pua. Unaweza ukatibiwa kwa kupewa antibiotics au kwa kupasuliwa ili kuondoa kabisa "sinus" yote iliyoathirika ili inayotengenezwa isichanganyike na yenye vijidudu. Hizo "sinus" ni mfano wa visahani ambavyo viko viwili yaani kulia na kushoto kwa pua.
Kama nilivosema awali, ni ugonjwa mdogo sana ambao kwa miaka 50 tulitakiwa tuwe tunaweza kuutibu hapa nchini. Wataalamu wa mabo ya Sinus wanasema kuwa kila binadamu amewahi kuugua ugonjwa huu wengi wetu huwa tunadhani ni kifafa!
Kuhusu kwenda India mie sipingi ila imekuwa too much! Hii ni kudharaulisha wataalam wetu wa afya kwamba hawana huo uwezo. Kisingizio kinakuwa eti wanaoenda India ni kwa sababu hatuna vifaa nchini vya kutibu hayo magonjwa! Jamani kwani ni tangu lini tumebaini hivyoo? Kwani hivo vifaa wanavotumia India havipo madukani? Au tukienda kununua huko wanakonunua wahindi hatutauziwa?
Naamini kama tukitaka "muhi2 " yetu iwe kama Apollo ya India inawezakana tuu! Ni kununua vifaa na kuwapeleka wataalamu wetu hukuhuko wanakosomeshwa wataalamu wa India! Ni suala la kuamua tuu na inawezekana.
Wao(akina Zitto, Mwakyembe, Mwandosya nk) wanapelekwa India! Je mimi na wewe tutaweza kumudu gharama za kwenda huko ikiwa ni pamoja na usafiri wa kwenda na kurudi, malazi na chakula?
Kwa waliowahi kwenda huko wansema gharama za matibabu si kubwa saana ila!
Jamani tubadilike sasa! Kila anaeumwa hata "malaria" anapelekwa India! Inauma sana jamani!
Nawasilisha
Dah kila raia angekuwa anapewa huduma na attention kama hii......2015 lazima niingie kwenye ligi ya kuongeza thamani ya maisha.

Kila la kheri Muhishimiwa Zitto. Ukishapona usisahau kuwajengea uwezo hao wa Muhimbili pia. Inawezekana wajomba au wajukuu zako wasipate bahati ya kwenda India..who knows?
 
Kumbe ni kweli ulipatwa na maradhi hotelini ukiwa na BIBI (Kimada)?
 
Back
Top Bottom